Featured Post Today
print this page
Latest Post

LOWASSA ATOBOA SIRI..BARAZA LA MAWAZIRI LILIMPINGA

LOWASSA ATOBOA SIRI..BARAZA LA MAWAZIRI LILIMPINGA

WAZIRI Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema Baraza la Mawaziri, lilimpinga asisafirishe maji kutoka Ziwa Victoria hadi wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Amesema kwamba, siku aliyowasilisha wazo hilo katika baraza hilo, mawaziri wote walimpinga, isipokuwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mohamed Seif Khatib.

Lowassa alitoboa siri hiyo jana, alipokuwa akizungumza katika harambee ya uchangiaji wa Shule ya Msingi ya Kanisa la AICT, Kahama, Shiyanga.

Pamoja na hayo, alisema anayetakiwa kupongezwa katika mradi huo ni pamoja na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kwa kuwa alishiriki kuufanikisha.

“Niwapeni siri moja, nilipendekeza waraka wa kutumia maji ya Ziwa Victoria kwa Rais Mkapa, naye akaniuliza, wale wakubwa tutawaweza? Nikamwambia tutawaweza, akauleta katika Baraza la Mawaziri.

“Kule mawaziri wote waliupinga, kasoro Rais Kikwete, ambaye wakati ule alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje pamoja na rafiki yangu, Mohamed Seif Khatibu.

“Mzee Mkapa baada ya kusikiliza mawazo yote, akaamua fedha zitolewe, na sasa mnafaidi maji safi kutoka Ziwa Victoria,” alisema Lowassa.

Ufafanuzi huo aliutoa baada ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, kumsifu Lowassa kwa kuleta maji mkoani humo, ambapo alisema wananchi wa Shinyanga wanayaita maji hayo kwa jina la Malowassa, yaani maji ya Lowassa.

Pamoja na hayo, wakati msafara wa Lowassa unaingia wilayani Kahama, wananchi walijaa barabarani na kumshangilia, huku baadhi wakionyesha maji kama ishara ya kutambua mchango wake katika maji hayo.

Lowassa, ambaye wakati maji yanapelekwa Shinyanga alikuwa Waziri wa Maji na Mifugo, alisema wakati alipokuwa katika juhudi za kupinga mkataba wa zamani wa kimataifa unaoipa Misri haki miliki ya maji ya Mto Nile unaoanzia Ziwa Victoria, alikwenda kwenye mkutano wa maji mjini Cairo, ambako alikutana na mambo mawili makubwa.

"Wakati nateremka pale airport, nilikuta ulinzi wa hali ya juu sana, nikauliza iweje mimi waziri tu nipewe ulinzi namna hii! Mwenyeji wangu akatabasamu tu.

“Siku ya pili yake, nikaenda kwenye mkutano na waandishi wa habari, sijawahi kukutana na idadi kubwa namna ile ya waandishi wa habari, wakati ule wao walikuwa wanamjua Mwalimu Nyerere na timu ya Simba tu ambayo iliwafunga, sasa walitaka kumjua huyo Lowassa ni nani mwenye jeuri na nguvu ya kutaka kutumia maji haya.

“Wakaniuliza, kwa nini nataka kutumia maji yale wakati kuna mkataba unaozuia, nikawaambia, kule Tanzania kuna watu wanakaa umbali wa kilomita tano tu kutoka ziwani, lakini hasa kina mama wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 20 kwenda kutafuta maji.

“Baadaye nikawaambia, tutayachota maji yale, mtake msitake, wakashangaa, nikaondoka na sasa mnaona faida ya msimamo wangu," alisema.

Awali, Mgeja aliwapiga vijembe wanasiasa wanaompiga vijembe Lowassa, kwa kusema kuna kikundi cha wanasiasa wahuni wanaomuonea wivu Lowassa.

"Kundi hili lishindwe na lilegee kwa jina la Yesu," alisema Mgeja, huku akishangiliwa na waumini, ambapo alimfananisha Lowassa na mto mkubwa Kkama Ruvu na kwamba hakuna anayeweza kukinga mikono kuzuia kasi ya maji yake.

Katika harambee hiyo, Lowassa alichangisha zaidi ya Sh milioni 220, zikiwamo ahadi na fedha taslimu, japokuwa malengo yalikuwa ni kupata Sh milioni 150.
0 comments

WAPINZANI WAMZUIA KIKWETE KUSIGN MUSWADA WA KATIBA

WAPINZANI WAMZUIA KIKWETE KUSIGN MUSWADA WA KATIBA


Wasema akisaini Muswada wa Katiba machafuko yanaweza kutokea

VYAMA vya upinzani nchini, vimeamua kuungana ili kunusuru mchakato wa Katiba mpya. Msimamo huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam, wakati wenyeviti wa vyama hivyo ngazi ya taifa, walipofanya mkutano na waandishi wa habari.

Vyama vilivyofikia uamuzi huo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilichowakilishwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, Chama cha Wananchi (CUF), kilichowakilishwa na Profesa Ibrahim Lipumba na Chama cha NCCR- Mageuzi, kilichowakilishwa na James Mbatia.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, aliyesoma tamko lao ni Profesa Lipumba, ambaye alisema ushirikiano wao umelenga kuhakikisha Katiba mpya inapatikana kwa maslahi ya Watanzania.


Alisema kwamba, ushirikiano huo umetokana na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kupitishwa bungeni Septemba 6, mwaka huu, kwa nguvu na wabunge wa CCM.

Alisema kuwa, muswada huo ulipitishwa ukiwa na kasoro mbalimbali, zikiwamo za CCM kuingiza vipengele bila kufuata utaratibu kwa maslahi yao na pia wananchi wa Zanzibar hawakushirikishwa ipasavyo.

“Muswada uliopelekwa bungeni, uliongezwa vifungu vingi ambavyo havikuwamo katika rasimu iliyopelekwa katika Serikali ya Zanzibar, kitendo hicho kinadhihirisha udanganyifu katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika suala la Katiba ya nchi inayotokana na wananchi.

“Sasa, yaliyojiri bungeni kwa siku tatu kuanzia Septemba 4 hadi 6, mwaka huu na yale yanayoendelea kusemwa na Serikali pamoja na CCM, ni mkakati wa kupitisha Katiba ambayo haikutokana na wananchi. Kwa maana hiyo, wenye nia njema na nchi, waunge mkono tamko hili,” alisema Profesa Lipumba.

Kutokana na kutoridhishwa na mchakato huo, wanasiasa hao walimtahadharisha Rais Jakaya Kikwete, asisaini muswada huo kwa kuwa marekebisho yaliyofanyika na taratibu zilizotumika kuupitisha, zilikwenda kinyume cha majadiliano na vyama na wadau yaliyofanyika mwaka 2011 na 2012.

Pia walimtaka Rais Kikwete kuurejesha muswada huo bungeni, ili ukafanyiwe marekebisho yatakayojenga tabia ya kuaminiana ili kuleta muafaka wa kitaifa wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

“Tunaanza kuunganisha umma ili kufanya uamuzi mzito wa kunusuru mchakato wa Katiba mpya, ambao unaendelea kutekwa na kuhodhiwa na CCM na tunafanya hivyo kwa kuwa madaraka na mamlaka yote yapo kwa wananchi ambao Serikali inawajibika kwao,” alisema Profesa Lipumba.

Ili kuonyesha kuwa wapinzani hao hawaridhishwi na mchakato wa Katiba mpya, alisema Septemba 21, mwaka huu, utafanyika mkutano wa hadhara wa pamoja eneo la Viwanja vya Jangwani, Dare es Salaam.

Alisema mkutano huo utakuwa ni hatua ya mwanzo ya ratiba za vyama hivyo kuzunguka nchi nzima kuelezea masuala mbalimbali yanayohusu mchakato wa Katiba mpya.

Akizungumza baada ya tamko hilo, Mbatia alisema kama Rais Kikwete ataridhia mchakato huo haramu, uamuzi wake utakuwa ndiyo chanzo cha machafuko nchini.

Alimtahadhirisha Rais Kikwete asiusaini muswada huo kwa sababu anaweza kuandika historia mbaya ya jambo alilolianzisha kwa nia nzuri.

“Mkono wa Rais Kikwete ambao utashikilia kalamu, ndio utakaokuwa na hatma ya taifa hili, anaweza kujenga historia mbaya ya jambo ambalo amelianzisha mwenyewe, ninamuomba aweke maslahi ya taifa mbele kuliko chama chake.

“Mkono wake ukithubutu kusaini muswada huo, ajue ndio mwanzo wa machafuko, tunajua wapo wanaosema anakiharibia chama chake, lakini ajue tunampa ushauri wa bure ili atambue hagombei tena, hivyo hakuna sababu ya kuogopa mtu.

“Tunataka Katiba ya miaka 50 hadi 100 na ifahamike kwamba, Watanzania hawajawahi kuandika Katiba yao, hatutaki CCM kuhodhi na kuifanya ni mali yao.

“Itakumbukwa kwamba, Muungano wa Tanzania na Zanzibar ni tendo la siasa la maridhiano, hivyo hivyo tendo la Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kati ya CCM na CUF lilifanyika kisiasa na ni la maridhiano.

“Tunaomba CCM waweke itikadi zao pembeni na wote tuseme Tanzania kwanza, siasa baadaye, maslahi ya taifa kwanza, chama baadaye, kwa kauli hiyo, tutapata Katiba mpya.

“Sisi tunashukuru Tume ya Jaji Warioba, kwani imefanya kazi nzuri na kuchukua mawazo ya kila kundi na vyama, yakiwamo ya Serikali tatu, sasa bila vyama vya siasa kuyasimamia haitapatikana Katiba ya Watanzania,” alisema Mbatia. 

Source:Mtanzania
0 comments

SHABIKI WA RICK ROSS AZIMIA BAADA YA KUKUTANA FACE TO FACE

SHABIKI WA RICK ROSS AZIMIA BAADA YA KUKUTANA FACE TO FACE


Rick Rozay is so fine he’s got chicks dropping like flies.
Earlier this week, Rick Ross and the MMG crew were doing a signing for their Self Made, Vol. 3 collaborative LP when a female fan came up and went crazy for Rozay. She approached the table and said, “You so sexy!” before falling to the floor were she stayed laid out for a few records.
Ross reacted by saying, “She alright? She just fainted….” but no one was really checking to see if she was okay. A few minutes later, she popped back up and said, “This is ain’t fake. This is real” and blew kisses.
Now, I don’t know if we can take this too serious since it was filmed by Rick Ross’s MMZ, the Maybach Music version of TMZ. Sounds like some random foolery to promote the new album, but for entertaining purposes, peep it below
0 comments

ZANZIBAR HAPAKALIKI...VIONGOZI WA DINI WAHOFIA ROHO ZAO

ZANZIBAR HAPAKALIKI...VIONGOZI WA DINI WAHOFIA ROHO ZAO

Na Imelda Mtema
HAKUNA lugha nyingine zaidi ya kusema Zenji (Zanzibar) sasa hapakaliki hasa kwa viongozi wa dini, achilia mbali raia wa kigeni kufuatia kushamiri kwa vitendo vya kuwadhuru kwa tindikali au silaha, Ijumaa Wikienda lina mfululizo wa mikasa na ifuatayo ndiyo ripoti kamili.
Padri Joseph Onesmo Mwang’amba akiwa hospitalini baada ya kumwagiwa tindikali.
Ukiachilia mbali mnyororo wa matukio hayo yaliyosababisha  makovu, ulemavu na vifo, tukio ambalo halijapoa ni la Ijumaa iliyopita ambapo Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Machui, Zanzibar, Joseph Onesmo Mwang’amba (60) kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
Tukio hilo lenye kuunga na mengine nyuma, lilijiri nje ya duka la huduma ya mawasiliano ya intaneti la Shine Shine lililopo Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar ambako padri huyo alikwenda kuperuzi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Afande Haji Hana alikiri kutokea kwa tukio hilo ambalo lilimfikisha mtumishi huyo wa kiroho kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja ambako anaendelea na matibabu.
Shehe Fadhil Suleiman Soraga baada ya kumwagiwa tindikali.
Tindikali hiyo ilimjeruhi padri sehemu za usoni, kifuani na mkono wa kulia.
Novemba 6, 2012; Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shehe Fadhil Suleiman Soraga alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana. Alijeruhiwa usoni na mwilini.
Desemba 26, 2012; watu wasiojulikana wamlipiga risasi Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Michael, Mpendae mjini Unguja na kumjeruhi vibaya.
Padri Ambros Mkenda akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi.
Faza Mkenda alipigwa risasi nje ya nyumba yake. Alikimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Unguja na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Februari 2013; Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa akiwa kwenye gari akielekea kanisani kuongoza ibada.
Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi aliyeuawa kwa kupigwa risasi.
Mei 23, 2013; Sheha wa Tumondo, Mohamed Omar Said alimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana. Alipata majereha sehemu ya kifuani na jicho la kulia na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Agosti 8, 2013; wasichana wawili raia wa Uingereza, Kate Gee (18) na Kristie Trup (18) walimwagiwa tindikali wakiwa katika matembezi ya kawaida Mtaa wa Shangani mjini Zanzibar na kujeruhiwa sehemu za uso na kifuani.
Kate Gee na Kristie Trup waliomwagiwa tindikali wakiwa katika matembezi ya kawaida Mtaa wa Shangani mjini Zanzibar.
Kufuatia mtiririko huo, habari zinadai kuwa hali ya maisha ya Zanzibar kwa sasa si shwari kwani viongozi wa kiimani wamekuwa wakitafakari upya jinsi ya kuishi visiwani humo au kurudi Bara.
Yapo madai kwamba, baadhi ya viongozi hao wa dini na raia wameingiwa hofu na wamepanga kuandamana ili kupinga hali ya hatari inayotokana na vitendo hivyo huku kundi moja lenye imani kali likitajwa kuhusika. Polisi bado inachunguza matukio yote hayo.
Source:Global Publishers
0 comments

Siasa Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja

Siasa Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja


shibuda_962c1.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu, ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya hiyo, Akongeza kwamba jambo la pili ni kwamba Ndugu Abdulrahman Kinana ni rafiki yake wa muda mrefu kwa hata wakati wakisoma shule wote walisoma moshi Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia shilingi Milioni moja "Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja" amemaliza Shibuda.
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MEATU SIMIYU) 

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger