Featured Post Today
print this page
Latest Post

LOGARUSIC ASEMA MECHI YA JUMAMOSI DHIDI YA MTIBWA, ITAWAIMARISHA ZAIDI


Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema mchezo wao wa kirafiki keshokutwa Jumamosi, utakuwa sehemu nzuri ya kukipanga kikosi vizuri kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.


Simba itashuka Dimbani keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuwavaa Mtibwa Sugar katika mechi maalum ya kirafiki.

Logarusic raia wa Croatia amesema anatarajia mechi hiyo itakuwa ni nzuri na tofauti na zile za michuano ya Mapinduzi hasa katika suala la kupanga timu.
“Kweli tulikuwa tunapanga timu kwa ajili ya mashindano na kujiandaa na ligi, lakini michuano ni michuano tu.

“Mechi ya Mtibwa imekuja wakati mwafaka na ikiwezekanba tunaweza kuomba moja kwa ajili ya kujiimarisha zaidi.
“Kuna mambo lazima tutarekebisha, lakini kuna mambo tumejifunza kwenye michuano ya Mapinduzi ambayo tutayafanyia kazi.
“Kawaida katika mchezo wa soka mnajifunza kila siku na hata katika ufundidishaji lazima urudie zaidi ya mara moja ili kitu kiwangie vizuri wachezaji na waweze kukikumbuka wakati wa utekelezaji,” alisema.
Katika mechi ya mwisho Simba ililala bao 1-0 dhidi ya KCC ya Uganda katika fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Mara ya mwisho Simba kucheza Uwanja wa Taifa jijini Dar, iliilaza Yanga kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
0 comments

PICHA:KOMANDO WA TANZANIA AKIVUNJA TOFALI LA NCHI SITA KWA KUTUMIA KICHWA..NOMA

PICHA:KOMANDO WA TANZANIA AKIVUNJA TOFALI LA NCHI SITA KWA KUTUMIA KICHWA..NOMA

Komandoo akivunja tofali kwa kichwa kwenye uwanja wa Amani siku ya kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
0 comments

BREAKING NEWS:LIYUMBA ASHINDA KESI


BREAKING NEWS:LIYUMBA ASHINDA KESI 

 

 MKURUGENZI wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ameshinda kesi ya kukutwa na simu gerezani iliyokuwa inamkabili hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia mahakama kuhusu tuhuma hiyo. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuanzia saa 3:30


 

 

 

 

0 comments

Ajali yaua watano kujeruhi wawili wilayani Handeni mkoani Tanga

Ajali yaua watano kujeruhi wawili wilayani Handeni mkoani Tanga


Na Rajabu Athumani, Handeni

WATU wanne wamekufa papo hapo na mmoja hospitali katika ajali ya basi aina Noa ilitokea jana majira ya jioni katika Kitongoji cha Mtakuja kata ya Misima wilayani Handeni na kujeruhi wengine wawili.

Mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Rashidi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa chuma kinajulikanacho kama propera shafti ambacho kilikatita na kusukuma gari pembeni na kupinduka zaidi ya mara tatu na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.

Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa dereva wa gari hilo aliyejulikana kama Miraji Shabani(22) ametoroka baada ya ajali kutokea na hajulikani alipo hadi sasa na polisi wanaendelea kumtafuta kwa mahojianao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ni kweli gari yenye namba za usajili T493 AUH aina ya Noa na kuua watu wanne hapo hapo na mmoja hospitali baada ya kukatika chuma wanachoita propera shafti hali iliyosababisha kuuwa watu watano katika ya saba waliokuwa katika Noa hiyo.

Kamanda Massawe alisema kuwa Noa hiyo ilikuwa ikitokea Handeni mjini kuelekea Misma kilomita 16 kutoka mjini ikiwa na wanafamilia hao saba wakiwa humo kwaajili ya shughuli zao binafsi za kifamilia na haikuwa gari ya kibiashara.

Kamanda Massawe aliwataja marehemu wa ajali hiyo kuwa ni Juma Nyeri (90) mkazi wa Misima,Athumani Yusuph (45),Zahara Changogo,Mwajuma Mzimu na Zuberi Abdallah wote wakazi wa Suwa wilayani Handeni na majeruhi ni Hemedi Said ambae baada ya kupatiwa matibabu alipewa ruhusa na kurudi nyumbani pamoja na dereva ambae alishakimbia hiyo haijulikani kuwa ameumia kiasi gani..



0 comments

B12, ADAM MCHOMVU NA DIVA WAMEPIGWA CHINI CLOUDS FM

B12, ADAM MCHOMVU NA DIVA WAMEPIGWA CHINI CLOUDS FM

Stori:  MUSA MATEJA
WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.


Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.

Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.


“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.

“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”
0 comments

RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho zitakazofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho zitakazofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey Zambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki alisema sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Februari 2, Mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Mwenyekiti wa CCMmkoa wa Mbeya
Charles Mwakipesile Mjumbe wa NEC
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey Zambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki akiwa na katibu wa ccm mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema



RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho zitakazofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari  katika Mkutano uliofanyika katika Ofisi za Chama hicho Mkoa zilizopo Sokomatola Jijini Mbeya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey Zambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki alisema sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Februari 2, Mwaka huu.
Zambi alisema maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama cha mapinduzi ambayo yatafanyika kitaifa Mkoani Mbeya na Raisi Kikwete kuwa Mgeni rasmi yataanza majira ya saa 12 alfajiri kwa  kufanya matembezi ya Mshikamano.
Alisema matembezi hayo yataanzia katika viwanja vya John Mwakangale (nanenane) na kuishia katika Ofisi za Chama Mkoa eneo la Sokomatola yakihusisha Viongozi wa Chama na Wananchi mbali mbali wa Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Aliongeza kuwa baada ya matembezi hayo Wananchi na viongozi watapata mapumziko kidogo na kisha kuendelea na sherehe katika Viwanja vya Kumbu kumbu ya Sokoine zitakazoanza majira ya Saa nane Mchana.
Aidha mwenyekiti huyo alikipongeza Chama cha Mapinduzi Taifa kwa kuuteua Mkoa wa Mbeya kuwa Mwenyeji wa Sherehe hizo ambazo hazijawahi kufanyika Mkoani Mbeya tangu kuzaliwa kwa Chama hicho Mwaka 1977.
Alisema ni fursa pekee ya wakazi wa Mkoa wa Mbeya ya kukutana na Raisi Kikwete ambaye ataweza kuwaeleza wananchi mafanikio yaliopatikana Mkoani Mbeya tangu kuzaliwa kwa Chama hicho hadi sasa.
Aliyataja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na Ongezeko la Vyuo vikuu ambavyo awali havikuwepo Mkoani Mbeya sambamba na kuimarishwa kwa miundombinu hususani ujenzi wa barabara za Lami ambazo Mbunge wa Chadema Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi anadai yeye ndiye amejenga.
Alisema mafanikio mengine wanayopaswa kujivunia wakazi wa Mkoa wa Mbeya ni pamoja na sekta ya Elimu, Afya, Maji na Umeme ambapo sehemu kubwa ya Mkoa wa Mbeya wenye wakazi zaidi ya Milioni Mbili na Wanachama wa chama hicho zaidi ya Laki tatu wakipata huduma bora za kijamii.
Zambi aliongeza kuwa kutokana na kufanyika kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM Mkoani Mbeya, Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho ambao awali ulitarajiwa pia kufanyika Mkoani hapa umeahirishwa na kuhamishiwa mkoa mwingine ambao haukutajwa.
Wakati huo huo Mwenyekiti huyo alizungumzia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwamba CCM haihusika nao kama baadhi ya watu wanavyodai.
Alisema Chama cha Mapinduzi hakifurahii migogoro ya vyama vya upinzani kwa sababu vilianzishwa kwa lengo la kuikumbusha Serikali iliyopo madarakani pindi inapofanya vibaya au kujisahau katika kufanya shughuli za kuwaletea Maendeleo Watanzania.
Alisema hata ndani ya CCM matatizo kama hayo hutokea lakini humalizwa kupitia vikao halali vya chama na kuendelea na shughuli zake kama kawaida na sio kukimbilia kwenye vyombo vya habari kutangaziana mabaya.

Na Mbeya yetu
0 comments

Rais Kikwete amsifu Mkapa

Rais Kikwete amsifu Mkapa


Rais Jakaya Kikwete, amempongeza Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwa kuchangia historia ya Tanzania kutokana na uamuzi wake wa kuchapisha hotuba alizozitoa katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake .Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa nakala za vitabu vya hotuba hizo iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema uamuzi wa kuchapisha hotuba hizo umechangia historia ya Tanzania na kubainisha kuwa hotuba za Rais si zake wala mali yake binafsi.

Rais Kikwete alisema Rais huyo mstaafu, amefanya jambo kubwa sana katika historia kwa sababu alichokuwa anafanya wakati wa utawala wake ni historia ya nchi na lazima kiwekwe kwenye kumbukumbu kwa ajili ya kuvionyesha vizazi vijavyo.

"Hotuba zitaendelea kuweka kumbukumbu na kuvionyesha vizazi vijavyo mambo yaliyotokea wakati wa urais wako, msimamo wako na wa nchi katika kipindi hicho na hata fikra zako zilizosaidia kusukuma mbele maendeleo ya nchi yetu," alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alimtaka Rais huyo mstaafu kuangalia namna ya kuweka historia ya uongozi wake katika kitabu kadiri alivyoshuhudia miaka 10 ya uongozi wa Tanzania na kusisitiza kuwa bado wanaendelea kusubiri kitabu chake hicho.
Alisema kuna haja kwa wadau mbalimbali wa elimu, hasa wale wenye mapenzi ya kusoma vitabu, kuchukua hatua za kuamsha ari na mapenzi ya Watanzania ya kusoma vitabu ambayo kwa sasa, imepungua kwa kiasi kikubwa.

Kitabu hicho kiko katika machapisho matatu kuonyesha kuwa pamoja na kwamba alikuwa Rais wa miaka 10, lakini kila siku ya uongozi wake ilikuwa tofauti na nyingine, hali kadhalika mwezi mmoja mwingine.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemwapisha Dk Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia na Jaffary Ally Omari kuwa Mjumbe wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Kabla ya uteuzi huo, Dk Mlima alikuwa Msaidizi wa Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa
0 comments

CHADEMA YAPATA PIGO TANGA,MWENYEKITI WA KATA WAO ARUDI CCM.

CHADEMA YAPATA PIGO TANGA,MWENYEKITI WA KATA WAO ARUDI CCM.

Na Oscar Assenga,Tanga
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kata ya Mwanzange jijini Tanga,Said Bakari amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuchoshwa na sera zisizotekelezeka ndani ya chama chake ambazo hazina mashiko.

Uamuzi huo aliutangaza katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata hiyo ulikuwa ukihutubiwa na Mwenyekiti wa cha Mapinduzi wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni ambao aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kati kwenye mkutano huo,Bakari alisema awali alijiunga na chadema akitokea chama cha mapinduzi akidhani  chama hicho kina mashiko na wananchi badala yake mambo aliyoyakuta hayakuwa kama alivyotarajia.


Alisema hasa kikubwa kilichomfanya kukirudia chama hicho ni kutokana na utendaji makini unaofanywa na viongozi wa chama hicho ambao umepeleka kuweza kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za wananchi.

Katika mkutano huo wanachama wengine waliojiunga na chama hicho waliweza kufikia idadi ya wanachama 111 ambao walikabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa CCM wilaya na baadae kula kiapo cha pamoja.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi hiyo kwa wanachama hao wapya,Mbughuni alisema chama hicho kitaendelea kujiimarisha lengo likiwa kuhakikisha wanaendelea kushika hatamu ya uongozi kwenye chaguzi zijazo wilayani hapa.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga(UVCCM) Salim Perembo aliwataka vijana kubadilika na kuacha kukaa vijiweni badala yake waunde vikundi vya ujasiriamali vitakavyoweza kuwakwamua kimaisha.

   "Vijana tusiwekeze akili zetu kwenye starehe badala yake tubuni
miradi ambayo inatuwezesha kuinua maisha yetu pamoja na jamii nzima inayotuzuguka "Alisema Perembo
0 comments

CCM YAVUNA WANACHAMA WAPYA 111 KATA YA MWAZANGE.

CCM YAVUNA WANACHAMA WAPYA 111 KATA YA MWAZANGE.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA TANGA KASSIM MBUGHUNI KULIA AKITO KADI KWA MMOJA YA WANACHAMA WAPYA WALIOJIUNGA NA CHAMA HICHO JUZI.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger