Featured Post Today
print this page
Latest Post

BALOZI WA CHINA TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI.

BALOZI WA CHINA TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya uendelezaji wa Ardhi na Mipango miji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akimweleza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (kushoto) namna Wizara yake inavyoendelea kuimarisha shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania ulioitembelea Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Matumizi endelevu ya Ardhi.
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akitoa ufafanuzi kuhusu uendelezaji wa ushirikiano kati ya China na Tanzania katika katika sekta ya ardhi hususan utoaji wa mafunzo kwa watalaam wa Ardhi, Matumizi endelevu ya Ardhi na Mipango miji nchini.
0 comments

AJALI NYINGINE YATOKEA JIJINI MBEYA LEO, 10 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA

AJALI NYINGINE YATOKEA JIJINI MBEYA LEO, 10 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA

Pichani ni Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo wakiiangalia basi hiyo ikiwa kando kando ya mto Kiwira.
Wananchi wa Mji wa Kiwira wakienda kuangalia ajali hiyo.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kiwira wakiangalia Baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukuia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaid ya watu 10 waliokuwepo kwenye basi hilo wamepoteza Maisha.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.
Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.
Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.(Muro)
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger