MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA.
Latest Post
WANANCHI kOROGWE WAUKATAA MRADI WA UMWAGILIAJI
WANANCHI kOROGWE WAUKATAA MRADI WA UMWAGILIAJI
Korogwe.
WANANCHI
wa Kijiji cha Mswaha Darajani Kata ya Mswaha wilayani Korogwe mkoani
Tanga wamekataa kuupokea mradi wa umwagiliaji wa kijiji hicho kwa madai
ya kujengwa chini ya kiwango.
Hatua ya wananchi hao waliiweka bayana katika mkutano wa kijiji hicho ambao ulifanyika Novemba 7 mwaka huu katika mradi huo uligharimu zaidi ya milioni 42 kuanzia hatua za awali mpaka mwisho.
Kilichopelekea
mradi huo kukataliwa na wananchi hao mbele ya diwani wa Kata hiyo,Aweso
Omari ambaye aliambatana na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Paulo Mzava
kilitokana na ukuta wa kukingia maji uliojengwa kumepasuka na hivyo
kushindwa kutumika licha ya kugharimu fedha hizo.
Akizungumza
katika mkutano hao mmoja ya wananchi hao ,Juma Mussa alisema wanamuomba
mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwapelekea wataalamu ili waangalie
jinsi mradi huo ulivyohujumiwa ikiwemo kuchukuliwa hatua wahusika.
“Ninaamini
endapo Mkurugenzi wa Halamshauri atakuja kuangalia mradi huo
yatapatikana mafanikio ikiwemo kulipatia ufumbuzi suala la mradi huo
“Alisema Mussa.
Mussa
alifika mbali zaidi kwa kumuomba mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo
kutembelea eneo hilo ili ajionee jinsi mradi huo ulivyoharibika na
kushindwa kufanya kazi huku wananchi wakiendelea kuteseka.
Akizungumzia
mradi huo,Diwani Aweso alisema mradi huo ulitengewa sh.milioni 35kwa
ajili ya utengenezaji huo wa mradi ambao ulipagwa kutumika kwenye
shughuli za umwagiliaji kwenye mbuga ya mswaha darajani.
“Baada
ya kuchelewa kwa mradi huo nililazimika kumtafuta diwani wa kata hiyo
Aweso ambapo alinijibu kuwa mradi huo utapasuka muda wowote ule kutokana
na kujengwa chini ya kiwango“Alisema Aweso wakati akizungumza na
mwandishi wa gazeti hili.
Aweso
alisema mkandarasi aliyepewa kujenga mradi huo alijenga chini ya
kiwango hali ambayo ilipelekea kushindwa kufanya kazi ipasavyo badala
yake kupasuka na kuendelea kuwapa tabu wananchi wa maeneo hayo.