Featured Post Today
print this page
Latest Post

ZITTO KABWE ATIMIZA AHADI YAKE,ATAJA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE.

ZITTO KABWE ATIMIZA AHADI YAKE,ATAJA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi.


Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.
  
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
  
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.
  
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.
  
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
  
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,” alisema Zitto.
  
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.
  
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.
  
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.
  
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.
  
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.
  
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).
  
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.
  
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesebu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.
  
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.
  
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini.

0 comments

UTAFIKIRI MAIGIZO KUMBE KWELI,HUYU KIJANA MZURI AJINYONGA UKO MOROGORO!!

UTAFIKIRI MAIGIZO KUMBE KWELI,HUYU KIJANA MZURI AJINYONGA UKO MOROGORO!!


Mwili wa mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja ukining'inia juu ya mti.

 Mwanaume huyu amekutwa amejinyonga usiku wa kuamkia juzi mjini Morogoro. Chanzo cha mtuhuyu kujinyonga hakijafahamika. Kwa mujibu wa askari aliyekuwepo eneo la tukio alidai kwamba askari wa doria waliokatiza kwenye eneo hilo majira ya saa 10 usiku walishuhudia mwili wa mtu huyo ukining'inia juu ya mtu.
 Askari akipanda juu ya mti kwa ajili ya kuushusha mwili wa marehemu.

0 comments

UMESHAWAHI JIULIZA KWANINI BAADHI YA DADA ZETU WAKIPIGA PICHA WANAGEUZA MAKALIO YAO? JIBU HILI HAPA

UMESHAWAHI JIULIZA KWANINI BAADHI YA DADA ZETU WAKIPIGA PICHA WANAGEUZA MAKALIO YAO? JIBU HILI HAPA


Mwanamke anayejiamini huonekana wa Tofauti katikati ya wanawake wengi...
Silaha pekee kubwa anayopaswa kuivaa mwanamke yoyote ni CONFIDENCE...Mwanaume anapoangalia Sifa za nani anapaswa kuwa ubavu wake anaangalia kwanza Sifa Hii...Utashangaa wenzio wote wanawezaje na wewe unashindwa nini,Jibu ndio hilo
Makalio Makubwa bila Confidence ni sawa na Al Shabaab bila Silaha...Inashangaza mwanamke na akili zake anapoteza muda,anajivunia Shape,''Oh nimebarikiwa,Nimejazia,Nna shape ya Ukwee' wakati kichwani zero ana akili za moto kama uji wa ulezi
Hayo Makalio zaidi ya kukalia makochi yangu na kuyazeesha Mapema kwa uzito usio na Maana kuna lipi la zaidi yataniongezea kwenye maisha yangu Labda kama nna mpango wa kufungua bendi ya Baikoko nyumbani kwangu.
Only Cheap girls hukazana kuonyesha jinsi gani Makalio ni dili na kuyatumia kama Kigezo cha kukamata Wanaume Cheap.Mwanaume anayekuwa moved na Mwanamke mwenye Makalio makubwa kama Kigezo pekee lazima akili yake ina ujauzito wa miezi 10 na lazima azae Kibwengo.

A Confident woman is an Asset, An Ass-oriented woman is an asshole!...Umeshawahi kujiuliza kwanini kila wakipiga picha wanaposti Facebook huku wameguza Makalio yao??They are Cheap Girls hunting for CHEAP MEN...Be A Different Woman...Be Confident
0 comments

"SITOI NG'O FEDHA ZA RAMBIRAMBI ZA ASKOFU KULOLA KWASABABU NIMEDHALILISHWA"...MZEE WA UPAKO


"SITOI NG'O FEDHA ZA RAMBIRAMBI ZA ASKOFU KULOLA KWASABABU NIMEDHALILISHWA"...MZEE WA UPAKO

Mchungaji wa Kanisa la GRC, Anthony Lusekelo ‘ Mzee wa Upako’ amesema hatatoa ng’o fedha za rambirambi za Askofu Moses Kulola kutokana na kudhalilishwa kulikofanywa na wahusika wa kukusanya fedha hizo.
Akizungumza na gazeti hili Jumamosi iliyopita kwa njia ya simu, Mzee wa Upako alisema badala yake fedha hizo shilingi milioni 15 sasa zitatumika kutibu maumivu aliyoyapata kutokana na vyombo vya habari kuandika utata juu ya ahadi yake ya kutoa rambirambi hizo.
“Kwanza mimi mtu aliyetajwa kuwa angekusanya fedha hizo ambaye ni Mweka Hazina wa Kanisa la EAGT, Mchungaji Praygod Mgonja  simjui kwa sura, nilishamueleza njia gani muafaka ya uwasilishaji wa fedha hizo, badala yake akatumia vyombo vya habari kunidhalilisha.

“Nilimwambia Mchungaji  Mgonja kuwa shilingi milioni kumi na tano siyo kama shilingi laki tatu; Zinapaswa kuwa na utaratibu unaoeleweka wa kutolewa. Nikamwambia mama Kulola (mke wa marehemu) azifuate mwenyewe ili aniombee baraka, akasema sawa, sasa nashangaa ananidhalilisha,” alisema Mzee wa Upako.
Alisisitiza kauli yake hiyo pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno wa simu kwa mwandishi wa habari hii kuwa hatatoa ng’o fungu lake aliloliahidi.
Aliongeza kuwa kwa sasa ameghairi kutoa fedha hizo kwa kuwa anadhani kuna njama fulani ambazo hakuzitaja na kwamba fedha hizo sasa atazitumia kutibu majeraha aliyoyapata baada ya habari kutoka katika vyombo vya habari.

Gazeti hili wiki iliyopita lilimnukuu Mchungaji Mgonja akisema kuwa hajapokea rambirambi za Mzee wa Upako ambazo ni shilingi milioni 15 na wengine walioahidi akiwemo Mchungaji Josephat  Gwajima aliyeahidi kutoa shilingi milioni 10 na Mchungaji Getrude Lwakatare (shilingi milioni moja) walishatoa.
Udaku Specially Blog
0 comments

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA JENGO LA HUDUMA YA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA RUFAA IRINGA

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA JENGO LA HUDUMA YA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA RUFAA IRINGA

aaaaa_49ee7.jpg

Mke wa rais mama Salma Kikwete katikati akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma leo kabla ya kuzindua jengo la huduma ya wanawake na watoto katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa

a_d85f1.jpg
bb_12ab6.jpg

Mfanyabiashara Salim Asas Abri katikati ambae ni mmoja kati ya wadau wakubwa wa uchangiaji wa maendeleo ya mkoa wa Irionga akiwa katika ufunguzi wa jengo hilo.

cc_79d46.jpg

Dr.Manyama mwenye tai akiwa na wadau wengine wakisimsikiliza Mama Salma Kikwete

Na Francis Godwin Blog
MKE wa Rais mama salma Kikwete amezindua wodi la kisasa la huduma ya wanawake na watoto katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa huku akipongeza jitihada kubwa zilizofanyika katika Hospital hiyo katika kuboresha huduma ya mama na mtoto.(P.T)

Mbali ya kuzindua jengo hilo bado mama Salma Kikwete amewashukia wakazi wa mkoa wa Iringa ambao wanaendelea kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kusaliti ndoa zao na kuwataka kuacha mara moja.
Akifungua wodi hilo leo Mama Kikwete alisema kuwa serikali imelenga kuendelea kuboresha huduma ya afya na kuwa mbali ya kuboresha majengo bado serikali imeendelea kuboresha elimu ya watoa huduma kama njia ya kuboresha zaidi huduma ya afya.
Hata hivyo alisema changamoto za madawa na madaktari serikali itaendelea kushughulika na kuwataka wanawake kuendelea kutumia majengo hayo na kuepuka kuwapeleka watoto kwa waganga wa kienyeji ama wao kujifungulia majumbani .
Kwani alisema kukamilika na kuboreshwa kwa huduma hizo ni kuepusha wazazi na watoto kuendelea kuwa na fikra potofu kuwa watoto wao wamelogwa pindi wanapokosa huku wakiacha kufika hospital na badala yake kwenda kwa waganga wa jadi.
Katika hatua nyingine aliwataka viongozi na wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuyatunza majengo hayo ambayo yamejengwa kwa fedha za wahisani .
" kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuhujumu miundo mbinu ya serikali kwa kuiba vifaa mbali mbali kwa madai kuwa ni mali ya serikali .....hili si jambo jema lazima wote tushirikiane katika vifaa hivyo ambavyo ni mali ya watanzania wote"
Mama Kikwete amesema kuwa kwa upande wake ataendelea kutoa ushirikiano kwa Hospital hiyo katika kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo ya ushauri na kufikisha changamoto hizo sehemu husika.
Japo alisema kuwa suala la uhaba wa madaktari serikali ni suala ambalo tayari serikali imeanza kulifanyia kazi ni pamoja na kuendelea kuongeza madaktari katika kuwapa mafunzo madaktari wapya ambao wataweza kuongezwa katika Hospital hapa nchini.
Alisema kuwa maambukizi ya UKIMWI Iringa ni asilimia 9.1 ambapo ni sawa na watu 9 kati ya 100 mkoani Iringa wameathirika idadi ambayo ni kubwa kuliko ile ya taifa ya wastani wa watu 5 ambao wameathirika hivyo mkoa wa Iringa bado upo juu kwa maambukizi hayo.
" Watu wa Iringa ari zaidi nguvu zaidi mmeiwaka katika maambukizi ya UKIMWI hivyo nawaombeni sana watu wa Iringa kujilinda zaidi na kuepuka kusaliti ndoa zenu na wale ambao bado kuona ama kuolewa basi kujiheshimu zaidi"
Pia aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara na wale ambao watabainika wameathirika wasisite kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI na kuachana na tabia ya kuacha matumizi ya dawa hizo.
Huku wale ambao bado hawajaambukizwa basi kutulia na kujilinda ili wasipate maambukizi hayo na kuwaomba wanawake wajawazito ambao watakubwa na maambukizi ya VVU basi kufika Hospital na kupima ili kuwezesha watoto kuzaliwa bila maambukizi.
Wakati huo huo mama Kikwete aliwataka wanaume ambao bado kupatiwa huduma ya Tohara kujitokeza kufanyiwa huduma hiyo ili kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger