TANAPA KUANZISHA MIRADI YA VIVUTIO VYA ASILI KWENYE VIJIJI VYA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI HIZO.
Hifadhi ya Taifa TANAPA inatarajia kuanzisha miradi ya
vivitio vya asili vilivyoko kwenye vijijini vya maeneo yanayozunguka hifadhi hizo
ili kuimarisha uchumi wa maeneo hayo na jamii inayozunguka hifadhi hizo nchini.
Hayo yameelezwa na Meneja Ujirani mwema Taifa Ahmed Mbagi
wakati akiongea na waandishi wa habari
za mazingira Mkoani Tanga TARUJA walipotembelea hifadhi ya saadani ikiwa ni
sehemu ya mafunzo yaliyoandaliwa na TANAPA .
Amesema miradi huyo ni sehemu ya mipango waliyokuwapo nayo
ya kuhakikisha vijiji vinavyopakana na hifadhi za taifa kunufaika na wageni
waoingia kwa njia ya vivutio vilivyoko kwenye maeneo yao kwa lengo la
kujiongeza kipato.
“Nia yetu ni kuona wanachi wananufaika na raslimali
walizokuwapo nazo kwa kuweka utaratibu wa kila maeneo kutangaza vivutio
walivyonavyo zaidi ya wanyama walioko kwenye hifadhi basi wajionee mila na
tamaduni zilizoko sehemu husika “.AlisemaMbagi.
Nae Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Hussein Mselo amesema
kuwa bado wananchi wa maeneo hayo hawana muako wa kutangaza vivituo vilivyoko
kutoka na kukosa uwelewa wa taratibu za uendeshaji wa vivutio hivyo.
“Hapa kijijini tuna vivutio kama soko la watumwa,mbuyo
nyonga ambao ulitumika kuwanyonga watumwa pamoja na makaburi ya wajerumani
wakwanza kurika saadani lakini kutoka na kukosa uwelewa wa kuvitangaza vivutio
hivyo tunakosa fedha kutoka kwa watalii”alisema Mselo.
Alisema kwa sasa waandaa utaratibu wa kuhakikisha wanatoa
elimu kwa wananchi wa maeneo ya jirani
yenye vivutio hivyo ili kujua umuhimu wake pamoja na fursa zilizopo ili waweze
kuiongezea kipato kitakacho saidia kijiji na wananchi wake.
Hifadhi ya Saadani licha ya kuwa na mbuga za wanyama ni moja
ya eneo la kwanza kuanzishwa kwa biashara ya soko la watumwa na waarabu
waliowahi kuishi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki karne ya 14 iliyopita.
Post a Comment