Mwendesha
pikipiki akiendesha pikipiki huku akiwa amesimama wakati wa mapokezi ya
bingwa wa dunia mkanda wa WBF Francis Cheka (SMG) wakati akitokea
jijini Dar es Salaam baada ya kumdunda Mmarekani Phil
Williams kwa pointi
CHEKA akiwaonyesha mashabiki mkanda wa duniani wa WBF eneo la stendi kuu ya daladala ziend
azo nje ya Manispaa ya Morogoro wakati akitokea Dar es Salaam. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Msafara ukiwa eneo la Masika ukitokea Msamvu baada ya kupokewa Nane Nane mjini Morogoro.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi
akifafanua jambo katika hafla fupi ukumbi wa Olduvai Lodge Mafiga,
kushoto ni Frnacis Cheka.
Hapa Cheka akiwakabidhi mkanda viongozi wa serikali katika hafla hiyo kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzina katikati ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jovis Sembeye.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jovis Sembeye naye kifafanua jambo katika hafla hiyo.
Huyu ni miongoni mwa waendesha pikipiki
ambaye kwa namna moja ama nyingine alikuwa akifanya vurugu kwa kuendesha
pikipiki bila kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Huyu naye alikuwa akiendesha pikipiki akiwa amekaa hivyo.
Hawa nao hivyo hivyo sijui kwanini wana usalama nao wasiwachukulie hatua za kisheria.
Na Juma
Mtanda, Morogoro.
BINGWA wa
dunia
mkanda wa WBF uzani wa Super Middle, Francis Cheka ‘SMG’ amewaeleza maelfu ya
mashabiki waliojitokeza katika mapokezi yake kuwa ubingwa alioutwaa baada ya
kumtwanga bondia Phil
Williams wa Marekani kuwa ni
ubingwa huo ni wa wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza
wakati wa mapokezi yake katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Olduvai
Mafiga Morogoro Cheka alisema kuwa endapo angepigwa katika pambano lake na
bondia, Williams aibu ingewaangukia wakazi wa Morogoro
na Tanzania kwa ujumla hivyo ubingwa huo ni wa watanzania wote.
Cheka
alisema kuwa yeye ndiye alikuwa mwakilishi kwa Tanzania katika ulingo kupambana
na Mmarekani katika kuwania ubingwa wa dunia wa WBF kupitia mchezo wa ngumu na ameshukuru
kumkung’uta kama angepoteza pambano hilo ana imani kila mtanzania angejisikia
vibaya kutokana na matokeo hayo.
“Nimefurahi
kuona watanzania kunipa sapoti katika mchezo huu na nawaomba waendelee hivi
hivi kutuunga mkono mabondia wote katika michezo yetu ya kimataifa ili kuweza
kufanya vizuri lakini kwa sababu nimemchapa Phil Williams na kutwaa ubingwa huo
wa dunia na kubakia Tanzania kuna kila cha kujivunia katika hili”. Alisema
Cheka.
Aliongeza
kuwa namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya njema iliyoniwezesha kunipa
nguvu katika pambano lile na kumtwanga mpinzani wangu, sifa hii sio ya Cheka
pekee bali ni kwa wana Morogoro na Tanzania kwa ujumla hivyo kila mmoja wetu
anayo haki ya kutembee kifua wazi kwa ubingwa huu”. Alisema Cheka.
Cheka
alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwake kutokana na aina ya bondia na nchi
anayotoka ina mabondia wenye viwango bora duniani hivyo alikuwa makini muda
wote wa mchezo kuhakikisha anamtandika makonde mpinzani ili kuweza kumshinda.
Naye
mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi alisema kuwa hatua aliyofikia Francis
Cheka ni hatua ya kupongezwa kwa kila mkazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla
hivyo baada ya mapokezi yaliyofanyika serikali itapnga hafla maalum ya
kumpongeza.
Amanzi
alisema kuwa Cheka ameiletea sifa Tanzania lakini na Morogoro ambako ndiko
makazi yake hivyo vijana kujituma katika shughuli zao na serikali ikishaona
juhudi binafsi serikali huingiza mkono wake katika kusapoti juhudi hizo.
Katika
mapokezi hayo yaliyoanza majira ya 9 alasiri kwa wakazi wa Morogoro kujitokeza
kwa wingi kando ya barabara eneo la Nane Nane huku Cheki akiwa amekaa katika
gari la wazi anyanyua mkanda juu kuanzia Msamvu, Masika, Posta, Stendi kuu ya
daladala na kuelekea katika ukumbi wa Olduvai Mafiga ambako hafla hiyo
ilimalizika majira ya saa 12 jioni.
Post a Comment