Featured Post Today
print this page
Latest Post

SIMBA YAVAMIA TANGA KWA HASIRA, COASTAL UNION YAWATULIZA

SIMBA YAVAMIA TANGA KWA HASIRA, COASTAL UNION YAWATULIZA


                                                                                                             
BAADA ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Yanga, kikosi cha Simba kesho jioni kitashuka katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuvaana na Coastal Union ya mjini humo.
Kikosi cha Simba kiliwasili Tanga jana mchana tayari kwa mchezo huo utakaochezwa kesho saa 10:00 jioni na tayari shamrashamra zimeshaanza kutawala jiji la Tanga.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekile Kamwaga ameuambia mtandao huu kwamba, kikosi cha Simba kiliwasili salama jana jijini Tanga tayari kwa mchezo huo wa kesho na wachezaji Hnery Joseph, Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud hawapo katika kikosi hicho.
“Timu imefika salama Tanga tangu jana mchana na hali ya kikosi kizima ni nzuri kinachosubiriwa sasa ni muda kufika ili tuweze kutazama pambano hili safi na la kuvutia kwetu sote, kwani Coastal ni timu nzuri ambayo ina wachezaji kadhaa ambao wamewahi kuwika na klabu mbalimbali za hapa nchini.
“Sisi kama Simba tunaamini tuna timu nzuri ambayo inaweza kupambana na timu yoyote na kutwaa ubingwa hivyo wakazi wa Tanga na miji ya jirani wajitokeze kwa wingi uwanjani kutazama pambano hili la kuvutia,” anasema Kamwaga.
Naye Mwenyekiti wa Coastal, Ahmed Aurora amesema kikosi cha timu yake kimejiandaa vya kutosha na hakuna tatizo lolote linaloikabiri timu yake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba.
“Sisi tupo vizuri kabisa tunaisubiri Simba kwa hamu kubwa kuweza kupambna nao kwani tumejiandaa vizuri chini ya kocha wetu Joseph Lazaro ambaye amejiunga nasi hivi karibuni akichukua nafasi ya Ahmed Morocco.
“Tuna wachezaji wengi wazuri ambao wamewahi kutamba na timu kubwa za Simba, Yanga na Azam, tunachohitaji sisi ni kufanya vizuri kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” anasema Aurora.
Wachezaji wa Simba waliowahi kuichezea Simba ni Haruna Moshi ‘Boban’, Juma Nyosso, Jerry Santo na Pius Kisambale ambaye pia amewahi kuichezea Yanga. Wachezaji wa Yanga waliowahi kuichezea Yanga ni Razack Khalfan, Atupele Green, Shaaban Kado na Kisambale.
0 comments

KAMISHNA MSAIDIZI MWANAMIZI (SACP) MSTAAFU JAMES KOMBE AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA OCEAN ROAD JIJINI DAR ES SALAAM.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0NccD_ggbBJh3LuWDtAVeTHmWGvcYMBj_Fxu9RIGnQ-wFweM8fdO52IMlBoS4MjArBtCxY1KhkTQri57QNyaNli9g-zviRoH_domj2S4XaWhLXBnzDDg1KU6qDE8C7mi5ZB726TfTvQ4s/s400/POLISI-762018.jpg 
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
ALIYEKUWA kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu James Kombe amef
ariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kifo hicho Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Advera Senso alisema, Kombe alifariki Oktoba 22 mwaka huu na taratibu za mazishi zinaendelea.

Aidha Senso alisema Marehemu Kombe alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani Kilimanjaro na alijiunga na Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka 1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda ambapo alipandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.

Baadhi ya vyeo alivyopitia na miaka ya kupata vyeo hivyo katika mabano ni pamoja na Sagenti wa Polisi (1973) Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1977), Mkaguzi wa Polisi (1984), Mrakibu Msaidizi (1986), Mrakibu wa Polisi(1991), Mrakibu Mwandamizi (1995), Kamishna Msaidizi wa Polisi (1998) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu mwaka 2010.

Baadhi ya nafasi alizowahi kuzitumikia katika Jeshi la Polisi ni pamoja na kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika wilaya za Dodoma, Tarime, Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC) katika mikoa ya Lindi, Arusha, Kigoma pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza ghasia Tanzania na hadi anastaafu alikuwa mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania.
0 comments

TASWIRA YA WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AENDELEA NA ZIARA YAKE MJINI CHENGDU CHINA.


Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Hinan Intternational Limited waliojipenga kuwekeza katika uboreshaji wa uzalishaji wa zao la pamba katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu jijini Chendu akiwa katika ziara ya nchini China Oktoba 22, 2013. Wann kusoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Nasoro Rufanga na watano kushoto ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.

Waziri mkuu, Mizengo Pida na Mkewe Tunu wakitembelea Kituo Cha Utafiti wa wanyama aina ya Panda nje kitogo ya jiji la Chendu nchini China Oktoba 22, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bio Energy Ya Berlin, Alexander Boiton baada ya mazungumzo yao mjini Chengdu akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 22, 2013. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chengdu De Tong Environmental Engineering Co Limited , Tong Boitin ba watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Katani Limited, Salum Shamte.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments

DUNIANI KUNA MAMBO,TAMBUA MAMBO MANNE AMBAYOHUKUFAHAMU HAPO KABLA!!

DUNIANI KUNA MAMBO,TAMBUA MAMBO MANNE AMBAYOHUKUFAHAMU HAPO KABLA!!

students1.Utafiti uliofanywa barani ulaya umegundua kuwa wanafunzi ambao ni mashabiki wa mchezo wa soka hufanya vibaya kwenye mitihani yao wakati timu zao zinapofanya vizuri yaani timu inaposhinda takwimu za matokeo ya mitihani huwa chini.

2.Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na The Happy Planet Index nchi inayoongoza kwa furaha duniani ni Costa Rica,marekani inashika nafasi ya 105 kwenye orodha ya nchi zenye furaha duniani.
San Jose Costa rica
San Jose Costa Rica
3.Kuna kitabu kimoja ambacho kinaitwa “what every man thinks about apart from sex” yaani “kitu ambacho wanaume wanafikiria tofauti na ngono”. kitabu hiki kimewahi kuweka rekodi ya mauzo ya juu , cha kushangaza kuhusu kitabu hiki ni kwamba kina kurasa 200 ambazo hazijaandikwa kitu chochote ndani yake.
KITABU4.Nchi ya marekani ni nchi ambayo inaongoza kwa kuwa na sheria za ajabu , mojawapo ya sheria hizo ni sheria iliyowekwa na serikali ya jimbo la North Carolina ambayo inasema kuwa ni hatia kuimba off key yaani ukiimba nje ya zile key za muziki basi umefanya hatia na unaweza kutozwa faini au kutumikia kifungo gerezani.
0 comments

PUMZIKA KWA AMANI MTANGAZAJI MAHIRI JULIUS NYAISANGA

PUMZIKA KWA AMANI MTANGAZAJI MAHIRI JULIUS NYAISANGA

Julius Nyaisanga 1R.I.P kwa Mtangazaji legend ambae atakumbukwa na Watanzania wengi nikiwemo Mimi D'JARO ARUNGU, ni legend ambae upekee wa sauti yake pamoja na ubunifu wa vipindi alivyoviendesha  vilimpa heshima na jina lake kukua kila siku kutokana na kumbukumbu aliyokua anaicha kwa watu kila anaposikika.

Julius Nyaisanga ambae alifariki dunia October 20 2013 hospitalini Morogoro kutokana na maradhi ya Presha na kisukari, ameagwa Dar es salaam October 22 2013 na kusafirishwa kwenda kuzikwa kwao Mara.
Mpaka anafariki, Nyaisanga ambae amewahi kufanya kazi na vituo vikubwa kama TBC Zamani Radio Tanzania na ITV/Radio One alifariki akiwa na umri wa miaka 53 ambapo ofisi yake ya mwisho kuifanyia kazi ilikua Abood TV/Radio Morogoro.
Julius Nyaisanga
Julius Nyaisanga 6
Julius Nyaisanga 2
Julius Nyaisanga 3
Julius Nyaisanga 8
Julius Nyaisanga 5
Julius Nyaisanga 9
Julius Nyaisanga 10
Julius Nyaisanga 4
Mke wa Marehemu
Mke wa Marehemu
0 comments

KANIPA DEADLINE EITHER NIKAJITAMBULISHE KWAO AMA TUACHANE KIMOJA..HELP

KANIPA DEADLINE EITHER NIKAJITAMBULISHE KWAO AMA TUACHANE KIMOJA..HELP

Nimekuwa kwenye uhusiano na mpenzi wa roho yangu kwa takriban miaka mitatu.
Kwa kipindi chote hicho tumekuwa tukiishi mikoa tofauti. Yeye anafanya kazi Babati na mimi nafanya kazi Dodoma.
Licha ya umbali uliopo tumeishi kwa upendo na kuaminiana na hata ndugu na wazazi wanajua kuhusu uhusiano wetu tukitarajia kuja kufunga ndoa baadae. 
Siku za karibuni amekuwa akisisitiza sana nikatoe mahali kwao nami nikawa namuambia sawa tutafanya hivyo na nimemueleza sababu ya kuchelewa ni matatizo ya kifamilia yanayonikabili.
Ghafla wiki iliyopita alikata mawasiliano na hataki pokea simu yangu wala kujibu sms.
jana nimekaa nawaza akanitumia sms kuwa nadhani nishaamua kama namhitaji niende kwao Marangu kabla ya tar 25 mwezi huu vinginevyo simuhitaji.

Kweli nimeishiwa nguvu kwa kuwa sidhani kama kwenda kwao kwa kuforce kwa deadline ni vyema. Anajua kuwa nampenda sana lakini sasa hakuna my love wala sweet.. Ni mwendo wa hey na hello yan full ubabe. Nishaurini wakuu maana natarajia kwenda lakini kwa sasa sijajipanga kusema kweli.


Udaku Specially Blog
0 comments

PICHA ZA WATUHUMIWA 13 WALIOKUTWA WAKIFANYA MAZOEZI YA AL-SHABAAB NA AL-QAEDA

PICHA ZA WATUHUMIWA 13 WALIOKUTWA WAKIFANYA MAZOEZI YA AL-SHABAAB NA AL-QAEDA



Hawa  ni  vijana  wa  kitanzania 13  ambao  walikamatwa  na  jeshi la polisi   Mtwara baada ya  kupata taarifa kwamba  walikua wakifanya mazoezi ya kivita kwa kutumia CD za  Al Qaeda na Al Shabaab ambapo walikamatwa na hizo CD  pamoja  na  silaha   mbalimbali  kama  ushahidi...


 Taarifa ya jeshi la Polisi leo  imesema kuwa , vijana  hawa walipelekwa Mahakamani na watarudishwa tena tarehe 4 November 2013.

Udaku Specially Blog
0 comments

WANAWAKE WENGI HUPENDA WANAUME WAPOLE KWA SABABU HII

WANAWAKE WENGI HUPENDA WANAUME WAPOLE KWA SABABU HII

Ukimuuliza binti yeyote mwenye ndoto ya kuolewa,,akutajie sifa za mume ampendae,sifa ya "awe mpole" itakuwa ktk orodha ya mwanzo kabisa.Ktk utafiti binafsi sifa hii imetajwa na wasichana 74 ikiwa ya kwanza,,wasichana 113 ikiwa ya 2.Lakini kwa wanawake walio ktk ndoa,,wanawake 20 walisema wanapenda mume mpole ikiwa sifa ya 1 na 42 waliobaki waliitaja ikiwa ya 2
Huo ni utafiti binafsi ambao ulitaka kujua tu UPOLE WA MWANAUME una nafasi gani kwa mwanamke

Lakini kwa nini wanawake au mabinti hupenda mwanaume mpole? Kwa nini mkorofi hatajwi kabisa? Je ni kweli ni watu wanaohitaji huruma kiasi hicho? Mtaalamu wa masuala wa mahusiano wa kimarekani Baruck Miller aliyetafiti mahusiano kwa miaka zaidi ya 20,,anasema "... Mwanamke anampenda mwanaume mpole ili AJITAWALE KTK MAHUSIANO..."
Siku zote,mwanamke anapenda awe huru kwenda apendapo au kupewa atakacho.Hivyo anapokuwa mbele ya mwanaume mpole hana wasi,,wala hana tabu ya kutimiziwa shida yake.Akikutana na mwanaume mpole sana kiasi cha kukaribia ujinga basi atamuendesha mume/mpenzi kama rimoti control.

Jambo wanalosahau wanawake ni kuwa,,upole wa wanaume wengi wanautafsiri kama ujinga,uzezeta au kuliona kundi hili la kuchuna wapendavyo.
Laiti wangekumbuka kuwa mwanaume mpole ni kama volcano tuli,,ikilipuka imelipuka basi sifa ya upole ingekuwa ya mwisho.

Udaku Specially Blog
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger