Featured Post Today
print this page
Latest Post

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MIZENGO PINDA ALIVYOZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI KTK HOTELI YA MKONGE JIJINI TANGA.

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MIZENGO PINDA ALIVYOZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI KTK HOTELI YA MKONGE JIJINI TANGA.

WAZIRI MKUU MH, MIZENGO PINDA AKITOKA NJE YA UKUMBI WA HOTELI YA MKONGE BAADA YA KUTOA HOTUBA KTK UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI.

MKUU WA WILAYA YA HANDENI MH, MUHINGO RWEYIMAMU ALIYEVAA SUTI NYEUSI AKITOA MAELEKEZO KWA MMOJA WA RAIA AMBAYE AKUFAHAMIKA UTAIFA WAKE KUHUSU FULSA ZA UWEKEZAJI ZINAZOPATIKANA KTK WILAYA YA HANDENI


0 comments

MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA MKOANI TANGA.

MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA MKOANI TANGA.


Mhe. Peter Kayanza Pinda , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika Mkoa wa Tanga kwa ajili ya Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini litakalofanyika Septemba 26-27 mwaka huu. Mara baada ya Mapokezi Mhe. Pinda atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Tanga katika ukumbi wa mikutano wa Tanga Beach resort.

 Mhe.  Pinda akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa

3 &4 Mhe. Pinda  akisalimiana na Viongozi wa ngazi za juu katika Mkoa wa Tanga.



.Mhe. Mizengo Pinda akifurahia burudani ya vikundi mbalimbali ( havipo pichani) mara tu baada ya kuwasili katika Mkoa wa Tanga. ( wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Ndedego na kulia kwake ni Mama Pinda , mke wa Waziri Mkuu Mhe . Pinda.

6&7. Burudani mbalimbali. Picha zote na Monica Laurent, Afisa Habari Mkoa wa Tanga.

0 comments

STAA WA BIG BROTHER MWISHO MWAPAMBA AELEZEA JINSI ANAVYO BAGULIWA NAMIBIA

STAA WA BIG BROTHER MWISHO MWAPAMBA AELEZEA JINSI ANAVYO BAGULIWA NAMIBIA

STAA wa Shindano la Big Brother, Mwisho Mwampamba, amesikitishwa na vitendo vya ubaguzi alivyofanyiwa na Polisi wa nchini Namibia, anakoishi na mkewe, Meryl Shikwambane, ambapo walimfuata kwenye nyumba yake na kumtaka aondoke nchini humo.

Mwisho ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akisema nchi hiyo sasa hivi imekuwa kama Afrika Kusini, ambako wageni, hasa wenye ngozi ya Kiafrika, hupata shida ya kuishi kutokana na kubaguliwa.

“Mimi nimeoa mtu wao na nimezaa naye mtoto, nashangaa kubaguliwa na polisi hao, pia inashangaza kuona wakiwahudumia vyema wageni kutoka barani Ulaya, lakini sisi Waafrika wenzao tunabaguliwa,” alisema Mwampamba.

Mkali huyo ameshangazwa kupewa hati ya kuishi nchini humo kwa miezi miwili pekee, wakati ameoa mwanamke wa nchi hiyo, huku akipata shida hiyo hata mipakani.
0 comments

HAYA KWELI MAJANGA:BAADA YA MASOMO KUWACHOSHA WANAFUNZI WA SECONDARY WAVUA NGUO WAKIWA DARASANI.

HAYA KWELI MAJANGA:BAADA YA MASOMO KUWACHOSHA WANAFUNZI WA SECONDARY WAVUA NGUO WAKIWA DARASANI.

The lamentations of parents of this generation is simply that students have lost focus in every sphere of life. One major obvious screen to watch the decadence is the results they push out these days. What has taken over the minds of these young ones is simply the internet and the dirty displays they see on TV, and this has no doubt created such a picture as this. What is your take?
0 comments

MMOJA WA MAGAIDI WA AL SHABAAB ALIKUWA AKIONGEA KISWAHILI KIZURI KABISA.

MMOJA WA MAGAIDI WA AL SHABAAB ALIKUWA AKIONGEA KISWAHILI KIZURI KABISA.

INGAWA duka la Westgate liko karibu dakika 15 tu kutoka nyumbani kwangu, nilikuwa nikienda kule kwa nadra kununua vitu. Mara kwa mara huwa kuna watu wengi katika duka hili katika siku za mwisho mwa wiki na hivyo niliona kama karaha. Jumamosi ilikuwa maalumu kwa sababu nilitaka kutumia muda wangu na mkwe yangu, Amina (si jina halisi) na baadhi ya marafiki zetu ambao watoto wao walikuwa wakishiriki katika shindano la upishi.


Tulikuwa juu ya ghorofa la mwisho saa 5.00 asubuhi. Shindano la upishi lilikuwa likiendelea. 

Baada ya muda, Amina aliamua kuelekea chini kwa ajili ya kununua vitafunwa. Sikuwa na njaa sana hivyo niliamua kubaki hapo hapo. Nilitaka kuangalia watoto wakipika.

Karibu saa saba na robo, Amina alikuwa hajarejea nilipokuwa, lakini sikuwa na hofu na nilibakia hapo hadi niliposikia sauti ya milio ya bunduki.

Nilishikwa na kihoro na kumpigia simu mwanangu. Ni ofisa usalama na nilidhani pengine angeweza kusaidia.

“Kuna milio ya risasi hapa. Naweza kusikia milio ya risasi. Tafadhari fanya unaloweza,” nilimwambia.

Niliongea naye kwa muda mfupi kwa simu kwa sababu nilitaka kuzungumza na mkwe wangu. Katika simu aliniambia kuwa alikuwa amejificha katika benki iliyo kwenye kituo hicho cha biashara. Alisisitiza kwamba yu salama na alitaka niwe mwangalifu.

Mazungumzo yetu yalihitimishwa ghafla nilipoona watu wawili wakija juu. Walikuwa na bunduki na haikunichukua muda nikaona mabomu ya kutupwa kwa mkono yakining’inia katika mikanda yao.

Nyuso zao hazikufichwa na tuliziona wazi kana kwamba walikuwa hawajali iwapo tungeweza kuwatambua baadaye. Mara moja nilianza kuwa na wasiwasi huenda nisitoke hai.

Katika kitambo hicho, hofu yangu ilikuwa kubwa. Magaidi walipoanza kurusha risasi na magurunedi holela, umati ukaangua kilio kwa kihoro. 

Watu walianza kukimbia kwa mshtuko huku mwelekeo wao ukiwa haueleweki. Nami nilikimbilia katika hema lililokuwa likitumika kama jiko la watoto na kujificha humo.

Awali nilidhani walikuwa wakifyatua risasi kwa bahati mbaya. Hata hivyo, punde nikaona kwamba wale watu waliokuwa wakikimbia huko na huko wakipiga kelele ni wale waliokuwa wamepigwa risasi. Huku kukiwa na makelele, niliwasikia magaidi wakiwaita Waislamu:

“Kama ninyi ni Waislamu, mnaweza kunyanyuka na kuondoka,” walisema.

Lakini haikuwa rahisi kama ilivyodhaniwa. Waislamu walitakiwa kuthibitisha imani yao. Walitakiwa kutaja jambo fulani kutoka aya za Korani kabla ya kuachiwa. Na hata baada ya hapo bado unaweza kupoteza maisha yako. Mwanamke mmoja ambaye alisema alikuwa Muislamu lakini hakuonekana kuwa Muislamu alipigwa risasi na kufa.

Sina uhakika kwa nini sikutumia dini yangu ili kujiokoa mapema. Pengine ilitokana na hofu. Pengine ilitokana na hali ya ukaidi.

Nikiwa nimejificha nyuma ya maboksi na meza katika hema, watu nisiowajua wakawa wa karibu nami kuliko marafiki. Magaidi lazima walijua tulipo; kulikuwa na maeneo mengi ambayo tungeweza kuyatumia kujificha.

Hata hivyo, tulitulizana wenyewe kwa wenyewe huku tukiwataka watoto wanyamaze kwa sababu sauti zingeweza kutufichua pale tulipo. 

Lakini pamoja na juhudi zetu zote za kuwatuliza wanyamaze, bado baadhi ya watoto hawa hasa wale wadogo walilia.

Tuliomba. Tuliwasilisha maombi yetu kimyakimya kwa Muumba wetu, pengine tukiona hiyo ni siku yetu ya mwisho kuwa hapa duniani.

Tulikuwa tumejificha kwa dakika 20 wakati nilipomsikia mmoja wa magaidi akipokea simu kupitia simu yake ya mkononi. Hakuzungumza kwa sauti kubwa, lakini ilikuwa sauti tulivu ya Kiswahili iliyosikika vema masikioni.

Maneno halisi ilikuwa vigumu kuyakumbuka. Lakini alisema kuwa ameua watu wengi na wengine zaidi walijeruhiwa.

Dakika chache baadaye baada ya kupokea simu, magaidi walirusha risasi ovyo juu ya paa na kuondoka. Nikadhani kwamba milio hiyo ya mwisho ililenga kutuogopesha na kutuonya tusijaribu kuondoka mahali tulipo.

Tuliokolewa muda mfupi baadaye na wakati nikitembea kutoka katia jengo hilo tuliona miili ikiwa imezagaa sakafuni, nilijisikia nisiye na msaada kwamba sikuweza kufanya lolote kuzuia hali hii. 

Nilikuwa huru lakini mkwe wangu alikuwa bado amenasa katika jengo. Nilipompigia simu alinihakikishia kuwa yu salama tena kwa sauti tulivu. Alinitaka nisiwe na wasiwasi, ombi ambalo halikuwezekana kwangu.

Amina aliokolewa saa 12 jioni. Saa kadhaa nikiwa nyumbani kwa mwanangu na kwa rafiki yangu kusubiri neno la matumaini kutoka kwake ilikuwa tete hakika.

Nilifarijika sana wakati alipompigia simu mwanangu akimtaka aende kumchukua kutoka Visa Oshwal.

Saa zaidi ya 24 baada ya ile iliyokuwa siku njema nikiwa na mkwe wangu iligeuka kuwa jinamizi, na bado ninatetemeka nikiikumbuka. Hata hivyo, nina furaha kuwa hai na ninashukuru Amina na mimi tulitoka Westgate bila majeraha.

*Hii ni simulizi ya mmoja wa watu waliookoka katika tukio la ugaidi la Westgate
0 comments

BAADA YA KENYA SASA AL-SHABAAB YAIGEUKIA TANZANIA....WATISHIA KUIVAMIA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

BAADA YA KENYA SASA AL-SHABAAB YAIGEUKIA TANZANIA....WATISHIA KUIVAMIA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi

WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.

Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.

Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio mengine Tanzania na Uganda.

Babile alisema taarifa zinaonyesha vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa watapata utajiri wa haraka.

Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.

“Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao… tumejipanga kuyakabili haya na kuushirikisha umma katika ulinzi,” alisema.

Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote litakalotokea.

“Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.

“Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline officers wetu wako makini mno.

“Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.

“Lakini hata kwenye mipaka yetu yote hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” alisema.

Baada ya kufanya mashambulio mjini Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.

Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho yataelekezwa Uganda na Tanzania.

Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate. 

Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.

“Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi, tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha hakuwa mtu hatari, tukamuachia.

“Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea… lakini tumeangalia taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka,” alisema Babile.

-Mtanzania
0 comments

AGNESS MASOGANGE AAHIDIWA NDOA MARA ATAKAPOTUA BONGO

AGNESS MASOGANGE AAHIDIWA NDOA MARA ATAKAPOTUA BONGO

MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi) yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.
0 comments

FLORA LYMO APOST PICHA ZINGINE NA KUTOA SOMA "HOW TO LOOK SEXY AT HOME' NAOMBENI MATUSI MAPYA PLEASE''


FLORA LYMO APOST PICHA ZINGINE NA KUTOA SOMA "HOW TO LOOK SEXY AT HOME' NAOMBENI MATUSI MAPYA PLEASE''

 HAHHAHAAA''HIVI WALE HUENDA BAHARINI HUWA WANAKWENDA KULE NA MAGUNIA AU  WANAKWENDAGA VIPI JAMANI ''MAANA NAONA NIMEWATETEMESHA SANA LAST WEEK ''BUT KWASABABU WENGI MLIPENDA NIMEONA NIWAONGEZEENI NA HII ITAKUWA FROM NOW 'KILA NITAKAPOJINAFASI WILL POST YOU A NEW SEXY PHOTO'S OF YOUR TOP IN TOWN'FLORA LYIMO FASHION POLICE" LOOK AT ME''' DO I CARE??? RUWA MANGI OTE KAPITSA MBAO''
 LETS NECKED THE ISSUE''MBUTA  NANGA!!  JAMANI JIPENDENI NA KUWENI SEXY AT HOME'''YANI KINA DADA/MAMA'' UKIWA UNAJIPENDA KWANZA NDIPO UNAWEZA KUPENDA VINGINE NA WENGINE'' NA MPENZI WAKO VILE VILE''
  COOL STRORY BRO ''TELL IT AGAIN!! aka.THE KUBWA JINGAAAAA''HIZI PICHA USIPOZIWEKA KWENYE YOUR UCHWARA BLOG' UTANIJUA MIMI MTOTO WA KICHAGGA NISIE OGOPA MTU WALA KITU ''TENA NISIE KWEISHA MAUTAMUU''
NAOMBENI MATUSI MAPYA PLEASE''' YALE MLONITUKANA MBONA YASHAPITWA NA WAKATI? MBUTA NANGA'' FLORA LYIMO FASHION POLICE ANAWAUNGULISHENIJE'' NA BADO MAMBO BADOOO''KUDADAMBIVUUUUUUUUUUU'''
0 comments

LEWANDOWSKI NI KAMA TAYARI AMEKWISHATUA BAYERN, MWENYEWE ASEMA ANAHAMIA BAVARIA JANUARI

LEWANDOWSKI NI KAMA TAYARI AMEKWISHATUA BAYERN, MWENYEWE ASEMA ANAHAMIA BAVARIA JANUARI

MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski hatimaye amethibitisha atasaini kama mchezaji huru kujiunga na wapinzani, Bayern Munich ifikapo Januari na kuhamia Bavaria Mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.  

Goneski: Robert Lewandowski has confirmed his 2014 move from Borussia Dortmund to Bayern Munich
Anaondoka: Robert Lewandowski amethibitisha kuondoka Borussia Dortmund kuhamia Bayern Munich mwakani

Baada ya tetesi kadhaa miezi ya majira ya joto, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 25 ataungana na kabi ya Pep Guardiola, Lewandowski ameacha Mkataba wake umalizike na ataruhusiwa kusaini Mkataba wa awali kujifunga Allianz Arena mwaka 2014.
Kwa mara ya kwanza tangu azuiliwe na kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp aliyegoma kuwauzia silaha yake wapinzani wake wa Bundesliga, Lewandowski amesema atajiunga na Munich kama mchezaji huru.

Akijibu swali kwamba atahamia Signal Iduna Park Januari, Lewandowski alisema: "Ndiyo, kwa sababu baadaye nitasaini Mkataba rasmi,"
Njia iko wazi kwa Lewandowski kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya baada ya kocha wa zamani wa Barcelona, Guardiola kumruhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Mario Gomez kutimkia Fiorentina, na kutoa nafasi kwa mshambuliaji mwingine. 
Goal machine: Lewandowski has scored four goals for Dortmund in six Bundesliga games so far this season
Mtambo wa mabao: Lewandowski amefunga mabao manne Dortmund katika mechi sita za Bundesliga msimu huu
Thumbs up: Bayern manager Pep Guardiola let Mario Gomez go, paving the way for Lewandowski up front
Dole: Kocha wa Bayern, Pep Guardiola amemruhusu Mario Gomez kuondoka, na kutoa nafasi ya Lewandowski kutua

Kuondoka kwa Lewandowski kutaacha pigo katika safu ya ushambuliaji ya Dortmund – ambako amefunga mabao 58 katika mechi 103 tangu ajiunge nayo mwaka 2010 kutoka Lech Poznan ya Poland.
Mwaka jana alifunga mabao 36 katika mashindano yote pamoja na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne katika Nusu Fainali moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu yake ikishinda 4-1 dhidi ya Real Madrid, kabla ya kufungwa na Bayern 2-1 katika Fainali, Uwanja wa Wembley, Mei mwaka huu.
Licha ya Munich kununua zaidi wachezaji bora na wa bei kubwa, bado timu zote zimefungana kileleni mwa Bundesliga baada ya mechi sita, kila timu ikiwa na pointi 16 na kutofautiana kwa wastani wa mabao tu ya kufunga na kufungwa
0 comments

PIGO KWA CHADEMA!!! MWENYEKITI, KATIBU NA WANACHAMA 380 WAHAMIA CCM HANDENI...FUATILIA ILIKUAJE HAPA

PIGO KWA CHADEMA!!! MWENYEKITI, KATIBU NA WANACHAMA 380 WAHAMIA CCM HANDENI...FUATILIA ILIKUAJE HAPA

 
Uongozi wa juu wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Handeni Mkoani Tanga umekihama Chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya na Katibu wake pamoja na wanachama 380 ambao wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)..
 
Tukio hilo linalotoa taswira mbaya kwa CHADEMA  na ishara njema kwa CCM limetokea juzi katika kata ya Kwamatuku, ambapo Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Bulembo alifanya mkutano wake wa hadhara na kupokea wanachama hao wapya wa CCM kutoka CHADEMA.
  
Viongozi hao wa Chadema ni pamoja na Mwenyekiti wa wilaya ya handeni, Luka Selemani, mwenyekiti wa kitongoji cha maguruwe, mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (Chadema) na Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya wilaya. 

Wengine ni Katibu wa wilaya hiyo, Athumani Ngido ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu Taifa na mwenyekiti wa kamati ya utendaji wa Mkoa wa Tanga., Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya wilaya hiyo, Jack son Fransis ambaye pia ni mwenyekiti wa kata ya Kabuku na mgombea udiwani wa Kata hiyo...

  
Mbali na hao, wamo Mwenyekiti wa Tawi la umoja wa Vijana wa Tawi la Kwamatuku, Abrahaman Mtengwa na mjumbe wa kushughulikia migomo ya chama hicho, Juma Mkomba..  
 
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Bulembo alisema kukimbia kwa viongozi na wanachama hao ni ishara kuu ya chama hicho kusambaratika vipande vipande katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu... 
 
Alisema kadiri siku zinavyokwenda Chadema kitazidi kusambaratika kutokana na baadhi ya viongozi wake kukumbatia madaraka huku wengine wakiachwa kuwa wapiga debe.
0 comments

SIMBA SC YAMKANA OKWI, YASEMA ALIKUJA KWA SHIDA ZAKE MWENYEWE DAR, WAO WANATAKA 'HELA' ZA WAARABU TU TAREHE 30

SIMBA SC YAMKANA OKWI, YASEMA ALIKUJA KWA SHIDA ZAKE MWENYEWE DAR, WAO WANATAKA 'HELA' ZA WAARABU TU TAREHE 30

Na Ezekiel Kamwaga,
SIMBA SC imesema kwamba haihusiki na ujio wa mshambuliaji wake wa zamani, Emmanuel Arnold Okwi nchini hivi karibuni na inatambua huyo ni mchezaji halali wa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa sasa.
“Katika siku za karibuni, vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimeripoti kuhusu uwepo nchini wa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu, Emmanuel Arnold Okwi kutoka nchini Uganda,”.
“Taarifa hizo zimeeleza mambo mbalimbali ikiwamo taarifa kuwa Simba Sports Club ina mawasiliano na mchezaji huyo na alikuja kwa mwaliko wa viongozi wa klabu. Baadhi ya vyombo vimekwenda mbali zaidi na kudai kuwa uongozi wa Simba unamshawishi mchezaji huyo avunje mkataba wake na klabu anayoichezea sasa ya Etoile du Sahel  (ESS) ya Tunisia,”.
Alikuja kwa shida zake; Emmanuel Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du Sahel

“Klabu inapenda kuuarifu umma kwamba Simba au kiongozi wake yeyote (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Sekretarieti haijahusika kwa namna yoyote ile na ujio wa mchezaji huyo hapa nchini. Hakukuwepo na mwaliko rasmi au usio rasmi kwa viongozi wa Simba,”.
Simba imesema kwamba taarifa zozote za kuhusisha ujio wa Okwi na uongozi wa Simba ni za upotoshaji na zina lengo la kuharibu heshima na hadhi ambayo uongozi huu umeijenga kitaifa na kimataifa kwenye tasnia ya soka.
Imesema kisheria, Simba haiwezi kumzuia mchezaji huyo kusafiri kwenda nchi yoyote anayotaka kama amefuata sheria zote za uhamiaji kwa kuwa Okwi ana mkataba na timu nyingine na Simba haihusiki na safari zake, matembezi yake au mipango yake ya kimaisha.
Uongozi wa Simba umesema unafahamu kwamba Okwi ni mchezaji halali wa ESS maana wenyewe ndiyo uliomuuza kwa klabu hiyo, hivyo kwa mujibu wa sheria za FIFA, klabu yeyote, ikiwamo Simba SC, haziruhusiwi kufanya mawasiliano na mchezaji huyo au yeyote yule halali wa klabu nyingine bila ruhusa ya klabu yake kama mkataba wa mchezaji husika umebakiza kipindi kinachozidi miezi sita. 
“Hii maana yake ni kwamba uongozi hauwezi kumshawishi mchezaji huyo kujiunga na klabu.
Ikumbukwe kwamba hadi sasa, klabu ya Simba, inaidai klabu ya Etoile du Sahel kiasi cha dola za Marekani 300,000 (laki tatu) ambazo zinapaswa kuwa zimelipwa kabla ya tarehe 30 mwezi huu wa tisa mwaka 2013. Kinyume cha hapo matokeo mengine yataamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya FIFA ambapo makubaliano husika yalisajiliwa,”.
Uongozi wa Simba umeomba vyombo vya habari na watu binafsi waache kutoa taarifa zozote za kuhusisha ujio wa Okwi na klabu au kwamba kuna mipango ya kumshawishi avunje mkataba wake kwani taarifa hizo hazina ukweli wowote.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger