Featured Post Today
print this page
Latest Post

AZAM YAANZA AFRIKA, YAWAKALISHA WAMAKONDE CHAMAZI LICHA YA KUBEBWA NA MAREFA ILE MBAYA

AZAM YAANZA AFRIKA, YAWAKALISHA WAMAKONDE CHAMAZI LICHA YA KUBEBWA NA MAREFA ILE MBAYA

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
AZAM FC imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.
Shukrani kwake mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 41 baada ya kutengewa pasi nzuri ya kichwa na Mganda Brian Umony na kufumua shuti kali.
Mchezo ulikuwa mkali dakika zote 90 na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili.
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Kipre Tchetche leo Chamazi

Mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Tchetche na Mganda Umony kwa pamoja na Mzanzibari Khamis Mcha ‘Vialli’ walikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Ferroviario.  
Kipindi cha pili, Ferroviario walicharuka zaidi na Azam nao walipoteza nafasi kama tatu za kufunga mabao mwanzoni. 
Refa Mutaz Abdelbasit Khairalla na wasaidizi wake Waleed Ahmed Ali na Aarif Hassan Eltom wote kutoka Sudan walionekana kabisa kuwapendelea wageni katika maamuzi yao. 
Dakika ya 70 beki mmoja wa Ferroviario aliunawa mpira wazi wazi kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Kipre Tchetche mbele ya refa, lakini akapeta. 
Kiungo mkabaji wa Ferroviario, de Beira akipiga tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umony leo Chamazi
Kipre Tchetche akimtoka beki wa kushoto wa Ferroviario, Emidio Matsinhe leo

Matokeo hayo yanamaanisha Azam itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo nchini Msumbiji, wakitakiwa kulazimisha sare ili kusonga mbele.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, Kipre Balou, Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha/John Bocco dk61, Kipre Tchetche na Brian Umony/Jabir Aziz dk81.
Ferroviarrio; William Manyatera, Zefanis Matsinhe, Emidio Matsinhe, Abrao Cura/Kiki Simao, Edson Morais, Reinildo Mandava, Valter Mandava/Hery Antony, Antonio Machava, Manuel Fernandes, Mario Sinamunda na Manuel Correia/Dje Buzana.  
0 comments

SIMBA SC YAKALISHWA NA MIGAMBO MKWAKWANI

SIMBA SC YAKALISHWA NA MIGAMBO MKWAKWANI

Na Oscar Assenga, Tanga
SIMBA SC imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa adhabu.
Wachezaji wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.
Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger