Featured Post Today
print this page
Latest Post

Hawa ndio mabilionea wanne vinara Tanzania

Hawa ndio mabilionea wanne vinara Tanzania

rostam 7da3e
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja Sh1.6 trilioni.
Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji 'Mo'. Katika orodha hiyo pia yumo Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma.
Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka 2011, amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni).
Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.
Mengi anashika nafasi ya pili kwa Tanzania na ya 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 milioni (Sh861 bilioni).
Forbes linaonyesha kuwa Bakhresa amefungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika, wote wakiwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni).
Rostam, Mengi na Bakhresa hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo huku Mo akisema kwamba asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa jana alikuwa katika mapumziko ya Sikukuu ya Ashura.
Tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote, ambaye anajenga Kiwanda cha Saruji huko Mtwara ndiye anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya Afrika, akiwa na utajiri wa Dola20 bilioni (Sh31.7 trilioni), akifuatiwa na familia ya Johanny Rupert ya Afrika Kusini yenye utajiri wa Dola7 bilioni (Sh10.7 trilioni) na Nick Oppenheimer, pia wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 6.6 bilioni (Sh10.3 trilioni).
1)Rostam Aziz
Jarida la Forbes limeripoti kuwa utajiri wa Rostam unachangiwa zaidi na biashara ya mawasiliano ya simu za mkononi, ujenzi na uchimbaji wa madini.Pia anamiliki Kampuni ya Caspian, ambayo inafanya kazi za kuchimba madini katika migodi inayomilikiwa na Kampuni za BHP Billiton na Barrick Gold.
Pia ana hisa katika Kampuni ya Hutchison Wampoa inayofanya kazi za kupakua mizigo bandarini na anamiliki majumba nchini na katika nchi za Mashariki ya Kati.
2) Mengi
Ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP.
Utajiri wake unatokana na kumiliki vyombo vya habari, kiwanda cha vinywaji baridi na madini.
Mengi anamiliki magazeti kumi na moja, vituo vitatu vya televisheni na takriban vituo 10 vya redio.
Pia ana mgodi wa madini ya dhahabu na viwanda vya CocaCola.
Kwa mujibu jarida hilo, Mengi alizaliwa katika familia maskini na baadaye kusomea uhasibu huko Uingereza na kufanya kazi huko.
Alijiunga na Chama cha Wahasibu cha Uingereza kabla ya kurejea Tanzania mwaka 1971 na kuajiriwa na Kampuni ya Ukaguzi ya Coopers & Lybrand Tanzania (sasa Price Water House Coopers) hadi mwaka 1989, alipoacha kazi na kujikita zaidi katika biashara.
3) Bakhresa
Said Salim Bakhresa ni mwasisi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bakhresa Group na ana utajiri wa Dola500 milioni (Sh783 bilioni).Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanza biashara ya kuuza viazi mbatata. Baada ya hapo alifungua mgahawa na baadaye kuingia katika biashara ya kusaga nafaka.
4) Mo
Mafanikio yake yamechangiwa zaidi baada ya kuendeleza mali ya wazazi wake. Anafanya biashara ya nyumba, kuuza mazao na viwanda vya mafuta.
Mo alirejea Tanzania baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani na kuendeleza biashara ya maduka ambayo yalianzishwa na baba yake.
Alinufaika baada ya kununua viwanda vilivyobinafsishwa na Serikali.
Alivifanya viwanda hivyo kutengeneza faida na kuinyanyua Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL) kuwa miongoni mwa kampuni zenye mafanikio makubwa Tanzania.
Mo pia anajihusisha na biashara ya usambazaji bidhaa, viwanda vya nguo na kilimo.
Jarida hilo lilipiga hesabu za utajiri wa wafanyabiashara hao kwa kuangalia thamani ya bidhaa zinazouzwa na kampuni zao, mikataba yao na hasa wale walio kwenye sekta ya mafuta na ukubwa wa kampuni zao.CHANZO MWANANCHI


0 comments


Mike Tyson akiri kutumia dawa za kulevya kwenye mapambano yake, alitumia u*me wa bandia ili kukwepa vipimo.

