Featured Post Today
print this page
Latest Post

SAID MAULID 'SMG' RUKSA KUITUMIKIA ASHANTI UNITED, WAWILI WAPATA ITC KUKIPIGA SAUZI

SAID MAULID 'SMG' RUKSA KUITUMIKIA ASHANTI UNITED, WAWILI WAPATA ITC KUKIPIGA SAUZI

Mchezaji Said Maulid aliyejiunga na Ashanti United akitokea nchini Angola msimu huu amepata ITC ambayo sasa inamwezesha kuchezea timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoingia mzunguko wake wa tatu keshokutwa (Septemba 14 mwaka huu).
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania wawili kucheza mpira wa miguu nchini Afrika Kusini.
Wachezaji hao; Robert Kobelo na Mohamed Ibrahim wamepewa hati hizo baada ya kuombewa na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kama wachezaji wa ridhaa ili wajiunge na klabu ya Cacau United ambayo timu yake inacheza Ligi Daraja la Pili katika Wilaya ya Cacau.
0 comments

MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI AJERUHIWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI...!!

MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI AJERUHIWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI...!!

Mwandishi wa Habari wa kujitegemea mkoani Singida wa Magazeti ya Mwananchi Communications Limited, Awila Silla akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, baada ya kupigwa mapanga na mtu asiyejulikana Jumapili iliyopita, mwaka huu, mjini Singida. Picha na Gasper Andrew. 

 Mwandishi wa Habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti mkoani Singida, Awila Silla amejeruhiwa baada ya kukatwa na mapanga kichwani na  mtu asiyejulikana.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 2 usiku Jumapili iliyopita maeneo ya Utemini ambapo alivamiwa na mtu huyo ambao mbali na kumjeruhi kwa mapanga, pia alimpiga ngumi na mateke na kumjeruhi katika jicho lake la kushoto.

Silla amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida ambapo alifikishwa na kijana mmoja (jina halikumbuki) ambaye alimkuta akiwa hajitambui.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa hana taarifa yoyote na kuahidi kuwa atafuatilia tukio hilo.

Silla ni mwakilishi wa gazeti hili mkoani humo na huandika zaidi Makala za kijamii na kiutamaduni.

Tangu afikishwe katika hospitali hiyo, watu mbalimbali walikwenda kumjulia hali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone.

Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini, Silla alisema, nilikuwa nikirejea nyumbani muda ya jioni nilipofika maeneo ya Utemini simu yake ya kiganjani ikaita na kulazimika kuzungumza ghafla akatokea kijana ambaye alikuwa amejifunika shuka la kimasai na kuanza kumfuata.

 “Nilipogundua yule kijana ananifuata kwa kasi nikaongeza mwendo lakini kila nilipojaribu kumkwepa alizidi kunifuata mpaka nilipofika karibu na uzio wa nyumba moja akanikaribia na kuanza kunivamia kisha kunibamiza katika geti la nyumba hiyo.”

Alisema baada ya kufanikiwa kunidhibiti akaanza kunicharanga na mapanga huku akidai nimpatie pesa, nikamwambia sina pesa lakini cha kushangaza akasema wewe huwa una hela.

Alinishangaza sana, inaonekana kama ananijua, lakini kila nilipokuwa namkaribia ili nimjue vizuri alikuwa anazidi kunisukuma nisimgundue.”

Kwa mujibu wa Silla, mtu huyo alimnyang’anya simu pamoja na mfuko uliokuwa na vifaa vidogo ambavyo alitoka kununua yakiwamo mafuta.
0 comments

MSANII WA BONGO MOVIES LULU APATA VITISHO

MSANII WA BONGO MOVIES LULU APATA VITISHO

Stori:  Jelard Lucas

KUFANIKIWA kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kumemfanya kinda huyo anayetingisha katika tasnia hiyo kupata vitisho kutoka kwa mastaa wenzake.

Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya fani hiyo zinasema katika uzinduzi huo, msanii huyo alifunika na kuonyesha dalili zote za kuwazima mastaa wenzake ambao kwa muda mrefu wamekuwa juu.

Taarifa hizo zinasema staa huyo wa Bongo Muvi anatafutwa kwa kila namna, usiku na mchana ili kuhakikisha nyota yake inafifia.

Madai hayo yamekuja zaidi baada ya uzinduzi huo kufana kwani pamoja na mambo mengine, hata jinsi alivyokuwa amejipanga kwa walinzi wake, lilikuwa ni jambo kubwa ambalo linafanana na inavyotokea katika shughuli za mastaa mbalimbali wa majuu.
Mwandishi wa gazeti hili aliamua kufunga safari hadi maskani kwao pande za Tegeta, lakini msanii huyo hakupenda paparazi afike kwao hivyo mazungumzo yao kufanyika kama ifuatavyo kwa njia ya simu ya kiganjani.

Mwandishi: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Salama tuu za kwako?

Mwandishi: Salama, vipi umesikia vitisho vyako kutoka kwa mastaa wa Bongo Muvi wanaodai kuwa umekuja kuwapita kisanii?

Lulu: Hapana sijasiki, lakini kama wanatoa vitisho lazima wakubaliane na ukweli kwamba lazima awepo wa kwanza na wa mwisho, wakaze buti.
Mwandishi: Umejipangaje kukabiliana na hilo?

Lulu: Najipanga kufanya kazi mimi kama mimi na wao wafanye kama wao, wakijifanya kuwa kama mimi haiwezi kuwa hivyo, mbona mastaa wa ughaibuni kama Beyonce na Rihanna wako tofauti? Lazima awepo wa kwanza mpaka wa 10 hatuwezi kulingana.

Mwandishi: Kuna lolote la kuongeza juu ya hilo ama wito kwa wasanii?

Lulu: Wajipange kufanya kazi kwa nguvu zote, wasifanye kama mimi wafanye kama wao,
Mwandishi: Asante Lulu nakutakia siku njema
Lulu: Ok, sawa kazi njema.
0 comments

WAHAMIAJI HARAMU WAIKOROGA SEREKALI


WAHAMIAJI HARAMU WAIKOROGA SEREKALI

*Taasisi zake mbili sasa zashikana uchawi
*Uhamiaji, RITA waingia katika malumbano
OPERESHENI ya kuwakamata na kuwaondoa wahamiaji haramu nchini, imechukua sura mpya baada ya taasisi mbili za Serikali kuingia katika malumbano. Hatua hiyo imekuja baada ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), kukanusha madai yaliyotolewa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba inachangia uwepo wa wahamiaji haramu.

Hivi karibuni Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo, alisema RITA imekuwa ikitoa vyeti vya kuzaliwa bila kuchunguza taarifa sahihi zinazohusu uraia kwa waombaji.

Idara hiyo ilikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa, kitendo cha RITA kuondoa fomu za uhamiaji zilizokuwa zikitumika kuhakiki uhalali wa mwombaji, kimechangia ongezeko la wahamiaji haramu. 

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko alisema amesikitishwa na taarifa hizo, huku akiitaka Idara ya Uhamiaji kuthibitisha madai hayo.

Saliboko alisema idara hiyo haijaitendea haki RITA kwa kutoa taarifa bubu ambazo hazina uthibitisho juu ya namna wakala huo unavyohusika na tatizo la wahamiaji haramu.

“Hiki si kipindi cha kulaumiana, kila mtu afanye wajibu wake, hizo taarifa kama ni za ukweli busara itumike, Idara ya Uhamiaji ionyeshe uthibitisho juu ya hili badala ya kutoa taarifa za jumla,” alisema Saliboko.

Kuhusu RITA kuondoa fomu ya uhamiaji, Saliboko alikiri kuondolewa kwa fomu hizo na kusema kuwa zilikuwa zinasababisha ucheleweshaji wa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa waombaji.

“Ni kweli tumeondoa hizo fomu, naomba nieleweke vizuri hizo fomu hazikuwa kwenye kanuni zetu.

