Mashindano ya Ngalawa yafana Tanga
Ngalawa zikiwa katika mstari kwa ajili ya kuanza mashindano katika pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.
Na
Mwandishi Wetu, Muheza
Mashindano
ya ngalawa yaliyofanyika jana Wilayani Muheza katika Kijiji cha Kigombe
yamefana huku Kampuni ya simu ya ZANTEL ikifanikisha kwa kutoa zawadi .
Kutokana
na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika mashindano hayo amewataka vijana washiriki katika michezo badala
ya kukaa vijiweni.
Kauli
hiyo aliitoja wakati akifungua mashindano ya kwanza ya Ngalawa mkoani
Tanga yaliyofanyika kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.
Mwidau
alisema kupitia michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi ikiwemo elimu na
ujunzi kutoka kwa wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za kimwili na kiakili.
“Mahindano
haya ya Ngalawa hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya kijiji lakini kupitia
kwa wadhamini Kampuni ya simu ya ZANTEL tumeweza kuyafanya kimkoa kwa lengo la
kuibua fursa za ajira kwa vijana na kwashirikisha watu katika michezo, ”alisema
Mwidau.
Nae
Meneja mauzo wa ZANTELTanzania Salum Ngururu, alisema
kuwa lengo la kudhamini mashindano hayo ni kurudisha faida wanayopata kwa
jamii kutoka na huduma zake na kuendelea kuwatambulisha bidhaa zinazotolewa na
kampuni hiyo.
Alisema
ZANTEL itakuwa ikiboresha zawadi za mashindano hayo kila mwaka ili yaweze
kuvuta washiriki wengi.
Mshindi
wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi laki tatu, kikombe cha ushindi pamoja
na medali za dhahabu. Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka
ambaye aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.
Mashindano
hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini zilizokuwa na washiriki watano
ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za Tanga, Pangani na Muheza huku Wilaya
ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na kushindwa kufanya maandalizi mazuri.