Featured Post Today
print this page
Latest Post

BASI LA YANGA LAPASULIWA KIOO NA MASHABIKI MBEYA CITY, MATAI MATATU YALIYOANDIKWA KIARABU YATOLEWA UWANJANI

BASI LA YANGA LAPASULIWA KIOO NA MASHABIKI MBEYA CITY, MATAI MATATU YALIYOANDIKWA KIARABU YATOLEWA UWANJANI


Basi la Yanga likiwa limepasulia kioo wakati linaingia Uwanja wa Sokine mjini Mbeya na mashabiki wa Mbeya City katika mchezo baina ya timu hizo Jumamosi. Timu hizo zilitoka 1-1.

Mkono wa kulia wa dereva la basi la Yanga SC, Maulid Kiula ulivyojeruhiwa na mashabiki wa Mbeya City

Maulid Kiula, dereva wa basi la Yanga

Meneja wa Uwanja wa Sokoine akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mayai matatu aliyoyaondoa katikati ya Uwanja kabla ya kuanza kwa mechi hiyo

Yanafaa kula? Mayai yaliyoandikwa Kiarabu yaliyotolewa uwanjani kabla ya mchezo kuanza

Bendera ya Mbeya City na maandishi wa Kiarabu

Basi la Yanga likiwa chini ya uangalizi wa Polisi Uwanja wa Sokoine lisishambuliwe zaidi

Mashabiki wa Yanga kutoka Tunduma

Walikuwepo mashabiki pia kutoka Dar es Salaam kama hawa tawi la Tandale kwa Mtogole, lakini hawakutamba mbele ya mashabiki wa Mbeya City
0 comments

YANGA SC ILIVYOSHIKWA NA MBEYA CITY LEO SOKOINE, MANJI HADI HURUMA

YANGA SC ILIVYOSHIKWA NA MBEYA CITY LEO SOKOINE, MANJI HADI HURUMA


Wachezaji wa Yanga SC wakishangilia bao la kusawazisha katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Timu hizo zilitoka 1-1.

Atumani Iddi 'Chuji' akimtoka mchezaji wa Mbeya City

Frank Domayo wa Yanga akipambana na mchezaji wa Mbeya City

Frank Domayo amefumua shuti

Said Bahanuzi anajiandaa kupiga krosi 

Didier Kavumbangu akipambana na beki wa Mbeya City...kulia ni Hussein Javu

Hussein Javu anapiga shuti

Beki wa Mbeya City akimdhibiti Hussein Javu, ili kipa wake adake mpira 

Said Bahanuzi akipiga shuti

Kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, David Burhan akidaka mpira mbele ya Didier Kavumbangu 

Wachezaji wa Yanga wakimzonga refa baada ya kukataa bao lao

Wachezaji wa Yanga wakimuambia refa amuangalia mshika kibendera kakubali bao

Mashabiki wa Mbya City

Hussein Javu kushoto akimtoka beki wa Mbeya City, huku Nizar Khalfan akijipanga kuomba pasi

Mwagane Yeyo wa Mbeya City akiruka mkugombea mpira wa juu na beki wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro'

Didier Kavumbangu akigombea mpira na beki wa Mbeya City

Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji akiwa ameshika tama jukwaani

Mshambuliaji wa Yanga SC, Simon Msuva ambaye alikuwa nje leo akiwa ameshika tama 

Haruna Niyonzima na Mrisho Ngassa wakiwa hawaamini macho yao

Shabiki wa Yanga SC, Paulina aliyesafiri kutoka Dar es Salaam kuja kuisapoti timu yake leo akiwa hoi Uwanja wa Sokoine leo 

Kikosi cha Yanga SC kilichoanza leo

Kikosi cha Mbeya City leo
0 comments

JAMBO TANGA, MWILI HUJENGWA KWA VYAKULA NA MAZOEZI, WATOTO WAPO WAPO KAZINI

JAMBO TANGA, MWILI HUJENGWA KWA VYAKULA NA MAZOEZI, WATOTO WAPO WAPO KAZINI
0 comments

SIMBA YAFANYA KWELI TAIFA, YANGA NA AZAM CHUPUCHUPU

SIMBA YAFANYA KWELI TAIFA, YANGA NA AZAM CHUPUCHUPU

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam.
WEKUNDU wa Msimbazi Simba leo wamefanya kweli katika mechi ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo iliendelea leo kwa kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Wakati Simba wakifanya mauaji leo mabingwa watetezi, Yanga SC wakilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji Mbeya City na Simba SC wakishinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati Azam FC imetoa sare ya 1-1 na wenyeji Kagera Sugar. 

Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabingwa watetezi walilazimika kusubiri hadi dakika ya 82 kujihakikishia japo kupata pointi moja mbele ya Mbeya City.
 

Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi, ndiyo walioanza mchezo huo kwa kasi wakishambulia zaidi kutokea pembeni na kulitia misukosuko lango la Yanga SC.
 

Mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu akiruka kupiga kichwa mbele ya mabeki wa Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine.

Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi, ndiyo walioanza mchezo huo kwa kasi wakishambulia zaidi kutokea pembeni na kulitia misukosuko lango la Yanga SC.
 

Pamoja na kocha Mholanzi, Ernie Brandts kuanzisha washambuliaji watatu, Didier Kavumbangu, Hussein Javu na Said Bahanuzi, lakini kuzidiwa kwa timu yao katika safu ya kiungo kuliwafanya wasiwe na madhara.
 

Hata hivyo, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na kipindi cha pili, Mbeya waliingia kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata bao dakika ya nne tu tangu kuanza kipindi hicho.
 

Krosi maridadi ya Hassan Mwasapili kutoka wingi ya kushoto iliunganishwa vizuri kwa kichwa na Mwagane Yeya ‘Morgan’ na kumpita kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ kama amesimama.
 

Baada ya bao hilo, Yanga walicharuka na kuanza kucheza kwa nguvu na kushambulia zaidi na almanusra mchezo uingie dosari dakika ya 58, baada ya Didier Kavumbangu kuuwahi mpira aliokuwa akiuchezea kipa wa Mbeya City, David Burhan na kuutumbukzia nyavuni, lakini refa akakataa bao.
 

Kipa huyo alidaka shuti la Nizar Khalfan na kuanza kuuchezea mpira kwa madaha akiudundaduna huku ameinama, ndipo Kavumbangu akamsogelea na kwa mchecheto mpira ukamtoka kipa huyo mikononi na mshambuliaji huyo wa Yanga akawahi kuusukumia nyavuni.         
 

Baada ya refa Andrew Shamba kukataa bao hilo, wachezaji wa Yanga walimtia kashikashi kidogo, kabla ya kuendelea na mchezo.
 

Timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini mabadiliko yaliyofanywa na kocha Brandts kuwaingiza mfululizo Jerry Tegete na Oscar Joshua kuchukua nafasi za Nizar na Bahanuzi kuliongeza uhai Yanga na matunda yake ni kusawazisha bao dakika ya 82 kupitia kwa Kavumbangu, akimalizia krosi David Luhende.
 

Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi tano baada ya kucheza mechi tatu, ikitoa sare mbili na kushinda moja, sawa na Mbeya City ambao pia wana pointi tano sasa baada ya sare mbili na kushinda mechi moja, zote nyumbani.
 

Mapema mashabiki wa Mbeya City walilitupia mawe basi la Yanga wakati linaingia uwanjani na kusababisha kioo cha mbele upande wa dereva kuvunjika na pia kumjeruhi dereva huyo.
 

Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji alikuwa jukwaani kushuhudia mchezo huo pamoja Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji na Mussa Katabro.
 

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Jerry Tegete dk59, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Hussein Javu na Said Bahanuzi/Oscar Joshua dk59.
 

Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Antony Matogolo, Yohana Morris, Mwagane Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga/Fidelis Castor dk82, Deus Kaseke, Yussuf Willson/Alex Sethi dk 59.  
 

Katika mechi nyingine za Ligi hiyo, Simba SC iliiendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Mtibwa Sugar 2-0.
 

Hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na kipindi cha pili, ndipo Wekundu wa Msimbazi walipong’ara, Henry Joseph akianza kufunga dakika ya 70 na Betram Mombeki akafuatia dakika ya 90.
 

Simba SC; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Kaze Gilbert, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha Ibrahim/Betram Mombeki dk64, Said Ndemla/Henry Joseph dk55, Amisi Tambwe, Amri Kiemba na Haroun Chanongo/Ramadhan Singano dk77.
 

Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif ‘Casillas’, Hassan Ramadhani, Paul George, Dickson Daudi, Salim Abdallah, Shaaban Nditi, Ally Shomary, Masoud Mohamed/Awadh Juma dk58, Juma Luizio/Mussa Mgosi dk46, Shaaban Kisiga/Abdallah Juma dk75na Vincent Barnabas.

Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Themi Felix Buhaja alitangulia kuifungia Kagera Sugar dakika ya 25 kabla ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kuisawazishia Azam FC dakika ya 55.


Katika mechi nyingine Coastal Union ilitoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mgambo Shooting bao pekee la Elias Maguri dakika ya 53 Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Oljoro JKT ilitoka sare ya 1-1 Rhino Rangers Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, wenyeji wakilazimika kusawazisha dakika ya 27 kupitia kwa Amiri Hamad baada ya Saad Kipanga kutangulia kuwafungia wageni dakika ya tano, wakati Ashanti United ililala 1-0 mbele ya JKT Ruvu, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam bao pekee la Amos Mgisa dakika ya 81.


Matokeo hayo, yanamaanisha JKT Ruvu inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake tisa baada ya kushinda mechi zote tatu, ikifuatiwa na Simba SC katika nafasi ya pili yenye pointi saba. Timu nyingi zimefungana kwa pointi tano katika nafasi ya tatu, zikiwemo Yanga, Azam na Coastal Union.
0 comments

FLOYD MAYWEATHER AMSHINDA SAUL CANELO ALVAREZ UKUMBI WA LAS VEGAS MAREKANI

Landing at will: Mayweather had little trouble connecting with Alvarez as he eased to victory in Las VegasMayweather
Still champion: Floyd Mayweather was hugely impressive in beating Saul Alvarez over 12 rounds in Las Vegas
Still champion: Floyd Mayweather was hugely impressive in beating Saul Alvarez over 12 rounds in Las Vegas

Beaten man: Alvarez was outclassed from start to finish as the Mexican tasted defeat for the first time
Beaten man: Alvarez was outclassed from start to finish as the Mexican tasted defeat for the first time
Landing at will: Mayweather had little trouble connecting with Alvarez as he eased to victory in Las Vegas
Landing at will: Mayweather had little trouble connecting with Alvarez as he eased to victory in Las Vegas
Floyd Mayweather produced another night of magic in the desert to brush aside the muscular young challenge from Mexican prodigy Saul Alvarez.
Not everyone appreciates genius at work and one of the judges gave the kid called Canelo a draw.
That was an insult to the finest boxer of his generation, who may come to be seen as one of the best of all time, the pound-for-pound Money man.
Now you see me: Mayweather's defence and footwork were once again in fine working order
Now you see me: Mayweather's defence and footwork were once again in fine working order
Admonished: Referee Kenny Bayless warns Alvarez as he struggles to contain Mayweather in Vegas
Admonished: Referee Kenny Bayless warns Alvarez as he struggles to contain Mayweather in Vegas
0 comments

VIONGOZI WA UPINZANI WAAMUA KUPANGA MBINU ZA KUMZUIA RAIS JAKAYA KIKWETE ASISAINI MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA 2013.

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa asaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 ili iwe sheria, viongozi wa upinzani nchini wameamua kuanza mchakato wa kumn
g’oa kiongozi huyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.

Wenyeviti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), leo wanatarajia kukutana na wahariri na waandishi wa habari kueleza mikakati na mbinu watakazozitumia kunusuru taifa lisiingie kwenye utungaji wa Katiba mpya itakayobeba masilahi ya chama tawala.

Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa mikutano ya hadhara, maandamano na elimu kwa umma juu ya athari ya muswada huo ni miongoni mwa mbinu zitakazotumiwa kuhakikisha Rais Kikwete hasaini muswada huo au serikali inapeleka tena mabadiliko ya sheria hiyo katika Bunge lijalo iwapo rais atasaini.

Wapinzani wanadai kuwa serikali iliubadili kwa nguvu muswada huo kwa kuondoa maoni muhimu ya wadau, pia walilalamikia kitendo cha wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge kutokwenda Zanzibar kuchukua maoni ya upande huo wa muungano.

Wakati wapinzani wakijipanga kuweka wazi mikakati ya kumshinikiza Rais Kikwete asisaini muswada huo, wadau mbalimbali wamemtaka kiongozi huyo atumie busara ili taifa lipate katiba itakayokuwa na manufaa kwa taifa kuliko inavyoonekana itikadi za vyama kugubika mchakato huo.

Wiki iliyopita akiwa Dodoma, Mbowe alikionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa wasitarajie kuwa kupitishwa kwa marekebisho ya muswada huo ndiyo Katiba mpya, bali kura ya maoni ndiyo itakayoamua jambo hilo.

Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa wapinzani wamejipanga kuhakikisha wananchi wanaitumia kura ya maoni kupinga mpango wa Rais Kikwete na serikali yake kupitisha Katiba mpya yenye mwelekeo wa kukibeba chama tawala.

Hoja za wapingaji
Kamati Maalumu ya Katiba, nayo imepinga marekebisho ya muswada huo ikiainisha eneo mojawapo lenye tatizo ni kuruhusu asilimia 72 ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kubeba wanasiasa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Khoti Kamanga, alisema iwapo Katiba mpya itaundwa bila upungufu unaoonekana sasa kupatiwa ufumbuzi itazalisha migogoro zaidi, itakayosababisha nchi kuingia kwenye machafuko.
Alikosoa Kifungu cha 8 na Kifungu kidogo cha 4 na 5 cha muswada huo kwamba vina kasoro, kwa kuruhusu wabunge wa Bunge la Katiba kufanya uamuzi kwa wingi wa kura badala ya kutumika utaratibu wa theluthi mbili kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, naye anapinga muswada huo kwa madai kuwa una upungufu mkubwa, ukiwamo wa Zanzibar kutoshirikishwa, pia kumpa nafasi kubwa rais kuteua watu kutoka katika asasi mbalimbali badala ya watu hao kuteuliwa moja kwa moja na asasi au asasi husika.
Hofu ya yaliyotokea Kenya
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa Tanzania inafuata njia iliyopitwa na Kenya katika kupata katiba mpya, ambayo ilipatikana baada ya kutokea machafuko mwaka 2007 mara baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Mwaka 2005, wananchi wa Kenya wakiongozwa na wanasiasa maarufu, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, waliibwaga serikali ya rais mstaafu wa nchi hiyo, Mwai Kibaki, katika kura ya maoni ya kuamua kuikubali au kuikataa rasimu ya katiba iliyokuwa imependekezwa na utawala wa rais Kibaki.
Ni kutokana na matokeo ya kura hiyo, uchaguzi mkuu wa 2007 ulizaa machafuko na mauaji ya mamia ya Wakenya wasiokuwa na hatia, baada ya kushindikana kupatikana kwa katiba mpya, hivyo utawala wa Kibaki kuamua kuitisha uchaguzi mkuu kwa kutumia katiba na sheria za uchaguzi za zamani zilizokuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu.
Wachambuzi wa siasa hapa nchini wanasema kuwa mwenendo wa hivi karibuni wa mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Tanzania unaonesha ishara za wazi za kutokea yaliyotokea nchini Kenya. Kwamba, kushindwa kufikia mwafaka baina ya wabunge wa Bunge la Tanzania lililomaliza vikao vyake hivi karibuni mjini Dodoma, kuhusu muundo wa Bunge Maalumu la Katiba ni uthibitisho wa wazi wa matatizo yanayoweza kutokea siku za usoni.
Bunge Maalumu la Katiba ndilo litakaloandaa rasimu ya mwisho ya Katiba mpya itakayopelekwa kwa wananchi mapema mwakani kwa ajili ya kura ya uamuzi, hivyo muundo wake na kukubalika kwake ni jambo muhimu na linalohitaji mwafaka wa kitaifa.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilipeleka mapendekezo ya kutaka uwakilishi wa Bunge hilo upanuliwe kutoka wajumbe 600 wa sasa na kuwa wajumbe 789 ili kulifanya bunge hilo lisihodhiwe na wanasiasa ambao zaidi ya asilimia 70 ni wanachama wa CCM.
Hata hivyo, pendekezo hilo lilishindwa baada ya wabunge wa CCM kutumia wingi wao katika Bunge hilo kuyakwamisha mapendekezo ya upinzani na badala yake kuamua kuendelea na muundo wa sasa unaoipa CCM haki ya kisheria ya kulihodhi Bunge la Katiba.
Wachambuzi hao wanatabiri kuwa kama Rais Jakaya Kikwete atakubaliana na msimamo wa wabunge wa chama chake, kwa kuitia saini sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba na hatimaye kuwa na Bunge la Katiba na baadaye kura ya maoni, basi kuna uwezekano katiba hiyo mpya ikakataliwa na wananchi katika kura ya maoni kama ilivyokuwa kwa Kenya mwaka 2005.
Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011, kama wananchi wataikataa katiba inayopendekezwa, basi katiba ya zamani itaendelea kutumika katika shughuli zote za nchi, ikiwamo kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, jambo ambalo linapingwa vikali na viongozi, wanachama, wafuasi wa vyama vya upinzani na wanaharakati.
Ni kutokana na mazingira haya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini wanaamini na kutabiri kuzuka kwa ghasia, machafuko na umwagikaji wa damu kama ilivyotokea Kenya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Alli, anasema: “Tunakabiliwa na hatari mbele yetu, maana tunakwenda kwenye kura ya maoni kuhusu Katiba mpya tukiwa tumemeguka vipande vipande. Tulipaswa kufika huko tukiwa wamoja kama taifa, tulipaswa kuwa na mwafaka wa kitaifa katika suala hili la katiba ya nchi badala ya kwenda kwa kuongozwa na itikadi zetu za kisiasa,” alieleza Bashiru na kuongeza:
“Machafuko na mauaji yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 yalitokana na makosa ya utawala wa rais mstaafu wa nchi hiyo, Mwai Kibaki, ambaye aliamua kuwadharau na kuwapuuza wananchi katika mchakato wa kuunda katiba ya nchi yao kama inavyofanyika sasa nchini mwetu, hili ni jambo la hatari sana,” alionya Bashiru.
Bashiru anasema kuwa ili kuufanya mchakato wa sasa wa Katiba mpya kuwa wa wananchi na kuepusha kuiingiza nchi kwenye machafuko na mauaji ya wananchi wasio na hatia, mchakato wote unapaswa kurudiwa.
“Ili yasitufike yaliyotokea Kenya, tunapaswa kuanza upya mchakato wa Katiba mpya, wananchi wapewe fursa ya kuumiliki mchakato mzima. Kwa mfano, wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanapaswa kuchaguliwa na wananchi, si kuteuliwa. CCM na wapinzani wanataka wajumbe wapatikane kwa kuteuliwa, mimi nasema huo si utaratibu sahihi, dhana ya Bunge la Katiba inataka wajumbe wake wapatikane kwa kuchaguliwa na wananchi, si kuteuliwa,” anabainisha Bashiru.
Ulivyopitishwa
Mjadala wa muswada huo uliopitishwa Ijumaa iliyopita na wabunge wengi wakiwa wa CCM, ulizua tafrani bungeni iliyosababisha Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) kutolewa nje na askari. Katika tafrani hiyo, baadhi ya wabunge wa upinzani walirushiana makonde na maofisa usalama, huku wabunge wote wa upinzani, isipokuwa Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, wakiususia. TANZANIA DAIMA.
0 comments

Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro awapa neno wananchi kuhubiri Rasimu ya Katiba pamoja na kufanya kazi za kimaendeleo

Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro awapa neno wananchi kuhubiri Rasimu ya Katiba pamoja na kufanya kazi za kimaendeleo

Na Fadhili Athumani, Moshi
MWENYEKITI wa CCM mkoani Kilimanjaro, Iddi Juma, amewataka Watanzania kuacha kutumia tabia ya kutumia muda mwingi kujadili Katiba na badala yake kujikita katika shughuli za kuimarisha uchumi pamoja na kutatua kero za wananchi.
Kauli ya kiongozi huyo, imekuja wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakizunguka nchi nzima kuwahamasisha wananchi kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba mpya hasa muundo wa serikali wanayoitaka.
Juma alisema kwa sasa kila mahali utakuta watu wakitumia muda mwingi wa wamekusanyana makundi makundi wakibishana kuhusu Rasimu ya Katiba hasa muundo wa serikali na kusahau kuwa kuna haja ya kujishughulisha ili kuimarisha uchumi wao na uchumi wa nchi.
Mwenyekiti huyo alisema  kujadili Rasimu ya Katiba bila kufanya kazi za maendeleo ni upuuzi utekelezaji Katiiba kunahitaji Fedha na hilo halitawezekana kama wananchi pamoja na Viongozi hawatazinduka na kuona haja ya kutmia muda wao vizuri.

“Viongozi sasa hivi sio wa Chadema, CCM, NCCR-Mageuzi, TLP, vingozi wa dini pamoja na Wananchi wanatumia muda mwingi kujadili ya Rasimu ya Katiba, utakuta watu wakiwa katika makundi wakibishana kuhusu Rasimu, Viongozi hasa hawa wenzetu wanazunguka kila mahali kuhamasisha maoni ya wananchi lakini wanasahau kuwahamasisha kufanya kazi”, alisema Juma
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Moshi Manispaa, Elizabeth Minde akizungumza baada ya chama hicho kutoa msaada wa fedha na vifaa vya nyumbani kwa waathirika wa janga la Moto lililotokea katika mtaa wa sabasaba kata ya Soweto, September 10 mwaka huu, alisema swala la muhimu ni kufanya kazi kwani mwenye njaa kamwe haitambui hata “ingepakwa rangi nyeupe”.
 
Mwenyekiti wa CCM, mkoani Kilimanjaro, Iddi Juma (katikati, aliyevaa kofia), Mwenyekiti wa CCM moshi Mjini, Elizabeth Minde (kushoto kwake) katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Aluu Seigamba (kulia kwake) na baaadhi ya viongozi wa chama wakati wakikabidhi msaada kwa familia 12, wahanga wa moto katika mtaa wa sabasaba, kata ya Soweto manispa ya  Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Minde ambaye ni Mwanasheria kitaaluma alisema endapo uchumi wa nchi utayumba, katiba kama ilivyo sheria inaweza ikaonekana haifai hata kama ingekuwa vipengele vizuri kiasi gani.
Katika Hatua nyingine Watendaji wa ngazi za chini wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamedaiwa kuhujumu ziara za vingozi wa juu wa CCM mkoani hapo pamoja na kukwamisha shughuli za chama katika maeneo wanayosimamia.
Malalamiko hayo yalitolewa jana na Wajumbe wa Mkutano wa Chama hicho katika ziara katika ziara ya Chama cha Mapinduzi katika Manispaa ya Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa, Iddi Juma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti huku wakionesha kuchoshwa na manyanyaso wanayopata mikononi mwa watendaji hao baadhi ya WanaCCM katika kata za Soweto, Shirimatunda Kilimanjaro na Karanga walidai watendaji hao wamekuwa wakihujumu ziara za vingozi wa juu wa chama hicho.
Katika mkutano na Wananachama wa Chama cha Mapinduzi katika Kata hizo, Baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo waliwaanyoshea kidole watendaji wa ngazi za chini wakiwemo makatibu wa kata na wenyeviti wao kuwa kikwazo kikubwa katika ziara za viongozi wakuu wa chama hicho.
Malalamiko hayo yalikuja baada ya kuwepo kwa hali isiyokuwa ya kawaia ya kuwepo kwa mahudhurio duni ya wanachama pamoja na taarifa za ziara hiyo kutolewa wiki mbili kabla ambapo ilidaiwa kuwa kikwazo ni baadhi watendaji hasa watendaji wa kata za Karanga na Shirimatunda ambao wanadaiiwa kuendekeza rushwa katika utendaji wao.
Hali iyo ilijitokeza baada ya mkutano wa Mwenyekiti huyo katika kata ya karanga iliyojumuisha kata zote tatu za Karanga, Shirimatunda na Soweto kuhudhuriwa na wanachama wachache pamoja na taarifa za ziara ya kiongozi huyo kutolewa wiki tatu kabla ambapo idadi iliyohudhuria kilikuwa hakizidi wanachama mia.
Akizungumzia malalamiko hayo za wananchama hao, Iddi Juma ambaye alionesha kukerwa na hali hiyo, alisema kwa sasa CCM imejipanga kuhakikisha kila mtu anawajibika katkaeneo lake la kazi na kuahidi kufikisha malalamiko hayo katika sehemu husika ili wote wanaotuhmiwa wawajibishwe.
“Hali hii inasikitisha sana, wananchi wanatutegemea kama viongozi wao, Sifa ya kiongozi ni kuongoza katika harakati za kutatua kero za mwananchi sio kuzidisha kero hizo, tutahakikisha swala hili linafika sehemu husika na tutafuatilia”, alisema Juma
Naye Katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Aluu Segamba alisema kuwa Chama hakitavumilia uona watu wachache wanainajisi Serikali na kuongeza kuwa watahakisha wanapambana na wahujumu uchumi.
“Watendaji wamekuwa wakilalamikiwa sana, kwa mfano watendaji wetu ambao tunawategemea kama chama tawala wameamua kutuoni jinsi gani wanavyoweza kuinajisi Serikali tena mbele ya macho yetu, mwakani tunaanza harakati za uchaguzi tunahitaji watu makini na hata hawa wanaofanya kazi kwa mazoea tutawatimua wote” alisema Segamba.
0 comments

Wafanyakazi walaumu:wahamiaji haramu wameajiriwa kwenye nafasi nyeti JNIA

Wafanyakazi walaumu:wahamiaji haramu wameajiriwa kwenye nafasi nyeti JNIA

julias_airport_489c3.jpg

Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam wamedai kuwepo kwa wafanyakazi ambao ni wahamiaji haramu katika uwanja huo, ambao wamekuwa wakipewa nafasi nyeti katika mamlaka hiyo.

Aidha, wameeleza kuwa wahamiaji hao haramu pia wamekuwa wakipatiwa vitambulisho nyeti kama watanzania halisi.

Wafanyakazi walimueleza Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana alipofanya ziara uwanjani hapo na kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) katika uwanja huo.


Mfanyakazi Dominic Bomani alisema licha ya juhudi za serikali kuwaondoa nchini wahamiaji haramu, kiwanja hicho cha ndege kimekuwa chimbuko la wahamiaji hao ambao wamekuwa wakipewa nafasi nyeti.

Aliomba serikali kusaidia katika kuwabaini na kuwaondoa wahamiaji hao ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi hizo ziweze kushikiliwa na watanzania ambao wako wenye sifa stahili.

Dk Mwakyembe alishukuru kwa taarifa hizo na kuahidi kufanyia kazi huku akimtaka mfanyakazi huyo kufika ofisini kwake ili kumpa taarifa zaidi.

"Nashukuru kwa taarifa hizo kwani hatukuwa nazo na ninaahidi kuanza kuzifanyia kazi na kutoa majibu yake haraka kuanzia Jumatatu (kesho)," alisema.
Kuwepo kwa wafanyakazi wahamiaji haramu kumeonekana huenda ikawa ndiyo sababu ya matukio
yaliyotokea katika uwanja huo ya kupitisha dawa za kulevya kutokana na wahusika kutokuwa na uzalendo na taifa hili.

Katika siku za hivi karibuni serikali ilianzisha operesheni za kuwarejesha makwao wahamiaji haramu kutoka nchi mbalimbali.

Operesheni hiyo iliyobatizwa jina la 'Kimbunga' iliahidiwa na Rais Jakaya Kikwete akiwa mkoani Kagera hivi karibuni, baada ya kuwataka wahamiaji haramu kurejea walikotoka au kufuata taratibu za kisheria za kuishi nchini, huku akionya kinyume cha hapo, kwa kuwa miongoni mwao wanajihusisha na ujambazi, watasakwa misituni, majumbani na hata ardhi itachimbuliwa, kutafuta silaha walizozifukia ilianza kwa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumalizika katika mikoa ya Geita, Kagera Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe, aliyekuwepo katika mkutano huo wa Rais Kikwete alisema ni wahamiaji haramu 11,601 tu walioondoka wakati uongozi wa mkoa huo, ulitarajia wahamiaji haramu kati ya 52,000 na 53,000 waondoke.

Mkuu wa Operesheni hiyo ya Kimbunga, Kamanda Simon Sirro alisema tangu operesheni hiyo ianze, wahamiaji haramu 1,851 wamekamatwa, ng'ombe 1,763 na silaha za moto saba, bunduki za kienyeji maarufu magobori sita na shotgun moja katika mikoa lengwa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Katika Mkoa wa Kigoma, operesheni hiyo imefanikiwa kukamata wahamiaji haramu 885, silaha mbili, gobori moja na shotgun moja na ng'ombe 200.

Mkoani Geita, wahamiaji haramu 246 wamekamatwa, magobori matatu, ng'ombe 240, sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kibuyu cha maji cha jeshi hilo.
Katika mkoa wa Kagera, wamekamata wahamiaji haramu 750, magobori mawili na ng'ombe 1,323. Mbali na silaha hizo zilizokamatwa, silaha zingine 65 zimesalimishwa; SMG tatu, shotgun 10 na magobori 52.
Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, silaha nyingi zilisalimishwa katika wilaya ya Biharamulo na ndizo zilizokuwa zikitumika katika utekaji na unyang'anyi katika mapori wilayani humo.

Jijini Dar es Salaam, Operesheni Kimbunga kwa ajili ya wahamiji haramu kwa mujibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, hadi jana wahamiaji 465 kutoka mataifa 17 wakiwamo walimu wanaofundisha shule za michepuo ya Kingereza wamekamatwa.

Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo alitaja waliokamatwa kuwa ni Warundi 181, Wakongo 38, Wanyarwanda watano, Waganda 16, Wakenya 38, Wapakistani sita, Wasomali 28, Wanigeria 12, raia wanane wa Msumbiji, 114 wa Malawi, wawili wa Cameroon na 10 wa India.
Aidha, walikamata raia watatu wa Uturuki, watatu wa Comoro, mmoja wa Afrika Kusini, mmoja wa China na mmoja wa Burkina Faso.

Alisema wahamiaji hao wengi wao ni vijana na wamekuwa wakijifanya walimu wa shule za michepuo ya Kingereza, lakini hawana taaluma hiyo, isipokuwa wanakijua Kingereza na wengine ni wauza kahawa, wafanyakazi wa ndani, walinzi, watunza bustani, wauza matunda na maji. --- HabariLeo, JUMAPILI

0 comments

Dawa ya mifugo yatengenezea gongo Dar

Dawa ya mifugo yatengenezea gongo Dar

mtambo 61142

Wakati Serikali ikiahidi kuongeza nguvu katika vita dhidi ya wauza dawa za kulevya nchini, imebainika kuwa kuna mtandao wa wafanyabiashara wa pombe haramu ya gongo unaopika na kuichanganya na dawa za mifugo ili kuiongezea ukali.

Mtandao huo unaomiliki mitambo ya kupika gongo katika eneo la Mto Kizinga uliopo Dambweni, Kata ya Kilungule, wilayani Temeke, unadaiwa kuchanganya pombe hiyo na dawa ya mifugo aina ya Multivitamin ambayo hutumika kurutubisha wanyama.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakipika gongo hiyo katika eneo hilo kwa miaka zaidi ya 10, huku baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa wakitajwa kuwalinda.
Kwa mujibu wa uchunguzi, eneo hilo lina mitambo zaidi ya minne ya kutengeneza gongo na kila mtambo unazalisha pipa moja lenye ujazo wa lita 200.

Uchunguzi ulibaini kuwa kila siku wanazalisha zaidi ya lita 800 za gongo ambayo huuzwa kwa rejareja na jumla. Bei ya rejareja kipimo kinaanzia Sh500 hadi Sh5,000, ambapo bei ya jumla ni Sh38,000 kwa ndoo yenye ujazo wa lita 20.

Kwa mtu anayefika kwa mara ya kwanza eneo hilo atakutana na makundi ya watu wakiwa chini ya miti wakijipumzisha wakati wakisubiri pombe hiyo kuwa tayari, huku wakazi wengine wa eneo hilo wakionekana kuendelea na shughuli zao kwenye bustani za mboga za majani zilizolimwa kando kando ya mto.

Mbali ya kuwa wanalindwa na baadhi ya viongozi wa mtaa, wameweka ulinzi wao wenyewe, kwa kuweka vijana zaidi ya 10 ambao hukaa katika eneo hilo kuhakikisha kuwa mtu anayefika katika eneo hilo wanamtambua.

Ukifika katika eneo ilipo mitambo yao, watu wanaofanya kazi ya kupika ni wacheshi, wanaojaribu kumsalimia kila mpita njia bila ya kuwa na hofu yoyote, huku mmojawao ambaye jina lake halikufahamika mara moja akisema kuwa wao ndio waliotengeneza barabara ya kupita magari inayoingia sehemu hiyo.

Mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuhofia usalama wake, alisema watu hao ndiyo wasambazaji wakubwa wa gongo jijini Dar es Salaam.

"Biashara hii inalipiwa 'kodi' kila mwezi, hawa jamaa huchangishana fedha halafu huwapelekea baadhi ya askari ambao huwalinda wasikamatwe, kuna wakati huchanga hadi laki tatu. Vigumu sana kukamatwa," alisema.

Gongo inavyotengenezwaUchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini pombe hiyo inatengenezwa kwa kutumia malighafi mbalimbali ikiwamo mapapai yaliyooza, vitambaa vichafu vilivyovunda, mihogo na wakati mwingine kinyesi cha binadamu hasa wakati bidhaa nyingine zinapoadimika.

Mfanyabiashara mmoja (jina linahifadhiwa) alisema amekuwa akipika gongo na kuigawa katika madaraja matatu; iliyopikwa kwa mapapai yaliyooza ndiyo inayopendwa zaidi na wateja wake ikilinganishwa na iliyotumia malighafi nyingine.

"Sisi tunatumia mapapai yaliyooza, tunaongeza na sukari pamoja na hamira, ikishaiva tunaitenga kutokana na madaraja yake. Gongo ya eneo hili inasifika sana kwa sababu ya ubora wake, hatuna tatizo la ukosefu wa maji kama walilonalo wenzetu ndiyo maana unaona tunaung'ang'ania huu mto hapa," alisema na kuongeza :
"Kama mapapai yakiadimika sana, tunaweza kupika kwa kutumia vitambaa vichafu au mihogo."

Akifafanua alisema wamekuwa wakitembea kwenye madampo kuokota vitambaa pamoja na takataka nyingine, kisha huziloweka kwenye maji kwa muda mrefu hadi zivunde ndipo huwa tayari kwa kupikia gongo.

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa mbali ya pombe hiyo kutengenezwa kwa kutumia takataka zinazookotwa kwenye madampo, pia huongezewa ukali kwa kutumia dawa za kuongezea vitamini mifugo.

Mteja mmoja wa pombe hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Sadick, alisema gongo inayopikwa eneo hilo imekuwa maarufu kwa kuwa kuna dawa ya mifugo ya Multivitamin ambayo huongezwa baada ya pombe hiyo kuiva.

"Mimi ninafahamu kuna dawa ya mifugo inawekwa kwenye hii gongo ili kuiongezea nguvu. Sijui ni dawa aina gani, lakini kuna jamaa huwa namwona anakuja kuuza hiyo dawa. Gongo iliyowekwa hiyo dawa inakuwa na nguvu sana,"alisema Sadick.
Mtaalamu wa Mifugo, Joseph Nong'ona alisema wanywaji wa pombe hiyo wapo katika hatari ya kudhurika kiafya kwa kuwa dawa ya Multivitamin inayotolewa kwa wanyama ina nguvu zaidi ikilinganishwa na ya binadamu, na kwamba mtu haruhusiwi kunywa maziwa au nyama ya mnyama aliyepewa dawa hiyo kwa siku tatu.

"Multivitamin anayopewa mnyama ina 'concentration' kubwa ikilinganishwa na ile ya binadamu, lakini pia ikumbukwe kuwa ile ni kemikali sijui inakuwaje inapochanganywa na gongo ambayo yenyewe tu ina madhara makubwa kiafya. Kwa kawaida mnyama akipewa dawa hiyo huwa tunashauri asikamuliwe mazima au nyama yake isitumike kwa siku tatu," alisema Nong'ona.

Akizungumzia biashara hiyo, Katibu wa Mtaa wa Kilungule, Juma Ahmed aliwatetea wafanyabiashara hao kwa madai kuwa hajawahi kupata taarifa zozote za kufanya uhalifu badala yake wamekuwa walinzi wa amani katika mtaa huo."Ni watu wazuri sana, sijawahi kusikia wamefanya jambo lolote baya, kwanza wamegeuka kuwa walinzi wa amani hapa mtaani kwetu... wanajua biashara wanayoifanya siyo halali kwa hiyo hawataki matatizo na mtu," alisema Ahmed.

Kamanda wa Polisi wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema suala la biashara ya gongo linatakiwa kudhibitiwa na jamii inayowazunguka wafanyabishara hao kwa kutumia ulinzi shirikishi"Wanataka kuipa Polisi kazi bure tu, jamii ndiyo inayohusika na suala hilo. Serikali ya mtaa kwa njia ya ulinzi shirikishi wanaweza kuamua kwenda kuvunja mitambo ya gongo," alisema Kiondo.

Akizungumzia tuhuma kuwa baadhi ya Polisi wanawalinda wafanyabiashara wa gongo, Kiondo alisema tuhuma hizo zimekuwepo muda mrefu na kwamba zimeshapitwa na wakati.

CHANZO MWANANCHI.
0 comments

Padri alitishiwa kifo miezi mitatu kabla;

Padri alitishiwa kifo miezi mitatu kabla;

padri_pix_d2d78.jpg
Padri Joseph Magamba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Machui Zanzibar aliyemwagiwa tindikali akisaidiwa kushuka kwenye ndege na Padri Thomas Assenga(kushoto) wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Zanzibar baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana kuelekea katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.Picha na Fidelis Felix
Siku moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang'amba kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo.

Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.


Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Dk Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili kukabiliana na matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali, yanayoshamili visiwani humo hivi sasa.
"Hatuwezi kuviacha vitendo hivi viendelee ... ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Dk Shein.

Dk Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang'amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.

Alisema kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu hufanya mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya vitisho.
"Unajua kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au la," alisema Padri Assenga na kuongeza:

Alisema Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.

"Mara baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha) na kituo cha polisi."
Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang'amba, alisema alimwagiwa saa 9:45 alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet cafe iliyopo eneo la Mlandege.

Padri Assenga alisema kabla ya kumwagiwa tindikali, Padri huyo alikuwa ndani ya internet akitoa 'photocopy' za nyaraka. Alipokuwa akitoa 'photocopy' (nakala) alipigiwa simu na mtu ambaye anamfahamu hivyo ikabidi atoke nje kuongea naye, lakini alivyokuwa akiongea alimwona kijana akija na kikopo alichokishika mkononi na kummwagia na kukimbia kuelekea katika mitaa ya eneo hilo," alisema Padri Aseenga.
Alisema mara baada ya hapo, alipelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, kwa matibabu baada ya kujeruhiwa usoni, kifuani na mikononi ambapo hivi sasa afya yake inaendelea vizuri.
Naye , Msemaji wa Jeshi la Polisi, Zanzibar Mohamed Muhina alisema, hana taarifa hizo za vitisho na kuahidi kulifanyia kazi.

"Tukio limetokea mchana kweupe na watu walikuwapo lakini wananchi wamekuwa hawatupi ushirikiano hivyo tunawaomba kutupa ushirikiano ili kukomesha vitendo hivi," alisema Muhina.
Tukio lilivyokuwa
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo, Padri Mwang'amba alisema kwamba lilitokea nje ya duka linalotoa huduma za mawasiliano ya mtandao (Sun Shine Internet Caffee) liliopo eneo la Mlandege Wilaya ya Mjini Unguja, ndipo alipotokea kijana mmoja na kumwagia tindikali.

Padri Mwang'amba akimweleza Dk Shein kuwa hali yake ni nzuri na anaweza kuona vizuri, lakini anatarajia kupata nafuu zaidi baada ya uvimbe kupungua katika sehemu za usoni na machoni mwake.
"Hali yangu ni nzuri lakini natarajia uvimbe ukipungua nitaona vizuri zaidi," alisema Padri Mwang'amba na kuongeza kuwa ilikuwa ni bahati kwake kwa kutoathirika sana.

Uwanja wa Ndege

Katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Kiongozi huyo aliwasili saa 4.16 asubuhi na ndege ya Shirika la Costal akiongozana na Padri Assenge.

Kiongozi huyo aliyekuwa akitembea taratibu, huku akijitahidi kujifunika mwili wake na kanga kuzuia mwanga wa Jua kutokuathiri zaidi mwili wake ulioathiriwa na tindikali.

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger