PANGANI YAHITAJI MIL 200 ILI KUTEKELEZA MIRADI YA AFYA.
JUMLA ya shilingi milioni 200 zinahitajika kila mwaka ili kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo katika Idara ya Afya wilayani Pangani mkoani Tanga iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi mzuri.
Kaimu Mganga wa wilaya ya Pangani,Dr.Frank Makunde aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari za vijijini mkoa wa Tanga (Taruja)walioitembelea halmashauri ya wilaya hiyo kwa lengo la kuzungumza na waataalamu kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.
Waandishi hao walikuwa wilayani Pangani kwenye semina ya wandishi wa habari za mazingira ambayo iliratibiwa na chama hicho na kufadhiliwa na shirika la hifadhi ya Taifa ya Tanzania (Tanapa) yenye lengo la kuwapa uelewa wanahabari juu ya umuhimu na uhifadhi wa mazingira.
Makunde amesema idara hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti hali ambayo inapelekea kukwamisha baadhi ya miradi yao muhimu kwa jamii zinazowazunguka na kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
Aliongeza kuwa mfumo manunuzi uliowekwa na serikali unakwamisha sana watendaji mbalimbali kwenye halmashauri hasa katika idara ya afya na kupelekea kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.
"Mfumo wa kuwalazimisha kununua vitu MSD wanapeleka maombi ya vitu wanaambiwa havipo hali ambayo inawapa usumbufu mkubwa wa kusubiri wakati uhitaji wetu ni kwa wakati huo hivyo kupelekea kukwambisha shughuli zetu za kila siku ....tunaiomba serikali iangalie mfumo wa MSD usiwe mmoja uwe zaidia ya mmoja ili kuleta ushindani "Alisema Makunde.
Aidha alisema idara hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa watumishi hali ambayo inapalekea watumishi wengine kufanya kazi za ziada na kueleza suala lengine linalowapa wakati mgumu sana ni kutokuwepo wa nyumba za kutosha za watumishi kitendo ambacho kinachangia watumishi wengine kutopenda kufanya kazi wilayani
humo.
Alieleza changamoto nyengine wanayokabiliana nayo ni uhaba wa vitendea kazi hasa kwenye wodi ya wakina mama wajawazito ikiwemo uchangia mdogo wa wananchi katika mfuko wa afya ya Jamii (CHF).
Post a Comment