Featured Post Today
print this page
Latest Post

3 wazuiliwa kwa mauaji ya watoto A Kusini

3 wazuiliwa kwa mauaji ya watoto A Kusini



Mtaa wa Dieplsloot una watu wengi wanaoishi kwa umaskini.

Watu watatu wamezuiliwa nchini Afrika Kusini kuhusiana na mauaji ya watoto wawili ambayo yalizua ghasia katika mtaa wa Diepsloot.
Kwa mujibu taarifa ya polisi, miili ya wasichana wawili walio na umri wa miaka miwili na mitatu ilipatikana imetpwa kwenye choo cha umma siku ya Jumanne baada ya wawili hao kupotea siku ya Jumamosi.
Ghasia zilizuka huku wenyeji wakiwatuhumu polisi kwa kukosa kulinda jamii ipasavyo.
Rais Jacob Zuma aliwasihi wasichukue sheria mikononi mwao.
"kitendo hiki cha unyama dhidi ya watoto wetu, sio kitu ambacho kinapaswa kufanywa katika jamii hii ambayo daima tunajitahidi kuiunda,'' alinukuliwa akisema Rais Zuma kwenye jarida moja la mtaani Soweto.
''Tunalaani vikali mauaji haya.''
Luteni kanali Lungelo Dlamini, alisema kuwa watu watatu wanahojiwa na polisi na kuwa wangali wanamsaka mtu wa nne anayeshuiwa kuhusika na kitendo hicho.
Alisema kuwa pia wanachunguza kuwepo uhusiano kati ya mauaji hayo na yale ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano aliyepatikana amefariki katika eneo hilo hilo, mwezi Septemba.
Kulingana na jarida la Star wenyeji wa Diepsloot, jamii masikini Kaskazini kwa Johannesburg, waliweka vizuizi barabarani na kuchoma magurudumu ya magari.
Maduka yanayomilikiwa na raia wa kigeni, yaliporwa huku waandishi wa habari wakishambuliwa.
Wasichana haio walikuwa na uhusiano wa kifamilia , na walipotea Jumamosi nyumbani kwao wakiwa wanacheza na marafiki zao.


0 comments

Angalia kisima kinachodaiwa cha maajabu kilichopo kijiji chaa Iyumbu mkoani Dodoma

Angalia kisima kinachodaiwa cha maajabu kilichopo kijiji chaa Iyumbu mkoani Dodoma

KISIMANI 1 f3a53
Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM). MAJI 1 fb354
Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.
MAJI 2 f8953
Mkuu wa kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akinywa maji yaliyochotwa kisima cha Bwibwi kilichopo Kijiji cha Iyubu Manispaa ya Dodoma, Kisima hicho kinachoaminika ni cha maajabu na mtu anayetumia maji yake hupata Mafanikio ya kiafya na kimaisha: PICHA NA JOHN BANDA
0 comments

RC GALAWA AKABIDHI ZAWADI ZA RAIS KIKWETE KWA VITUO VIWILI TANGA.

RC GALAWA AKABIDHI ZAWADI ZA RAIS KIKWETE KWA VITUO VIWILI TANGA.


MKUU WA MKOA WA TANGA ,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA KULIA AKISALIMIANA NA AFISA MFAWIDHI WA MAHABUSU YA WATOTO JIJINI TANGA NG'WANZA MUHANGWA LEO KABLA YA KUWAKABIDHI ZAWADI KUTOKA KWA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE ZA SIKUKUU YA  IDD EL HAJI

KULIA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIMKABIDHI MBUZI AFISA MFAWIDHI WA MAHABUSU YA WATOTO  NGWANZA MUHANGWA WA KWANZA KUSHOTO ANAYESHUHUDIA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO NA DIWANI WA KATA YA USAGARA CARLOS HIZZA

KULIA MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIKABIDHI MBUZI KWA KITUO CHA KUTUNZA WAZEE MWANZANGE

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA ALIYESIMAMA AKIZUNGUMZA NA WAZEE WANAOISHI KATIKA KITUO CHA KUTUNZIA WAZEE MWANZANGE WA KUSHOTO KWANZA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO NA KULIA KWAKE NI DIWANI WA KATA YA DUGA MH.KOMBO

WAZEE WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA KWA UMAKINI MKUBWA LEO

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAZEE WANAOISHI KATIKA KITUO CHA KUWATUNZA WAZEE MWANZANGE MARA BAADA YA KUWAKABIDHI ZAWADI ZA IDDI EL HAJ KUTOKA KWA MH RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE.
MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIKABIDHI ZAWADI ZA SIKUKUU YA IDDI EL HAJI ZILIZOTOLEWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,MH JAKAYA MRISHO KIKWETE WAZEE WANAOISHI KWENYE KITUO CHA KUWALEA MWANZANGE JIJINI TANGA.

PICHA ZOTE NA PASKAL MBUNGA,TANGA.
TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga ,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa leo amekabidhi zawadi zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwet kwa vituo viwili kwa ajili ya sikukuu ya Idd El Haji.
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na mbuzi mmoja kwa kila kituo,mchele,mafuta ya kupikia,chumvi na sabuni.
Vituo hivyo ni kituo cha mahabusu nya watroto cha barabara ya 15/16 na kituo cha kutunzia wazeee cha mwanzange vyote vya jijini Tanga.
Awali akisoma kwa mkuu wa mkoa wa Tanga,Afisa Ustawi wa Jamii kwenye kituo hicho,Clara Kibanga walimshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kikwete kwa kuwapatia msaada huo na kuwakumbuka wazee.

Katika msafara huo kulikuwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Juliana Malange na wakuu wa idara kutoka halmashauri ya Jiji la Tanga.

RC TANGA AKERWA NA UCHAFU KATA YA USAGARA NA MZINGANI.

MKUU WA MKOA WA TANGA AKITOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WA KATA YA MZINGANI NA USAGARA BAADA YA KUKERWA KUTOKANA NA UCHAFUA ULIOKITHIRI MAENEO YA KATA HIZO.
Na Oscar Assenga,Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Jiji la Tanga Juliana Malange kuwasimamishia mshahara wa mwezi wa kumi maafisa watendaji wa kata Mzingani na Usagara kutokana na maeneo yao kukutwa yakiwa machafu.

Amesema wasimamishiwe mishahara hiyo mpaka hapo mkurugenzi atakapokwenda kuyakagua maeneo hayo na kuyakuta kwenye hali ya usafi na baadae ampelekee taarifa mkuu huyo wa mkoa ili aruhusu wapewe mishahara.

Gallawa ametoa agizo hilo wakati alipotembelea maeneo hayo kuangalia hali ya usafi ambapo alibaini baadhi ya maeneo kuwa na uchafu uliokithiri na ndipo alipotoa kauli hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kila mara anapopita katika maeneo hayo huyakuta machafu kila siku kitendo ambacho kinalifanya eneo hilo kutokuwa katika mandhara nzuri.

Maafisa watendaji hao ni Said Bendera ambaye ni mtendaji wa kata ya Mzingani na Senyenge Mbaruku wa kata ya Usagara.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga asema wakati wa ziara yake ya kuzunguka maeneo mbalimbali jijini Tanga mtaa utakaokutwa na uchafu atawajibika Afisa Mtendaji.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka maafisa watendaji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala la usafi katika maeneo yao ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya nzuri.

Hata hivyo watendaji hao walimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuwa watahakikisha ndani ya wiki moja maeneo yao yatakuwa katika halai nzuri ya usafi.
0 comments

MAMA WA MWANDISHI NA MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO, ANASTAZIA PETER UFOO ALIPIGWA RISASI TANO MWILINI MWAKE NA KUPELEKEA KUFARIKI DUNIA KATIKA MAUAJI YALIYOFANYWA NA MZAZI MWENZAKE UFOO NYUMBANI KWAKE KIBAMBA MKOANI PWANI.


MWILI wa Anastazia Saro, mama mzazi wa mtangazaji na mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita, ulifanyiwa uchunguzi jana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), na kukutwa na risasi tano.

Anastazia aliyeuawa wakati akisuluhisha ugomvi kati ya binti yake Ufoo na mzazi mwenzie, Anthery Mushi, alikutwa na risasi hizo katika sehemu kadhaa za mwili wake.


Mushi mbali na kumuua Anastazia, pia alimjeruhi kwa risasi Ufoo kisha kujilipua mwenyewe na kufariki dunia papo hapo.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Allelio Swai, Mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya Anastazia wakati akizungumza muda mfupi kabla ya mwili huo kutolewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, na kupelekwa Kibamba kwa ajili ya ibada ya mazishi tayari kusafirishwa kwenda Machame kijiji cha Shari kwa ajili ya mazishi leo.

Swai alisema kuwa katika uchunguzi wa mwili huo ambao hata hivyo, hakumtaja daktari aliyeufanya, baadhi ya ndugu wa marehemu walihudhuria.

Swai alifafanua kuwa risasi hizo zilikutwa katika maeneo ya mapafu, maini na tumbo.

Kwa mujibu wa Swai mwili huo ulitakiwa kufanyiwa uchunguzi mapema asubuhi, lakini ulichelewa kutokana daktari huyo kuwa na majukunu mengine, walilazimika kusubiri kwa muda.

Mwili wa mama huyo uliondolewa hospitalini hapo saa 7:30 mchana baada ya kukamilika kwa taratibu zote.

Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili huo na kuondoa risasi hizo, alikataa kuzungumza chochote zaidi ya kusema: “Siwezi kulizungumzia jambo hili kwa kuwa nimeshakamilisha nilichotakiwa kukifanya.”

Baadhi ya ndugu wa marehemu Anastazia waliokuwapo eneo hilo na walioshuhudia uchunguzi wa mwili, walisikika wakisema kuwa kitendo alichokifanya Mushi ni cha kinyama kutokana na kutumia risasi nyingi kumuua ndugu yao.

Wakati huo huo, Ufoo hataweza kushiriki mazishi ya mama yake kutokana na matibabu anayoendelea kuyapata, hospitalini hapo.

Swai aliiambia NIPASHE kuwa walimtaarifu Ufoo juu ya mipango ya mazishi ya mama yake na kwamba naye ametoa ruhusa ili mama huyo azikwe hata kama yeye (Saro) hataweza kuhudhuria mazishi hayo kutokana na hali yake.

“Niliongea na Ufoo ili kumfahamisha kuhusu mipango ya mazishi naye alitutaka tuendelee na mipango hiyo hata kama yeye atashindwa kumzika mama yake, lakini cha msingi alituomba tuhakikishe kuwa mama yake anazikwa salama,” alisema Swai.

MWANASAIKOLOJIA AMZUNGUMZIA MUSHI
Wakati hayo yakijiri, Mhadhiri Mwandamizi katika mambo ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Kitila Mkumbo, amesema kulingana na taarifa za mauaji ambazo amekuwa akizisoma kwenye vyombo vya habari juu ya mauaji hayo yalivyofanyika, ni dhahiri muuaji alikuwa amefikia ngazi ambayo hasingeweza kuacha kufanya unyama huo.

Alisema mtu huyo alikuwa amejiandaa kufanya tukio hilo kwa muda mrefu kimkakati na kimaandalizi.

Alifafanua kuwa mhusika wa tukio hilo alikuwa ameshafikia katika hatua ya mwisho ya maamuzi inayoitwa tafsiri ya akili ambayo huwa ni vigumu kwa mtu kujizuia kutenda jambo.

Alisema kuna hatua tatu ambazo ni stress (msongo wa mawazo), depression (sonona) na tafsiri ya akili ambazo mtu anaweza kuzipitia kabla hajachukua maamuzi.

“Kuna kitu kinaitwa fluctuation, lazima kilitokea kati yake na familia hiyo siyo bure, lakini angekuwapo yeye mwenyewe angetueleza, sisi hatuwezi kujua,” alisema Dk. Mkumbo.

Dk. Mkumbo alisema kuwa sehemu aliyokuwa anafanya kazi marehemu Mushi (Darfur) siyo kigezo kikubwa cha kuamua kufanya tukio lile japokuwa watu wengi wanaoishi katika mazingira ya kuona maiti za watu huwa ni wepesi kuua.

Alisema hicho siyo kigezo cha marehemu kufanya kitendo hicho kwa kuwa hakuna mwanadamu asiyeogopa kifo.

Kuhusiana na iwapo wanajeshi wanaotoka katika operesheni za kijeshi nje ya nchi kama wanapatiwa ushauri (councelling), Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Erick Komba alisema: “Mafunzo anayopata mwanajeshi yanalenga kumjenga na kumpa uwezo wa kuyakabili mazingira mbalimbali ndani na nje ya nchi kimaumbile na kisaikolojia,” alisema.

Meja Komba alisema mwanajeshi ana uwezo wa kuishi kwenye mazingira yoyote kwa kipindi kirefu kijasiri.

“stress management-(jinsi ya kubaliana na msongo) inafanyika vizuri kwa kufanya michezo mbalimbali kwa pamoja ambayo inaimarisha fiziki (ukakamavu),”

Aliongeza kuwa maisha ya mwanajeshi ni ya umoja na ushirikiano, kitu ambacho kinamfanya ayakabili mazingira yake vizuri, na kuweza kutekeleza majukumu ya jeshi kiufasaha na kiuweledi.

Alisema kwa kipindi wanapokuwa katika operesheni mbalimbali za ulinzi wa amani pamoja na mambo mengine wanapewa ushauri.

HALI YA UFOO YAZIDI KUIMARIKA
Ofisa Habari wa MNH, Aminiel Aligaesha, alisema jana kuwa hali ya Ufoo inaendelea vizuri kulinganisha na siku za nyuma.

Alisema kwa sasa yupo katika jengo la matibabu ya moyo na kueleza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya daktari anayemuhudumia, Ufoo anahitaji mapumziko zaidi.

“Kwa sasa Ufoo haitaji kuonana na mtu, anahitaji kupumzika zaidi kama daktari alivyoniambia na kwa kifupi yupo katika wodi ya kawaida tu,” alisema Aligaesha.

SIMANZI YATAWALA KUAGA ANASTAZIA
Mwili wa marehemu Anastazia uliagwa jana katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibwegele Kibamba Shule kabla ya kuelekea kijiji cha Shari Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.

Waumini na wanakwaya ya Uinjilisti wa Kanisa hilo waliangua vilio baada ya jeneza la mwili wa marehemu ambaye alikuwa mwanakwaya na mweka hazina wa kanisa kufika kanisani hapo.

Kadhalika, ibada iligubikwa machozi na simanzi, hali iliyosababisha kusimama kwa muda.

Mchungaji wa Kanisa hilo, Magret Shekolowa, aliwaeleza waumini hao kuwa na moyo wa subira hasa katika kipindi hiki na kuwataka kuacha kulia badala yake waiombee Tanzania kwani kumekuwa na matukio mengi ya mauaji ya kinyama.

Akitoa salamu za rambirambi Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhavile, huku akitokwa na machozi ya huzuni alisema: “Jana nilikwenda kumuona Ufoo akaniomba nitoe salama za mwisho nisimame kwa niaba yake, nami nasema poleni sana.”

Marehemu alizaliwa mwaka 1957 huko Mbulu mkoani Arusha na alifariki juzi baada ya kushambuliwa kwa risasi tano na Mushi.
Chanzo:nipashe
0 comments

JE,HUYU MWANAMKE ALISTAHILI ADHABU HII YA KUCHOMWA NA KISU JICHONI!!


JE,HUYU MWANAMKE ALISTAHILI ADHABU HII YA KUCHOMWA NA KISU JICHONI!!
Mwanamke mmoja ambaye mpekuzi wetu toka Nigeria hakuweza kulitambua jina lake amechomwa kisu jichoni na mume wake baada ya kufumaniwa akigawa tunda kwa mwanaume mwingine ambaye ni rafiki yake wa damu....


Inaarifiwa kwamba, mume wake alipewa taarifa na jirani yao kwamba mkewe yuko ndani na mwanaume mwingine ambaye ni rafiki yake....

Baada ya taarifa hiyo, mume huyu alifunga safari kuelekea kwake na akamkuta mkewe akisaliti penzi lao ndani ya kitanda chao..


Kitendo hicho kiliongeza hasira kwa jamaa huyo ambaye alijikuta akimchoma mkewe kisu jichoni.
0 comments

MCHUNGAJI WA KANISA ASHIKWA AKITAZAMA PICHA ZA NGONO INTERNET CAFE.

MCHUNGAJI WA KANISA ASHIKWA AKITAZAMA PICHA ZA NGONO INTERNET CAFE.

A pastor escaped a beating yesterday after he was rescued by members of his congregation when he was caught red-handed watching p*rn at a cybercafé in Kisumu town.
0 comments

HUU NDIO MUAFAKA ULIOFIKIWA KATI YA RAIS KIKWETE NA KAMBI YA UPINZANI JUU YA VUGUVUGU LA KATIBA MPYA

HUU NDIO MUAFAKA ULIOFIKIWA KATI YA RAIS KIKWETE NA KAMBI YA UPINZANI JUU YA VUGUVUGU LA KATIBA MPYA

 
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana mambo mawili makubwa baada ya kuweka pembeni tofauti za kiitikadi na kutanguliza masilahi ya taifa walipokutana jana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliitishwa na Rais Kikwete ili kuondoa sintofahamu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa Septemba na Bunge lilipokutana mjini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana jioni ilisema katika mkutano huo ilikubaliwa kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya sheria hiyo.
Pia Rais na vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa lengo la kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
“Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini,” iliongeza taarifa hiyo.
Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, Isaack Cheyo ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na Nancy Mrikaria ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema. Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.
Wengine ambao waliambatana na wenyeviti wao ni Mohamed Mnyaa na Julius Mtatiro wa CUF, Tundu Lissu na John Mnyika wa Chadema na Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.
Vicheko Ikulu
Vicheko na bashasha vyatawala Ikulu
Ilikuwa fursa kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi hao baada ya kipindi cha miezi miwili cha kurushiana maneno baina ya viongozi wa Bunge, Serikali, CCM waliokuwa wakivutana na viongozi wa vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi.
Kama mtu yeyote angeulizwa kutabiri katika tukio lililotokea jana lingetokea basi angekuwa na wakati mgumu kutokana na ukali wa maneno na malumbano katika kipindi chote baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge wa Septemba.
Rais Kikwete alionekana mwenye furaha tele wakati alipokutana na viongozi wa vyama hivyo na kivutio zaidi ilikuwa pale alipokutana na Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Tundu Lissu.
Viongozi hao walisalimiana huku wote wakitabasamu na kuashiria kuwa waliamua kuweka tofauti zao pembeni na kuangalia masilahi ya nchi.
Kumbuka katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Septemba, Rais Kikwete alimshutumu Lissu kwa kusema kwamba katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa yeye hakuheshimu mawazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Rais Kikwete alikaririwa akisema kauli hiyo ya Lissu ni uzushi, uongo na uzandiki wa hali ya juu, huku akisisitiza kuwa mbunge huyo alitoa kauli hiyo ili kupotosha ukweli na pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wajumbe 166 wa Bunge Maalum la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alipinga tuhuma hizo na kusisitiza Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) bila ya ridhaa yao.
Chikawe, Wassira na Lukuvi ndani
Mawaziri watatu, ambao walitetea kwa nguvu kupitishwa kwa muswada ule ndani na nje ya Bunge walihudhuria mazungumzo hayo.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira walikuwemo kwenye mazungumzo ya jana.
Mawaziri hawa kwa nyakati tofauti walitetea kuwa mchakato wa muswada ule haukuwa na matatizo yeyote na kushikilia kuwa lazima Rais lazima asaini muswada kwani ulikuwa umepitishwa kihalali na Bunge.
Pia walikuwa wameshikilia kuwa safari hii kulikuwa hakuna mambo ya mazungumzo kati ya Rais na upinzani.

Chanzo cha sintofahamu
Wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wa muswada huo wakipinga matayarisho yake kutoshirikisha upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya muswada huo.
Katika hatua nyingine, taarifa kutoka Ikulu zilisema kwamba Rais Kikwete alisaini muswada huo tangu Oktoba 10 mwaka huu siku ambayo wapinzani walipanga kufanya maandamano nchi nzima.
Katika mahojiano na Mwananchi jana jioni, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema muswada huo tayari ulikwishasainiwa na Rais na kama kuna marekebisho yatafanywa.
Mwananchi ilimtafuta Rweyemamu baada ya kusikia akithibitisha kusainiwa kwa muswada huo katika mahojiano na BBC Idhaa ya Kiswahili jana.
Akizungumza na Mwananchi Rweyemamu alisema, “Rais ameshasaini tangu Oktoba 10, unajua kulikuwa hakuna tatizo lolote kuhusu muswada huu kwa sababu ulifuata taratibu zote bungeni.”
Rweyemamu alisema kuwa awali Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais atakutana na wapinzani, pia atausaini muswada huo.

“Muswada umepitishwa bungeni na yeye amekamilisha kazi kwa kuusaini ili kuwa sheria. Alipokutana na wapinzani leo (jana) amewaeleza hilo na wameridhika” alisema Rweyemamu.


0 comments

Dk Shein:Hakuna maendeleo bila amani

Dk Shein:Hakuna maendeleo bila amani

baraza_586f6.jpg

Wafuasi wa dini ya Kiislamu jana waliadhimisha Idd El-Haj katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania huku Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akitaka Watanzania wasahau suala la maendeleo bila ya amani na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) likimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kukutana na wapinzani.
Akihutubia Baraza la Idd El-Haj jana katika Chuo Kikuu cha Taifa (Suza) kilichoko Mkoa wa Kusini Unguja,Dk Shein alisema mipango ya maendeleo ya nchi haiwezi kufikiwa bila ya kuwapo kwa mazingira ya amani na utulivu.

Alisema vitendo vya hujuma dhidi ya raia vinavyofanyika kwa kutumia tindikali lazima vipigwe vita na wananchi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini. "Inafaa tuelewe kuwa, bila ya amani hatutoyafikia malengo tuliyojiwekea ya kuendeleza ustawi wa nchi yetu na watu wake,"alisema Dk Shein.

Dk Shein alisema kwamba vitendo vya hujuma dhidi ya raia wasiokuwa na hatia vimekuwa vikisababisha hofu kwa wananchi na wageni na vinakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu dhidi ya waja wake.

Aidha alisema watalii wanaotembelea Zanzibar wanavutiwa na ukarimu wa wananchi wake pamoja na hali ya amani na historia ya visiwa vya Zanzibar.

"Tusichezee wala tusidharau amani tuliyonayo badala yake,tuitunze na tuiendeleze kwani inapotoweka inachukua muda mrefu kuirejesha sawa na kujenga nyumba ni kazi kuliko kubomoa,"alisema Dk Shein.

Hata hivyo, aliwataka wananchi kuunganisha nguvu zao kupitia vikundi vya Polisi jamii kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuwafichua watu wanaotaka kuchafua sifa ya Zanzibar.
Alisema kazi ya kulinda amani ya nchi ni jukumu la kila mwananchi kuahidi Serikali itaendelea kuwasaka wahusika wa vitendo hivyo na kuhakikisha wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

Dk Shein alisema kuwa,Serikali itaendelea kutekeleze dira ya Maendeleo ya 2020 pamoja na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini kwa wananchi wake (MKUZA) na tayari ufanisi wa mipango hiyo umeanza kuonekana licha ya kuwapo changamoto.

"Uchumi wetu umekuwa kwa asilimia 7.0 kutoka 6.7 kwa mwaka 2011 tofauti na ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.3 katika Bara la Afrika,"alisema Dk Shein.

Bakwata wamempongeza Rais Kikwete siku moja baada ya Rais Kikwete kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema,Cuf,NCCR-Mageuzi,TLP na UDP,Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limepongeza hatua hiyo na kuita yenye manufaa kwa taifa.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam juzi,Rais na vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa lengo la kusukuma mbele mchakato huo kwa maslahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.

Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Suleiman Lolila akitoa salamu za Baraza la Idd jana katika Msikiti wa Al Farouk uliopo Makao Makuu ya Baraza hilo, Kinondoni Dar es Salaam,alisema uamuzi wa Rais Kikwete una lengo la kuhakikisha mchakato wa Katiba unaoendelea unamalizika kwa amani.

Naye Mgeni rasmi kwenye baraza hilo, Waziri wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe, aliwataka Watanzania kuilinda amani iliyopo nchini na kuepuka ushabiki wenye lengo la kuhatarisha mustakabali wa amani nchini.

Imeandikwa na Mwinyi Sadallah, Ibrahim Yamola na Pamela Chilongola.
0 comments

Utafiti: Wasio na elimu waongoza kumpenda Rais Jakaya Kikwete

Utafiti: Wasio na elimu waongoza kumpenda Rais Jakaya Kikwete


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini (REPOA),Profesa Samuel Wangwe akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutoa matokeo ya utafiti uliongozwa na taasisi ya Afrobarometer. Picha na Silvan Kiwale.  

Na Goodluck Eliona, Mwananchi

  • “Asilimia 60 ya waliosoma elimu ya sekondari na kuendelea wanaunga mkono utendaji wa Rais, lakini 40 hawakubaliani na utendaji wake,” ilisema taarifa ya matokeo ya utafiti huo uliofanyika kati ya Mei hadi Juni mwaka jana.


Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebaini kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wenye elimu ya darasa la saba na wale wasiosoma, ndiyo wanaokubaliana na utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete.
Ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina la ‘Namna Watanzania wanavyouangalia utendaji kazi wa Bunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Asasi ya Afrobarometer, inaonyesha kuwa asilimia 77 ya waliokosa elimu ndiyo wanamuunga mkono Rais Kikwete.
Afrobarometa ni Asasi ya Kimataifa inayojumuisha taasisi tatu za Institute for Democracy ya Afrika Kusini, Ghana Centre for Democratic Development ya Ghana na Political Science Department ya Chuo Kikuu cha Michigan cha Marekani.
Mtafiti Msaidizi wa Afrobarometer, Stephen Mwombela akisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema asilimia 72 ya wale walioishia darasa la saba ndiyo wanamuunga mkono Rais.
Wakati asilimia 23 ya watu wasiosoma ndiyo hawamkubali Rais na asilimia 28 ya wale walioishia darasa la saba, pia hawaridhishwi na utendaji wa kiongozi huyo.
Mwombela, hata hivyo, alisema utafiti huo uliohusisha watu 2,400 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wasomi wa kiwango cha sekondari na kuendelea wanaunga pia mkono utendaji wa Rais, lakini siyo kwa kiwango cha juu kama wale ambao hawajasoma.
“Asilimia 60 ya waliosoma elimu ya sekondari na kuendelea wanaunga mkono utendaji wa Rais, lakini 40 hawakubaliani na utendaji wake,” ilisema taarifa ya matokeo ya utafiti huo uliofanyika kati ya Mei hadi Juni mwaka jana.
Matokeo ya utafiti huo yanatofautiana na yale ya mwaka 2008, ambayo yalionyesha kuwa wasomi walikuwa wanamuunga mkono Rais kwa asilimia 92.
Pia katika matokeo ya utafiti huo wa mwaka 2008, ulionyesha kuwa wasiosoma walimuunga mkono kiongozi huyo kwa asilimia 92.
Imani ya wananchi kwa Rais
Ripoti hiyo ilisema pia imani ya wananchi kwa utendaji wa Rais imeshuka hadi kufikia asilimia 74 kwa mwaka jana, tofauti na asilimia 94 ya mwaka 2005 wakati aliposhika wadhifa huo.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger