Latest Post
WAKALI WAPYA WA SIMBA SC, KAZE NA TAMBWE WAIFUATA TIMU KAHAMA TAYARI KWA MCHEZO WA KWANZA WA LIGI KUU DHIDI YA RHINO
WAKALI WAPYA WA SIMBA SC, KAZE NA TAMBWE WAIFUATA TIMU KAHAMA TAYARI KWA MCHEZO WA KWANZA WA LIGI KUU DHIDI YA RHINO
Wakali wawili; Kaze Gilbert kulia akipata chakula cha mchana na Tambwe Amisi, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Na
wachezaji hao waliochelewa kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana,
wataungana na kikosi cha Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’
tayari kuanza kazi Msimbazi.
Wawili
hao ndio pekee waliokuwa wanasubiriwa kukamilisha kikosi kizima cha
Wekundu wa Msimbazi, tayari kwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Wote
wamesajiliwa kutoka Vital’O ya Burundi, mabingwa wapya wa Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame katika michuano iliyofanyika
Sudan mwaka huu.
Tambwe
aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo ambayo timu za Tanzania,
Simba SC na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC zilijitoa kwa kuhofia
machafuko yaliyokuwa yakiendelea nchini humo.
Kaze
aliibuka beki bora wa mashindano hayo, yaliyoshuhudia Vital’O ikitwaa
taji lake la kwanza kabisa la michuano hiyo, licha ya kwamba ni timu
kongwe kwenye mashindano hayo ya CECAFA.
Wawili
hao wanafikisha idadi ya wachezaji wanne wa kigeni wa Simba SC, kasoro
mmoja kufika kikomo kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, baada ya Waganda,
kipa Abbel Dhaira na beki Joseph Owino.
Simba
SC imepanga kukamilisha idadi ya wachezaji wa kigeni kwa kumsaini Moses
Oloya anayecheza Vietnam kwa sasa ambaye pia anawaniwa na mahasimu wao,
Yanga SC.
NYAMLANI, MALINZI WARUDISHA FOMU ZA KUOMBA URAIS TFF, NGOMA INOGILE KARUME MADEGA AWAVAA KARIA NA NASSIB
NYAMLANI, MALINZI WARUDISHA FOMU ZA KUOMBA URAIS TFF, NGOMA INOGILE KARUME MADEGA AWAVAA KARIA NA NASSIB
Walioomba
nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein
Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona,
Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha
Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon
Mbise na Omari Walii.
Ahmed
Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo,
Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David
Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe
Kiteve, James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William
Lugenge.
Athuman
Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein
Mwamba, Stewart Ernest Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange,
Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah
Mohamed.
Wengine
ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar
Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Jamal Malinzi amerudisha pia fomu za Urais
Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee.
Kwa
upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu;
Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).
Amejitosa; Imani Madega atachuana na Ramadhan Nassib na Wallace Karia katika nafasi ya Makamu wa Rais TFF
Walioomba
nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael
Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas
Masui Magunguma.
MUME WA MTU AFUMANIWA GEST AKIWA NA BINTI YAKE ANAYEMLEA.
MUME WA MTU AFUMANIWA GEST AKIWA NA BINTI YAKE ANAYEMLEA.
Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar ambaye ni dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na binti yao wanayemlea.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00 jioni ambapo Temba ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kimara na Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.
Baada ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri aliitaarifu wanahabari ambapo alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
Kwa mujibu wa mke wa Temba, siku kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa mawasiliano ya kimapenzi kati ya mumewe na binti yao hivyo akalazimika kufanya uchunguzi wa kina.
Mama Temba alisema kuwa katika harakati zake, siku ya tukio alifuma ujumbe wa simu ‘SMS’ kwenye simu ya binti huyo, aliposoma alishtuka kuona ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa mumewe.
Kwa kuwa hakuamini alichokisoma, mama Temba ilibidi amwite binti yake ili amweleze vizuri juu ya ujumbe huo.
Alisema kuwa binti huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri chini ya miaka 18, hakuwa na hiyana alimweleza ukweli juu ya tabia ya baba yake huyo kumtaka kimapenzi.
Aliendelea kusema kuwa alipombana kujua kama ‘walishaduu’, binti huyo alidai kuwa amekuwa akimtolea nje.
Mama huyo alisema kuwa hakuwa na papara mara baada ya kuambiwa taarifa hizo, alichokifanya alimtaka binti yake huyo amkubalie na amwambie baba yake huyo wapange wakutane wapi.
Mama huyo alijifanya binti yake na kuanza kuchati na mumewe masuala ya mapenzi bila kufahamu kuwa anachati na mkewe.
Katika kuchati, Temba alituma SMS: “Tulia natafuta mtu wa kumwachia gari (daladala) halafu nitakutumia SMS kukuambia tukutane wapi, leo nataka nifungue ukurasa wa mapenzi na wewe, mwanangu nakuhakikishia utakuwa na maisha mazuri sana.”
Baada ya kukubaliana kukutana gesti hiyo, mama huyo alikwenda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Kimara-Rombo na kupanga jinsi ya kumnasa.
Majira ya saa 10: 00 jioni, Temba alipata mtu wa kumwachia daladala na kutinga katika gesti hiyo kisha kumtumia SMS binti huyo akimtaarifu ameshafika.
Tofauti na alivyotarajia, ujumbe huo ulitua kwa mkewe ambaye alimwambia binti huyo amfuate mara moja lakini ahakikishe ‘tunda’ halitafunwi.
Ilidaiwa kuwa binti alipofika chumbani alimkuta mtu mzima akiwa amevaa taulo tayari kwa kuvunja amri ya sita na binti yake huyo bila kujua kuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni kulikuwa na mkewe na polisi.
Ilisemekana waliachiwa kama dakika kumi na tano ndipo timu nzima ya polisi wakiongozwa na mkewe wakaingia ndani kwani hawakufunga mlango na ‘shughuli’ ilikuwa bado haijaanza.
Habari zilisema kuwa mwanaume alipomuona mkewe anaingia chumbani akiwa ameongozana na polisi nusura apasuke kwa mshtuko kwani alishindwa kuyaamini macho yake.
Ilielezwa kuwa mume alijaribu kutumia kila aina ya lugha kumuomba msamaha mkewe lakini mke aliamuru askari kumtaiti kwa kumpiga pingu na safari ya kwenda kituoni ikaanza.
Kabla ya kupelekwa kituoni jamaa huyo aliibua timbwili zito na kusababisha watu kukusanyika na kuongoza msafara kuelekea polisi huku akitembezwa na taulo mtaani huku mkewe akimbebea nguo nyingine ikiwemo ‘boksa’.
“Yaani hata siamini, mume wangu nilimuamini sana kumbe ananizunguka,” alisema mke wa Temba kwa huzuni.
Alipofika kituoni, Temba aliandikisha maelezo ambapo hadi mashushushu wetu wanaondoka eneo hilo, kulikuwa na watu kibao waliokuwa wakipiga kelele.
ZIJUE SABABU 5 ZINAZOFANYA WANAWAKE WENGI KUKOSA WAUME WA KUWAOWA KWA 100%.
ZIJUE SABABU 5 ZINAZOFANYA WANAWAKE WENGI KUKOSA WAUME WA KUWAOWA KWA 100%.
1.Umalaya – Ule wakati binti anaanza kuchanua badala ya kujitunza nakujiheshimu yeye ndio anatumia nafasi hiyo kuuchezea mwili wake kila
mwanaume anayemtongoza anamkubali mwisho anajikuta ana maboyfriend zaidi ya mmoja, hapo anaanza kuangalia sasa maslahi na sio upendo wa dhati anajikuta kaingia kwenye wrong choice basi ataendelea kusakanyia mwengine na mwengine na mwengine ili akutane na right choice hapo kuna mabuzi kibao kuna waume za watu na vijana matapeli wote anabambana nao mwisho anashtukia yuko above 30 ana anza kulia ohh na mkosi sijui nuksi nk.
2. Maringo – Nipale wakati binti anapokua nakujishtukia kuwa yeye ni mrembo wa ukweli, basi hapoa ataanza kujisikia kuwa yeye ni yeye kudharau wengine na kujiona babkubwa na kuwa too much selective, inapotoke kijana kampenda atakapomfata huwa anamuangalia nakumuona hana hadhi ya kuwa na yeye, itaendelea hivyoooooo mwisho atakuja kukutana na kijana mtanashati wa ukweli hapo ndio atajiaminia huyo ndio mwenye hadhi yake kumbe gubegube, mpaka aje kugundua kashaumizwa anaanza sasa kuumizwa kila mara hapo ataamua sasa kujishusha na kusarandia vijana wa kawaida, kila atakae date nae anakuta ni mchumba wa mtu au mume wa mtu au bf wa mtu, hapo ndio tayari keshakua majeruhi wa mapenzi basi itabidi aishie kuchuna mabuzi fumba na kufumbua yuko above 30 anaanza kulia nina mkosi ohh nuksi nk.
3. Roho ya kukataliwa – samahani maana hii ipo spiritual zaidi mtaniwia radhi, kiukweli kuna watu wana roho ya kukataliwa utakuta ni msichana mrembo tabia nzuri na sifa zote nzuri anazo shida ni akwamba wachumba wanamkataa dk za mwisho, ikumbukwe huyu sio muhuni anajiheshimu na anajitambua vizuri, atapata mchumba ghafla mchumba atamtema nakwenda kwa msichana mwingine inaweza kuwa kashamvisha hata pete ya uchumba wameshatambulishana hata kwa wazazi haijalishi mwanaume atamtema tuu, hawa kwakweli ndio wanaongoza kwakujiita wana mkosi nuksi nk.
4. Majini Mahaba – Baadhi ya wasichana wana majini mahaba kwahiyo kuolewa kwao imeshakua ni tabu anaweza apate mchumba afe au mwanaume abadilike tabia nakumchukia au mwanaume aanze kuwa Malaya na kushindwa kumvumilia hatimaye wanaachana mauzauza yanakuwa kibao kwenye mapenzi yake mwisho anajishtukia yuko above 30 anajiona ana mkosi na nuksi.
5. Marafiki wabaya – Msichana anaweza kuwa haolewi kumbe marafiki alionao sio wema kwake, ukipata mchumba tayari umeshaenda kumweleza shosti wako au mashosti zako, bila wewe kujua wanampeperusha, watakuzunguka ,watatembea nae, watamtega, watakuongelea vibaya, watakuloga, watamloga, watakuharibia mpaka utaachwa kila mara usipokua mjanja ukashtuka ndio hivyo uanajikuta uko abave 30 unaanza kulia ohh nina mkosi sijui nuksi nk.
Mpaka hapo nina amini kwa wewe msichana ambaye huolewi kuna fungu lako moja kati ya hayo hapo juu, sasa chakufanya jitambue na ujipange upya kama ushapita above 30 usihofu sana hata miaka 60 wanaolewa bado.