“Tulifikia uamuzi wa kuziondoa baada ya kuona zinasababisha adha na usumbufu mkubwa wa kutoa vyeti vya kuzaliwa.

“Anapotokea mwombaji ambaye vielelezo vyake vinatiliwa shaka, tunashirikiana na idara hiyo na vyombo mbalimbali vya usalama ili kubaini uraia halisi wa mwombaji.

“Si kweli kwamba tunawapa vyeti wahamiaji, utaratibu wetu kabla hatujatoa cheti kwa mtu mzima huwa tunamuhoji, msajili kama hajaridhika anashirikiana na idara nyingine hadi kupata ukweli,” alifafanua.

Hata hivyo, Saliboko alisema utoaji wa vyeti hivi sasa unafanywa kwa umakini mkubwa kwa sababu baadhi ya wahamiaji haramu wanahaha kutafuta uhalali wa kuishi nchini.

“Tumejipanga vizuri watumishi wa RITA wameongeza umakini zaidi tangu ‘Operesheni Kimbunga’ ianze tofauti na siku zilizopita,” alieleza mtendaji huyo.

Utapeli waingia ndani yake

Wakati operesheni hiyo ikifanyika, kumeibuka wimbi la watu wasiokuwa waadilifu kutumia mwanya huo kwa ajili ya kutaka kujinufaisha kwa kufanya vitendo vya utapeli.

Habari za kuaminika ambazo MTANZANIA limezipata, baadhi ya Watanzania wamekuwa wakiwafuata wahamiaji haramu na kuwatishia kuwa ni watu wa usalama wa taifa. 

“Hawa wahamiaji haramu wanajulikana maeneo wanayoishi na hata wengine biashara zao zinajulikana, sasa kinachofanyika, baadhi ya watu (Watanzania), wanajifanya wao ni watu wa usalama.

“Wanavaa suti wanawafuata wanawatisha wanawauliza vyeti na kuwauliza maswali, wanawachukua katika magari na kwenda kuwatelekeza na kuwaambia hawatakiwi kurudi mjini, huku nyuma wengine wanachukua mali zao,” kilisema chanzo chetu.

Hivi karibuni wahamiaji haramu 465 kutoka mataifa mbalimbali, walikamatwa jijini Dar es Salaam.

Idadi kubwa ya wahamiaji hao ni vijana ambao walikuwa wanajishughulisha na biashara mbalimbali zikiwamo uuzaji kahawa, matunda na maji.
0 comments

Mtanzania anaswa AKILAWITIWA na Mzungu CHOONI.

Mtanzania anaswa AKILAWITIWA na Mzungu CHOONI.

MDOSI au Kanjibai aliyefahamika kwa jina moja la Milah ambaye ni bosi wa kampuni moja ya ujenzi yenye makao yake Mwenge jijini Dar alinaswa chooni akiwa na mfanyakazi wake, John Carlos ‘Shabani’ (watu walimpachika jina la Shabani kutokana na Kanjibai wa kwenye Komedi) ikidaiwa walikuwa katika mazingira ya ulawiti...


Ishu hiyo nzito ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wawili hao walikuwa chooni humo kwa zaidi ya nusu saa na kuwasababishia usumbufu watu waliokuwa wakitaka kutumia choo hicho.

   KISA KILIPOANZA
Siku hiyo ya tukio, mtu mwenye sauti ya kiume alipiga simu kwenye chumba cha habari , Mwenge jijini Dar na kupasha juu ya tukio hilo. Alisema:

Mtoa habari huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuwaambiwa waandishi wetu waliompokelea simu wachukue Bajaj au Bodaboda ili kuwahi.
  
Sosi huyo kabla ya kukata simu aliweka wazi ramani ya kufika kwenye choo hicho na kusisitiza kwamba muhimu kuwahi kwa sababu huenda wanagombana.

Kufuatia msisitizo huo, waandishi  wetu makini  waliwasha pikipiki zao, kila mmoja na yake na kushika njia kuelekea eneo la tukio.
  
Hata hivyo, kwa kuamini wanaweza kukutana na lolote, waliona ni vyema kwanza kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge ambapo walipewa askari wawili kuelekea eneo la tukio.

ENEO LA TUKIO SASA
Timu hiyo iliwasili kwenye eneo la tukio. Mlango wa choo hicho ulikuwa umefungwa lakini kwa mara moja tu haikuwa rahisi kugundua kama ulifungwa kwa funguo au kawaida tu.
  
 Afande mmoja alijitolea kugonga mlango wa choo hicho ili kupima ushirikiano utakaotolewa na wawili hao au mmoja wao.
  
Sauti iliyoonekana ni ya Kanjibai kutokana na kushindwa unyoofu wa lugha ya Kiswahili ilisikika ikiuliza:
“Nani wewee… taka nini huku?”


Afande: Sisi ni askari polisi, fungua haraka tunajua mko wawili humo ndani, fungua.

Kanjibai: Subiri kidogo.
Baada ya dakika kadhaa ,  mdosi huyo alifungua mlango na kukutwa akiwa na ‘Shabani’.


WALICHOKUWA WAKIKIFANYA CHOONI
Katika maswali ya harakaharaka nje ya choo hicho kila mmoja alisema la kwake ambalo aliliamini linaweza kumchomoa kwenye skendo hiyo mbaya.
  
‘Shabani’ alisema yeye aliingia kwenye choo hicho baada ya kuitwa na bosi wake huyo ambapo alishindwa kumkatalia kwa kuogopa kupoteza ajira yake na kama inavyojulikana maisha ya Dar bila kazi ni ngumu kuyamudu.
  

Alipoulizwa walichokuwa wakikifanya ndani ya choo hicho, Shabani alibaki akiwatumbulia macho maafande.
  
Kwa upande wake Kanjibai alipotakiwa kujieleza kisa cha kuingia chooni na mfanyakazi wake, alisema alimuomba wazame humo ili akamnyoe. Yaani Kanjibai alitaka kunyolewa.

IKAFIKA ZAMU YA KUPELEKWA KITUONI
Afande mmoja aliamuru wawili hao wapelekwe kituo cha polisi, lakini kabla ya kuanza safari, mdosi huyo aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali na kutoa vitu vyake kadhaa na kuwakabidhi wadosi wenzake waliofika ‘kumsaidia’ muda mfupi baada ya kunaswa.
  
Halafu aliingiza mkono kwenye mfuko mwingine na kutoa mafuta aina ya KY ambayo mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’ lakini askari alimwambia mafuta hayo yanatakiwa kituoni kwa ajili ya ushahidi hivyo asiwape nduguze.

Breki ya kwanza ilikuwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Mwenge ambapo baada ya mahojiano mafupi walihamishiwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ ambapo walihojiwa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
0 comments

Tundu Lissu atunisha msuli....Akataa uamuzi wa CCM kutaka kuifuta kesi yake.

Tundu Lissu atunisha msuli....Akataa uamuzi wa CCM kutaka kuifuta kesi yake.

WAKATI viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwasili mjini Dodoma kuungana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, katika rufaa ya kupinga ubunge wake inayoanza kusikilizwa leo, mbunge huyo amekataa uamuzi wa CCM kutaka kuifuta kesi hiyo.

Juzi CCM kupitia kwa wakili wake, Godfrey Wasonga, iliwasilisha barua katika Mahakama ya Rufaa Dodoma na nakala kwa Lissu ikiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.
 
  Kwa mujibu wa wakili huyo, sababu ya kuomba kufutwa kwa kesi hiyo ni walalamikaji wote kujitoa na kuapa mahakamani kuwa hawakuwa tayari kuendelea na kesi hiyo.
  
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema kuwa viongozi kadhaa wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, wajumbe wa Kamati Kuu na wabunge kadhaa wa chama hicho tayari walikuwa wamewasili mjini Dodoma.

Hata hivyo, akizungumzia kesi hiyo, Lissu alisema kuwa hatakubali ‘withdrawal’ isipokuwa anataka ‘dismiss with cost’.

Lissu alisema kuwa Wasonga atalazimishwa kulipa gharama kwa kuwa hati ya kiapo cha Selema ni ya mwezi Juni 25, mwaka huu, na kwamba kutaka kuiondoa siku mbili kabla ni uhuni.
  
Shabani Selema na Paskali Hallu ni wanachama wa CCM wakazi wa kijiji cha Makiungu, mkoani Singida, ambao walifungua kesi ya msingi ya kupinga ubunge wa Lissu.
  
Lakini baada ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kumtangaza Lissu kama mbunge halali, walikubaliana na hukumu hiyo ya Aprili 27, mwaka huu.
  
Mara kadhaa wananchi hao wamenukuriwa wakimlalamikia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwa anawashinikiza kuendelea na rufaa hiyo licha ya kwamba walishajitoa.
  
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wasonga, ambaye alikuwa akiwatetea wanachama hao katika kesi hiyo, alisema kuwa baada ya kuwasiliana na wateja wake walimwambia hawakuwa tayari kuendelea na kesi hivyo.
  
“Ni kweli walalamikaji wote wamejitoa na mimi kama wakili sioni haja ya kuendelea; nitakuwa namwakilisha nani?
“Niliongea nao jana hakuna; mwenye nia ya kuendelea na kesi,” alisema.
  
Rufaa hiyo imepangiwa kusikilizwa katika Mahakama ya Rufani na Jopo la Majaji watatu, Salumu Massati, Engela Kileo na Natalia Kimaro.
  
Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo, mahakama ilitarajiwa kusikiliza pingamizi zilizotolewa na upande wa walamikiwa ambao ni Lissu na jamuhuri za kupinga rufaa hiyo na jopo hilo la majaji litatoa maamuzi.
  
Tayari Lissu alitoa hoja saba za kupinga rufaa hiyo, ambazo ni mkata rufaa Seleman ambaye ndiye mlalamikaji namba moja kupinga kwamba hajakata rufaa kwa hati ya kiapo ya Mei 24 mwaka huu.
  
Alisema hoja nyingine ni notisi ya kiapo kutopelekwa kwa mjibu rufaa ambaye ni yeye kinyume na masharti ya kanuni ya 84 (1) ya Kanuni za Adhabu za Mahakama ya Rufaa Tanzania za mwaka 2009.
  
“Vile vile nakala zote rekodi za rufaa hazijathibitishwa usahihi wake na wakata au wakili kinyume na masharti ya Kanuni ya 96 (5) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa Tanzania za mwaka 2009.
  
“Rufaa hii pia imepitwa na muda wake kwa sababu hati ya ucheleweshaji iliyotolewa na Msajili wa Mahakama Kuu haijasainiwa, haina tarehe wala muhuri kinyume na Kanuni ya 90 (1) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania za mwaka 2009,” alisema.
  
Lissu aliongeza kuwa walalamikaji walitakiwa kukata rufaa siku sitini baada ya notisi ya rufaa kutolewa na kwamba tarehe ya mwisho ya kukata rufaa ilikuwa Julai 3 mwaka jana lakini rufaa hiyo ilikatwa Mei 7 mwaka huu.
  
“Hoja nyingine ni kwamba rufaa hiyo si halali kwa kuwa imeacha nyaraka muhimu ikiwemo maombi ya mwenendo wa shauri wa kusamehewa gharama za dhamana,” alisema.

Lissu alisema pia katika rufaa hiyo, amri iliyomshindisha kesi si halali kwa kuwa haionyeshi tarehe ambayo amri hiyo ilitolewa kinyume na kanuni ya 9 ya Kanuni za Masijala za Mahakama Kuu za mwaka 2005.
  
Alisema pia wakata rufaa wamesindwa kuwasilisha mahakamani hoja za maandishi za kuunga mkono hoja za rufaa yao ndani ya siku 60 au kuomba muda wa kuziwasilisha.
  
Pia hoja nyingine ni kushindwa kuwasilisha hoja hizo za maandishi kinyume cha Kanuni ya 106 (1), (2) na (9) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania za mwaka 2009.
  
Kesi ya kupinga ubunge wa Lissu ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012 na Jaji wa Mahakama Kuu, Moses Mzuna, aliyetoa hukumu April 27, mwaka huu, na kumtangaza Lissu kuwa mbunge halali wa Singida Mashariki kwa kigezo kuwa hoja zote zilizotolewa na wanachama hao wa CCM hazitoshi kutengua au kubatilisha ubunge wake.


Tanzania Daima.
0 comments

BINADAMU 200,000 KWENDA KUISHI MILELE KATIKA SAYARI YA MARS KUANZIA MWAKA 2016.

Greda itakavyokarabati ardhi kuwezesha watu kuishi Mars.

Greda itakavyokarabati ardhi kuwezesha watu kuishi Mars
Imesema kuwa mifumo ya kwenda huko itajar
ibiwa mara 8 kabla haijatumiwa kusafirisha watu na kwamba safari itakuwa salama kuliko ile ya kwenda mwezini.article-0-16D5B5EA000005DC-73_634x242

Muonekano wa ardhi.

TIKETI ya one way kwenda kuishi kwenye eneo tasa, lenye ardhi ya ajabu, joto linaloweza kugota 150°C, inaweza isiwe na mvuto kwa wengi, lakini mpaka sasa watu laki 2 kutoka nchi 140 duniani wametuma maombi yao kuwa sehemu ya wakoloni wa kwanza kwenda Mars.


Waombaji wamekubali kuishi kwenye sayari hiyo nyekundu kwa maisha yote yaliyosalia na watashutiwa kwenye reality TV show.

Kampuni ya Uholanzi ya Mars One inajiinda kwenda kwenye sayari hiyo October 2016 kuandaa mazingira na makazi kuwekwa huko mwaka 2018. Chanzo: Bongo5, Chanzo cha awali: Daily Mail.
0 comments

WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUSHUDIA UHAMAJI WA MAKUNDI YA WANYAMA AINA YA NYUMBU KUTOKA HIFADHI YA MASAI MARA KWENDA SERENGETI.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Kayanda Peter Pinda, atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Siku ya Mara, maarufu kama (Mara Day), zinazofanyika katika wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara kuanzia Septemba jana hadi Septemba 15, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, alisema madhumuni ya maadhimisho hayo ni kushuhudia tukio kuu la kuhama kwa makundi makubwa ya nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara kwenda Serengeti.

Alisema lengo jingine ni kuuenzi Mto Mara, ambao asili yake ni kutoka milima ya Mau nchini Kenya na ambao hupitia katika mapori ya akiba na wanyama walioko katika hifadhi hiyo hutegemea maji ya mto huu.

“Kwa kutambua umuhimu wa bonde hilo, kikao kilichofanyika mwaka juzi mjini Kigali, Rwanda kiliamua kila mwaka yafanyike maadhimisho ya Siku ya Mara na mwaka jana wenzetu wa Kenya walifanya sherehe hizi katika sehemu moja iitwayo Muroti na mwaka huu ni zamu yetu,’’ alisema Tupa.

Alifafanua kuwa katika maadhimisho hayo wamealika wageni 110 na kati ya hao wageni 200 watatoka nchi jirani ya Kenya wakiwamo mawaziri wa maji, Tamisemi, Maliasili, Mazingira - Ofisi ya Makamu wa Rais na wadau mbalimbali wa mazingira nchini.

Mkuu huyo alibainisha kuwa faida za maadhimisho hayo ni kuimarisha ushirikiano, uhifadhi wa bonde la Mto Mara, kuleta mwamko kwa Watanzania ili waweze kufahamu uhifadhi na utalii hasa wa ndani.

Alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mara kuhudhuria sherehe hizo ili waweze kushuhudia namna mkoa huo ulivyojiandaa, pia watapata fursa ya kutembelea mabanda na kujionea mambo mbalimbali.

Kwa mjibu wa Tupa, kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni: “Mara Mali Yetu, Urithi Wetu Tuutunze."
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger