Featured Post Today
print this page
Latest Post

WAGANDA WAHOJI FIFA OKWI KWENDA YANGA




Uongozi wa Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) umendika barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutaka kujua uhakika kuhusiana na mshambuliaji Emmanuel Okwi kuuzwa Yanga.

Taarifa zinasema katika mtandao wa MTNfootball kwamba OKwi alijiunga na Yanga kwa kitita cha sola 100,000 lakini Fufa kupitia bosi wake, Edgar Watson imetaka kujua uhalali kuhusiana na uhamisho wake.

Fufa kupitia Watson imetaka kujua kama ni sahihi kwa kuwa kwamba ni sahihi Okwi aliyepelekwa SC Villa kwa mkopo akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia kama anaweza kucheza Yanga.

Okwi alidumu SC Villa kwa miezi miwili akiichezea timu hiyo katika Ligi Kuu ya Uganda na kufanikiwa kufunga mabao matatu.

Lakini Mkurugenzi we SC Villa, Edgar Agaba ameiambia MTNFootball.com, Okwi alikuwa mchezaji huru kabla ya kwenda kujiunga na Yanga.

Okwi amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na kusababisha vurugu kubwa hasa Simba wanapinga kwa kuwa wanahitaji kulipwa fedha zao dola 300,000 kutoka Etoile du Sahel.
0 comments

AZAM FC WAFUNGA 'SOFA ZA HATARI' CHAMAZI, KOMBE LA SHIRIKISHO PALE PALE MWAKANI

AZAM FC WAFUNGA 'SOFA ZA HATARI' CHAMAZI, KOMBE LA SHIRIKISHO PALE PALE MWAKANI

Mafundi wakiendelea na zoezi la uwekaji wa viti vya kisasa katika majukwaa ya Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Klabu ya Azam inataka kuutumia Uwanja huo kwa michuano ya Afrika pia mwakani na inapambana na muda kuhakikisha uboreshaji unakamilika mapema ili mechi zake za Kombe la Shirikisho icheze hapo mwakani.
Siti za kulala
Hiki ni moja ya vyumba vya kubadilishia nguo kwa ajili ya timu, unaweza kujionea ni cha kisasa kabisa
Mafundi wamemaliza kazi ya kupaka rangi na sasa mabinti wanafanya usafi
Chumba cha mikutano, ni cha hadhi ya juu
Eneo hili ndilo timu zitakuwa zinatokea kuingia uwanjani
0 comments

SIMBA SC KAMILI GADO ZENJI, LOGARUSIC RAHA TU IVO NA OMWANWA NDANI YA NYUMBA, YANGA WAANDAE KAPU JUMAMOSI TAIFA

SIMBA SC KAMILI GADO ZENJI, LOGARUSIC RAHA TU IVO NA OMWANWA NDANI YA NYUMBA, YANGA WAANDAE KAPU JUMAMOSI TAIFA

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KIKOSI cha Simba SC kimekamilika kambini eneo la Chukwani, Zanzibar kufuatia wachezaji wapya kutoka Gor Mahia ya Kenya, kipa Ivon Philip Mapunda na beki Donald Mosoti Omwanwa kujiunga na wenzao jana visiwani humo, tayari kwa mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na wachezaji hao wawili waliosajiliwa wiki iliyopita, wachezaji wengine wapya waliosajiliwa dirisha dogo, kiungo Awadh Juma na mshambuliaji Ally Badru nao pia wameingia kambini jana.
Beki 'Adui'; Donald Mosoti Omwanwa tayari yuko kambini na Simba SC Zanzibar

Badru na Awadh walikuwa na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, michuano iliyomalizika Alhamisi iliyopita nchini Kenya.
Kocha mpya wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic ameingia kambini na wachezaji wote waliosajiliwa kuandaa kikosi cha kuiadabisha Yanga Jumamosi Uwanja wa Taifa.    
Furaha zaidi kwake ni kwamba, wachezaji alioomba mwenyewe wasajiliwe Ivo na Omwanwa wamewasili mapema na sasa Jumamosi atakuwa na jeshi kamili la kuanzisha zama zake mpya Simba SC.
Simba SC ambayo mara ya mwisho ilitoa sare ya 3-3 na Yanga ikitoka nyuma kwa mabao 3-0 hadi mapumziko, inaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuoni na inatarajiwa kurejea Dar es Salaam siku moja kabla ya mechi ya Mtani Jembe.
0 comments

DK. SLAA AWAHIMIZA WANACHUO KUTUMIA ELIMU YAO THABITI KUWAAMSHA WANATABORA DHIDI YA ELIMU YA MAENDELEO, SOMA ZAIDI HAPA

DK. SLAA AWAHIMIZA WANACHUO KUTUMIA ELIMU YAO THABITI KUWAAMSHA WANATABORA DHIDI YA ELIMU YA MAENDELEO, SOMA ZAIDI HAPA



Dk. Slaa, katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Akiongena kwa takribani masaa mawili na wanachuo kikuu kishiriki cha SAUT leo jioni katika ofisi za kanda hapa mkoani Tabora.








Dk. Amesisitiza vijana wenye elimu iwe tunu ya manufaa ya Watanzania kwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya fikra za wananchi walio wengi kwani wanawategemea sana wao kama wasomi waliofanikiwa kupata elimu inayowasaidia kupambanua mambo kwa uelevu zaidi.

Akisisitiza, amesema uwepo wa wanavyuo hao iwe mfano wa kuigwa si tu katika kupanua wigo wa kisiasa ila hata katika maendeleo ya wananchi katika fikra zao kwanza kwani wimbi la wanasiasa linaweza sahau kuhimiza maendeleo ikiwa ndio sehemu na chachu ya ugumu wa maisha ya wananchi walio wengi. Alodai kuwa maendeleo yeyote yale hayaji kwa miujiza ila kwa utendaji madhubuti ambao vijana wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kufanikisha hilo.

Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na baadhi ya wanachuo waliouliza juu ya migogoro mingi iliyomo katika chama hicho pinzani alijibu na kusema kuwa migogoro mingi inapikwa ili kukivunja nguvu chama hicho.

0 comments

TAZAMA PICHA JINSI ILIVYOKUWA NDANI YA PANTONI BAADA YA KIVUKO KUPOTEZA MWELEKEO MCHANA WA LEO

TAZAMA PICHA JINSI ILIVYOKUWA NDANI YA PANTONI BAADA YA KIVUKO KUPOTEZA MWELEKEO MCHANA WA LEO



Ilikuwa ni mida ya saa nane mchana ambapo Pantoni kubwa ya Mv. Magogoni ikiwa imesheheni abiria ikiwavusha kutokea Posta kuelekea Kigamboni , ilipatwa na wakati mgumu baada ya kushindwa kutia nanga ili iweze kusimama na abiria waweze kushuka..
Tukio hilo ambalo chanzo chake kimetokana na Injini za Pantoni hilo kushindwa kufanya kazi  haikuweza kutia nanga kwa muda wote huo.. na ambapo kulikuwa na upepo mkali sana ambao ulisababisha  Pantoni hiyo kukosa muelekeo na kuanza kuambaa ambaa mpaka maeneo ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere kisha kusukumwa zaidi hadi eneo la bandari ya Zanzibar.
Hata hivyo baada ya hali kuzidikuwa si nzuri walilazimika kuita meli ndogo za uokoaji ambapo meli ya kwanza haikuweza kuvuta pantoni hiyo na kulazimika kuongeza meli nyingine ili iweze kuongeza nguvu pamoja na boti za Jeshi la polisi ambazo zote zilifika na kwa ushirikiano mkubwa ziliweza kufanikiwa zoezi hilo la kuirudisha pantoni hiyo katika eneo lake husika. 
Na abiria ambao walinusurika kuweza kushuka na kuendelea na shughuli zao za kawaida..

0 comments

KENYA YAFIKIA PABAYA MACHANGU DOA WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO.


KENYA YAFIKIA PABAYA MACHANGU DOA WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO.

Makahaba mjini Nairobi Kenya waliungana na wenzao duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga unyanyasaji dhidi yao.

Waliandamana Jumanne kulalamikia kile wanachosema ni unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi pamoja na askari wa baraza la jiji wakati wakiendesha biashara zao.

Walikusanyika katikati ya mji na kuelekea katika ofisi za baraza la jiji kuwasilisha malalamiko yao wakisema kuwa wamechoka kuhangaishwa na polisi na wanataka ulinzi.
Mwanaharakati wa maswala ya biashara ya ngono, John Mathenge aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji, alisema kuwa wengi wao wameuawa na kunyanyaswa hata na wateja wao pamoja na maafisa wa usalama.

Siku hii ya kimataifa, huadhimishwa kila mwaka tarehe 17.
Biashara ya ngono imeharamishwa nchini Kenya lakini baadhi ya watetezi wa makahaba wanasema kuwa katiba haijaeleza bayana ikiwa mtu atakayekamatwa akijihusisha na biashara hiyo achukuliwe hatua gani za kisheria.
Mathenge alielezea kuwa lazima watu wakome kuwabagua wanaofanya biashara ya ngono, kwani ni kazi kama kazi nyingine tu.
Wengi walilalamika kuwa jamii imepuuza watu wanaofanya biashara ya ngono wala haiwatetei wakati wanaponyanyaswa au kuuawa .
Ripoyi iliyotolewa mwaka jana kuhusu makahaba mjini Nairobi ilisema kuwa wanahangaiswa sana na askari wa baraza la jiji na kuwa wengi wao huachiliwa tu pindi wanapotoa rushwa.
0 comments

"KAMA SI KANUMBA YANGENIKUTA MAZITO.." LULU AFUNGUKA

"KAMA SI KANUMBA YANGENIKUTA MAZITO.." LULU AFUNGUKA

SURA ya mauzo katika sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ 

ametoa ya moyoni kuwa kama siyo kuwekwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya Segerea, Dar basi yangemkuta mazito.


Lulu alikaa Gereza la Segerea kwa takribani miezi kumi baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ 
aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.

Nyota huyo wa Filamu ya Foolish Age alifunguka mambo ya kushangaza hivi 
karibuni juu ya tukio hilo kupitia Kipindi cha Take-One, kinachorushwa  na 
Clouds TV.
 TATIZO FOOLISH AGE
Lulu alikuwa akizungumzia filamu yake hiyo ya Foolish Age ambapo 
alisema sinema hiyo inawasihi wasichana ambao wanapitia kipindi cha balehe 
ambacho ni hatari sana kwao.

“Kwa kweli kipindi cha foolish age ni cha hatari sana, nilicheza filamu hiyo
 ili kuwaasa wasichana wenzangu.
“Asikwambie mtu, mimi mwenyewe nilikokuwa nikielekea si kuzuri kabisa.

 KAMA SIYO KANUMBA
“Ukweli ni kwamba kama siyo matatizo (kifo cha Kanumba) nikaenda 
mahabusu sijui ingekuwaje sasa hivi. Kukaa jela kulinisaidia kusitisha kasi ya 
tabia yangu, nikatoka nikiwa mpya.
“Yangenikuta mazito zaidi maana kipindi kile ilikuwa hatari tupu,”
 alisema Lulu ambaye ni mrembo wa haja.
 Staa huyo aliongeza kuwa kipindi hicho kilikuwa cha hatari na hakitamani 
kijirudie hata kidogo katika maisha yake.
Alisema kwamba si ajabu inawezekana kipindi hicho ndicho kilisababisha 
matatizo yote yaliyomkuta. Alisema alikuwa akielekea kubaya.
 HATAKI KIJIRUDIE
“Ni kipindi ambacho siwezi kukuhitaji tena katika maisha yangu si kizuri 
na kinatisha maana kuna wakati nilikuwa sisikii la mtu yeyote hata mama 
yangu mzazi,” alisema Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu haonekani
 akirandaranda mjini kama zamani.

Kabla ya utulivu huo alioupata nyuma ya nondo, Lulu alikuwa hakauki 
kwenye kumbi za usiku za starehe huku akilewa tilalila na kuyaweka 
maisha yake hatarini endapo angefanyiwa kitu mbaya.

 Lulu alihusishwa na kifo cha Kanumba kwa kuwa siku ya tukio alidaiwa kuwa 
naye eneo la tukio ambapo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana 
akisubiri kesi ya kuua bila kukusudia.

0 comments

MILIONI 20 KUTUMIKA UKARABATI UWANJA WA CCM MKWAKWANI

MILIONI 20 KUTUMIKA UKARABATI UWANJA WA CCM MKWAKWANI

  Na Oscar Assenga,Tanga.

UONGOZI wa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga umetenga kiasi cha  sh.milioni 20 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo ambapo fedha hizo zitatumika kwa awamu mbili tofauti.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM),Gustav Mubba akiwa eneo la uwanja huo leo wakati harakati za kuukarabati zikiendelea

sehemu ya uwanja wa Mkwakwani ikiwa imetifuliwa kwa ajili ya ukarabati leo


Akizungumza na TANGA RAHA BLOG leo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(CCM) Gustav Mubba(pichani Juu)alisema awamu ya kwanza ya ukarabati huo ilianza tokea Novemba Mosi kwa kukarabati vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji pamoja na kuuweka imara mfumo wa maji taka na safi.

 

Mubba alisema matengenezo mengine ni ufumuaji wa mfumo wa kumwagilia maji uwanjani badala ya kuweka mpira uwanjani wanaweka mfumo wa kumwagilia kupitia mashine ya paipu.


Aidha alisema awamu ya kwanza inatarajiwa kutumia sh.milioni 7 mpaka kumalika kwakea na kiasi kilichobakia kitatumika kwa awamu inayofuatia lengo ni kuhakikisha uwanja huo unakuwa wa kisasa zaidi.

 

Alisema matengenezo mengine yatakayofanyika ni kuweka mageti ndani ya uwanja ili kuweza kuzuia mashabiki wa soka kuingia uwanjani mara baada ya mechi kumaliza ambapo suala hilo linasababisha vurugu kutokea au timu pinzani kuletewa fujo.


Katibu huyo alisema pia ukarabati huo utaendana sambamba na uwekaji upya wa mabenchi ya ufundi uwanjani ambayo hutumiwa na timu shiriki wakati wa michezo mbalimbali ikiwa inaendelea.
0 comments

MAGAZETINI LEO DESEMBA 19, 2013.

MAGAZETINI LEO DESEMBA 19, 2013.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger