skip to main |
skip to sidebar
Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani, Nelson
Mandela, ametolewa hospitali ambako amekuwa akitibiwa mapafu tangu mwezi
wa Juni.
Taarifa katika tovuti ya rais wa Afrika Kusini imeeleza kuwa Bwana
Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwengine inabadilika.
Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.
Nyumba ya Bwana Mandela imebadilishwa ili kumruhusu kupata matibabu ya mgonjwa mahtuti akiwa nyumbani.
Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.
Copyright © 2011.
TANGA LEO - All Rights Reserved
Post a Comment