JIJI LA TANGA LAENDELEA KUZOROTA KTK USAFI
Na Mwananjia Anaroti & Mercy Kifimbo
Hali ya usafi jijini Tanga imeendelea kuzorota kutokana na mamlaka husika kushindwa kuondoa taka katika mitaa mbalimbali na kudhibiti mifumo ya maji taka jijini.
Kituo hiki kimeshuhudia mrundikano wa taka katika mitaa mbalimbali hasa maeneo ya Chumbageni ambazo zinatoa harufu mbaya, hali inayoweza kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu pia kuwa mazalia ya wadudu waenezao magonjwa kama nzi na mbu.
Wakazi wa maeneo hayo ambao majina yao hawakutaka yafahamike wamesema wamekutwa kadhia hiyo kutokana na mamlaka husika kushindwa kuondoa taka kwa wakati na wanaiomba mamlaka husika kushughulikia tatizo hili kwa haraka iwezekanavyo.
Nae Afisa usafi wa jiji Sylvester Magobo amesema kuwa na uhaba wa vitendea kazi kama magari na mapipa ya kukusanya taka umepelekea halmashauri kushindwa kuzoa taka kwa kiwango cha juu.
Hata hivyo mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Tanga (UWASA) imeomba radhi kutokea kwa tatizo la kuziba kwa bomba kubwa linalosafirisha maji taka kuelekea baharini na kueleza kuwa wapo katika harakati za kutatua tatizo hilo ndani ya siku chache zijazo.