Tyson ameanika ukweli huo kwenye kitabu chake ‘Undisputed Truth’ ambapo amesema alikuwa anatumia uume wa bandia kukwepa vipimo vya kuangalia kama ametumia madawa ya kulevya ambavyo vilikuwa vinachukuliwa kwa njia ya kupima haja ndogo.
“I had to use my whizzer, which was a fake pen*s where you put in someone’s clean urine to pass your drug test.” Ameandika Tyson.
Mike Tyson amefunguka jinsi alivyokuwa akiwachezesha wapimaji ambapo siku zote alikuwa anatumia uume wa bandia uliojazwa haja ndogo ya mtu mwingine katika timu yake, na kisha kuzuga kama anautoa mwenyewe hivyo vipimo vinakuwa fake.
Tyson amesema alikuwa anatumia dawa za kulevya aina ya Cocain na Marijuana mara kwa mara, na akakumbushia moja kati ya situation alizokuwa amevuta ni pale alipokuwa ameenda kwenye press conference na Lennox Lewis huko New York, mwaka 2002 ambapo alitaka kumvaa Lenox pale pale.
 “I lost my mind,” Tyson recalled. “I looked over at him and wanted to hit the motherf---er.” Yanasomeka maandishi ya Tyson.
0 comments

KUMBE HICHI NDICHO ANACHOPENDA HUYU MSANII WA KIKE KUTOKA THT.MMMMH HATARI.

KUMBE HICHI NDICHO ANACHOPENDA HUYU MSANII WA KIKE KUTOKA THT.MMMMH HATARI.

MWANAMUZIKI, Lina Sanga, ameweka wazi kitu anachokipenda kwenye maisha yake ukiachilia
muziki anaoupiga. Unakijua kitu hicho ni nini? Ni viatu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Lina anasema kuwa anapenda viatu kuliko kitu kingine chochote kiasi kwamba anaweza kushuka kwenye gari sehemu yoyote kama ameona kiatu kizuri dukani.

Anasema kuwa hata kama akivaa nguo ya siku nyingi kiasi gani, lakini kama miguuni amevaa kiatu kipya hujisikai huru na mwenye furaha, kuliko akikosa kiatu anachokipenda.

Anasema chumbani kwake ana jozi 50 ya viatu anavyovivaa, lakini pia anazo jozi nyingine 30 za viatu ambavyo bado hajavivaa kabisa kwani bado anatafuta nguo za kuvalia viatu hivyo.

“Yaani hapa naona bado kabisa. Ninaongeza viatu karibu kila siku maana ninavyoviona madukani vipo vya kila aina nami napenda sana viatu, ” anasema.

Aliongeza kuwa hajawahi kuishi bila kutamani kununua kiatu ambacho amekiona mahali na kila akinunua anakutana na kingine, hivyo siku zote ameishi akinunua viatu bila kujali idadi ya alivyo navyo.

Kwa upande mwingine, Lina anasema kuwa kama akiambiwa achague kati ya kusafiri, kuangalia luninga na kusoma vitabu, atachagua kusafiri kwa kuwa akiwa safarini anajifunza vitu vingi kwa kuona na si kuhadithiwa. Aidha anasema kuwa awapo safarini, husinzia kwa bahati mbaya tu lakini ingekuwa ni uwezo wake asingekuwa akisinzia hata kidogo ili aweze kuona kila kilichopo njiani.

“Kama nimelala safarini ujue ni kwa bahati mbaya, lakini mimi mwenyewe huwa sitaki kabisa. Huwa ninataka nione kila kitu cha njiani, ni raha yangu pia,” anasema.

Anaendelea kueleza baadhi ya vitu anavyovipenda katika maisha yake kuwa ni pamoja na kuvaa magauni ya mtindo wowote, iwe mafupi au marefu.

Anasema kwa kuwa ana umbo la kuvutia, haoni haja ya kujibana kwa kupenda kuvaa suruali kama wasichana wengi wa siku hizi.

“Huwa navaa suruali sikatai, lakini sipendi sana kwa kuwa sipendi kujibana na ndiyo maana napenda kuvaa magauni ambayo kama una shepu nzuri hayana shida. Kwa jinsi nilivyo, kila nguo nikivaa naiona sawa kwa kuwa nipo poa,” anasema.

Anafafanuwa kuwa siyo kwamba havai nguo nyingine, anavaa kwa kuwa hawezi kuvaa nguzo za aina moja kila siku, lakini ili awe huru na kuona amependeza, huvaa gauni.


0 comments

AUNT, WOLPER, SNURA WAFUNGA MTAA KWA MAUNO

AUNT, WOLPER, SNURA WAFUNGA MTAA KWA MAUNO


Stori: Hamida Hassan
Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary.

Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.

“Yaani wewe ulikosa mambo,  Snura alitoa shoo na mapacha wake utadhani alikuwa amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake Vanitha ambaye anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa akimsimulia mwandishi wetu.

Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.
-Global Publishers
0 comments

MWIMBAJI MKONGWE SQUEEZER AZILAUMU REDIO KUDIDIMIZA WASANII WAKONGWE


MWIMBAJI MKONGWE SQUEEZER AZILAUMU REDIO KUDIDIMIZA WASANII WAKONGWE

Squeezer ametoa wimbo mpya unaoitwa ‘Mtemi Pesa’ aliomshirikisha Belle 9, kama jina linavyojieleza wimbo huo unazungumzia jinsi pesa inavyotawala kila kitu.

Akizungumza na kipindi cha Planet Base cha Planet FM Morogoro, Squeezer ambaye pia ni kaka wa rapper wa kike Dataz amesema baadhi ya vyombo vya habari vinachangia katika kuwadidimiza wasanii wakongwe kutokana na baadhi yao kuwabeba wasanii wapya kutokana na kuwa na masilahi nao.

“Mi nafikiri kuna baadhi ya media zinadidimiza wakongwe kwa makusudi kwa sababu wanajua wana nguvu hiyo na wanaweza, na hiyo yote ni kwasababu ya kuweza kuwamiliki ambao wanaweza kuwalipa kile kidogo walichonacho”.

Rapper huyo wa ameongeza kuwa wasanii wapya hawajui thamani yao tofauti na wasanii wakongwe kama yeye wanaojitambua.
-Bongo5.com
0 comments

Dk. Mwakyembe aibukia bandari ya Tanga

Dk. Mwakyembe aibukia bandari ya Tanga

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
 
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametangaza rasmi kumalizika kwa fungate kwa watendaji wa serikali mkoani Tanga ikiwamo Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato (TRA) na Jeshi la Polisi, kutokana na kuhusika moja kwa moja na mtandao wa magendo hasa upitishaji wa dawa za kulevya na pembe za ndovu.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa bandari bubu 49 mkoani Tanga ambazo zimekuwa zikihusika na upitishaji wa bidhaa kwa  magendo ili kukwepa kodi, zikiwamo dawa za kulevya, wahamajia haramu na pembe za ndovu.

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na watendaji wa TPA, TRA, wafanyabiashara na wadau wanaotumia bandari ya Tanga muda mfupi tu baada ya ziara ya ukaguzi katika wilaya ya Pangani na bandari ya Tanga.

Alisema ili kuthibitisha kauli yake hiyo atawataja kwa majina wahusika na vinara wa mtandao huo na kwamba kuanzia sasa anatangaza rasmi vita baina yao.

“Tunawajua kwa majina msione tumekaa kimya tu na mitandao yenu tunaijua…jeshi la Polisi wanasaidia kuwasindikiza, yaani Tanga imekuwa ni kituo cha kupokea bidhaa haramu…sasa honeymoon (fungate), ndugu zangu imekwisha,” alisisitiza Waziri huyo.

Dk. Mwakyembe alieleza kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wa TRA mkoani hapa na kusema kuwa ataliwakilisha kwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa ili hatua za haraka zichukuliwe.

Awali, akizungumza katika mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Kipande Madeni, aliwataka watendaji wa mamlaka hiyo mkoa wa Tanga kuendela kujituma katika utekelezaji wao ikiwamo kufanya kazi kwa saa 24 kama wanavyofanya Dar es Salaam.

Naye Kaimu Meneja wa TPA Mkoa wa Tanga, Freddy Liundi, alisema kuwa bandari hiyo inatarajia kupokea vifaa aina ya Baji vyenye uwezo wa kupakua mzigo hadi wa tani 3,500 kwa kontena 196 zenye urefu wa futi 20 mwezi Disemba, mwaka huu.
 
0 comments

ZIARA YA WAZIRI WA UCHUKUZI DR.MWAKYEMBE MKOANI TANGA

0 comments

WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI JIJINI TANGA WATISHIA KUSITISHA HUDUMA

WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI JIJINI TANGA WATISHIA KUSITISHA HUDUMA

Na Oscar Assenga, Tanga.
BAADHI ya wamiliki wa vyombo vinavyotoa huduma ya Usafiri jijini Tanga wametishia kusitisha kuendelea kutoa huduma hiyo kutokana na gharama kubwa wanazozipata wakati wa matengenezo yanayotokana na ubovu wa barabara zilizopo jijini Tanga.
Hatua hiyo inatokana na baadhi ya barabara za jijini Tanga kuwa na mashimo hali ambayo inapelekea kuleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji wake hasa nyakati zinapokuwa zikinyesha mvua.
Mwenyekiti wa Muungano wa wasafirishaji abiria mkoa wa Tanga,(Muwata) Hatwabi Shabani  alisema barabara ambazo zimekuwa kero kubwa sana ni Sahare, Makorora, Mikanjuni, Raskazone mwisho,Japani,Kivumbitifu na Kasera.
Shabani alisema kutokana na ubovu wa njia hizo wamiliki wa magari zinazofanya safari zake katika maeneo hayo wamekuwa wakipata hasara na hivyo kumuomba mkurugenzi wa Jiji la Tanga kuangalia uwezekano wa kuzifanyia matengezo barabara hizo.
Mwenyekiti huyo alisema wao kupitia muungano wao wanaomba maeneo hayo yafanyiwe matengenezo madogo madogo angalau kufukia yale mashimo ambapo magari mengi yanaharibika kitendo ambacho kinapelekea baadhi ya wamiliki kutaka kuhamisha magari kutokana na gharama kubwa za matengenezo.
Aliongeza kuwa wanaiomba Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanazifanyia kazi changamoto hizo ili chama hicho kiweze kutoa huduma bora kwa wakazi wa Jiji la Tanga.
0 comments

ZITTO AFICHUA KASHFA NZITO TUME YA UCHAGUZI TANZANIA

ZITTO AFICHUA KASHFA NZITO TUME YA UCHAGUZI TANZANIA

TUME ya Uchaguzi nchini (NEC) inadaiwa kuingia katika mchakato wa mwisho wa kuzipa zabuni ya kuandaa vifaa vya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kampuni za M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution zinazodaiwa kuwa na rekodi mbaya ya utendaji.

Tanzania Daima limedokezwa kuwa mkakati huo unahusishwa na  njama za kutaka kukibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo kwa kuchakachua matokeo ya kukibakiza madarakani.

 Kampuni hizo ambazo katika zabuni ya Tume ya Uchaguzi zimetajwa kushirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya M/S SCI Tanzania Limited, mbali ya kutojulikana zinapotoka, pia ndizo zimekuwa na gharama kubwa kuliko kampuni nyingine zilizoomba kazi hiyo.

Kiwango ambacho kampuni hizo zilitaja na kukubaliwa na NEC kwa ajili ya kuandaa vifaa vya kielektroniki vya kusajili wapiga kura (Biometric Voters Registration) ni zaidi ya euro milioni 60, sawa na sh bilioni 126.3, wakati kampuni zinazofuata zikihitaji kuanzia euro milioni 40.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ni mmoja wa viongozi waliofichua mkakati huo, akidai unafanywa na serikali ya CCM ili kuhakikisha wanajiandaa kudhibiti kila eneo ili waweze kubaki madarakani.

Alisema lengo ni kuhakikisha mchakato wa vitambulisho vya kupigia kura vya kielektroniki vina kuwa na faida kwa CCM na kukiingizia fedha chama hicho za kutumia kwenye uchaguzi huo kupitia mfumo huo dhaifu wa vitambulisho hivyo.

Zitto alisema kutokana na hali hiyo, amemwandikia Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Serikali (CAG) barua ya kutaka ukaguzi wa zabuni hiyo ufanyike kwa kushirikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kujiridhisha.

“Wenzetu CCM wanafanya mikakati ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuhakikisha wanapata fedha za kutosha na hata mazingira mabaya ya vifaa vitakavyotumika katika upigaji kura na sasa wameshaingia hata katika Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kutengeneza mazingira,” alisema Zitto.

Aliongeza kuwa kiasi kilichotolewa ni kodi ya Watanzania na kwamba ni vema taifa likajiridhisha kuwa matatizo yaliyotokea Kenya na Ghana hayatajirudia Tanzania, hasa wakati wa upigaji kura.

 Gazeti hili limeona barua hiyo ya Zitto kwenda kwa CAG, ya Novemba 7, 2013, yenye kichwa cha habari; ‘Zabuni ya  Biometric Voters Registration (BRV KITS) No. IE/018/2012-13/HQ/G/19 yenye thamani ya sh bilioni 126.3.’

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini anasema kuwa  NEC imekuwa katika mchakato wa zabuni tajwa hapo juu.

“Zabuni hiyo sasa imeanza kuleta malalamiko miongoni mwa wananchi kutokana na kinachosemekana kuwa kampuni iliyopewa zabuni hiyo haina uwezo kiteknolojia, pia bei zao ni kubwa.

“Katika mafunzo ya hivi karibuni ya SADCOPAC jijini Nairobi tuliazimia kuwa ni vema kwenye zabuni nyeti kama za namna hii, SAIs wawe na uwezo wa kufanya ukaguzi kabla ya zabuni kutolewa na kuanza kutekelezwa,” alisema.

Kwa mujibu wa nyaraka za NEC ambazo Tanzania Daima linazo, kampuni zilizopewa tenda ya pamoja yenye kugharimu kiasi cha dola 78, 987,636.00, sawa na sh 126,291,375,455 ni M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution ambazo hazijulikani nchi zinapotoka zikiwa zinashirikiana na M/S SCI Tanzania Limited.

 Katika nyaraka hizo kampuni zilizokosa tenda na ambazo zimelalamika kwa Mkurugenzi wa NEC namna mchakato wa kutoa zabuni hiyo ulivyoendeshwa zimeainishwa kuwa ni M/S Zetes SA ya nchini Ubalgiji, M/S IRIS Corporation Technology ya Malaysia, M/S Lithotech Exports ya Afrika Kusini, M/S Safran Morpho ya Ufaransa na  M/S Avante International Technology, Inc ya Marerkani.

 Kampuni hizo zinahoji njia na sababu zilizowafanya wakose tenda hiyo licha ya kuwa na uzoefu, vifaa bora pamoja na kuwa na kiwango kidogo cha gharama tofauti na kampuni iliyopewa kazi.

 Katika moja ya malalamiko yao, Kampuni ya M/S Morpho, inalalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo licha ya kuwa na sifa za kimataifa za kufanya kazi huku ikiwa imetoa bei nafuu kuliko kampuni iliyopata kazi.

 “Tulikuwa miongoni mwa washindani muhimu kwa kuwa kiwango chetu kilikuwa ni sh bilioni 97.8 ambazo ni sawa na euro 44,939,912 + sh 3,843,736,140.

“Ujuzi, vigezo na uzoefu wetu havilingani, duniani kote tumefanya kazi katika maeneo mengine kwa ufanisi na tunashindwa kuelewa kivipi walishinda hao ambao wamepata kazi kwa kiwango cha zaidi ya sh bilioni 27.8 ikilinganishwa na yetu,” ilisomeka sehemu ya barua.

 Alipotafutwa Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema hawezi kuliongelea suala hilo katika simu na kuomba mwandishi awasiliane na Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Dk. Sist Cariah, ambaye alisema mchakato wa kupata kampuni ulifuatwa kisheria.

Dk. Cariah alisema si kweli kwamba kampuni iliyopewa kazi haina uwezo bali malalamiko yanatoka kwa watu walioshindwa kupata kazi hiyo.

Alipoulizwa juu ya uzoefu wa kampuni hiyo na wapi ilifanya kazi, Dk. Cariah alisema kwa maelezo waliyonayo ni kwamba kampuni hiyo ina uzoefu wa miaka 35 wa kufanya kazi, huku akishindwa kuainisha sehemu ilizowahi kufanya kazi.

Kuhusu wapi zimetoka kampuni hizo, Dk. Cariah alisema suala la kutoainishwa kimaandishi ni makosa ya kawaida, huku akitaja kuwa zinatoka katika nchi ya India na Australia.

Kuhusu gharama, Dk. Cariah alisema licha ya makampuni mengine kutaja gharama za chini, zingeweza kuwa na gharama kubwa zaidi wakati wa kukamilisha kazi hiyo kutokana na kuwa na gharama zilizojificha.

Chanzo :Tanzania Daima

0 comments

STEWART HALL APATA KAZI SUNDERLAND

STEWART HALL APATA KAZI SUNDERLAND

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA Muingereza, Stewart Hall atakuwa Kocha Mkuu wa akademi ya Symbion Power inayoanzishwa nchini kwa ushirikiano wa klabu ya Sunderland AFC ya England na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.
Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Tanzania, Peter Gathercole, amesema leo kwamba akademi hiyo itakuwa na vituo Kidongo Chekundu (Sports Park) na Elite Football Academy, Dar es Salaam.
Stewart Hall enzi zake Azam FC

Hall, mwenye leseni ya UEFA ya ukocha na Mkufunzi wa shirikisho hilo, amepewa kazi hiyo baada ya mafanikio yake akiwa na klabu ya Ligi Kuu, Azam FC na timu ya taifa ya Zanzibar na Birmingham City alipokuwa Mkurugenzi wa akademi.  
Kabla ya hapo, Hall alikuwa kocha wa timu za taifa za Saint Vincent na Grenadines, pamoja na Pune FC ya India. 
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Hall alisema, “Mradi huu hakika utasaidia kuinua soka ya vijana kwa viwango vyote, timu za taifa na klabu. Vijana wadogo watafundishwa ufundi, mbinu, kujengewa uimara wa kimchezo na maarifa ya soka ya kisasa,”alisema.
Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC, Margaret Byrne, amesema: “Tunafurahi mradi wa akademi unaendelea vizuri. Kuteuliwa kwa  Stewart ni hatua ya kufurahisha na tunatarajia kila mmoja kufanya kazi kwa bidii ili kuvuna matunda baadaye.”
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, alitemebelea akademi ya Sunderland akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete Juni mwaka huu ambako walifikia makubaliano na Sunderland AFC na Symbion Power Tanzania juu ya mradi huu.
0 comments

KIM ATEUA NUSU KWA NUSU MADOGO NA MAFAZA KUUNDA STARS YA KUIKABILI KENYA

KIM ATEUA NUSU KWA NUSU MADOGO NA MAFAZA KUUNDA STARS YA KUIKABILI KENYA 

Boniface Wambura, Ilala
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Nusu kwa Nusu; Taifa Stars na Future Taifa Stars jana Karume

Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger