WAFANYABIASHARA WA SOKO LA TANGAMANO WALILIA HUDUMA YA CHOO.
Sanura Nyangasa /Veronica Julius
Wafanyabiashara wa gulioni maarufu la tangamano wameiomba halimashauri ya jiji la tanga kuwapatia huduma ya choo kwani imekuwa ni tatizo kubwa kwa wanaohitaji huduma ya choo katika eneo hilo.
Hayo yamesemwa na RAJABU SAIDI ambaye nimfanyabiashara wa nguo katika soko hilo katika mahojiano na kituo hiki ambapo amesema kuwa ukosefu wa choo katika gulio hilo imetokana na choo kilichopo kwa sasa kutumiwa na viongozi tu na kupelekea wafanyabiashara kulazimika kutoka nje ya eneo hilo kufuata huduma hiyo muhimu.
Naye HUSENI AWADHI ambaye pia ni mfanyabiashara katika soko hilo amesema viongozi wa jiji la Tanga hawawathamini wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) na badala yake kuwajali wafanyabiashara wakubwa.
Sambamba na hayo mama SHEILA ambaye pia ni mfanyabiashara wa soko hilo hakusita kutoa ushauri kwa kusema wanaomba kujengewa choo katika eneo hilo kwani imekuwa usumbufu kwa upande wao kutokana kulazimika kutoka mbali na biashara zao kufata huduma hiyo muhimu.