WAUGUZI NA MADAKTARI WASITISHA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA NI BAADA YA HOSPITALI KUKUMBWA NA MAFURIKO
Huu
ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita kati kati ya Hospitali ya
Palestina amapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu
katika kila kona ya Hospitali hiyo
Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha
Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali
Kushoto
ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na
matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali
katika makazi ya watu.
Hii ndio hali halisi ya Chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya Sinza Palestina
Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya Hospital hiyo
Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate hudumiwa
Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
Hapa hata hapapitiki
Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha
Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
Huu
ndio Mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya
hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya Mtaro huo kuziba.Picha zote
Zimeletwa hapa http://kilinyepesi.blogspot.com/ na Dar es salaam yetu
--
--
Mapema
mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini
Dar es salaam kumesababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi
kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara , nyumba za
watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua
hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba
zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014 zimesababisha
usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza -
Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na
kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa maji hayo. Na wengine kukimbia
katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Walikwepa
maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tuu lakini yalikuwa ni Machafu
yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya
maji machafu imepita hapo.
Baada
ya mvua hiyo kwisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya
dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Akiongea
kwa Simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu
mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo
zinanyesha kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao
baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri
wamesema wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji
hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.