WANAODAIWA KUWA NI WAVUVI HARAMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO BAADA YA KULIPUKIWA NA MABOMU YAO WAKATI WAKIVUA

WANAODAIWA KUWA NI WAVUVI HARAMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO BAADA YA KULIPUKIWA NA MABOMU YAO WAKATI WAKIVUA

Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. (Picha na Elizabeth Kilindi)
 Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono.
 Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na barutiwakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono.
  Mmoja wa majeruhi waliolipukiwa na baruti wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. 

Elizabeth Kilindi, Tanga
Wakazi wawili wa kata ya Tangasisi tarafa ya Pongwe wilayani Tanga wamejeruhiwa vibaya viungo mbalimbali vya mwili  kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivua kwa kutumia dhana za uvuvi haramu kwenye kisiwa cha Karange.

Tukio hilo limetokea mnamo Novemba 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kisiwa  ambapo majeruhi hao wakiwa kwenye ngalawa yenye namab za usajili TTA 315 wakati wakijianda kutegesha baruti hizo ndipo zilipowalipukia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Freisse Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majeruhi hao kuwa ni Hamis Omari ambaye amekatika mkono wa kulia na ameumia jicho la kulia, huku majeruhi mwingine Adamu Selemani amekatika mikoni yote miwili, pamoja na kupoteza macho yote mawili.

“Hali ya majeruhi wote wawili ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo ni mbaya hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uvuvi haramu ulivyo na madhara makubwa kwa jamii pamoja na viumbe wa baharini “alisema Kamanda Kashai.

Kamanda Kashai alitumia fursa hiyo kuwa taka wakazi
wanaoishi maeneo ya bahari kutoa taarifa ya watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ili kuweza kuwachukulia hatua mapema kabla ya kutokea kwa madhara zaidi.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger