Featured Post Today
print this page
Latest Post

WAZIRI MKUU PINDA AMUONYA VIKALI MAGUFULI


WAZIRI MKUU PINDA AMUONYA VIKALI MAGUFULI




WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amemuonya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa mara nyingine tena kuacha tabia ya kufanya uamuzi wa jambo lolote bila kushirikisha pande zinazohusika.

Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mgomo wa wasafirishaji wa mizigo na abiria ulioanza Oktoba 5, mwaka huu, Pinda alisema Serikali imeamua kurejesha kwa muda wa mwezi mmoja asilimia tano ya uzito wa mizigo uliozidi kwenye mizani.


Alisema hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja.

Alisema mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao.

“Chimbuko la mgogoro huu, ni tangazo la Dk. Magufuli alilotoa Oktoba mosi, mwaka huu la kuondoa ofa ya asilimia ya uzito uliozidi, baada ya uamuzi huo wadau wa usafirishaji wa malori na mabasi waliingia kwenye mgomo na kulalamikia hatua hiyo.

“Kutokana na mgogoro huu, nililazimika kukutana na Dk. Magufuli, baadhi ya mawaziri wa wizara zenye uhusiano na masuala haya, wanasheria na wataalamu wa masuala ya usafiri na uchumi.

“Kilichoongeza mgogoro ni tafsiri ya vifungu vya sheria na kwenye kanuni ya 7 (2) na 7(3) ambacho kinaeleza wasafirishaji wa magari yenye uzito uliozidi, lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria, wanatakiwa kupunguza mzigo, kupinga na iwapo watashindwa kutekeleza, watatakiwa kulipia mara nne ya tozo za kawaida.

“Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na halikuwa sheria kamili, ndio maana limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya.


“Nakubaliana na Dk. Magufuli, wapo baadhi ya wasafirishaji ni wakorofi na hawataki kufuata sheria…ndio maana walifanya mazoea ingawa wapo wengine wazuri na hao nawapongeza sana kutii sheria.

-Mtanzania

0 comments

Speech by Dr Slaa at The University of Samford, USA

Speech by Dr Slaa at The University of Samford, USA

Mr. President, the faculty, staff, students, invited guests and the public at large. Allow me to express my gratitude, for the cordial welcome at your lovely campus. It is one of a kind, and If I could, I would have stayed much longer to learn more on your success that I could take back to our young people. The environment and the surroundings are as beautiful as the people themselves. Along the way, I have met great people with great hearts, and I thank you for that

Likewise, receive greetings from the people of Tanzania. I was quite impressed with your level of research, and the homework you have done trying to know Tanzania, I was also particularly touched by some of you in the audience that knew the geography of my country; and even trying to challenge me . Mrs. Macquire, “People of Mto wa Mbu” are definitely

 proud of you for being such a good Ambassador. We thank you, and Tanzania needs more of you that will help in exposing it to the people of America

The Samford community, my journey has been long and tedious; I have travelled through hills and valleys of trials and tribulations. However, due to the need and challenges we face as a nation, physical fatigue of travel would not stop me from marching forward. I am determined to work with my countrymen to see our nation of Tanzania reach the Promised Land.

Tanzania is a great and rich country, with rich culture and rich people at heart. Her people have sent me on a study tour. They have sent me to learn the secrets of your success as a society

Tanzania is one of the most blessed countries on the face of the earth. It has abundance of natural wealth, and for those who understand the world history, know that the best game parks are in Tanzania. It is the place believed to be the cradle of mankind.

Tanzania is the home of Mt. Kilimanjaro, Serengeti national park, Ngorongoro crater, and Olduvai Gorge where the first man is believed to have lived. We have some of the world best beaches; our people are very hospitable and extremely welcoming. I welcome all of you to Tanzania

For a long time, Africa has been known as a dark continent infested with disease, poverty, starvation, illiteracy and never endings wars. This might have been created in your minds with the images in your televisions. I can’t blame you, because this is the truth you know

However, this is far from the reality. Africa and Tanzania in particular is the new frontier. Tanzania is a country rich in natural resources and only lacks human capital. It is a country with rich land and plenty of water bodies
Many African leaders are believed to come to Washington and other western capitals begging for handouts known as foreign aid. This has created a notion in the minds of many that Africans are poor and lazy.

This is not the case.

Africa is transitioning from mismanagement, dictatorship and corruption that have plagued the continent. Corruption is the main vice depriving Tanzanians and other Africans a chance to a better education, better healthcare and economic prosperity.

Well, I am not here to beg, because my country is rich. I know clearly well that, foreign aid does not come cheaply. It comes with a condition of signing up our sovereignty

I am not here for foreign aid, and CHADEMA party which I represent does not believe on foreign AID. This is my party’s philosophy, and any sane human being would not want to live off handouts, or going around begging because foreign aid is only needed as short term relief for countries coming out of calamities. Rwanda needed help to so it could emerge out of the ruins of genocide. Once it did, it became less interested on the foreign aid now a success economic story in Africa

Foreign aid is a form of slavery which creates a false sense of entitlement. It confines a beggar into a psychological and mental prison of his own creation, becoming incapable to make any meaningful decision of his own. He does not think on how to get out of his difficulties as long as he knows that, someone somewhere will help him.

CHADEMA party believes that all too often, foreign aid creates dependency by the receiving country onto the giving country and winds up in the pockets of corrupt rulers.

Foreign aid money are your taxes, your sweat which should work for your benefit not for people sitting on their wealth. More important than your dollars, are your brain trust, investments and technological advantage. This is what we need to utilize our resources and also in planning for years beyond our non-renewable resources

Our country rich in resources is being exploited by foreign entities, while our President is busy trotting the world begging for mosquito nets. With our resources, we can make our own mosquito nets without them being donated to us. Chadema party which I represent is poised to changed that, and the most important tool we need is the development of human capital

We need our resources to benefit our people. We need to create jobs for our people, we need to improve our health care, we need to improve our education, our infrastructures, communication and economy as a whole. And this is only possible if can with the wealth that we have all we need is better education for our people

We are currently having inequitable trade, where far eastern countries are exporting their poor populations to compete for jobs with our citizens. They are even exporting to us their prisoners to work on our roads yet millions of our young men have no jobs. This is not possible in any civilize society, unfortunately, because our rulers have signed contacts shrouded in secrecy whose contents are only known to them

Some of these individuals have turn to insult us as a nation. They are now interfering on our sovereignty, publicly aligning themselves with political parties. A whole ambassador standing on a political platform to address a political rally, and has ignored the public call for him to leave the country!

This is not the kind of trade we are looking for. We are looking for partners that will work with us to develop our resources in order to benefit our people; Partners that will bring to our country new skills, and also create jobs for our graduates. We need your expertise so we can turn our country into a bread basket of Africa. America is the world’s land of milk and honey where everyone wants to be, that’s the model we want to learn from

Well, we have come to realize, that if you feed us today with your milk and honey, our meals for tomorrow may not be guaranteed. We instead want to know how you made your country into a land of milk and honey so we can be able to feed ourselves for unforeseeable future and also feed the rest of the world. We have the potential but lack the expertise, and the know how is what we need

Tanzania is not an island; it is part of the global community where all humans have the liberty to visit whenever they want. Our boarders are open for all, as long as our laws and culture are respected. All we need is trade partnership that will guarantee fifty-fifty trade, in which the country benefits equally with the investor.

The younger American generation, I am inviting you to visit Tanzania; I am talking to you as the investors of tomorrow. Come and explore the endless possibilities my country has for you. We need investors that will bring into our country, a set of skills and creativity to turn our hardwood into high quality, made in Tanzania products, as opposed to bringing cheap furniture made of plywood while hauling away our valuable timber

Chadema party believes on the free market economic philosophy in which individual creativity is rewarded. We need your partnership in fostering individual innovation within our people. We don’t need your tax money; neither do we need your mosquito net donations, we need your skills.

We don’t need shoe boxes, we need to know how to make our own shoes. We need your technological know how
CHADEMA party’s priority number one is education! Priority number two is education and so is the priority number three.

We believe on education to be the only way for Tanzania to rise from the abject poverty it is in today. We have no alternative but train our young people who will in turn, employ their intellectual creativity into full practice to enable Tanzania become an economic giant in a continent long forgotten

Samford is one of the American’s finest educational institutions. It is producing some of the world finest, from school teachers to the finest lawyers. It is my hope that we see your institution open its doors to our support and in preparing Tanzania’s aspiring scientists, teachers, and accountants to become innovators.

In our effort to make our country a unique success story, I am challenging you the young people to go out to the world, and open new trails for others to follow. Tanzania has its doors open for you

Thank you all for listening.

Dr Slaa afanya mahojiano na radio mbili za kitaifa nchini Marekani


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa ambaye yupo kwenye ziara ya "VISION TANZANIA" nchini Marekani,. leo amefanya mahojiano na vituo viwili vya radio hapa nchini kueleza mambo mbalimbali kuihusu Tanzania.
Saa tatu asubuhi kwa saa za Marekani ya Mashariki, Dr. Slaa alikuwa katika studio za 93.1 WIBC Indiannapolis kwenye Garrison Show
0 comments

Dr. Slaa Awaonya CCM na Kikwete Kutokufanya Usanii Na Maisha Ya Watanzania

Dr. Slaa Awaonya CCM na Kikwete Kutokufanya Usanii Na Maisha Ya Watanzania

 

Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilibrod Slaa akiendelea na ziara yake iliyopewa jina la “Vision Tanzania” leo ametembelea chuo kikuu cha Indiana ambako ametembelea kitivo cha utafiti wa nishati mbadala “Center for Renewable Energy” ambako alilakiwa na Vice Chancellor wa Chuo hicho.

Dr. Slaa amependezwa kuona jinsi wanafunzi na wanajeshi wanavyoshirikishwa katika utafiti kwa manufaa ya nchi. Dr. Slaa alijionea mashine ya ndogo ya aina yake inayotumia takataka na hata majani kutengeneza umeme pamoja na gesi ya hydrogen kwa wakati mmoja, mtambo uliogunduliwa kwa ushirikiano kati ya chuo kikuu cha Indiana na Jeshi la Marekani. 

Bahati mbaya wanafunzi kama hawa nchini kwetu serikali imewanyima nafasi ya kukuza vipaji vyao na kutusaidia kwenye maswala ya utafiti. Wanajeshi wetu waadilifu, wachapakazi na wazalendo wamekatishwa tamaa. Gari la nyumbu walilotengeneza linaoza na mradi mzima umekufa. Wastaafu wametelekezwa hadi malipo yao wanadhulumiwa na serikali dhalimu ya CCM. Hiyo ndiyo CCM

Kwa miaka zaidi ya 50, serikali ya CCM imekuwa ikitoa ahadi za kumaliza tatizo la umeme. Mpaka sasa, CCM bado wanaendelea na ahadi zao kana kwamba watanzania bado wamelala. Ni swala la fedheha na aibu kubwa kwa nchi kama Tanzania kuzunguka kuomba misaada wakati tunacho kila tunachohitaji kujitengenezea umeme wa kutosha alisema Dr. Slaa

Tanesco ambayo ingekuwa inatutengenezea umeme wa kutosha kwa matumizi yetu na kuuza nje ya nchi umeme wa ziada, imegeuka kuwa shamba la bibi na kichaka cha mafisadi. Wizara nayo imekuwa makao makuu ya matusi kwa wawekezaji na watanzania. Waziri muhongo badala ya kutafuta suluhisho ya matatizo yeye amekuwa mtambo wa matusi. Anawaambia watanzania wakawekeze kwenye juice na matunda. Hii ndio maana tunasema kwamba CCM ni janga la mtanzania

Tunachotaka kujua ni Uhusiano wa Symbion na serikali ya CCM. Tunataka kujua hii kampuni ya Symbion inamilikiwa na nani . Kwa sababu ni hii Symbion ndiyo ilitokana na Dowans ambayo ilizaliwa na Richmond. Makampuni ambayo yanatafuna kodi zetu hadi wa leo. Wanatudanganya watawashtaki mafisadi wa Tanesco, tunawaomba waanze na mafisadi papa wa EPA na Richmond

Rais Kikwete na CCM wamekuwa janga. Leo Kikwete anaagiza shule zote za kata ziwekewe umeme. Umeme gani wanaozungumzia na utatoka wapi wakati wameshindwa katika kipindi cha miaka zaidi ya hamsini. Watanzania wamechoshwa na usanii. CCM wamebaki kugawana vyeo kindugu na kirafiki. Hawana uchungu na nchi, wanachojali ni kiasi gani wataweza kuiba. Inabidi watanzania wajitayarishe kuin’goa CCM madarakani kupitia sanduku la kura alisema Dr. Slaa.



Mwanafunzi wa Kitanzania katika chuo cha Indiana akimpokea Dr. Slaa

Kutoka Kushoto, Mwanafunzi wa Kitanzania, Dr. Slaa, mwanajeshi mtafiti pamoja na Mwenzie ambaye ndiye kiongozi wa utafiti

Dr. Slaa akikagua mtambo wa utafiti uliogunduliwa na Wanafunzi na walimu katika chuo cha Utafiti wa Indiana. Mtambo ni wa kutengenezea gesi ya hydrogen pamoja na umeme mbadala (renewable energy) unaopatikana kutokana na takataka

Meya pamoja na mkuu wa polisi nao walikuja kumuona Dr. Slaa na kumkaribisha kwenye jiji lao

Dr. Slaa baadae jioni alikutana na wakurugenzi wa mashirika makubwa ya nishati (renewable energy) nchini marekani ambao wako tayari kufanya kazi na CHADEMA kuiletea Tanzania umeme wa bei nafuu. Baadhi ya hawa wawekezaji wamewahi kuja Tanzania lakini Tanesco kama kawaida yao wakawakwamisha. Chadema inajipanga kuwaletea watanzania unafuu wanaoulilia

Viongozi wa chuo kwenye picha ya pamoja na Dr. Slaa
0 comments

Serikali inatambua na kutuhamini ushiriki wa Wanawake-Mwalimu

Serikali inatambua na kutuhamini ushiriki wa Wanawake-Mwalimu

WAZIRI-PICHA1 c0a8e
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto ,Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya wasichana waelimishaji rika mkoa wa Tanga yaliyohusisha wasichana wapatao 150 kutoka wilaya za Muheza,Lushoto, Pangani,Mkinga na Tanga yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la maendeleo ya wanawake (TAWODE). (HM)

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto ,Ummy Mwalimu amesema serikali inatambua na kuthamini ushiriki wa wanawake katika shughulia mbalimbali za maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Mwalimu alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya wasichana waelimishaji rika mkoa wa Tanga yaliyohusisha wasichana wapatao 150 kutoka wilaya za Muheza,Lushoto, Pangani,Mkinga na Tanga yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuratibiwa na asasi ya kiraia ya (TAWODE) yenye makazi yake jijini Tanga.
Alisema hali hiyo inajidhihirisha katika malengo ya millennia,Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ikiwa ni mkakati wa pili wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (Mkukuta 11) na Sera ya Taifa ya wanawake na Jinsia ya mwaka 2000.
Naibu Waziri huyo alisema wizara yake inajukumu kubwa la kuwajengea uwezo wanawake na wanaume ili waweze kushiriki katika ngazi zote za utekelezaji wa miradi na mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kufaidika sawa kwenye maendeleo yao.
Aidha alisema jambo jengine ni kuhamasisha na kuwezesha jamii kuwapatia watoto haki ya kuishi,kuendelezwa, kulindwa,kutokubaguliwa na kushiriki katika maendeleo ya Taifa na hivyo itatoa miongozo ya kuzuia na kupinga aina zote za ukatili na ubaguzi wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
"Ni ukweli usiopingika kuwa ukimwendeleza mwanamke, umeendeleza Taifa zima na kuwekeza kwa mwanamke ni kuwekeza katika taifa endelevu "Alisema Mwalimu
Alitoa wito kwa wadau wote kuchukua hatua za kumuwezesha mtoto wa kike
na kushughulikia mazingira hatarishi yanayomkabili katika kipindi cha ukuaji ili wasipate mimba za utotoni ikiwemo maambukizo ya virusi vya ukimwi na kukosa au kupunguza fursa zake mbalimbali za kujiendeleza.

Awali akuzungumza katika mafunzo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa TAWODE
,Fatuma Hamza Mganga alisema madhumuni ya semina hiyo ni kuwajengea
uwezo wasichana wenye umri kati ya miaka 10 mpaka 24 na kuchochea
uwezo na ubora wa kutambua ueledi na umuhimu wao katika maendeleo yao
na jamii kwa ujumla.

Mganga alisema pia semina hiyo ilikuwa na madhumuni ya kuwawezesha
katika kujiamini,kujitambua na kuthubuti. Chanzo: Oscar Assenga

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger