Ufaransa yataka kuepusha kugawika kwa taifa la CAR
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Rais wa Ufaransa ameiambia Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanajeshi wa
Ufaransa walioko huko watafanyakazi kuiepusha nchi hiyo isigawike, na
kuwapokonya silaha wanamgambo na makundi ya wahalifu wanaowapiga vita
Waislamu.
Akiwasili mjini Bangui kutoka Nigeria, alikohudhuria sherehe ya miaka
100 ya muungano wa nchi hiyo, Rais Hollande alikutana na rais wa mpito
wa Jamhuri ya Afrika ya kati Catherine Samba-Panza na pia kuwahutubia
wanajeshi wa Ufaransa. Hii ni ziara ya pili ya Francois Hollande tangu
mwezi Desemba mwaka jana na inakuja wakati kukiwa na ongezeko la
wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Siku ya Jumanne bunge la Ufaransa lilipiga kura kurefusha muda wa
wanajeshi wa Ufaransa nchini humo, licha ya Wafaransa wenyewe kutounga
mkono ushirikishwaji wa wanajeshi wao katika koloni lake hilo la zamani.
Baadhi ya wanajeshi walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema watu milioni moja
wameikimbia nchi hiyo tangu kuanza kwa ghasia za kimadhehebu mwaka
uliopita na kwamba watu wapatao milioni 1.3 wanahitaji msaada wa haraka
wa chakula katika nchi hiyo ya Afrika.
Miezi minne iliopita, Ufaransa ilituma wanajeshi wake ambao kwa sasa
wamefikia takriban 2000 katika nchi hiyo ilio na idadi kubwa ya
Wakristo, na waasi wa Kiislamu wa kundi la Seleka walichukua madaraka
baada ya mapinduzi waliyofanya mwezi Machi mwaka Jana, na wamekuwa
wakisukumwa nyuma na wanamgambo wa kundi la "anti-balaka."
Kando na kuwepo kwa wanajeshi wa Ufaransa, Wanajeshi 6000 wa kulinda
amani wa Umoja wa Afrika (MISCA) pia wapo nchini humo huku takriban
wanajeshi 1000 wa Umoja wa Ulaya wakiwa bado wanatarajiwa kuwasili
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Samba Panza atoa wito wa kuundwa kikosi cha kulinda amani cha U.N
Hata hivyo akizungumza mjini Geneva, baada ya miezi miwili ya kusimamia
shirika la Umoja wa Mataifa la ulinzi wa Raia mjini Bangui, Philippe
Leclerc, amesema bado nchi hiyo haina wanajeshi wa kutosha wa kulinda
amani.
Posted by
Unknown
9:38 PM