WAZIRI WA FEDHA DK.WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA
Waziri
wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63)
amefariki dunia.
Taarifa za hivi punde zinasema Waziri huyo
wa fedha katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete amefariki dunia
hii leo baada ya kuugua na kulazwa nchini Afrika Kusini.
Mgimwa aliyezaliowa January 20, 1950 na
kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)
alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Binafsi ya Milpark ya nchini humo.
Dk.
Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa
kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2010.
Hospitali
hiyo ya Milpark ndiyo imekuwa ikitumiwa na Serikali ya Tanzania kupeleka watu
wanaoumwa na mtu wa karibuni zaidi kuhudumiwa katika hospitali hiyo ni marehemu
Dk. Sengondo Mvungi.
Tutawapa
taarifa kamili ya Msiba huo mkubwa wakati wowote kuanzia sasa.