Featured Post Today
print this page
Latest Post

WAKULIMA WATAKA KUJENGEWA SOKO


kulima 21339
Muheza. Wakulima wa Vijiji vya Kwemhosi, Bembe na Mtombuzi, wilayani Muheza mkoani Tanga wameiomba Serikali kuwawekea soko la uhakika la kuuzia mazao yao.
Wakizungumza mjini hapa juzi, wakulima hao walisema wamechoshwa kulanguliwa na watu waliodai ni madalali, baada ya kuwawekea vitisho vya kuacha kupeleka mazao yao masoko ya mjini.
P.T

Walitaja vitisho hivyo kuwa ni ushuru wa forodha, mapato na kutokuwa na leseni ya kufanya biashara, hivyo kulazimika kuwauzia kwa bei ya chini.
"Unajua wakulima wa vijijini tuna woga hasa unapoambiwa kuna watu wa mapato na wakamataji wasiokuwa na leseni... Hawa madalali wamekuwa wakitumia mbinu hii kujitajirisha," alisema Rukia Karata.
Na Salim Mohammed(mwananchi)
0 comments

CCM YAFUKUZA MADIWANI 8 WA MANISPAA YA BUKOBA.

 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, leo kimewafukuza madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kupitia chama hicho na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea
Waliofukuzwa ni:
  1. Richard Gaspar (Miembeni )

  2. Murungi Kichwabuta (Viti maalum)

  3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

  4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

  5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

  6. Robert Katunzi (Hamugembe)

  7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

  8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)



Source:mpekuzihuru.
0 comments

WANYARWANDA WALIOTIMULIWA TANZANIA WAKIMBILIA UGANDA AMBAKO NAKO WAMEKATALIWA.

Wengi wa wahamiaji haramu waliokuwa mkoani Kagera ambao wengi wao ni wanyarwanda wamekimbilia Uganda kama wakimbizi lakini makambi ya wakimbizi huko Uganda yamekataa kuwapokea.
Pamoja na serikali ya Rwanda kupitia ubalozi wake Uganda kufanya jitihada ya kutaka kuwarudisha Rwanda lakini wakimbizi  hao  wamegoma  kurudi  kwao  kwa  hofu  ya  kuuawa  wakirudi  Rwanda....
 Source:  jamii forum
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger