Featured Post Today
print this page
Latest Post

MBARONI KWA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

MBARONI KWA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA


Na Peter Mtulia, Tanga.

JESHI la polisi mkoani Tanga linamshikilia kijana Said Abdalah mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kwanjeka mjini hapa kwatuhuma za  kukamatwa na madawa yanayoyo dhaniwa kuwa  ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilogram moja.
 
Mtuhumiwa huyo amekamatwa mnamo juni 4 majira ya saa nane mchana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, ACP Costantine Masawe akiwa ofisini kwake amesma mtuhumiwa  ambaye pia ni mfanya biashara wa Makorora mjini humu amekamatwa kupitia taarifa zilizotoka kwa raia wema.

Kamanda Masawe amesema baada ya taarifa ndipo askari walifika eneo alipokuwamtuhumiwa na kumkamata na kwamba mpaka sasa thamani ya madawa hayo haijatambulika hadia  mkemia wa serikali atakapotoa uthibitisho wa dawa hizo na uzito wake halisi.

Masawe amesema wakiwa katika harakati za kushughulikia suala hilo watu wawili Amri Mohoreja mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Donge na Hassan Mwandani mwenye miaka 24 mkazi wa Mikanjuni walitaka kuwashawishi maofisa Polisi kupokea rushwa ya shilingi 8,600,000 ili wapindishe ukweli na kumwachia mtuhumiwa

Amesema watu hao baada ya kusikia kukamatwa kwa mwezao Said Abdala mtuhumiwa wa madawa hayo ya kulevya waliwasiliana kwa njia ya simu na maafisa wa polisi ambao waliwekeana miadi ya kukutana eneo la Harbours Club. 

Amesema ndipo Juni 4 majira ya 2;30 usiku walifanya mtego na kufanikiwa kuwatia nguvuni wakiwa na fedha hizo. 

Taratibu za kisheria zinaendelea ili watuhumiwa kufikishwa mahakamani huku akiwapongeza askari wake kwa kukataa kupokea rushwa na kuitaka jamii kuzidi kushirikiana nao kufichua wanaousika na uhuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya nchini.


0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger