Featured Post Today
print this page
Latest Post

SALAMU ZA RAMBIRAMBI.....

SALAMU ZA RAMBIRAMBI.....

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MZEE MANDELA, ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO KITAIFA, BENDERA KUPEPEA NUSU MLINGOTI
5cb8Nelson-Mandela1_c2069.jpg

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.


Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".

Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.
Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.
06 Desemba,2013
0 comments

Basi la mfano la kuenda kasi latua Dar es Salaam tayari kwa majaribio yatakayofanyika leo jijini humo

Basi la mfano la kuenda kasi latua Dar es Salaam tayari kwa majaribio yatakayofanyika leo jijini humo

BREAKING NEWS!!!!!!! BASI LA MAJARIBIO LA DART LIMEWASIRI. LEO LITAFANYA SAFARI YA MFANO SAA TISA JIONI KUANZIA OFISI ZA DART UBUNGO PLAZA KUELEKEA KIMARA NA KWENDA KIVUKONI NA KUREJEA UBUNGO. LITATUMIA NJIA MAALUM ZILIZOJENGWA (BRT DEDICATED LANES) ... TUNAJENGA KWA AJILI YAKO 2014 BARABARA YA MOROGORO ITAMEREMETA ..... hili hapa kama huamini. Pichani ni mdau wa mambo ya usafiri, Deo Mutta Mwanatanga, akiwa amepozi katika basi hilo na kilichoandikwa ni maneno yake mwenyewe katika akaunti yake ya facebook leo.
0 comments

MAKAMBA AONGOZA UZINDUZI WA AZAM TV

MAKAMBA AONGOZA UZINDUZI WA AZAM TV

 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akizungumza kwenye uzinduzi wa Azam TV uliofanyika Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel mwishoni mwa Juma ambapo amesema Azam TV imekujali kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa Digitali na kutoa fursa ya ajira kwa Vijana wa Tanzania wenye vipaji sanjari na kuitangaza nchi yetu katika bara la Afrika hasa kwenye upande wa Soka na Filamu.
Azam TV itaanza kurusha matangazo yake Desemba 6 mwaka huu, Watanzania kaeni mkao wa kula kupata King’amuzi kwa bei rahisi ambacho kitakuwa na chaneli zisizopungua 50.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Tv, Rhys Torrington akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Azam Television jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
 Naibu waziri Januari Makamba akifuatilia maelezo ya awali ya Azam TV

 Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo wa Azam TV.
 Mkurugenzi wa vipindi wa Azam Tv Efe Atiyio akifafanua juu ya program mbalimbali za Azam Tv


Wadau katika uzinduzi
 Wasiwasi Mwabulambo akiwa na wafanyakazi wenzake wa Azam TV
 Januari Makamba, akitoa neno
 Wageni waaalikwa
Lucy Ngongoseke Kihwele (kulia)akiwa katika pozi na dada yake
 Huu ndio ungo wa Azam TV
 Uzinduzi ndio huooo
Staff wa Azam Media wakiwa wameshika vifaa vya Azam TV
 Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya SSB Ltd. Said Muhammad Said (kushoto) akielezea ubora wa Kisumbuzi cha Azam Tv kwa mmoja wa waalikwa.
Wasanii wa Filamu nchini nao walihudhuria uzinduzi huo wa Azam TV, toka kushoto ni Natasha, Monalisa na Hemed wakiwa na mdau mwingine wakiangalia kipeperushi cha Azam TV.
0 comments

ZIUNGENI MKONO TAASISI ZINAZOPAMBANA NA UKATILI NA UNYANYASAJI WA WANAWAKE NA WATOTO-TUNU PINDA.

ZIUNGENI MKONO TAASISI ZINAZOPAMBANA NA UKATILI NA UNYANYASAJI WA WANAWAKE NA WATOTO-TUNU PINDA. 

MKE WA WAZIRI MKUU WA TANZANIA MAMA TUNU PINDA AKIZUNDUA KAMPENI YA TANGA TUNAWEZA LEO ILIYORATIBIWA NA ASASI YA TREE HOPE.


 

Na Paskal Mbunga,Tanga.
 MKOA wa Tanga umehimizwa kuziunga mkono taasisi zinazopambana dhidi ya ukatili na unyanyasi kwa wanawake na watoto ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa.

Akizindua rasmi leo kampeni ya “Tunaweza Mkoa wa Tanga” inayoerndeshwa na asasi ya Tree of Hope ya jijini hapa, Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda alisema suala la ukatili wa kijinsia katika jamii yetu linaendelea kushika kasi na kuleta madhara mengi yakiwemo ulemavu mwilini, msongo wa mawazo, kuvunjia kwa ndoa ama kusababisha wanandoa kuathiriwa na magonjwa hatari, ukiwemo UKIMWI, na wakati mwingine vifo.


Mama Pinda alisema kwamba Mkoa wa Tanga umefikisha asilia 15.7 kwa ukatili wa kimwili (physical violence) na asilimia 11.3 ya matukio ya ukatili wa kingono (sexual violence).  Hii ni kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa mwaka 2010 (Tanzania Demographic & Health Survey),

Mke wa Waziri Mkuu ambaye alionekana kutishwa na takwimu hizo, aliutaka uongozi wa Mkoa wa Tanga kuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa huku akionya kwamba hali hiyo sio ya kufumbiwa macho.

Alisema ili kupambana na hali hiyo, Serikali ya Tanzania ilitunga sera ya Jinsia ya mwaka 2000 ikiandaa Mkakati wa miaka 15 wa kuondoa ukatili kwa wanawake na watoto katika jitihada ya kukabiiliana na changamoto hizo.

Mama Pinda alikemea tabia potofu zilizozoeleka miongoni mwa wanawake kwamba kupigwa na mume ni jambo la kawaida na linalokubalika kwa baadhi ya makosa ambayo mwanamke anapomkosea mumewe ni lazima aadhibiwe.

Alitaja mazoea hayo ni pamoja na kuafiki kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo ataondoka bila kuaga kwa mume. Pia mume ana haki ya kumpiga mkewe endapo atazembea kuangalia watoto.  Pia tabia nyingine ni mke kukubali kupigwa na mume kutokana na kubishana naye.

Mama Pinda alizitaka asasi za kiraia kuungana pamoja katika mapambano dhidi ya ukatili wa kinsia na kusisitiza kwamba kampeni ya “Tunaweza”Ni mkakati muhimu katika kutokemeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa aliwataka wakinamama kuiunga mkono kampeni hiyo kwa kujishughulisha na miradi ya uzalishaji mali ambayo kwayo itawaweka huru pasi na utegemezi mkubwa kutoka kwa wanaume. 
Aliwataka akinamama kuzitumia taasisi ya kifedha kwa ajili ya kujijengea mitaji ya kufanya biashara.
Kwa upande wake,Mratibu wa Asasi ya Tree of Hope FortunataManyeresa aliitaka jamii kuwa mstari kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kuwalinda watoto na wanawake.
 Alisema asasi hiyo tayari imeshaeneza huduma zake katika wilaya zote nane za mkoa wa Tanga lengo likiwa ni kuhamasisha wakazi wa mkoa wa Tanga kupata mwamko wa kuweza kupambana na tatizo hilo ambalo lilojengeka kwa misingi ya tamaduni za kikabili
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger