Featured Post Today
print this page
Latest Post

MWIGIZAJI WA FILAMU ATAPA JERAHA BAADA KUJERUHIWA NA CHUPA KATIKA UKUMBI WA STAREHE WA CLB BILLICANAS JIJINI DAR ES SALAAM.

MWIGIZAJI WA FILAMU ATAPA JERAHA BAADA KUJERUHIWA NA CHUPA KATIKA UKUMBI WA STAREHE WA CLB BILLICANAS JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mwigizaji wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Aunty Ezekiel akiwa anauguza jeraha la kidonda baada ya kudaiwa kujeruhiwa na chupa katika ukumbi wa starehe wa Club Billicanas jijini Dar es Salaam.
 Aunty Ezekile
MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Aunty Ezekiel imeripotiwa kupata majeraha katika mkono wake wa kushoto baada ya kuchimbwa na chupa yenye ncha kali, sakata hilo la hatari lilitokea Club  Billicanas wakati wa show iliyokifanyika hapo chini ya Madam Wema Sepetu chanzo chetu kimetuhabarisha.
Chanzo cha ugomvi hadi leo bado kitendawili baada ya kutoka fununu kuwa uenda ugomvi huo unahusishwa na kumgombea bwana yaani mwanaume ambaye waliwahi kumgombea siku za nyuma lakini kupigana kidogo ambapo mmoja alitoka nduki na kuacha msala ukitulia. CHANZO http://mwanahabariuswazi.blogspot.com

Chanzo chetu bado kinafuatilia tukio hilo kwa ukaribu kisha tutakujuza kulikoni hadi nyota wetu kutaka kuharibiwa show yake ambayo ndio inapa ajira katika uigizaji, tunampa pole kwa majeraha yaliyompata , huku tukisubiri atusimulie sakata leo hakuwa tayari kupokea simu yetu.

 

0 comments

MAJANGA ARSENAL, PODOLSKI NJE WIKI TATU...RAMSEY NA WILSHERE NAO 'TIA TIA MAJI'

MAJANGA ARSENAL, PODOLSKI NJE WIKI TATU...RAMSEY NA WILSHERE NAO 'TIA TIA MAJI'

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas Podolski ataukosa mchezo wa Jumapili wa wapinzani wa London Kaskazini, dhidi ya Tottenham baada ya kuumia nyama katika mchezo wa Ligi ya Mabinwa jana dhidi ya Fenerbahce.
 
 Blow: Lukas Podolski added to Arsenal's injury woes as the striker was taken off on a stretcher
 
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerymani anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia katika dakika za mwanzoni za kipindi cha pili kwenye ushindi wa 2-0 katika mchezo huo wa marudiani, hivyo timu yake kusonga mbele hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Waturuki.
 
Kocha Arsene Wenger amesema: "Tmetugharimu mno kwa majeruhi hayo, kwa sababu tunampoteza Podolski.
 
Blow: Lukas Podolski added to Arsenal's injury woes as the striker was taken off on a stretcher

Blow: Lukas Podolski added to Arsenal's injury woes as the striker was taken off on a stretcher
Blow: Lukas Podolski added to Arsenal's injury woes as the striker was taken off on a stretcher
"Podolski atakuwa nje kwa wastani wa siku 21,"alisema.
Aaron Ramsey alifunga mabao yote katika usiku huo Arsenal ikijikatia tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 16 mfululizo.
Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales naye pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioumia, akitoka nje kabla ya mwisho wa mchezo na kuiacha Gunners ikimalizia mechi na wachezaji 10. 
Kiungo Jack Wilshere pia naye alipatwa na misukosuko, alipokabiliana na Raul Mereiles na Bruno Alves, na kumuachia maumivu.
Soldiering on: Jack Wilshere clutches his ankle but he refused to come off as Arsenal beat Fenerbahce
Majanga juu ya majanga: Jack Wilshere aliumia kifundo cha mguu, lakini akaendelea na mechi Arsenal ikiifunga Fenerbahce

Wenger alisema: "Sifahamu kiasi gani Ramsey ameumia. Sifahamu Wilshere anaendeleaje. Tutaangalia hiyo kesho (leo)  asubuhi. Makwanja mawili kwa Wilshere yalisikitisha, lakini anaonekana yuko sawa.
"Jack atakuwa sawa Jumapili. Natumai hivyo kwa Aaron pia. Nilimuona akitoka nje zikiwa zimesalia dakika tatu au nne mechi kumalizika, lakini sijui anajisikia vibaya kiasi gani. Alitaka kubaki uwanjani,".
Wenger alitaka kumtoa nje Wilshere, kutokana na historia ya matatizo ya maumivu ya kifundo cha mguu kwa mchezaji huyo, lakini mchezaji huyo akaamua kuendelea kucheza.
"Nilitaka kumtoa nje, ndiyo," Wenger alisema.
Goal hero: Aaron Ramsey appeared to leave the game before the end holding his groin
Shujaa wa mabao: Aaron Ramsey aliondoka uwanjani kabla ya mwisho wa mechi kutokana na maumivu ya nyonga

"Ilibidi tucheze na wachezaji 10. Tulikuwa mbele kwa mabao 2-0, walitakiwa kufunga mabao matano ndani ya dakika 10. Hata tulipobaki na wachezaji 10 tungeweza kuepuka hilo,".
Huku tayari wachezaji wake wengine, Mikel Arteta na Alex Oxlade-Chamberlain wakiwa majeruhi, huu ni mtihani mwingine kwa Wenger katika siku za mwishoni za pazia la usajili.
Kuna taarifa Juan Mata mkubwa, baba na wakala wa kiungo wa Chelsea, alikuwa Uwanja wa Emirates jana kuangalia mechi hiyo.
Wanted: Arsenal boss Arsene Wenger has admitted his interest in Chelsea star Juan Mata
Anatakiwa: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa na nia ya kumsajili nyota wa Chelsea, Juan Mata

Kufuatia kiungo huyo wa Hispania kupoteza namba katika kikosi cha kwanza Chelsea katika mechi dhidi ya Manchester United usiku wa Jumatatu, tetesi zinasema anaweza kuuzwa.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekanusha taarifa hizo na Wenger anaamini itakuwa shughuli pevu.
"Nampenda yeye,"alisema Wenger, ambaye alizidiwa kete katika kuwania saini ya mchezaji huyo wa zamani wa Valencia na Chelsea miaka miwili iliyopita.
"Niliangalia mechi hiyo jana (juzi) na nimesikia, kama wewe, Juan Mata anaweza kutiwa sokoni,"alisema Wenger ambaye hata hivyo anaamini klabu zinazoshindania ubingwa ni vigumu kuuziana wachezaji zenyewe kwa zenyewe.

 

0 comments

ETO'O KUTUA CHELSEA NDANI YA SAA 48...MOURINHO ANAMKUBALI KULIKO WOTE TORRES, BA NA LUKAKU

ETO'O KUTUA CHELSEA NDANI YA SAA 48...MOURINHO ANAMKUBALI KULIKO WOTE TORRES, BA NA LUKAKU

Chelsea bound: Samuel Eto'o may reunite with Jose Mourinho who managed him at Inter Milan

KLABU ya Chelsea iko katika hatua za mwishoni za kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala na dili hilo linaweza kukamilika ndani ya saa 48.
Tayari wamekwishamsajili Willian kutoka Anzhi ambaye anasubiri kibali cha kufanya kazi leo na usajili wa Eto'o utakuwa sehemu ya Pauni Milioni 32 zilizotengwa.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi tu wa mwaka mmoja.
Kifaa cha Chelsea: Samuel Eto'o anaweza kuungana na Jose Mourinho aliyekuwa kocha wake Inter Milan
Eto'o alianzia soka yake Ulaya katika klabu ya Real Madrid, lakini alicheza mechi tatu tu na akapelekwa kwa mkopo katika miaka yake minne na klabu hiyo ya Jiji la Hispania.
Alitengeneza jina alipokuwa akichezea Mallorca kabla ya kusajiliwa na Barcelona. Aliiwezesha kushinda Ligi ya Mabingwa, akifunga dhidi ya Arsenal katika Fainali mwaka 2006.
Baadaye akaenda kuungana na Jose Mourinho Inter Milan, na hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchaua kutua Chelsea. Kocha huyo Mreno anaweza kuwa na imani naye zaidi kuliko washambuliaji wake wa sasa, Fernando Torres, Romelu Lukaku au Demba Ba.
Forward power: Eto'o should complete his deal to Stamford Bridge in the next two days
Mshambuliaji wa nguvu: Eto'o anaweza kukamilisha uhamisho wake kutua Stamford Bridge ndani ya siku mbili hizi

 

0 comments

JESHI LA POLISI LAMWAGA AJIRA.

               JESHI LA POLISI LAMWAGA AJIRA.


JESHI la Polisi nchini, limetangaza ajira mpya kwa vijana waliohitimu kidato cha nne na sita mwaka jana. Taarifa za jeshi hilo, ambazo zimewekwa kwenye mtandao wa jeshi hilo, zinasema vijana katika mikoa yote wanatakiwa kufika kwenye ofisi za makamanda wa polisi mikoa kwa ajili ya usaili.

Taarifa hiyo, ilisema kila mkoa umepangiwa siku yake na kwamba kila kijana anapaswa kuwa na vyeti halisi vya elimu yake pamoja na cheti cha kuzaliwa. “Kwa wale wote walioomba nafasi hii, wanapaswa kufika kwenye ofisi husika, hasa vijana waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012 na wale waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013.

“Katika kundi hili, wapo waliochaguliwa wajitokeze kwenye usaili kabla ya kujiunga na jeshi la polisi,” ilisema taarifa hiyo.

“Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha, ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili.

“Jeshi la Polisi, halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili ilhali jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.

“Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema kuwa kila mwombaji anapaswa kuwa na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.

“Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema ni mapema kutoa idadi kamili ya vijana wanaotakiwa kwa sababu bado wapo kwenye mchakato.

“Siwezi kukwambia tunachukua wangapi, tumetangaza nafasi za kazi bado tupo kwenye mchakato… hii inategemeana na bajeti yetu tuliyonayo, tukikamilisha tutawaambia tu,” alisema Senso.
 
0 comments

WANAUME WAWILI HUKO KENYA WAKUBALI KUMUOA MWANAMKE MMOJA.

WANAUME WAWILI HUKO KENYA WAKUBALI KUMUOA MWANAMKE MMOJA.

 

Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda kwa  kusaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu. 
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao. Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
 
Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
 
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
 
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
 
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
 
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angefunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
 
 Lakini walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi kwa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao, alishindwa. Akasema anawapenda wote wawili.
 
Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda kumjulia hali.'
 
Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
 
 Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.

 

0 comments

MBUNGE WA JIMBO LA RUNGWE MAGHARIBI, PROFESA DAVID MWAKYUSA ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 40 KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA LA SABATO LA SWEBO- NTOKELA WILAYANI RUNGWE.

MBUNGE WA JIMBO LA RUNGWE MAGHARIBI, PROFESA DAVID MWAKYUSA ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 40 KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA LA SABATO LA SWEBO- NTOKELA WILAYANI RUNGWE.

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akizungumza na waumini wa kanisa la Wasabato wa Swebo Ntokela kuashiria ufunguzi wa harambee ya ujenzi wa kanisa.

