Featured Post Today
print this page
Latest Post

Ummy: Nitavalia njuga bei ya gesi

Ummy: Nitavalia njuga bei ya gesi

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Ummy MwalimuNAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Ummy Mwalimu, ameahidi kulivalia njuga suala la bei za nishati ya gesi kwa lengo la kuhakikisha kila mwanamke wa Kitanzania ananufaika na nishati hiyo.
 
Naibu Waziri huyo alisema hayo alipokuwa akifungua warsha ya mafunzo kwa madiwani wanawake kutoka halmashauri zote za Mkoa wa Tanga yalioandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tawode.
Alisema kina mama wengi wamekuwa wakitumia mkaa katika matumizi yao ya nyumbani  kutokana na kushindwa kumudu gharama za nishati ya  gesi ambayo kwa hivi sasa bei yake iko juu.
“Kwa kweli nitalivalia njuga suala hili sitakubali kumuona mwanamke wa Kitanzania akitaabika kutumia mkaa na ikiwa tuna majiko ya gesi tushushe  gharama za majiko haya, ili kuwe na urahisi wa matumizi ya nyumbani,” alisema Ummy.
Mkurugenzi wa Tawode, Fatuma Hamza, alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwafundisha viongozi wanawake kujua mbinu za utawala bora kwa maendeleo ya wanawake na taifa kwa ujumla.
Alisema kutokana na msingi huo, taasisi hiyo imeweka kipaumbele cha juu suala la utawala bora na usawa wa jinsia, ili kufanikisha mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kupitia utekelezaji wa progamu mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, aliwataka madiwani hao wanawake kuhakikisha wanakuwa na mshikamano kwa upande wa kuwatetea wanawake katika bajeti zinazopangwa na halmashauri zao.
Chanzo;tanzania daima
0 comments

TANZANIA YAANDALIWA MAOMBEZI MAALUM YA AMANI

TANZANIA YAANDALIWA MAOMBEZI MAALUM YA AMANI 

 Na Kenneth John

Kituo cha nyumba ya maombezi kimeandaa kongamano maalum lenye dhamira ya kuombea kampeni za uchaguzi mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu mwaka 2015, pamoja na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya unaoendelea kwa lengo la kudumisha amani ya nchi.

Akizungumza na waandisha wa habari jijini Dar es salaam muanzilishi na msimamizi wa kituo hicho Apostle Patrick Kayimbi Emmanuel amesema kuwa katika kampeni za uchaguzi kinachofanya kazi sana ni ulimi, kwa maana ulimi ndio unaongea , na pale ulimi usipokuwa na nguvu ya Mungu unaweza kuvuruga amani ya nchi , hivyo wameona ni vyema kuombea uchaguzi wa nchi pamoja na kiungo hicho muhimu , ili kuepusha kutoweka kwa amani.
Ulimi usipotawaliwa na nguvu za mungu utaleta vurugu kubwa sana baada ya kampeni maana familia moja na nyingine hawatapatana tena “Alisema Apostle Patrick.

Aidha ameongeza kuwa watanzania wasifunge mikono kwaajili ya kufurahia amani iliyopo sasa, bali wazidi kuomba amani kwani maombi pekee ndiyo yanaweza kuleta maisha ya amani na utulivu nchini.

Akizungumzia kuhusiana na mchakato wa katiba Apostle Patrick amesema mchakato wa katiba ni miongoni mwa mambo watakayo yaombea kwenye kongamano hilo ni pamoja na mchakato wa katiba, kwa lengo la kuhakikisha katiba ya faida na yenye Baraka kwaajili ya wananchi wote watanzania inapatikana .Halikadharika Apostle ameipongeza tume ya katiba mpya pamoja na Mhe; Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwapatia watanzania haki ya kushiriki katika mchakato huo, kitu ambacho Apostle Patrick amesema huwa hakifanyiki katika nchi nyingi, na hivyo kuwaomba wananchi kupokea katiba jinsi itakavyoletwa mara baada ya tume kumaliza kazi yake.
Ameongeza kuwa endapo watanzania wote watamlilia Mungu basi mwaka huu utakuwa ni mwaka wa ushuhuda kwa nchi, lakini pia amesema hata vyama vya siasa vitatafautiana kwa sera zao ila lugha zao zitakuwa ni moja.

Sambamba na hayo Apostle Patrick ameiomba serikali kuwasaidia kuanzisha kituo cha watoto yatima, kwa lengo la kuwasaidia watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifika kituoni hapo wakiwa na shida mbalimbali huku wakihitaji msaada.Na pia ametoa wito kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na vyama vya siasa kuzidi kuhubiri amani ndani ya nchi.

Ikumbukwe kwamba kongamano hilo litafanyika Tabata Ugombolwa na litaanza rasmi februari 16 na kuhitimishwa Machi 2 , huku likijumuisha viongozi mbalimbali wa kimataifa ambao ni Bishop Drabraham Mandrandelle(Canada),Prophet Fordger Coetzee(Namibia),Apostle Peter Mwanga(Zambia),Evangelist Freddy Kayimbi(DR Congo) pamoja na Bishop Elie Kabengele(Kenya) Sambamba na mtumishi wa Mungu Peter Mitimingi.

 

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger