Featured Post Today
print this page
Latest Post

UKATILI WA KIJINSIA WAZIDI KUOTA MIZIZI MBEYA

UKATILI WA KIJINSIA WAZIDI KUOTA MIZIZI MBEYA

Mtoto Jesca Varelia 10   mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Mlimani sinde jijini Mbeya anatumikishwa na mama yake wa kambo kuuza mboga muda wa masomo  
Moja ya wateja wakinunua Mboga hizo toka kwa mtoto Jesca
   
0 comments

BREAKING NEWS: KLABU YA SIMBA SPORT CLUB YATIMUA MAKOCHA WAKE ABDALLAH KIBADENI NA MSAIDIZI WAKE, JAMHURI KIHWELU KISA....!!!!

Julio (kulia) na Kibadeni (kushoto) wameondolewa kazini. 

Julio na Kibadeni wameondolewa kazini baada ya kamati ya utendaji iliyokutana jana kufikia uamuzi kwamba wawili hao utendaji wao si sahihi.

Tayari Simba imekamilisha mazungumzo na kocha mwingine mzungu, si yule Bobby Willliamson ambaye aliandikwa na gazeti moja nchini kwamba ndiye kocha mpya wa Simba.
CREDIT GPL
0 comments

Kagame, Museveni na Kenyatta washtakiwa Korti ya Jumuiya

Kagame, Museveni na Kenyatta washtakiwa Korti ya Jumuiya

kagamepx_deab7.jpg

Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.(P.T)
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.

Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.

Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.
0 comments

SIMBA SC YAMSIMAMISHA RAGE, SASA NI VURUGU TUPU MSIMBAZI

SIMBA SC YAMSIMAMISHA RAGE, SASA NI VURUGU TUPU MSIMBAZI

Na Mahmoud Zubeiry, Kariakoo
KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC kilichokutana jana, kimefikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kwa kukiuka taratibu na maadili ya uongozi.
Rage amesimamishwa siku mbili tu baada ya kusajili wachezaji wawili wapya, akiwemo Awadh Juma pichani

Simba SC imeitisha Mkutano na Waandishi wa Habari ambao utafanyika saa 5:30 makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam kuelezea kwa undani suala hilo.
Wazi hatua hii inazidi kuivuruga klabu, kwani tayari aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ naye amejiuzulu na nafasi yake inashikiliwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Itang’are ‘Kinesi’.
Maana yake Simba SC inaendeshwa bila kiongozi Mkuu wa kuchaguliwa na hiyo inaweza kushinikiza uchaguzi haraka. 
HABARI ZAIDI ZITAFUATIA BAADA YA MKUTANO WA KLABU NA WAANDISHI WA HABARI.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger