SEMINA YA TARUJA YAANZA PANGANI LEO.
WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO
Wanahabari wametakiwa kutumia kalamu zao katika kuhakikisha
jamii zinazoishi kandokando kuzunguka hifadhi za Taifa zinakuwa na ushirikiano
katika maswala mazima ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kuweza kuwa na
hifadhi endelevu.
Hayo yalielezwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan
Kijazi wakati akifungua mafunzo ya siku sita ya uandishi wa habari za hifadhi
na utunzaji wa mazingira kwa waandishi
wa habari za vijijin na mazingira TARUJA, inayofanyika wilayan Pangani Mkoani
Tanga.
Alisema TANAPA inatambua umuhimu wa vyombo vya habari na
kwamba shirika limekuwa likitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari ili
kuweza kuhakikisha waandishi wanaandika habari zinazohusu uhifadhi kwa weredi.
‘’Natambua umuhimu wa vyombo vya habari hivyo ndio maana tunashirikiana navyo kwa
ukaribu zaidi wani jamii inapata taarifa kupitia kalamu zenu ,ni vema mkatambua
sera na sheria ili muweze ktusaidia hata kutatua migogoro kwa kutumia kalamu
zenu”alisema Kijazi.
Alisema ushirikiano ni muhimu ili kuhakikisha hamasa
inajengeka katika jamii inaona umuhimu wa kuhifadhi mazingira na maswala ya
uhifadhi na kwamba kwa kufanya hivyo nchi itakuwa na hifadhi endelevu kwa
kizazi cha sasa na baadae.
Kijazi alizungumzia changamoto zinazoikabili shirika hilo
kuwa ni ujangili uliokithiri pamoa na kuvamiwa kwa mapito ya wanyama ambo
ambalo linaleta migogoro isiokuwa na tia baina ya jamii na shirikka.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
TAJURA George Semboni alisema kufuatia changamoto za kimazingira na uhifadhi
katika hifadhi za Taifa ndizo
zilizopelekea wanahabari kuona umuhimu wa kuomba mafunzo ili kutumia taaluma ya
uandishi kutoa elimu kwa amii kuhusu maswala ya uhidhi.
‘’Hata sisi waandishi sio wote
tunaoelewa faida zitokanazo na uwepo wa mbuga ndio maana mambo yanayorushwa
hewani ni malalamiko ya wananchi dhidi ya watendaji wanaofanya kazi katika
maeneo ya uhifadhi ambao wanatimiza wajibu wao kisheria’’alisema Sembon.
Mafunzo hayo ya siku sita
yanashirikisha waandishi wa habari ,viongozi wa chama na serikali pamoja na
wanchi wanaoshi kando ya hifadhi ya taifa ya Saadani yanatariwa kufungwa
mwishoni mwa wiki hii.