Featured Post Today
print this page
Latest Post

KOCHA ALIYEMUIBUA VAN NISTERLOOY AJA KESHO KUFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA

KOCHA ALIYEMUIBUA VAN NISTERLOOY AJA KESHO KUFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA

Atakuwa kocha mpya wa Yanga? Hans van der Pluijm anatarajiwa kutua kesho kwa mazungumzo

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga SC imemualika kwa mazungumzo, kocha ‘babu’, Johannes Franciscus ‘Hans’ van der Pluijm, aliyewahi kuifundisha Berekum Chelsea ya Ghana, ambaye anaweza kutua Dar es Salaam kesho iwapo atafanikiwa kupata ndege.

 
Hakuna nafasi katika ndege za kutoka Ghana kuja Dar es Salaam na babu huyo anahaha kutafuta ndege ya kuunganisha na kama akifanikiwa basi atakuja nchini kesho, ikishindana wakati wowote mapema wiki ijayo.


Pluijm anakuja kufanya mazungumzo na Yanga, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuridhishwa na wasifu wake katika orodha ndefu ya walimu zaidi ya 30 walioomba kazi Jangwani.
 
Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.
Enzi zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338 ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa timu hiyo.

 
Alianza vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Van Nisterlooy aliibuliwa na van der Pluijm

Aprili mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake, John Metgod. 
 
Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.
Baada ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja. 

 
Ajax ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka 1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-juniors Feyenoord ya Ghana, ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.

 
Mwaka 2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka jana na kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzo mwa msimu, akivuna pointi nane kati ya 21.

 
Je, mwalimu huyu ataisaida Yanga SC, au imeuvagaa mkenge mwingine baada ya kumtema Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts mwezi uliopita?

0 comments

Ariel Sharon afariki dunia.

Ariel Sharon afariki dunia.

Aliyekuwa waziri Mkuu wa Israel, Ariel Sharon amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Alikuwa katika hali ya umahututi kwa miaka nane tangu mwaka 2006. Chanzo:BBC 
0 comments

MCHUNGAJI GWAJIMA AVAMIWA NA MAJAMBZI USIKU NA KUNUSURIKA KUUAWA MARA TATU

MCHUNGAJI GWAJIMA AVAMIWA NA MAJAMBZI USIKU NA KUNUSURIKA KUUAWA MARA TATU

ILITOKEA lakini haikuandikwa kwa sababu haikudakwa! Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makazi yake kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkas, Kawe jijini Dar, Josephat Gwajima alinusurika kuuawa mara tatu kufuatia kuvamiwa na majambazi watatu mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, Gwajima alisema tukio hilo lilijiri nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar ambapo siku ya kwanza, majambazi hao waliingia nyumbani kwake saa nne usiku wakiwa wameficha sura na kumkuta yeye sebuleni ambapo walimuuliza, ‘Gwajima yuko wapi?’


“Ni kweli nilinusurika kifo na majambazi, walinivamia mara tatu nyumbani. Zilikuwa siku mbaya maishani mwangu. Siku ya kwanza walikuja na bunduki huku wameficha sura, walinikuta sebuleni, wakaniuliza alipo Gwajima, niliwajibu ametoka, wakaondoka wakisema watarudi kesho yake.


“Nilijua ni utani, lakini kweli siku iliyofuata saa nne usiku walikuja tena, wakanikuta ndiyo naingia nyumbani, wakaniambia niko chini ya ulinzi, nilimuomba Mungu aokoe maisha yangu kwani nilipatwa na mshtuko, wakahoji; ‘Gwajuma yuko wapi?’ Kabla sijajibu mmoja akasema; ‘huyu bwana mdogo ndiye tuliyemkuta jana,’ wakaondoka.


“Sikuwa na wazo la kuripoti polisi ila nilimwamini Mungu aliye hai. Siku ya tatu walipitia juu ya paa kwa kung’oa vigae na kushukia chumbani wakiwa na bunduki.


“Mimi nilikuwa kitandani na mke wangu, wakauliza tena Gwajima yuko wapi? Nikawajibu bado hajarudi, wakasema; ‘haka (Gwajima) ndiyo kale kale ka bwana mdogo ka jana.’


“Mungu mkubwa, kwa nje zilisikika kelele za mbwa kisha wakatoweka ghafla, niliona ni siku za majaribu kwangu, nilimwomba Mungu atupilie mbali majaribu yale, baada ya siku kadhaa niliamua kuhama kwenye nyumba ile.


“Ila nakumbuka ile siku ya mwisho walisema tunamtaka Gwajima kwa sababu anajifanya kufufua misukule kisha anataja majina yetu.
“Ndipo nilijua kumbe kisa ni kufufua misukule. Najua umbo langu ndiyo mkombozi wa yote kwani waliponiona walijua Gwajima hawezi kuwa na umbo dogo kama mimi nilivyo,” alisema Gwajima.
Katika mahojiano marefu na gazeti hili, mchungaji huyo alisema kuwa mpango wa kumuua uliofanywa na mtu ambaye aliwahi kutajwa jina na binti msukule aliyemfufua kanisani kwake. Alisema mtu huyo aliyetajwa na msukule ni  mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (jina hakumtaja).


0 comments

MOTO WAMWAKIA PROFESA TIBAIJUKA NI BAADA YA KUZOMEWA NA WANANCHI.

MOTO WAMWAKIA PROFESA TIBAIJUKA NI BAADA YA KUZOMEWA NA WANANCHI.


Viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati wa masuala ya ardhi, wamesema kuzomewa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ni matokeo ya makosa
yanayowafanywa na Serikali kuwapendelea wawekezaji wa nje na kuwapuuza wananchi.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Profesa Tibaijuka kuzomewa na wananchi waliokerwa na kitendo cha kumruhusu mwekezaji kuendelea kumiliki shamba la Kapunga, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya lenye ukubwa wa hekta 7,370.

Wananchi hao walikasirishwa na kitendo cha Profesa Tibaijuka kubadili msimamo wake awali wa kumpokonya ardhi mwekezaji huyo kwani mara ya kwanza alishawaeleza viongozi wa vijiji kuwa serikali itawarudishia eneo lao.

Mwekezaji huyo alitakiwa kumiliki ekari 5,500 lakini serikali ilimmilikisha ekari nyingine 1,870 ambazo ni mashamba ya wanakijiji.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Ardhi, Yefuz Myenzi alisema hayo ni makosa ya serikali kuwapa ardhi wawekezaji wa nje bila kutenga ardhi ya wanavijiji.

“Serikali inabinafsisha hadi vijiji ambako wananchi wangeweza kulima na kuendesha maisha yao, unategemea nini wakimwona kiongozi wa serikali ni lazima watamzomea,” alisema Mnyezi.

Alisema ubinafsishaji wa ardhi unafanywa na ngazi za juu za taifa bila kuushirikisha uongozi wa ngazi za vijiji hali inayosababisha vurugu katika maeneo mengine.

“SiYo katika Shamba la Kapunga tu, kuna maeneo mengi ambako wawekezaji wa kigeni wamepewa ardhi lakini wao wanaikodisha kwa wananchi kitendo ambacho ni kosa,” alisema.

Myenzi alisema katika maeneo yenye matatizo kama hayo, Rais anatakiwa kutumia madaraka yake kwa kubadilisha matumizi ya ardhi ili wananchi waweze kupewa kwa ajili ya kilimo.

Viongozi wengine

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema viongozi wa Serikali wanawapendelea wawekezaji wa nje na kuwapuuza wanavijiji.

“Migogoro hii ya ardhi inavyochukiza watu kama kiongozi utakwenda kusuluhisha na kutoa majibu yasiyowaridhisha wananchi, basi viongozi wataendelea kuzomewa kama Waziri huyo,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema wananchi wanakatishwa tamaa na viongozi wa serikali kuwapendelea wawekezaji.

“Ajira pekee inayotegemewa vijijini ni kilimo, serikali inabinafsisha hadi mashamba ya wanavijiji, wamekata tamaa ndiyo maana wanazomea ovyo. Viongozi hawana nia ya dhati kutatua migogoro iliyopo,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa NCCR -Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema ili kuondokana na migogoro, wawekezaji wanatakiwa kuwa na vibali vya ardhi kutoka katika uongozi wa kijiji.

“Wanakijiji ndiyo wenye ardhi, migogoro ya namna hii isingetokea kama wangeshiriki kutoa vibali kwa wawekezaji,” alisema.

DC amtetea Tibaijuka

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Gulam Hussein Kifu amesema pamoja na kwamba wananchi wa kijiji cha Kapunga wanataka mgogoro huo umalizike haraka, lakini anaamini uamuzi wa Profesa Tibaijuka kufanya mazungumzo na mwekezaji wanayevutana naye utaleta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Profesa Tibaijuka alisema majuzi kuwa Kampuni ya Kapunga Rice Project inamiliki kihalali mashamba kwenye eneo hilo na kudai kuwa serikali ndiyo yenye makosa kwenye mgogoro huo.

Mashamba hayo mara ya kwanza yalikuwa yanamilikiwa na Kampuni ya Taifa ya Kilimo (Nafco) lakini yalibinafsishwa na kuchukulikuwa na mwekezaji huyo.

Kifu alisema pamoja na kwamba wananchi wengine hawakuridhika na uamuzi wa Waziri lakini anaamini kuwa Profesa Tibaijuka ndiyo yuko sahihi kuzungumza na wawekezaji ili waliachie eneo hilo kwani hawan.


0 comments

Hii ni kutoka Kenya jamaa amefufuka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Hii ni kutoka Kenya jamaa amefufuka akiwa chumba cha kuhifadhia mait

0 comments

UVUNAJI WA MAZAO YA BAHARI UMEPUNGUA KUTOKA TANI 481 HADI TANI 316 MKOANI TANGA

UVUNAJI WA MAZAO YA BAHARI UMEPUNGUA KUTOKA TANI 481 HADI TANI 316 MKOANI TANGA

 Tanga.
HALI ya uvunaji wa  mazao ya baharini katika mkoa wa Tanga imepungua kutoka tani 481 zilizopatikana mwaka 2011/2012 zenye thamani ya fedha za kitanzania 4,821,440,915.15 zilizosafirishwa nje ya nchini hadi kufikia tani 316 kwa mwaka 2012/2013 ambapo upungufu huo wa tani 165.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa wakati akizungumza na TANGA RAHA BLOG ambapo alisema upungufu huo umesababishwa na hali ya soko la mazao kama Pweza kwa nchi Ulaya kupungua.

Gallawa alisema sekta ya uvuvi mkoani Tanga imeendelea kutunza mazingira ya uzalishaji wa mazao ya majini kwa kudhiti uvuvi haramu  ambapo mwaka 2011-2012 jumla ya doria 120 zilifanyika na  kufanikiwa kuwakamata wahalifu 20 na kuwafikisha mahakamani.
Licha ya kuwakamata watuhumiwa hao pia walikamata vyombo vya baruti 6  na baruti 10 na bunduki 5 za kuvulia zilikamatwa,Samaki wa baruti kilo 240 walikamatwa na kutekelezwa na makokoro  ikiwemo juya 60 ambavyo vilikuwa vikitumika kwenye uvuvi haramu.
Aidha alisema jumla ya kesi 22 zilifuatiliwa mahakamani ambapo kesi CC 06/2009 inayohusu mtu mmoja kwa kosa la kupatikana na samaki wa baruti ilitolewa hukumu ya kifungo cha miezi mitatu jela na kesi CC 363/09 inayohusu mtu mmoja kupatikana na samaki w baruti iliyotolewa hukumu ya kumuachia huru mshtakiwa  wakati kesi nyengine zilikuwa zikiendelea.
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka 2012-2013 Jumla ya doria 44 zilifanyika na kesi 10 zilifuatiliwa mahakamani ambapo jumla ya vyombo vya baruti 20 vilikamatwa pamoja na sanmaki wa baruti 160 walikamatwa.
Aliongeza kuwa pia magari 20 yanayosafirisha mazao ya samaki kwenda mikoa mbalimbali yalikaguliwa ambapo kwenye mwaka huu mikuki,mishale ya kuchomea samaki 20 ilikamatwa ikiwemo makokoro na juya 5 zilikamatwa.
0 comments

WAGOSI WA KAYA WAANZA RASMI KAMBI YA MAZOEZI OMANI

WAGOSI WA KAYA WAANZA RASMI KAMBI YA MAZOEZI OMANI 






















TIMU ya Coastal Union jana iliwasili jijini Muscat Oman usiku saa sita na kufikia katika hoteli ya City Centre.
Kaimu balozi wa Tanzania nchini Oman, ndie alietupokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mascut na kutuelekeza vema kuhusu masual mazima ya mji huo.
Nae mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Talib Hilal alikuja hotelini na kuzungumza nasi juu ya masuala mazima ya soka nchini hapa.
Talib, ndie mwenyeji wetu ambae anaratibu kila tukio tutakalofanya kuhusu mechi na mazoezi ya timu. Vilevile atahakikisha maisha yetu mjini Mascut yanakuwa rahisi kwa kusimamia masuala ya usafiri na mambo yote muhimu.
Kesho saa tisa alasiri timu itashuka dimbani katika uwanja wa Musanaa ambapo tutacheza mechi ya kirafiki na timu ya Musanaa ambayo ipo ‘top four’ ya ligi kuu ya Oman.
Aidha zipo taarifa zilizotolewa na moja ya gazeti la udaku juu ya hali mbaya ya maisha kwa timu ya Coastal Union, nchini Oman. Lakini nadhani picha zinazungumza maneno mengi kuliko maandishi. Hivyo kwa nafasi ya usemaji nahakikisha kuwa vijana wapo katika hali nzuri na hakuna matatizo yoyote.
Kwa mujibu wa mkuu wa msafara ambae pia ni mwenyekiti wa Wagosi, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu itacheza mechi nne za majaribio kabla ya kurudi Tanzania baada ya wiki mbili.
Taarifa nyingine zitaendelea kutolewa kupitia vyanzo vyote vya Coastal Union……
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
10 JANUARI, 2014
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger