Featured Post Today
print this page
Latest Post

MKWASA AWATEMA MWADINI, BANDA NA TSHABALALA STARS KILA MMOJA NA SABABU ZAKE, WENGINE WAGONJWA

MKWASA AWATEMA MWADINI, BANDA NA TSHABALALA STARS KILA MMOJA NA SABABU ZAKE, WENGINE WAGONJWA


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana ofisi za TFF, Uwanja wa Karume                                                                                 
Wachezaji Said Ndemla (kulia) na Simon Msuva (kushoto) wakiwa kwenye basi lao tayari kwa safari ya Uwanja wa Ndege      

 
 KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewaengua wachezaji watano katika kikosi chake kinachoondoka leo jioni kwenda Kampala kumenyana na wenyeji, Uganda mwishoni mwa wiki. 
Stars itakuwa mgeni wa Korongo wa Uganda Jumamosi Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2016 Rwanda.
Na Mkwasa amewaengua beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kiungo Abdi Banda wote wa Simba SC kwa sababu ni majeruhi, wakati Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu na Andrew Vincent wa Mtibwa Sugar wameachwa kwa sababu za kiufundi na Mwadini Ally wa Azam FC ni mgonjwa.
 
Mkwasa ameteua wachezaji 20 wanaoondoka jioni ya leo kwenda Kampala, ambao ni makipa; Mudathir Khamis (KMKM) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga), mabeki ni Juma Abdul (Yanga), Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC) na Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Simba SC) na Deus Kaseke (Mbeya City).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam FC), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ali (Mtibwa Sugar).
Mara baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kurithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuatia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kwanza na Uganda, Mkwasa alitaja kikosi wachezaji 26 na kuwa nacho kambini kwa wiki moja hoteli ya Kiromo, Bagamoyo huku mazoezi akifanya uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
Mbali na wachezaji hao, benchi la Ufundi litaongozwa na Mkwasa, Mshauri wake wa Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, Msaidizi wake Hemed Morocco, kocha wa makipa, Manyika Peter, Mtunza Vifaa Hussein Swedi ‘Gaga’, Meneja Omar Kapilima pamoja na Mratibu Msafiri Mgoyi. Stars inatakiwa kushinda 4-0 Jumamosi ili kusonga mbele CHAN
0 comments

JK ASHUHUDIA KUSIMIKWA CHIFU KINGALU WA 15 KIJIJINI KINOLE.

JK ASHUHUDIA KUSIMIKWA CHIFU KINGALU WA 15 KIJIJINI KINOLE.


01

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia kusimikwa kwa Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 katika kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.

02

Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 akitolewa nje baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kabla hilo kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.

03

Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 akichomeka fimbo yake ya Uchifu kabla ya kuketi  meza Kuu na Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kabla hilo kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.
PICHA NA IKULU
0 comments

MBUNGE WA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI-CHADEMA JOSHUA NASSARI AMALIZA MIKUTANO YA KUHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KWA KUTUMIA CHOPA

Rubani wa Helkopta akimfunga mkanda Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mikutano ya hadhara ya kuhasisha wananchi kujitokeza kujinadikisha katika daftarai la kudumu la wapiga kura.
Wananchi katika kata ya King'ori wakimpokea Mbunge Nassari wakati alipowasili katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji zoezi la uandikishaji .
Kada wa Chadema ,Samwel Nnko akizunumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya King'ori .
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ,akiwa na mtoto aliyevalia fulana iliyoandikwa Dogo Janja jina ambalo Nassari alipewa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliompatia Ubunge,
Mbunge Nassari akiwahutubia wananchi katika kata ya King'ori jimbo la Arumeru Mashariki akihamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Ng'arenanyuki waliofika katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji juu ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura .
0 comments

WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUUNDA KITENGO MAALUMU

WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUUNDA KITENGO MAALUMU


Na Peter Mtulia
Msimamizi wa masuala ya ushiriki wa watanzania wa wizara ya nishati na madini Neema Apson akizungumzia jinsi wizara ya nishati na madini inavyoshiriki katika kuhakikisha taarifa zinawafikia wananchi kwa usahihi kuhusiana na mafuta na gesi katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo. pia wizara hiyo itaunda kitengo maalumu kwaajili ya kusimamia masuala ya gesi na mafuta na kuwajulisha wananchi kushiriki vyema katika nishati zitolewazo hapa nchini.

Mkuu wa Biashara wa British Concil Hugh Penrhyn Jones akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.

 Mratibu wa kitengo cha uwajibikaji wa makampuni na mazingira-kituo cha sheria na haki za binadamu,Wakili Flaviana Charsles akiuliza swali katika mkutano wa kujadili masuala ya mafuta na gesi pamoja na changamoto zake kwa jamii katika mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo ya mafuta na gesi wakimsikiliza mtoa maada katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo)
1 comments

WIZARA YA UCHUKZI WAKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA CHINA

WIZARA YA UCHUKZI WAKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA CHINA


Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Kiwanja cha ndege cha Guang Dong kutoka nchini China, wakati ulipotembelea Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Ujumbe umeonyesha nia kuwekeza katika Viwanja vya Ndege vya Tanzania. (Habari Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).                                                                               

 Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing wakati ujumbe huo ulipokutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing (kushoto), akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi baada ya ugeni huo kukutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi.
0 comments

Coastal Union yajiandaa na mechi ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo

Coastal Union yajiandaa na mechi ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo

unnamed
Kocha Mkuu wa Coastal Union,Jamhuri Kihwelu “Julio”  (kulia) akisisitiza jambo kwa wachezaji wa timu hiyo mara baada ya
kumalizika mazoezi yao juzi kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Picha kwa Hisani ya Coastal Union.
0 comments

Rais Zuma awatembelea waathirika wa ghasia

Rais Zuma awatembelea waathirika wa ghasia

Südafrika Präsident Jacob Zuma
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini

Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini amewaomba raia wa kigeni kubakia nchini humo wakati wakati akikatisha ziara yake ya kiserikali nchini Indonesia kushughulikia wimbi hilo la chuki dhidi ya wageni. 

Wiki tatu za ghasia zinazoongezeka dhidi ya wageni nchini Afrika kusini zimesababisha kiasi watu sita kuuwawa na kuwalazimisha wahamiaji 5,000 kutafuta hifadhi katika makambi ya muda.
Machafuko hayo , ambayo yameanzia katika mji wa mashariki wa bandari wa Durban kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, yanabeba ghasia za hisia za chuki dhidi ya wageni ambazo ziliikumba Afrika kusini mwaka 2008 wakati watu 62 walipouawa.
Xenophobie in Südafrika Raia wa Afrika kusini akishikilia bango linalosema "tupinge chuki dhidi ya wageni".
Katika tukio la hivi karibuni kabisa, polisi jana Jumamosi(18.04.2015) wamesema wageni waliouwawa wamefariki kutokana na kuchomwa visu mjini Alexandra , mji ulioko kaskazini mwa Johannesburg. Eneo hilo linaloishi watu masikini limekuwa lengo ya ghasia nyingi katika siku hiyo, ambapo maafisa wa polisi walifyatua risasi za mipira kuwatawanya watu waliokuwa wakifanya uporaji.
Zaidi ya watu 30 wamekamatwa usiku ya Jumamosi kuzunguka mji wa Johannesburg pekee. Akiwa chini ya mbinyo kuzuwia kurudiwa mauaji yaliyotokea mwaka 2008, Zuma alisafiri kwenda Durban kutembelea kambi wanayohifadhiwa wageni waliokimbia makaazi yao kutokana na ghasia hizo, lakini alikabiliana na mapokezi yasiyokuwa mazuri kutoka kwa kundi lililomsubiri, ambalo lilipaaza sauti, "rudi nyumbani, rudi nyumbani" na umechelewa , umechelewa".
"Kama serikali , hatuwaambii nendeni zenu". Sio kila raia wa Afrika kusini anasema , nendeni zenu". Ni idadi ndogo sana ya watu ambao wanasema hivyo," Zuma amesema katika kambi ya Chatsworth, ambako alikabidhi hundi ya dola 4,100 kuwasaidia wahanga wa ghasia za chuki dhidi ya wageni.
Ameahidi kumaliza ghasia hizo na alilihakikishia kundi hilo la watu kwamba kuna nafasi kwa wageni nchini Afrika kusini. "Hata kama kuna wale wanaotaka kurejea nyumbani, wafahamu kwamba wakati tutakapositisha ghasia wanakaribishwa kurejea, " Zuma amesema.
Gewalt gegen Ausländer in Südafrika geht weiter Mkaazi wa Afrika kusini akiwa na gongo na ngao tayari kwa mapambano na wageni
Zuma afuta ziara
Kiongozi huyo wa Afrika kusini alitarajiwa kusafiri kwenda Indonesia jana Jumamosi, lakini alitangaza kufuta ziara hiyo "kushughulikia suala hilo nyumbani linalohusiana na mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni."
Uamuzi huo umekuja wakati hali ya tahadhari inaongezeka nchini Afrika kusini---na kutoka Umoja wa Mataifa pamoja na miji mingine mikubwa-- kuhusiana na mashambulio hayo.
Nchi jirani za Zimbabwe , Malawi na Msumbiji zimetangaza mipango ya kuwaondoa raia wake. Ikiakisi wasi wasi wa kimataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema wahanga wengi walioshambuliwa, "ni wakimbizi na wanaohitaji hifadhi ya kisiasa ambao wamelazimika kukimbia nchi zao kutokana na vita pamoja na kukamatwa."
Kinachoelekezewa kidole cha lawama kwa kiasi kikubwa kutokana na ghasia hizo ni hotuba mwezi uliopita iliyotolewa na mfalme Goodwill Zwelithini, kiongozi wa kabila la Wazulu, ambapo amewalaumu wageni kutokana na kiwango cha juu cha uhalifu nchini Afrika kusini na kusema ni lazima"wafunge virago na kuondoka".
Südafrika Fremdenfeindliche Ausschreitungen Mhamiaji akikimbia wakati polisi akijaribu kuzuwia ghasia hizo
Mfalme huyo amekuwa akisema maneno yake yametafsiriwa vibaya.
Wakati mzozo huo ukiendelea, Zuma ameyataka makanisa yote kufanya sala maalum kwa ajili ya amani na urafiki leo Jumapili.
"Tunafahamu kwamba wengi wa watu wetu wanaamini kuhusu haki za binadamu na amani na kwamba wanaheshimu utu wa kila mtu anayeishi katika nchi hii," amesema katika taarifa iliyotolewa jana Jumamosi.
"Wanafahamu kwamba mahali palipo na hali ya wasi wasi na tofauti, haya yanaweza kutatuliwa kwa njia ya Afrika kusini, kupitia majadiliano, na sio kupitia ghasia na ukandamizaji."
Hasira miongoni mwa mataifa jirani na Afrika kusini
Ghasia hizo zimezusha hasira katika mataifa mengine ya Afrika.
Nchini Msumbiji kundi la watu wapatao 200 siku ya Ijumaa lilizuwia kivuko cha kusini kati ya nchi hizo cha Lebombo, wakirusha mawe dhidi ya magari ya Afrika kusini.
Südafrika Fremdenfeindliche Ausschreitungen Kundi la raia wa kigeni likijaribu kujilinda
Nchini Zambia , redio inayomilikiwa na mtu binafsi ilisitisha kupiga muziki wa Afrika kusini katika hatua ya kupinga mashambulizi hayo dhidi ya wageni. Na katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, waandamanaji walifika katika ubalozi wa Afrika kusini kulaani kile walichokiita "mauaji ya kiwendawazimu na ya kikatili" dhidi ya Waafrika wenzao.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amelaani ghasia hizo siku ya Jumamosi, akielezea "hali ya kushitushwa na kuchukizwa".
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger