Latest Post
YAW BERKO KUANZA KESHO MAPINDUZI
YAW BERKO KUANZA KESHO MAPINDUZI
Kocha
Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema kesho atatoa nafasi kwa kipa Yaw Berko
rais wa Ghana kuanza katika kikosi cha kwanza.
Logarusic raia wa Croatia amesema
itakuwa nafasi nzuri kwa Berko kuanza ili aweze kumuona.
Simba kesho inashuka dimbani kuivaa KMKM
katika mechi yake ya pili ya Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza akiwa katika kambi ya Simba
mjini Zanzibar, Logarusic alisema Berko na wachezaji wengine ambao hawakupata
nafasi ya kucheza wataipata.
“Pia Humud, nitataka kumuona na ndiyo
maana naitumia michuano hii kwa ajili ya kutengeneza timu.
“Hivyo nitajitahidi kuendelea kutoa nafasi kwa karibu kila mmoja ambaye ninaamini anastahili,” alisema.
IVO ASEMA ANAFURAHIA MAISHA SIMBA SC…NI KAMA ALIKUWEPO KITAMBO SANA
IVO ASEMA ANAFURAHIA MAISHA SIMBA SC…NI KAMA ALIKUWEPO KITAMBO SANA
Na Mahmoud Zubeiry, ZanzibarKIPA namba moja wa Simba SC, Ivo Mapunda amesema kwamba anafurahia maisha katika klabu hiyo na anatamani kuisaidia ishinde mataji zaidi, baada ya mwishoni mwa mwaka kuipa taji la kwanza, Nani Jembe.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY mjini hapa, Ivo alisema kwamba anafurahi namna anavyokubalika na kuheshimika kuanzia na benchi la Ufundi, wachezaji wenzake, viongozi na hata wapenzi wa Simba SC.
Anafurahia maisha Msimbazi; Ivo Mapunda amesema anajisikia kama alikuwepo miaka kadhaa Msimbazi |
“Huu ni mwanzo mzuri kwangu, najisikia vizuri na ninafurahia kuwa hapa, lakini pia hii ni changamoto kwangu kuweza kuisaidia zaidi klabu hii, ili ishinde mataji zaidi. Kwa ushirikiano wa pamoja na wachezaji wenzangu, naamini tunaweza,”alisema Ivo.
Kipa huyo wa zamani wa mahasimu, Yanga SC amesema anajisikia kama alikuwepo katika klabu hiyo miaka kadhaa iliyopita, kutokana na namna ambavyo amezoea maisha mapya haraka Msimbazi.
Amesema kwamba ana matumaini makubwa watabeba Kombe la Mapinduzi, michuano inayoendelea visiwani humo hadi Januari 13, mwaka huu.
“Tunahitaji hata sare dhidi ya KMKM ili kufuzu Robo Fainali, hilo tunaweza tena kwa kuwafunga kabisa. Tukifika Robo naamini kwa uzoefu wetu tunaweza kucheza hadi fainali. Na tukifanikiwa kufika fainali tutapigana tushinde turejee na Kombe Dar es Salaam,”alisema.
Ivo ameidakia mechi zote mbili za michuano hiyo Simba SC dhidi ya AFC Leopard ya Kenya na KCC ya Uganda ikivuna pointi nne, bila nyavu zake kuguswa hata kwa bao la kuotea. Baada ya Simba SC kuifunga Leopard 1-0 na sare ya 0-0 na KCC, itashuka tena dimbani kesho Uwanja wa Amaan, kumenyana na KMKM Saa 2:00 Usiku katika mchezo wa mwisho wa Kundi B.
Tayari Ivo amekwishaidakia Simba SC mechi tatu tangu ajiunge nayo mwezi uliopita akitokea Gor Mahia ya Kenya, ikiwemo ya Nani Mtani Jembe Desemba 21, mwaka jana dhidi ya mahasimu, Yanga ambayo Wekundu wa Msimbazi walishinda 3-1.
RC ataka waandishi kuitangaza Tanga
RC ataka waandishi kuitangaza Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa
amewataka waandishi wa habari mkoani Tanga kuutangaza mkoa wao
kiutalii, pamoja na vivutio vyake na kuacha kuandika habari ambazo
hazina faida kwa jamii na Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
juzi wakati akielezea maendeleo ya Mkoa wa Tanga mwaka 2013/14, Gallawa
aliwataka waandishi wa mkoa huo kuitumia vyema kalamu yao kwa
kuvitangaza vivutio vilivyoko mkoani humo.
Alisema Mkoa wa Tanga una vivutio vingi vya
utalii, lakini vimekuwa havitambuliki ndani na nje ya nchi kutokana na
kutotangazwa katika vyombo vya habari na hivyo kuwa chanzo cha
maendeleo kudidimia na Serikali kukosa mapato.
“Nashangazwa kuona Tanga ina vivutio vingi vya
kiutali zikiwemo fukwe, mapango pamoja na mbuga ya wanyama, lakini sioni
watalii wa ndani wala wa nje wanaokuja---tuweni wazalendo tupate
maendeleo” alisema na kuongeza:
“Nadhani mko waandishi wa vyombo vyote hapa nchini
na natambua kuwa mko mahiri katika kuandika na msomaji kuvutika kwa
kile mnachokiandika,sasa kwanini hamuutangazi mkoa wenu kiutalii au
mmeghafirika,nawakumbusha” alisema Gallawa
Gallawa alisema Mkoa wa Tanga umejaliwa kuwa na
vivutio vingi vikiwemo mbuga ya wanyama ya Saadan, Mapango ya watu wa
kale yalioko Amboni pamoja na fukwe nzuri za bahari za Pangani.
Alisema endapo waandishi wa habari wataweza
kuzitumia vyema kalamu zao kwa kuutangaza mkoa huo kiutalii maisha ya
watu yataweza kubadilika ikiwa ni pamoja na biashara kuchangamka na
Serikali kuweza kupata mapato kutoka kwa wageni.
Akizungumzia matajiri kuzichangamkia fursa
zilizoko mkoani humo, Gallawa aliwataka kuwa wabunifu na kuweza kuweka
vitega uchumi na kuacha wageni kuwa waanzilishi na kuja kujutia baadae.
Alisema kuna fursa nyingi ambazo wenyeji wanaweza
kubuni na kuweza kupata vipaumbele katika sekta nzima ya uwekezaji
ikiwemo kujenga mahoteli pembezoni mwa bahari na usafirishaji wa
watalii kwa njia ya anga mbugani.
Aliwataka watu hao wenye uwezo kuwa wabunifu wa
miradi mbalimbali kwani jambo ambalo litaweza kuisaidia Serikali katika
suala zima la maendeleo na kiuchumi
Kijiji cha Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga chapewa cheti cha ardhi yao
Kijiji cha Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga chapewa cheti cha ardhi yao
MATUKIO KATIKA PICHA YA FAINALI YA MASHINDANO YA KOMBE LA MWIDAU CUP
MATUKIO KATIKA PICHA YA FAINALI YA MASHINDANO YA KOMBE LA MWIDAU CUP
Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi
Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa
mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani jana
|
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akihutubia kabla ya kuchezwa kwa fainali kati ya timu ya APL Mwera na Torino (kulia) ni Katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Salehe Swazi.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya Mwidau CUP, Amina Mwidau
akijadiliana na viongozi wenzake wakati wa mchezo wa fainali ya Mwidau CUP kati
ya APL Mwera dhidi ya Torino leo mjini hapa.
PATO LA MKOA WA TANGA LAONGEZEKA TOKA TRILIONI 1.78 HADI TRILIONI 2.009
PATO LA MKOA WA TANGA LAONGEZEKA TOKA TRILIONI 1.78 HADI TRILIONI 2.009
Na Oscar Assenga
Pato
la Mkoa wa Tanga limeongezeka kutoka trilioni 1.78 hadi kufikia
trilioni 2.099 kwa mwaka 2012 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia
17.8.
Taarifa
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapa desemba
30 mwaka huu kuhusiana na mafanikio ya Mkoa wa Tanga ya mwaka 2012 hadi
2013.
Gallawa
amesema katika ongezeko hilo Mkoa umechangia wastani wa asilimia 4.69
ya pato la Taifa ambalo ni Trilioni 44.7 kwa mwaka 2012 kulinganisha na
37.5 Trilioni kwa mwaka 2011.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema pia pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka
wastani wa shilingi laki 8,86,343 mwaka 2011 hadi shilingi 1,26,432 kwa
mwaka 2012 ambapo wastani wa kitaifa ni shilingi 1,025,038 kiasi ambacho
Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya nane kati ya mikoa 25 ya Tanzania bara
tangu mwaka 2010.
Aidha
katika utekelezaji wa malengo ya kukuza uchumi Mkoa wa Tanga umeandaa
mkakati wa kutekeleza miradi kwa kutumia mfumo wa tekeleza sasa kwa
matokeo makubwa kwa miaka 2013 hadi 2015.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Mkoa ameainisha vipaumbele katika maeneo ya kukuza
mapato kwa mtu mmoja mmoja kufikia wastani 1.5, kuendeleza huduma za
jamii za elimu
kwa kuongeza ufaulu kutoka asilimia 32 hadi 60 msingi na sekondari na
maji kufikia asilimia 50 ifikapo 2015 kwa kutoa huduma za maji kwa
umbali usiozidi mita 400 kutoka eneo la makazi.
MADIWANI BUMBULI WAPEWA SOMO.
MADIWANI BUMBULI WAPEWA SOMO.
(Katibu wa January Makamba(Hoza Mandia ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Milingano)
Na Raisa Said, Bumbuli
MADIWANI
wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto wametakiwa kusimamia ipasavyo
maazimio na mikakati wanayopitisha katika vikao vyao ili kuwaletea
maendeleo wananchi wa Jimbo hilo.
Ushauri huo
umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Bumbuli, January Makamba
akizungumza katika mahojiano na waandishi wa Habari hivi karibuni kufuatia
kikao maalumu cha wajumbe wa Kamati ya Madiwani wa CCM kilichoitishwa kwa niaba
yake na Katibu wake Hoza Mandia.
Mbunge huyo
amesisitiza kuwa madiwani wanapaswa kusimamia maazimio waaliyoyapitisha katika
kikao hicho ili kuiharakisha maendeleo kwa wananchi wa eneo hilo ambalo limebahatika kuwa Halmashauri
kamili.
Katika maazimio
hayo madiwani walimshauri Mbunge ajipangie utaratibu wa kuwasIliana kwa simu na
madiwani angalau kila baada ya wiki au kadri atakavyoona inafaa zaidi ili
kupata taarifa na kujua changamoto gani zilizopo katika jimbo hilo.
Pia waliazimia
kuwa kero zote za wananchi zinazohusui miradi ya maendeleo ziwasiklishwe kwa
kupitia vikao husijka na madwani wahusike kumuona mkurugenzi ili kupata majibu
ya ufumbuzi wa kero hizo
Kikao hicho pia
kiliazimia kuwa kila diwani awe amekamilisha na kuwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye vikao husika ndani ya mwezi mmoja na
nakala ya taarifa hiyo iliyopitishwa iwasilishwe kwa katibu wa CCM wilaya na
kwa mbunge.
Mbunge huyo
alisisitiza kuwa hayo yote yaliyoazimiwa yasimamiwe kwa faida ya wananchi na
Chama cha mapinduzi.