Watoto wakiingia kanisani kwa ukakamavu mkubwa kushiriki harambee hiyo.
Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa akiwa meza kuu pamoja na viongozi wa Kanisa la Sabato siku ya harambee.
Kwaya ya Kanisa hilo ikitumbuiza kanisa hapo siku hiyo ya harambee.
Katibu mkuu wa kanisa la Sabato Jimbo la Nyanda za juu kusini Mchungaji Steven Letter akisoma neno la Mungu kuashiria ufunguzi wa Harambee hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na waumini wakifuatilia kwa makini zoezi la Harambee lililokuwa likiendelea kanisani hapo.
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee hiyo, Award Mpandilah  na Jose Mwapamba wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Award Mpandila akisimamia zoezi la uchangiaji wa harambee lilipokuwa likiendelea.
Kamati ya maandalizi ya harambee hiyo ikiwa katika picha ya pamoja.
Award Mpandila akimkabidhi hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee hiyo Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa.
Mwonekano wa jengo la kanisa hilo lilipoishia na kulazimu kufanya harambee ili kumalizia ujenzi wake.

Profesa David Mwakyusa Waziri wa Afya wa Zamani  na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Rungwe Magharibi(CCM) amefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milion 40 katika harambee ya uchangiaji ujenzi wa kanisa la Sabato la Swebo lililopo Ntokela Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Katika Harambee hiyo  Profesa Mwakyusa ambaye alikuwa Mgeni rasmi, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo aliwasihi waumini  wa kanisa hilo kuacha tabia ya kunung’unika pale wanapojitoa kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali za kikanisa ambazo zinafanywa na makanisa hayo  ili kusaidia jamii.
Imeelezwa kuwa baadhi ya waumini wamekuwa na moyo wa kujitolea pindi misaada mbali mbali inapohitajika katika makanisa, badala yake huanza kuumia  katika mioyo yao kwa kile walichotoa kwa kuona wametoa kiasi kingi.
Prof. Mwakyusa alisema  kama waumini wameamua kujitoa kwa ajili ya shughuli  za kanisa  hawana budi kunung’unika ndani ya nafsi zao kwani kazi ya mungu ni kujitolea si busara muumini kutoa msaada halafu ujutie baadaye.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi  mmoja wa wajumbe wa kamati  ya maandalizi  ya harambee hiyo  Bw.Awadi Mpandila  alisema kuwa lengo la kuanzisha ujenzi huo wa kanisa kulitokana na wingi wa waumini katika  kanisa hilo ambao wanafikia 835.
Award alisema kuwa ujenzi huo ulianza  mwaka 2002 na kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa ni mil.279 na zinazohitajika ili kuweza kukamilisha jengo
hilo ni sh. Mil.90.
Mbali na kukamilika kwa Harambee hiyo Mpandila anatoa wito kwa wadau na marafiki wa karibu ambao walipewa kadi za mwaliko lakini walikwama kufika kuendelea kuchangia kutokana na fedha zilizopatikana kutokidhi kiwango.
Alisema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kupaua na kumalizia jengo la kanisa hilo ambalo hatua za ujenzi wa awali umekamilika hivyo Wadau na marafiki wamekumbushwa kumtolea Mungu kupitia ujenzi wa kanisa hilo.
Hata hivyo katika harambee hiyo jumla ya sh. Mil.46 zilipatikana huku fedha iliyochangwa papo kwa papo ni sh. Mil.23 huku ahadi zikiwa mil.23 .
Aidha katika harambee hiyo ,Prof. Mwakyusa alichangia zaidi ya mil.2 pamoja na familia yake.

0 comments

TASAF II ilivyogeuza changamoto ya uhaba wa chakula kuwa fursa ya uchumi na maendeleo kwa wananchi wa korogwe vijijini

TASAF II ilivyogeuza changamoto ya uhaba wa chakula kuwa fursa ya uchumi na maendeleo kwa wananchi wa korogwe vijijini 

Mzee Rajabu Kufa mlemavu wa macho na mkazi wa kijiji cha Kwetonge kilichopo kata ya Mashewa mmoja wa wakazi wa Korogwe ambao wamenufaika na mradi wa TASAF II wa ufugaji ng’ombe kupitia kikundi cha Jipemoyo.

Watu wengi duniani huziona changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku kuwa ni vikwazo vya kutofikia malengo waliyojiwekea au wanayopaswa kuyafikia kama binadamu.Ni watu wachache sana wenye ujasiri wa uthubutu katika maisha yao,hata ikawapelekea wenye busara kutengeneza msemo wa “uoga wako ndiyo umasikini wako” wakilenga  kuwatia watu moyo na kuwataka kuthubutu hasa katika masuala yenye changamoto. 

Korogwe vijijini yenye ukubwa wa kilomita za mraba 3544,kata 20,vijiji 122,vitongoji 610 na jumla ya Wakaazi 242,038 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 ni moja ya jamii iliyojipatia manufaa kwa kutumia hekima za msemo huo.Korogwe ambayo kilimo ndiyo njia kuu ya wakaazi wake kujipatia chakula na kipato kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2010 imekuwa ikipata mvua za kubahatisha jambo lililopelekea kukabiliwa na uhaba wa chakula kwa baadhi ya maeneo na maeneo mengine kukumbwa na njaa hata kupelekea Serikali kupeleka chakula cha msaada. 

Pamoja na kukabiliwa na changamoto hiyo wakaazi hao hawakukaa na kuiangalia njaa ikiharibu maisha yao,badala yake kwa kutumia fursa zilizopo kama Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF II) iliyokuwa ikitekeleza program zake wilayani humo waliiona ni nafasi nyingine ya kujipatia maendeleo endelevu,wakaonesha uhitaji wao,wakathubutu na kwa kushirikiana vyema na Wataalamu wa kada mbalimbali katika Halmashauri, leo hii Wananchi hao  wanajivunia mafanikio yao. 

Edward Lukinisha ambaye ni mratibu wa Mfuko wa maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe anaeleza kwa kina jinsi jamii ya wanakorogwe ilivyofaidika na changamoto ya uhaba wa chakula kwa kuigeuza kuwa fursa ya kiuchumi,na kwamba sasa Wananchi hao wanayo miradi inayowaingizia kipato na kuwahudumia kila siku hata wameondokana kabisa na changamoto ya uhaba wa chakula. 

“Korogwe ilipotangazwa kuwa ni moja ya wilaya zinazokabiliwa na uhaba wa chakula,TASAF kama Mfuko wa kusaidia jamii katika fedha za bajeti kuanzia mwaka 2010 tulikaa na baadhi ya vijiji na kuwataka waibue miradi ambayo si tu ingekidhi haja ya kumaliza uhaba wa chakula kwa wakati huo,bali pia ingekuwa ni miradi endelevu hata kwa vizazi vijavyo” alisema Lukinisha. 

Anafafanua kuwa uibuaji wa miradi hiyo iliyogawanyika katika Sekta kuu tatu za mawasiliano,kilimo na ufugaji uliolenga kukabiliana na uhaba wa chakula ulikuwa katika sura mbili,miradi ambayo ingeinufaisha jamii moja kwa moja na miradi ya vikundi.Katika miradi ya jamii iliwapasa  wanajamii wenyewe kuibua miradi endelevu ambayo ingeinufaisha jamii nzima na kisha kubainisha kaya zizoathiriwa zaidi na uhaba wa chakula, hivyo wale wenye uwezo wa kufanya kazi katika kaya hizo ndiyo ambao wangefanya kazi ya ujenzi wa mradi wa jamii na kulipwa ujira ambao ungewasaidia kupata chakula kwa wakati huo,na wakati huo huo jamii nayo ingenufaika kwa kupata mradi endelevu. 

Moja ya miradi iliyojengwa wilayani humo kutokana na changamoto hiyo ni barabara ya  kijiji cha Changarikwa kilichopo kata ya Magamba Kwalukonge.Barabara hiyo ilichimbwa kwa urefu wa km 5.5 na upana wa mita 4.5 kwa gharama ya Tsh ml 32 zilizotolewa kwa Wananchi hao kama ujira. 
 
Rukia Hamisi aliyekuwa mmoja wa washiriki katika ujenzi wa mradi huo anasema barabara hiyo ilianza kuchimbwa mwaka 2010 na kukamilika 2011,ambapo wataalamu wa Halmashauri walipima na kutoa ushauri na wao Wananchi walichimba kwa ujira wa Tsh 3000 kwa kutwa.Fedha ambayo anasema ndiyo ilikuwa ikimsaidia kununua chakula kwa ajili ya familia yake. 

 “Barabara hii licha ya kuwa sasa inatusaidia sana kwa usafirishaji wa mazao yetu,lakini wakati wa kuitengeneza ilitusaidia sana kwani tulioichimba tulilipwa na fedha ile tuliitumia kwa kununua chakula kwani hatukupata kabisa mazao kwa mwaka ule.”Anasema Rukia.

Naye bi.Ndatima Shemshi anaongeza kuwa hapo mwanzo walitembea umbali mrefu kwa miguu kwani ilikuwa ni vigumu kwa magari kufika kijijini kwao,lakini sasa magari yanaingia hadi kijijini na kubeba mazao yao kama mahindi na ngwasha ambayo hununuliwa sana na Wakenya kwa ajili ya kutengenezea biskuti. Hata hivyo mama huyo ana ombi maalum kwa wadau wenye uwezo kuwekeza zaidi katika barabara hiyo ili iweze kutokezea kitongoji cha Mlembule katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Mombo ambako ndipo kuliko na barabara kuu inayounganisha nchi za Afrika Mashariki kupitia Arusha. 

Sekta ya mawasiliano inapewa nafasi pia katika kijiji cha Makumba  ambapo wanakijiji hao kwa pamoja wanaamua kujenga kivuko kitakachounganisha kijiji chao na kijiji cha Kazita.Wanakijiji hao wa Makumba wanapata msukumo wa kujenga kivuko hiki ili kuisaidia jamii  kubwa ya wenzao waishio katika kijiji cha kazita katika vitongoji vya Magunga na Mtemiroda huku huduma zote muhimu za kijamii zikipatikana kijiji cha Makumba. 

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Makumba Petro Harawa anasema kimsingi vijiji hivyo viwili ni kama kijiji kimoja cha watu 3069 huku 800 kati yao wanaoishi Kazita wakitenganishwa na bonde korofi hasa nyakati za mvua,hivyo kama kijiji waliona ni vyema kujenga kivuko kitakachowaunganisha nyakati zote na ndipo TASAF II ilipowapatia ml 28 na kuanza ujenzi wa kivuko hicho Mei 2012.

Oddos Komba Mwanakijiji wa Kazita pamoja na kushukuru kwa kuondokana na njaa pia anasifu jitihada za Serikali za kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na uchukuzi vijijini kwa kuielezea kadhia waliyokuwa wakiipata hapo awali hasa nyakati za masika huku akitolea mfano wa mwaka 2006  pale wanafunzi wa kijiji cha kazita waliposhindwa kufanya mtihani wa darasa la nne kutokana na mvua kubwa kusababisha mahali hapo kutokupitika na kukifikia kijiji cha Makumba ambako ndikokuliko na shule.
Sambamba na mawasiliano miradi mingine iliyokusudiwa kuinufaisha jamii nzima ni ile ya Sekta ya kilimo, ambayo ni ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji.Katika utekelezaji wa kusudio hilo vijiji vinne ambavyo ni Chekelei, Mazinde Mheza,Mazinde Goha na Makangara Songea vilinufaika nayo. 

Michael Cassian ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya mradi wa mfereji wa umwagiliaji kijiji cha Chekelei anasema kuwa wao walipatiwa ml 31 ambazo zimeweza  kuchimba na kujenga mfereji wenye urefu wa mita 200 pamoja na vigawa maji nane.Mradi huo ulioanza kujengwa mwaka 2011 ulikamilika 2012 na tayari Wakulima wameanza kutumia katika msimu huu wa kilimo wakiwa na matumaini ya kuongeza uzalishaji wa mpunga mara dufu kwa sababu sasa hivi maji yanafika mashambani kwa uhakika na kwa kipimo kinachotakiwa. 

Wakati Chekelei wakisubiri mavuno, kijiji cha Mazinde Goha wao wanajivunia mavuno ya matunda aina ya matikiti maji tani sita katika msimu wa kwanza kabisa April 2012 mara tu baada ya kukamilika kwa mradi wao Januari 2012, na sasa wanajipanga kufanya kilimo cha pilipilihoho,vitunguu , nyanya na mbogamboga kwa kipindi cha kiangazi. 

Iddi Uledi Mwenyekiti wa kikundi hicho kiitwacho Songambele anasema walipatiwa ml 8.9 za kuchimba kisima na ununuzi wa mipira yenye uwezo wa kuhudumia ekari 15 za shamba ambazo walipewa na kijiji,lakini mpaka sasa wametumia ekari nne tu huku wakiendelea na juhudi za kufyeka pori lililobaki ili waweze kunufaika zaidi  

Katika harakati hizo za kuwapunguzia Wananchi makali yatokanayo na uhaba wa chakula TASAF II iliwekeza pia katika sekta ya mifugo huku wanufaika wakishuhudia ya kwamba wamepata faraja kubwa kwa kupata miradi ya ufugaji ng’ombe na mbuzi kwani mbali ya kuwapatia kipato pia imeimarisha afya zao kwa kunywa maziwa kila siku. 

Miradi hiyo ya ufugaji ilitolewa kwa vikundi vya watu kumi na nne na kumi na tano kwa vigezo vya kuathiriwa na uhaba wa chakula na kuwa katika makundi maalumu ambayo ni walemavu,wajane na wagane, na kwa kuzingatia uwiano wa jinsia. 

Rajabu Kufa ni mlemavu wa macho na mkazi wa kijiji cha Kwetonge kilichopo kata ya Mashewa anasema yeye amenufaika na mradi wa TASAF II wa ufugaji ng’ombe kupitia kikundi chao cha Jipemoyo.Anasema ng’ombe wake aliyempa jina la Sara amekuwa mkombozi mkubwa sana kwake hasa kwa kuzingatia hali yake isiyomwezesha kufanya kazi nyigine ngumu. 

“Ng’ombe huyu ananisaidia sana kwani napata lita nne kila siku ambazo naziuza kwenye kituo cha maziwa kilichopo hapa kijijini kwetu,napata pesa za kujikimu mahitaji yangu kutokana na ng’ombe huyu,hivyo imenisaidia kuondokana na tatizo la kuombaomba na kuwa na uhakika wa kupata chakula kila siku”.Anasema Kufa. 

Mzee huyu anakiri kuwa hawezi kumhudumia ng’ombe wake yeye mwenyewe,lakini ng’ombe huyo wa asili aliyeboreshwa ili kutoa maziwa ana afya njema sana.Kufa anasema ng’ombe huyo  huhudumiwa na mtoto wake ambaye humkatia majani ya kutosha kwa siku nzima kila asubuhi kabla ya kwenda kwenye shughuli zake.  

Anaongeza kuwa kijana wake ana furaha sana kumhudumia ng’ombe huyo kwani amempunguzia majukumu ya kumgharamia yeye kifedha.Mzee Kufa anaishukuru Serikali kwa kuleta mradi wa TASAF kwa wahitaji kama yeye na kusema kwake yeye hakika Serikali imemjali sana,pia anaishukuru Jamii ya kijiji chake kwa kuuona uhitaji wake  na kumchagua kupewa ng’ombe huyo. 

Naye Bi. Stara Ponda mjane aishie katika kijiji hicho cha Kwetonge anasema mbali ya ng’ombe wake kuimarisha afya ya familia yake wakiwemo watoto ambao ni wajukuu zake anaowalea kwa kunywa maziwa lakini pia ng’ombe huyo humsaidia kupata mahitaji  ya shule ya watoto  kwa kuuza maziwa kila siku.

Wakati Wananchi hao wakifurahia ufumbuzi wa tatizo la uhaba wa chakula na kujipatia miradi ya maendeleo, Afisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Kakulu Lugembe anakiri kuwa katika kipindi cha mitatu  maeneo mengi ya Halmashauri yamepitia kipindi kigumu cha upungufu wa chakula hata kupelekea Serikali kuleta chakula cha msaada. 

“Novemba 2012 Halmashauri ilipokea tani 111.8 za mahindi ya msaada toka Serikalini na kugawa katika vijiji 60 vya Kata 12 na Machi 2013 ilipokea tani 350.6 na kugawa katika vijiji 63 vya kata 12” anasema Lugembe. 

Hata hivyo anasifu jitihada zilizochukuliwa na TASAF II kwani zilisisimua uwajibikaji kwa kuwa suala la upungufu wa chakula husababishwa na mambo mengi ikiwemo uvivu wa mtu husika,majanga kama  mafuriko na mabadiliko ya tabianchi.Anaielezea hali ya chakula kwa mwaka huu kuwa ina ishara njema kwani hali ya mazao mashambani ni nzuri ukiachilia mbali kata nne tu za Mashewa,Mkomazi,Mkalamo na Mazinde.  

Lugembe anawapongeza zaidi Wananchi waliochagua ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji kwa kueleza kuwa kwa sasa kilimo cha uhakika na tija ni cha umwagiliaji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotabirika.Anaeleza kuwa hata Halmashauri imeelekeza nguvu zake katika ujenzi wa skimu za umwagiliaji ikiwemo ya Kwemkumbo katika mamlaka ya mji mdogo Mombo na katika bonde la Mkomazi ambazo zinatarajiwa kukamilika mwaka 2014. 

Anatoa wito kwa Wananchi kutumia kanuni bora za kilimo kwa mazao yote,kulima mazao mbadala yanayostahimili ukame kama mtama,muhogo na viazi vitamu na zao la biashara la alizeti kwa maeneo yasiyo na mvua za kutosha.Anasisitiza zaidi Wananchi kutumia chakula kwa uangalifu,kujiwekea akiba na kuacha uuzaji holela ili kuepuka upungufu wa chakula mara kwa mara.          
 

 

0 comments

Jinsi uboreshwaji wa Miundo Mbinu Mkoani Tanga umesaidia kukuza Uchumi

Jinsi uboreshwaji wa Miundo Mbinu Mkoani Tanga umesaidia kukuza Uchumi 

Mkoa wa Tanga umejaliwa kwa kuwa na ardhi nzuri na yenye rutuba, fukwe nzuri za bahari za kihistoria, safu za milima ya Usambara inayovutia, mabonde na maporomoko mazuri ya maji  na mbuga za wanyama ambazo huvutia sana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutoa fursa nyingi za kimaendeleo kwa wawekezaji wa ndani na nje.

Mkoa huu ni kiungo muhimu sana katika historia ya uchumi nchini Tanzania. Kwa upande wa Kaskazini Tanga imepakana na nchi jirani ya Kenya, vilevile imepakana na Mikoa ya Kilimanjaro na Manyara upande wa magharibi, imepakana na Mikoa ya Morogoro na Pwani upande wa kusini na upande wa Mashariki imepaka na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Kuwepo kwa miundo mbinu mizuri ya barabara, reli, bandari na usafiri wa anga vyote kwa pamoja vinauweka Mkoa wa Tanga katika nafasi nzuri ya kuwa miongozi mwa Mikoa ambayo mtu mmojammoja au mashirika huvutiwa kuwekeza. Ni fursa hizi zote pamoja na ushirikiano mzuri wa wadau mbalimbali, wananchi na Serikali, Mkoa umeweza kupiga hatua katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiulinzi, kitekinologia, kimazingira na kiutamaduni.

Wakazi wa Tanga pia wamepata fursa ya kufikiwa na huduma za kijamii kwa wepesi zaidi kutokana na kuwa na usafiri wa uhakika. Jambo hili limesaidia kuokoa muda na hivyo wananchi kujishughulisha na uzalishaji badala ya kutumia muda mwingi njiani kwenda kufuata huduma za kijamii kama afya n. k.

Barabara ya Tanga –Horohoro ni barabara yenye kiwango cha lami na urefu wa kilometa 65 ambayo inaunganisha Mkoa wa Tanga na Nchi jirani ya Kenya. Ikianzia kutoka Wilaya ya Tanga inaunganisha  Wilaya ya Mkinga  na kisha kuunganisha nchi ya Kenya. Wakazi wa Tanga kwa sasa wana fursa ya kusafirisha mazao yao ya biashara katika Wilaya zilizotajwa na pia kuyapeleka mazao yao  nchi jirani ya Kenya. Hivyo kupanua wigo wa masoko ya biashara kwa wakazi wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete  ( Mwenye koti la blue bahari) akiwa na Mwenyeji wake  Mhe. Chiku Gallawa  ( wa tatu kushoto kwake ) wakati wa ufunguzi wa barabara ya Tanga- Horohoro  eneo la Kasera Wilayani Mkinga mwezi Aprili mwaka huu.
Nayo barabara ya yenye kilometa 65 kwa kiwango cha wami inayounganisha Wilaya ya Handei na Korogwe ambayo iko mbioni kukamilika inategemewa kuwa kiungo kikubwa cha usafiri na hivyo kuboresha maisha ya wakazi wa Tanga na wawekezaji.
Barabara ya Handeni- Korogwe yenye kilometa 65 kwa kiwango cha lami.

Uwepo wa Uwanja wa Ndege ambao hurahisisha usafiri wa anga. Wakazi wa Tanga na Wageni huweza kuokoa muda kwa kutumia njia ya anga ambayo hutumia muda mchache kuweza kufika katika maeneo mabalimbali ya Tanzania na nchi zingine. Nayo Bandari ya Tanga ni muhimu sana katika uchumi wa Tanga. Uboreshwaji wake katika  kujenga bandari ya nchi kavu ya Mwambani itasaidia kukidhi mahitaji ya wakazi wa Tanga, Tanzania na dunia kwa ujumla.
Bandari ya Tanga
Jina Tanga lilitolewa na wafanyabiashara wa kishirazi likiwa na maana nne ambazo ni Tambarare, mabonde ya Kijani, Barabra za milima na Kilimo cha Milimani. Mkoa wa Tanga ni mkulima na msafirishaji mkubwa wa zao la Mkonge duniani ambalo ni  muhimili wa kukua kwa uchumi wa nchi ya Tanzania.
Zao la Mkonge
Mkoa wa Tanga una eneo la ukubwa wa quare km 27,342 na jumla ya idadi ya watu 2,045,205 wakiwemo wanaume 992,347 na wanawake 1,052,858 ( sense ya  2012) na una jumla ya Wilaya nane ambazo ni Handeni, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga, Pangani na Tanga Halmashauri za Wilaya, Miji na Jiji zipo 11 ikiwemo mpya ya Bumbuli iliyoanzishwa hivi karibuni.
Kwa kuzingatia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025, ambapo sekta za Viwanda, Biashara na Masoko zinatakiwa kuwa miongoni mwa mihimili mikuu katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa kulifanya Taifa lifikie kiwango cha kati cha maendeleo ya uchumi, Mkoa wa Tanga kwa kutekeleza majukumu yake umeamua kushirikisha Sekta Binafsi katika kuendeleza sekta ya Viwanda, Biashara na Masoko.
Lengo kuu la mkakati huo ni kuongeza ufanisi katika uzalishaji katika mkoa wetu sambamba na kujenga uchumi endelevu, unaostahimili ushindani katika masoko ya ndani na nje ikiwa ni chachu ya kuchochea kasi ya maendeleo kiuchumi.
Kihistoria Mkoa wa Tanga ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, kijerumani na mwishoni Waingereza ukiwa lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu za ndani za Africa Mashariki na Kati na sehemu mbalimbali za dunia kupitia bahari ya Hindi. Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali, wenyeji wa Tanga wamerithi tamaduni, lugha na ustarabu wa mataifa mbalimbali ya Washirazi, Waarabu , Wachina, Wahindi, Wareno, Wajerumani, Waingereza na Waswahili.

 

0 comments

Raia wa Rwanda ateswa na kuachiliwa Uganda


 Raia wa Rwanda ateswa na kuachiliwa Uganda

Mkimbizi mmoja raia wa Rwanda ambaye alitoweka nchini Uganda wiki iliyopita amepatikana akiwa hana ufahamu baada ya kuteswa.

Maafisa wa serikali ya Uganda wanasema kuwa waliomteka Pascal Manirakiza, walimdhulumu kabla ya kumuacha karibu na eneo la makaburini mjini Kampala.
Bwna Manirakiza, alikuwa mmoja wa raia wa Rwanda ambao waliiambia BBC kuwa wanatafuta hifadhi nchini Uganda mwezi uliopita.

Wakimbizi hao wameishutumu jeshi la serikali ya Rwanda kwa kuwasajili kwa lazima kupigana katika vita vinavyoendelea Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hata hivyo jeshi la Rwanda limepuuzilia mbali madai hayo, na kusema watu hao wakitoa madai hayo ili kupewa hifadhi nchini Uganda.

Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa uliitisha kufanyika kwa uchunguzi kufuatia kutekwa nyara kwa wakimbizi watatu raia Rwanda nchini Uganda.

Rwanda inakana kuhusika

Serikali ya Rwanda kwa upande wake pia imekanusha kuhusika na utekaji nyara huo.
Polisi mjini Kampala walimpata Bwana Manirakiza, mwenye umri wa ishirini na mitatu, akiwa hana ufahamu karibu na maeneo ya makaburini, alisema afisa mmoja mwandamizi katika ofisi ya waziri mkuu Douglas Asiimwe.


Ramani ya Congo
''Alikuwa na majeraha mengi na kuvuja damu, pia kulikuwa na ishara kuwa walikuwa ameteswa sana'' Alisema Asiimwe.
Manirakiza kwa sasa anapokea matibabu katika hospitali kuu ya taifa ya Mulago mjini Kampala chini ya Ulinzi mkali.

Afisa huyo wa serikali ya Uganda amesema wanatarajia raia huyo wa Rwanda kupona na kupata ufahamu siku chache zijazo ili kuelezea zaidi wale waliomteka nyara.
Wiki iliyopita, mkimbizi mwingine ambaye Umoja wa Mataifa ulikuwa umeelezea wasi wasi kuhusu hali yake, Joel Mutambazi, ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda amewekwa chini ya ulinzi wa ofisi ya rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Wakimbizi wadai kutekwa nyara

Awali, Mutambazi alikuwa amekamatwa na maafisa wa polisi baada ya serikali ya Rwanda kutoa idhini ya kukamatwa kwake.
Umoja wa Mataifa ulipinga kukamatwa kwake na kuitaka serikali ya Uganda kutoa hakikishom kwa wakimbizi wote walioko nchini humo.

Polisi wa Uganda

Serikali ya Uganda imekataa ombi la serikali ya Rwanda ya kutaka afisa huyo wa zamani kurejeshwa Nyumbani.

Mmoja wa wakimbizi hao hajulikani aliko.
Mwezi uliopita, Manirakiza aliliambia BBC kuwa alikuwa mwanafunzi nchini Rwanda na alilazimishwa kujiunga na wapiganaji wa waasi wa M23 nchini Congo, lakini alifanikiwa kutoroka na kutafuta hifadhi nchini Uganda.

Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimeishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo yamepingwa vikali na Rwanda.
Mwaka wa 2010, aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda Faustin Kayumba Nyamwasa alitorokea nchini Afrika Kusini.

Nyamwasa alidai kuwa serikali ya rais Paul Kagame ilikuwa na njama ya kutaka kumuangamiza, baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa mjini Johannesburg.
0 comments

Marekani yapima mikakati ya kijeshi dhidi ya Syria

Marekani yapima mikakati ya kijeshi dhidi ya Syria

Kufuatia shambulizi la silaha za sumu lililoua mamia nchini Syria, yaonekana muda wa kutafuta suluhu ya muafaka umekwisha. Marekani inaona msitari mwekundu umevukwa, na inapima uwezekano wa kuingilia kijeshi. 

Baada ya kutokea shambulizi linalodhaniwa kuwa la kemikali, ambalo liliwauwa mamia ya raia na kujeruhi zaidi ya 3000 nchini Syria kwa mujibu wa shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka, mataifa mengi ya magharibi na hasa Marekani, yanaaamini kuwa rais Bashar al-Assad ndiye anawajibika kwa shambulizi hilo. Kwa sababu kwa miezi kadhaa rais wa Marekani, Barack Obama, alionya kuwa matumizi ya silaha za kemikali yatamaanisha kuwa msitari mwekundu umevukwa, katika mazingira haya, laazima utawala wa Assad uchukuliwe hatua nzito. Kwa mujibu wa vyanzo vya Usalama vya Marekani, Ikulu ya mjini Washington inajadili njia tatu za kuchukuwa.

Eneo la kuzuiwa kuruka ndege linaweza kuwasaidia pakubwa waasi.  
 Eneo la kuzuiwa kuruka ndege linaweza kuwasaidia pakubwa waasi.
 
Eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka

Njia ya kwanza ni kuweka eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka nchini Syria, hii ikimaanisha kuwa Wamarekani watazipiga marufuku ndege na helikopta za utawala katika baadhi ya maeneo. Hii itamaanisha kuwa vikosi vya Assad havitaweza tena kuwashambulia waasi kupitia angani. Hans-Joachim Schmidt, kutoka taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro ya Hessian, anasema hatua hii ingekuwa ya msaada mkubwa kwa waasi kwa sababu "Assad hangeweza kuwashambulia waasi kwa kutumia helikopta na ndege zake za kivita. Hii ingewanufaisha moja kwa moja waasi."


Lakini Paul Rogers, mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka shirika la ushauri la Oxford Reseach Group la Uingereza, anasema Marekani laazima izime mifumo ya ulinzi wa angani ya Syria, jambo ambalo anasema litakuwa ghali na la hatari sana kwa kuzingatia kuwa Urusi iliahidi kuipatia Syria mitambo ya kisasa. Juu ya wasiwasi huo, Hans-Joachim Schmidt anasema ikiwa kweli Urusi imekwisha iuzia Syria mitambo hiyo ya kisasa, basi Wamarekani watapata taabu sana. Lakini anasema haoni uwezekano mkubwa kwa Marekani kutumia mkakati huu, kwa sababu utawavuta zaidi katika mgogoro huu, kitu ambacho serikali ya Marekani haitaki. Wakati huo huo, kanda isiyoruhusiwa kuruka ndege laazima iidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na huko Urusi na China bila shaka zitatumia kura ya turufu kuizuia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.  
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.
 
Mashambulizi dhidi ya maeneo ya kimkakati

Njia nyingine ni kushambulia maeneo ya kimkakati kwa makombora na maroketi kama vile viwanja na njia za kurukia ndege, na hivyo kudhoofisha uwezo wa jeshi la angani la Syria. Marekani ina meli kadhaa za kivita na nyambizi katika bahari ya Mediterannean, ambazo zinaweza kutumiwa kutekeleza mashambulizi ya namna hii na kufanya vigumu kwa ndege kuruka na kutua.


Lakini uharibifu kwa njia za ndege unaweza kukarabatiwa haraka. Schmidt anaiona njia hii kuwa ndiyo yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kutumiwa, licha ya ukweli kuwa nayo itahitaji kuidhinishwa na baraza la usalama. "Wamarekani hawataki kujiingiza moja kwa moja katika mgogoro huu, hivyo shambulio la kijeshi lingekuwa ishara yenye ufanisi, japokuwa yenye mipaka, ya kuzuia matumizi zaidi ya silaha za kemikali," anafafanua mtafiti wa amani na utatuzi wa migoro Hans-Joachim Schmidt.
 
Kuwapatia waasi silaha

Njia ya tatu inaweza kuwa kuwapatia silaha waasi. Hadi sasa Marekani haijawapatia msaada wa silaha waasi, ukiachilia mbali misaada ya kawaida kama vile vifaa vya tiba. Lakini Rogers anasema waasi wamekuwa wakipokea vifaa vya kijeshi kutoka Saudi Arabia na Umoja wa falme za Kiarabu kupitia Uturuki na Jordan. Lakini anasisitiza kuwa uwezekano wa waasi kupatiwa silaha moja kwa moja na Marekani ni mdogo sana, kwa sababu watahitaji kupewa mazoezi kwanza kabla hilo halijafanyika. Hofu nyingine 

 kuhusiana na hili, ni silaha hizo kuangukia mikoni mwa kundi lenye itakadi kali la Al-Nusra Front.

Rais Bashar al-Assad akisalimiana na wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni.  
 Rais Bashar al-Assad akisalimiana na wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni.
 
Na diplomasia je?

Lakini Uingiliaji wa tahadhari bado unabaki kuwa uingiliaji, na kwa hivyo Marekani bado inasita kufanya hivyo, kwa kuzingatia madhara yake. Tayari rais Bashar al-Assad ameonya kuwa hatua yoyote ya kuingilia kati kijeshi itasababisha moto utakaoizingira kanda nzima ya mashariki ya kati. Iran nayo inaweza kuliimarisha kundi la Hezbollah dhidi ya Israel na kundi la Taliban linaweza kuzidisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani.

Schmidt kwa hivyo anapendekeza njia ya nne ambayo haizungumzwi katika vyombo vya habari kwa sasa: Shinikizo la diplomasia. Hata hivyo, mtaalamu huyo anahisi kuwa uamuzi wa kuishambulia Syria kijeshi umekwisha chukuliwa na kinachosubiriwa ni lini na vipi. Kinachoonekana sasa ni kwamba Marekani inatafuta washirika katika operesheni hii.

 

0 comments

WAGOSI WA NDIMA WAJA LEO WARUDI LEO


                          HABARI ZA ASUBUHI TANGA, WAGOSI WA NDIMA WAJA LEO WARUDI LEO



            KUNAPOPAMBAZUKA KILA MMOJA ANATAFAKARI WAPI ATATAFUTIA MKATE                                        WA SIKU, ASUBUHI NJEMA WAGOSI WA NDIMA


                                     
                            SHUGHULI ZA MAENDELEO NAZO KAMA KAWA

                               
                                        MAZOEZI NI MUHIMU
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger