Featured Post Today
print this page
Latest Post

ASKOFU WA KANISA LA EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA (EAGT) AFARIKI DUNIA.

Askofu,Dk Moses Kulola.
 

DAR ES SALAAM.
VILIO, simanzi na maombi ya kunena kwa lugha vilitawala jana katika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Temeke Dar es Salaam wakati waumini na ndugu wa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Moses Kulola (83) walipopata taarifa za kifo cha kiongozi huyo.
Katibu Mkuu wa EAGT, Brown Mwakipesile alisema kuwa Askofu Kulola alifariki dunia jana saa tano asubuhi kwenye Hospitali ya Africa Medical Invesment (AMI), Dar es Salaam.
Mwakipesile alisema afya ya Askofu Kulola ilian za kubadilika Mei mwaka huu akiwa mkoani Mwanza ambako alipelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando ambako alibainika kuwa na matatizo ya moyo.
 
 “Kanisa liliamua kuchukua jukumu la kumpeleka Hospitali ya Apollo, India kwa matibabu zaidi na baada ya kuona afya yake inatengemaa aliruhusiwa kurejea nchini, lakini Agosti 16, mwaka huu hali ilibadilika ndipo tukampeleka AMI alikofikwa na mauti,” alisema Mwakipesile.
 
Alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibwa kwa sasa. Hata hivyo, wanafarijika kwa upande mwingine wakiamini kwamba Mungu amemchukua mtumishi wake kwa wakati alioukusudia.
 
Alisema mwili wa Askofu Kulola utasafirishwa kwenda Mwanza Jumamosi jioni kwa ndege baada ya kuagwa kanisani hapo. Atazikwa kwenye Uwanja wa Kanisa la EAGT Bugando.
 
Askofu Kulola ni mmoja wa viongozi wa dini waliokuwa na jina kubwa nchini na alifanya kazi za utumishi wa kanisa kwa miaka 53 kwa kuhubiri na kuwaombea wenye matatizo mbalimbali.
 
Mtoto wa kwanza wa askofu huyo, Goodluck Kulola alisema wamejifunza mambo mengi katika maisha ya baba yao, ikiwamo upendo na unyenyekevu ulioongozwa na uchaji Mungu.
 
“Baba alikuwa ni asiyependa kabisa migogoro ya kidini, kisiasa yaani ikitokea hali ya uvunjifu wa amani wa namna yoyote ile alikuwa anaumia sana. Alipenda watu kwa ujumla ametufundisha upendo.”
 
Askofu Kulola ameacha mke wake aitwaye Elizabeth, ambaye alibarikiwa kupata naye watoto 10 na wengine wawili wa kuasili. Hata hivyo, watoto watatu walishafariki dunia. Ameacha wajukuu 44 na vitukuu 10.
 
Askofu Kulola, ambaye alizaliwa 1928, alianza Shule ya Misheni ya Ligsha Sukuma mwaka 1939, baadaye alijiunga na Shule ya Bwiru kabla ya kusomea Usanifu Majengo huko Israel kisha kuanza kazi ya kumtumikia Mungu mwaka 1950.
 
Alifuzu Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Theolojia katika Chuo Kikuu cha California State Christian Marekani. 
 
MWANANCHI
0 comments

Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni awalipua wapinzani

Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni awalipua wapinzani

Na Rahimu Kambi, Handeni
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, amesema wananchi wengi wamegundua kuwa wapinzani hawana lengo zuri kwa maisha yao, ndio maana wanazidi kukiamini chama chao.
 
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, wilayani hapa, Malunde alisema kwa sababu hiyo, wanaamini kuwa CCM itaendelea kuwa mkombozi kwa wananchi wote nchini.
Alisema mara kadhaa sera za viongozi wa upinzani zimeshindwa kujitosheleza, sanjari na kufanya mambo mengi ya kuwagawa Watanzania.
Aidha alijaribu pia kuzungumzia mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa wanachama wa CCM na Watanzania wote wanaendelea kuthamini mchango wa chama chao kwa kuongoza serikali kwa ajili ya kuwapatia maisha bora kwa kila Mtanzania.

“Tunashukuru kwakuwa wananchi wote wameelewa janja ya wapinzani na namna wanavyotaka kuwayumbisha Watanzania.
“Hili ni jambo jema kwa viongozi wote na ifikie wakati kila mtu aone namna ya kujiweka sawa na vyama vya upinzani, hasa kama kinachofanywa ni kuwachanganya Watanzania,”  alisema Malunda, ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga.
0 comments

Mkuu wa shule ya sekondari ya Kwamatuku wilayani Handeni aelezea mikakati ya shule yao

MKUU wa shule ya Sekondari ya Kwamatuku, iliyopo Kata ya Kwamatuku, wilayani  Handeni, mkoani Tanga, Faustine Mroso, amesema pamoja na changamoto wanazokutana nazo, lakini shule yake imejipanga imara kuwapatia wanafunzi elimu bora.
 
Mroso ameyasema hayo siku chache baada ya kuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne, waliotia hofu ya ufindishwaji katika shule hiyo.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Mroso alisema kuwa si kweli kama shule yake haifundishi vizuri, hivyo wanafunzi hao waendelee kujiandaa kwa kusoma kwa bidii, huku uongozi wa shule yake ukiwa umejipanga imara kuwaandaa wanafunzi hao.

Alisema shule yake ilikaguliwa mapema mwaka huu na kuonekana ina mipango kabambe yenye maendeleo ya kielimu, hivyo kinachosemwa dhidi ya wanafunzi hao si kweli.
"Mimi  katika shule hii si mwenyeji, maana nimekuja mapema mwaka huu, hivyo naomba wanafunzi wanipe ushirikiano kwa lolote linalotokea kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanajiandaa vizuri kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” alisema Mroso.
Kwa mujibu wa Mroso, shule yake ina uongozi mzuri pamoja na mipango ya kuwaandaa vyema wanafunzi, ikiwa ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanakuwa katika nafasi nzuri.
Awali, baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo walilalamikia uongozi wa shule kwa madai kuwa ufindishwaji wao si mzuri na unaweza kuwaweka katika nafasi mbaya kwenye mitihani yao ya kidato cha nne baadaye mwaka huu.
Chanzo; Handeni kwetu.
0 comments

Mgombea udiwani mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF sasa akichulia chama chake

Mgombea udiwani mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF sasa akichulia chama chake

Handeni. 
ALIYEKUWA mgombea udiwani Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mwamini Andrew, amesema haoni sababu ya kubaki katika chama kisichokuwa na dhamira ya kuwaongoza Watanzania.
 
Mwamini Andrew, Mgombea Udiwani mwaka 2010 Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa tiketi ya CUF, pichani.
Mwamini ameyasema hayo wakati hivi karibuni aliuhakikishia mtandao huu kuwa ameamua kuachana na CUF na kuamua kurudi kuhamia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Andrew alisema kwamba Watanzania wanahitaji kuongozwa vyema na kupatiwa maendeleo, hasa wale wanaoishi vijijini.

Alisema vyama vya siasa mfano wa CUF haviwezi kuwa na jipya kiasi cha kuwakomboa Watanzania, hivyo kwake yeye kuondoka ni jambo lenye mashiko kwa kiasi kikubwa.
“Niligombea udiwani kwa tiketi ya CUF, lakini kwa sasa hamu sina kutokana na changamoto nyingi zinazokikumba chama hasa mipango na ushirikiano kati ya wanachama na viongozi kukosekana.
“Naamini mipango yangu ilienda vizuri, huku nikiamini kuwa lengo ni kufanikisha maendeleo kati ya wananchi na serikali, sanjari na viongozi wa vyama vyote vya siasa,” alisema Andrew.
Kauli ya kijana huyo inaweza kuwa mwiba mkal kutoka kwa vijana wanaoamini kuwa chama cha CUF kimepoteza mvuto ndio maana wengi wamekuwa wakikihama kwa kasi ya ajabu.
0 comments

SAMUEL ETO'O ATAMBULISHWA RASMI CHELSEA.



SAMUEL ETO'O ATAMBULISHWA RASMI CHELSEA.
 
0 comments

HII NDIO ADHABU ALIYOPEWA MRISHO NGASA.


              HII NDIO ADHABU ALIYOPEWA MRISHO NGASA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa amesema kamati yake haikumhoji winga wa Yanga, Mrisho Ngassa ilijitosheleza na maelezo ya kimaandishi.
Ngasa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano na kutakiwa kuilipa Simba kiasi cha Sh45 milioni kufuatia kubainika kusajili mikataba ya klabu mbili kwa wakati mmoja.

Klabu yake ya Yanga imekata rufaa kupinga uamuzi huo, ambapo pamoja na mambo mengine inaona mchezaji wake hakupewa haki ya kujieleza kufuatia tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.

Lakini jana wakati Mwenyekiti, Mgongolwa akizungumza na gazeti hili alisema kamati yake inafanya kazi na vielelezo vya maandishi, hivyo hawakuona sababu ya kumwita Ngasa.
“Kimsingi, watu wanatakiwa kufahamu, sisi kama kamati tunatumia maelezo ya maandishi ambayo ndio vithibitishoi vyetu, na kama ushahidi wa vielelezo utakuwa na upungufu ndipo tunapomwita mchezaji,” alisema Mgongolwa. Akifafanua alisema: “Kuna wachezaji wengi usajili wao umeonekana kuwa na matatizo, lakini hatukuwai kuwahoji.”
SOURCE: MWANANCHI
0 comments

JK ataka suluhu na Rais Kagame


                        JK ataka suluhu na Rais Kagame

jk_kagame_62bfe.jpg
RAIS Jakaya Kikwete amemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, kuwa msuluhishi wa mgogoro wa chini kwa chini unaoendelea kati ya Tanzania na Rwanda
Uamuzi huo, ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pinda alitangaza uamuzi huo, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu ambapo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alitaka kujua hatua za Serikali katika kile kinachoonekana Tanzania kutaka kutengwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mbowe, alisema hatua ya nchi za Rwanda, Kenya na Uganda kuendesha vikao kupitia wakuu wa nchi ikiwemo kujitoa kwa nchi ya Rwanda kutumia Bandari ya Dar es Salaam, kunaashiria mwelekeo mbaya.


0 comments

Kilimo cha michikichi kutekelezwa Kisarawe;

Kilimo cha michikichi kutekelezwa Kisarawe;

MICHIKICHI_47d9a.jpg

SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) limesaini makubaliano ya kuendeleza mradi wa michikichi katika Kijiji cha Kimala Misale wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani na Kampuni ya Naval Bharat PTE Ltd (NBS) ya Singapore. Mkurugenzi wa NDC, Gideon Nasari akizungumza baada ya makubaliano hayo kuwa mradi huo utagharimu Sh bilioni 160 katika eneo la hekta 10,000
 
Alisema mbali na kulima michikichi, pia kutaanzishwa kiwanda cha kuchakata mafuta yanayotokana na michikichi.
"Mradi huu utasaidia kupunguza vitendo vya kusafirisha michikichi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuchakatwa na kupunguza uagizaji wa mafuta hayo kutoka nje ya nchi," alisema Nasari.

Alisema kati ya hekta 10,000 za mradi huo, hekta 2,000 zitawanufaisha wakazi wa Kijiji cha Kimala Misale na masalia ya michikichi yatazalisha umeme wa megawati 10.
NDC itawekeza katika mradi huo kwa asilimia 20 wakati NBS itawekeza kwa asilimia 80, alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NBS, Devineni Ashwin alisema mradi huo utaanza mara moja tathmini ya mazingira itakapofanyika na kupata vibali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba alisema wilaya hiyo imekubaliana mradi huo utekelezwe kwa sababu inaamini utakuwa na mafanikio.
Chanzo:mtanzania
0 comments

ARSENAL, BARCA zapangwa makundi ya KIFO LIGI YA MABINGWA

ARSENAL, BARCA zapangwa makundi ya KIFO LIGI YA MABINGWA

arsenal fd47f

MABINGWA mara saba wa Ulaya, AC Milan, waliotolewa na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa misimu miwili iliyopita, wamepangwa kundi moja na vigogo hao wa Katalunya katika hatua ya makundi msimu huu baada ya droo iliyopangwa jana. (HM)

Arsenal ambayo kocha wake Arsene Wenger anapambana kusajili jina kubwa kabla ya pazia kufungwa, imepangwa Kundi F pamoja na Marseille ya Ufaransa, Borussia Dortmund ya Ujerumani na Napoli ya Italia.

Mabingwa mara tisa, Real Madrid wamepangwa kundi moja na Juventus, B ambalo pia lina timu za Galatasaray and FC Copenhagen.

Mabingwa watetezi, Bayern Munich wamepangwa na CSKA Moscow, Manchester City na mabingwa wa Czech, Viktoria Plzen Kundi D, ambayo inawapa njia nyeupe ya kufuzu.

Chelsea, mabingwa wa misimu miwili iliyopita, wamepangwa na Schalke 04, FC Basle na Steaua Bucharest Kundi E, timu mbili ambazo ilizifunga kuelekea kutwaa taji la Europa League msimu uliopita.

Mabingwa mara tatu wa taji hilo, Manchester United imepangwa na Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen na Real Sociedad katika Kundi A.

AC Milan na Barcelona wamekutana mara sita katika misimu miwili iliyopita na Wakalunya wameng'ara dhidi ya Wataliano.
Timu ya Serie A ilifungwa mabao 4-2 jumla katika hatua ya 16 Bora mwaka jana na 3-1 jumla katika Robo Fainali misimu miwili iliyopita, wakati timu hizo zilipokutana pia kwenye hatua ya makundi.

Timu hizo mbili zimepangwa katika Kundi H, sambamba na mabingwa mara nne Ajax Amsterdam na mabingwa wa 1967, Celtic, ambao walikutana na Barcelona katika hatua ya makundi msimu uliopita na kupata ushindi wa kukumbukwa wa nyumbani. Chanzo: binzubeiry


0 comments

Diamond amkabidhi Mzee Ngurumo gari aina ya Funcargo;

Diamond amkabidhi Mzee Ngurumo gari aina ya Funcargo;

DIAMOND SHOW 020-1 8998c
Msanii Diamond Platnum amefanya kufuru usiku huu kwa kutoa zawadi ya Gari kwa Mzee Ngurumo Mwanamziki wa miaka mingi na mkongwe nchini aliyestaafu majuzi kufanya kazi za mziiki.

Tukio hilo limetokea usiku huu ndani ya ukumbi wa SERNA HOTELkatikati ja jiji la DSM ambapo Diamond Platnum anazindua video yake ya wimbo wa #one fun.

DIAMOND SHOW 025 b03d6

Mzee Ngurumo amesema"Haamini macho na masikio yake,hanachakusema zaidi ya ASANTE kwa msanii huyo"Lakini pia amesema hajui hata mke wake atasemaje baada ya kumwona akiingia na gari ndani ya nyumba yake.

Mzee ngurumo amekuwa na matatizo ya kiafya siku za karibuni nakupelea kustaafu mziki kabisa.Wazee wa msondongoma ndio wanajua makali ya Mzee Ngurumo.


0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger