Featured Post Today
print this page
Latest Post

Wabunge Chadema, CUF watoka nje..;

Wabunge Chadema, CUF watoka nje..;

mbowe_chadema_08064.jpg

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa.Wabunge waliotoka bungeni jana yapata saa 12.15 ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi huku Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP, Augustine Mrema akiendelea kubaki ukumbini.
Kitendo cha wabunge hao wa upinzani kilionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika wakiwakejeli kwa kupiga meza huku wakisema: "Kwendeni zenu, tumewazoea."

Wakati wabunge hao wakiondoka, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikuwa akiwasisitiza wabunge wanaobakia wawe watulivu, maana kuna usalama wa kutosha ndani ya ukumbi huo.
"Mnaotoka nimewaona wote na mnanijua," alisikika Naibu Spika Ndugai akiwatahadharisha wabunge wa upinzani waliosusa mjadala huo.

Wabunge wa CCM waliendeleza vituko ambapo baada ya wapinzani kutoka, wabunge Juma Nkamia (Kondoa Kusini), Hilary Aeshi ( Sumbawanga Mjini) na Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) walikwenda kukaa katika viti vya kambi ya upinzani.

Kabla ya kutoka kwa wabunge hao wabunge wawili kutoka CUF waliomba mwongozo wa Spika, wakitaka muswada huo kuondolewa ili kuwapa nafasi Wanzanzibar kutoa maoni yao.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohamed Mnyaa (CUF) aliomba mwongozo akitaka muswada huo uondolewe, hadi hapo Wazanzibar watakaposikilizwa.

Alisema kuwa kwa maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wamesikiliza maoni ya wadau wengi, lakini Zanzibar hawakwenda kuwasikiliza wadau wa eneo hilo.
"Na hili suala zima katika masuala ya katiba linahitaji usawa wa washirika, tunazungumza kitu kinachohusiana na Zanzibar na Tanzania Bara, ili kupata maoni ya nchi nzima kuna uhalali gani wa Bunge hili kuendelea na mjadala huu?" alihoji.
Hata hivyo, alikatizwa na kelele za Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), ambaye alitoa taarifa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilialika wajumbe mbalimbali ikiwamo Zanzibar.
"Miongoni wa wajumbe walioalikwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali ambao walikuja mbele ya Katiba," alisema Pindi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Mbunge wa Konde, Khatibu Said Alli (CUF), alitaka mwongozo wa Spika kuhusiana na ujumbe mfupi wa maneno ambao aliupokea ukimtisha, kutokana na kitendo chao cha kumuunga mkono Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu.
"Unashabikia mambo ya Tundu Lissu leo, endelea ila mtashughulikiwa," aliunukuu ujumbe huo na kuongeza kuwa hafahamu umetoka kwa mbunge gani ila wahudumu wa Bunge ndio waliompelekea.
Akijibu mwongozo huo, Ndugai alisema kuwa ni miongoni mwa mambo ambayo anayachukua na kuyafanyia kazi ni suala hilo. Pia Ndugai aliomba ujumbe huo apelekewe.
"Hii ni demokrasia mara nyingi imeshatolewa miongozo, jibu linatolewa hapo hapo ama baadaye na kwa hoja zilizotolewa inakilazimu kiti kupata ushauri hapo baadaye," alisema Ndugai.
Hata hivyo, baada ya Ndugai kutoa majibu hayo, wabunge wa upinzani waliamua kutoka ndani ya ukumbi huo.
Baada ya wabunge hao kutoka Naibu Spika Ndugai aliendelea na ratiba ya Bunge kwa kusema, jambo hilo halikupangwa kumalizika jana na kwamba litaendelea kujadiliwa hata ikibidi hadi keshokutwa.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisimama kabla ya mjadala kuendelea na kutetea hoja kuwa makundi yote yalisikilizwa tofauti na inavyodaiwa na wapinzani.
"Hata katika marekebisho ya sheria mbili hizi, mimi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali tumekutana na viongozi wengi na mawaziri na ndiyo maana tumeahirisha Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni," alisema.
Alisema, yeye (Lukuvi) alikuwa Mwenyekiti wa ujumbe uliotumwa na Rais kuitisha makundi ya siasa ambayo yalijadili muswada huo. Lukuvi alisema kuwa, pande zote zimeshiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao, "kama hizi ni sarakasi za kisiasa mimi sijui."
Baada ya kutoka, wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walifanya mkutano wa pamoja kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa, wabunge hao walikubaliana kufanya kila njia kuhakikisha wanazuia mjadala huo leo.
Pia wabunge wa CCM nao walikutana nao mara baada ya Ndugai kuahirisha kikao cha jioni.
Lissu achafua hali ya hewa
Hotuba ya Lissu ndiyo iliyochafua hali ya hewa baada ya kuituhumu Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kwa kutohoji watu wa Zanzibar wakati wakikusanya maoni kuhusu muswada huo.
Alisema licha ya kamati hiyo kukusanya maoni ya taasisi za kidini na za kiraia, taasisi za elimu ya juu na za kitaaluma, vyama vya siasa na asasi nyingine, lakini bado haikwenda Zanzibar kukusanya maoni ya watu wa huko.
"Wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya muswada huu ni Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa kabisa, licha ya sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar," alisema Lissu.
Pamoja na suala hilo, Lissu alitaka pia Rais wa Jamhuri ya Muungano aondolewe madaraka ya kuteua Wajumbe wa Bunge Maalumu wasiokuwa wabunge au wawakilishi kuwa inavuruga au kuondoa kabisa dhana ya uwakilishi wa wananchi na uhalali wa kisiasa katika mchakato wa Katiba Mpya.
Pia alipendekeza kuongezwa kwa idadi ya wajumbe ifikie 792, kwani Tanzania ina idadi ya watu milioni 45 kwa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Lissu pia alitaka wawakilishi wa Zanzibar waongezwe bungeni, kwa Zanzibar itakuwa na wajumbe 219 kwenye Bunge lenye wajumbe 604, sawa na takriban 36% ya wajumbe wote. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka idadi iwe nusu kwa nusu kati ya pande mbili za Muungano.
Wajumbe 166
Kutakuwa na wajumbe 166 wasiotokana na Bunge na Baraza la Wawakilishi watateuliwa na Rais. Kutakuwa na Wabunge 357 na Wawakilishi 81 na kufanya Bunge Maalumu kuwa na jumla ya wajumbe 604.
Chikawe asoma muswada
Mapema akisoma muswada huo, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe alisema Rais atakaribisha makundi mbalimbali kuwasilisha majina yasiyozidi matatu kila kundi ambao watateuliwa kama wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba. Alisema pia Kifungu cha 27 (2) kitatoa fursa kwa uhuru wa maoni katika mijadala ya Bunge Maalumu na maoni hayo hayatahojiwa mahakamani au sehemu yoyote nje ya Bunge Maalumu.
Chikawe alisema Bunge Maalumu la Katiba litakaa kwa siku 70 mfululizo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili rasimu hiyo. Hicho kitakuwa kikao kirefu zaidi cha Bunge kuwahi kukaa nchini Tanzania.
"Kutokana na unyeti wa suala lenyewe muswada huo unampa nguvu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuongeza siku 20 ili kujadili katiba," aliongeza Chikawe.
Imeandikwa na Daniel Mjema na Sharon Sauwa


0 comments

Museveni awakutanisha Rais Kikwete na Kagame

museven_d895a.jpg
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Wakati hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni, uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya Jiji la Kampala.
Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23.
Mbali na viongozi hao wa Tanzania na Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia.
0 comments

Siri ya ushindi wa Francis Cheka dhidi ya mmarekani yafichuka.

Siri ya ushindi wa Francis Cheka dhidi ya mmarekani yafichuka.

SIRI ya ushindi alioupata bondia maarufu nchini, Francis Cheka ‘SMG’ dhidi ya Mmarekani Phil Williams imefichuka baada ya mke wa bondia huyo kutoka Morogoro, Tosha Azenga kutoa la moyoni. 


Akizungumza katika mapokezi ya mumewe mwishoni mwa wiki iliyopita alipowasili mkoani hapa, Tosha alisema mumewe amekuwa akifanya vizuri kutokana na ukweli kwamba kila anapokaribia pambano huwa anamnyima unyumba.
  
“Siri ya mafanikio ya mume wangu ni kufanya mazoezi sana na zaidi ya yote anapokuwa na mchezo huwa simpi tendo la ndoa ambalo ni sumu kali ya mazoezi.
 

“Kwa mfano, gemu la juzi na yule Mmarekani, siku chache kabla sikumpa kabisa tendo la ndoa na yeye anakubaliana na mimi kwani anajua nafanya hivyo kwa nia njema, faida yake mmeiona,” alisema Tosha aliyemzalia Cheka mtoto mmoja wa kiume aitwaye Historia

Ushuhuda wa mwanamke huyo ulipongezwa na baadhi ya wadau hasa wanaojua madhara ya kufanya mazoezi sana kisha kuendekeza ngono kwani ni vitu viwili visivyochanganyika.
“Anachofanya ni sawa, huwezi kuwa unafanya mazoezi ya mpira au ngumi kisha ukitoka hapo unaenda kufanya mapenzi, wanaoendekeza hivyo ndiyo hao unasikia leo kafanya vizuri kesho kavurunda,” alisema Hassan Tolu wa Kihonda.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro aliyekuwepo kwenye mapokezi ya Cheka, Mhe. Saidi Amanzi alimpongeza ‘Mrs Cheka’ kwa uamuzi wake ambao umesababisha bondia huyo apeleke heshima nyumbani.
 
“Tumpongeze kwanza Cheka kwani licha ya yeye kuwa bondia na kuwachapa watu kila kukicha lakini muangalieni mkewe, hana alama yoyoye ya kichapo kwenye uso wake.
 


“Pia nimpongeze mama huyu kwani alidai kwamba mumewe anapokuwa na pambano huwa hamgusi kabisa,” alisema mheshimiwa huyo na kushangiliwa na umati uliofurika kwenye mapokezi hayo.

 
Usiku wa Agosti 30, mwaka huu Cheka aliandika historia kama lilivyo jina la mwanaye kwa kumtwanga kwa pointi bondia Phil Williams kutoka Marekani na kutwaa ubingwa wa dunia unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi la Dunia uzani wa Super Middle.


0 comments

MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA RASMI MKOA WA DSM

MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA RASMI MKOA WA DSM

Picture_398_054e6.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuuwa Chama cha Skauti Tanzania Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Picture_324_6daab.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuuwa Chama cha Skauti Tanzania Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam
Picture_402_a4f95.jpg Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Terminal one.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

0 comments

JWTZ lasitisha likizo....Hali ya utayari wa Kijeshi ( Military readiness) yatangazwa.

JWTZ lasitisha likizo....Hali ya utayari wa Kijeshi ( Military readiness) yatangazwa.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesitisha wapiganaji wake kwenda likizo na kuwaita waliokuwa likizo kurudi makambini. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani kabisa vya kiinteligensia vijulikanavyo kama ‘KAINZI’,  uamuzi huo umeenda sambamba na kuweka hali ya utayari wa kijeshi (military readiness) kufikia asilimia 50 ( katika hali ya utulivu na amani nchini hali ya utayari wa kijeshi huwa asilimia 25 )

Kwa mujibu wa chanzo  hicho ambacho kimekuwa kikifuatilia mwitikio wa vyombo vyetu vya usalama kufuatia kuongezeka kwa hali ya utete katika eneo la maziwa makuu,  vikosi vya jeshi nchini kufikia jana vilikuwa vimeshasomewa taarifa hiyo ya kusitisha likizo na hata pasi za kutoka makambani huku maafisa wake ambao walikuwa nje ya vituo vyao vya kazi wakitakiwa kurudi makambini. 


Uamuzi huu hata hivyo haujawa wazi kama unahusu wapiganaji wote nchini au ni wa Brigedia za Tabora au Brigedia za vikosi maalum tu.

Kwa mujibu wa chanzo hicho cha kuaminika Brigedia za Tembo na Kifaru (Tabora) tayari zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kufanya ‘movement’ yoyote ya kijeshi. 


“Unajua tangu sakata la Rwanda lianze ,  vyombo vyetu vya usalama na inteligensia vimeona kuwa kuna sababu ya msingi ya kujiweka katika hali ya utayari wa kijeshi” kilisema chanzo hicho. 

Baada  ya  kufuatilia zaidi na kwa kina habari hizi,  inaonekana kuwa kuna taarifa za kiusalama ambazo zimesababisha uamuzi huu kuchukuliwa. Pamoja na uamuzi huu , habari hizi zinadokeza pia kuwa JWTZ linaweza kuwaita baadhi ya reserve ili kuliongezea nguvu zaidi. 

Kwa kawaida kama ilivyokuwa kabla ya Vita ya Kagera baadhi ya maafisa wanaoweza kuongeza nguvu jeshini ni pamoja na wale kutoka vyombo vingine vya usalama kama Polisi, Mgambo, Magereza, n.k ambavyo vinaweza kutakiwa kutoa idadi fulani ya watu kujiunga na JWTZ.

Pamoja na maamuzi hayo,  chanzo hicho kiliarifu  kuwa hata wapiganaji wa JWTZ ambao walikuwa wanaandaliwa kwenye shughuli mbalimbali za kulinda amani nao wamesitishwa sasa hivi na wanapelekwa kwenye moja ya mikoa iliyoko mpakani kwa sababu ambazo mtoa habari wetu hakutaka kuziweka wazi.
0 comments

MBAKAJI ACHANGANYIKIWA KUAMBIWA MWANAMKE ALIYEMBAKA ANA VIRUSI VYA UKIMWI

MBAKAJI ACHANGANYIKIWA KUAMBIWA MWANAMKE ALIYEMBAKA ANA VIRUSI VYA UKIMWI 

Mbakaji ambaye alifungwa jana anasubiria vipimo kubaini kama ameathirika na virusi vya ukimwi kutoka kwa muathirika wake.

Richard Thomas, mwenye umri wa miaka 27, alianguka chini pale polisi walipomtaarifu kuhusu hali ya afya ya mwanamke huyo na anasubiria kusikia kama ameathirika na virusi hivyo visivyotibika.

Thomas, mkazi wa Leigh huko Greater Manchester, alimfahamu mwanamke huyo na alijua kwamba ana ugonjwa mwingine lakini hakuwa akijua kuhusu virusi vya ukimwi. Mahakama ilielezwa alishitushwa pale alipotakiwa kupelekwa hospitali, Mahakama Kuu ya Liverpool ilielezwa.

Alijipeleka nyumbani kwake katikati ya usiku na  mwanamke huyo akazinduka usingizini na kukuta Thomas akimbaka.
"Alitulia na hakuna aliyemwongelesha mwenzake. Alipangisha kaptula yake na kuondoka," alisema mwendesha mashitaka Harry Pepper.

"Alikamatwa na kuhojiwa na alisema alikuwa amelewa kupita kiasi, kutumia cocaine na kurukwa akili na hakuweza kukumbuka tukio hilo," aliongeza.
Wakili wake, Virginia Hayton, alisema kwamba bado hawezi kukumbuka shambulio hilo lakini alipoelezwa kuhusiana na hilo alisema kwamba mwanamke huyo 'hawezi kusema uongo, anaeleza ukweli. Kama anasema nimefanya hivyo, basi nimefanya'.

Akimfunga Thomas miaka mitano na miezi minne jela Jaji Mark Brown alisema kwamba amefanya 'kosa hili lisilopendeza' wakati mwanamke huyo akiwa amelala fofofo, akiwa amemeza vidonge vya usingizi, na ilimwacha akiwa mwenye mateso na wasiwasi.

Pia alimwamuru Thomas kusaini Rejista ya Wahalifu wa Kujamiiana kwa maisha. Thomas alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke huyo Julai 20 mwaka huu.
Hayton alisema kwamba Thomas, ambaye hapo kabla alishawahi kutiwa hatiani lakini si kwa makosa ya ubakaji, 'katili' na 'hawezi kuelewa kwanini alifanya vile na inamsumbua mno'.

Alisema kwamba alianza kutumia bangi akiwa na umri wa miaka tisa, kunywa pombe kupita kiasi akiwa na umri wa miaka 11, kutopea dawa za kulevya hadi kufikia kurukwa akili na cocaine akiwa na umri wa miaka 13 na aliwekwa chini ya uangalizi maalumu mwaka uliofuata.

Amekuwa akijaribu kuwasiliana na familia yake lakini hawataki kufanya chochote kumsaidia na sasa atakuwa mbali na mpenzi wake na binti yao mdogo na mabinti zake wengine wawili wakubwa aliowapa katika mahusiano yake ya awali.

Hayton aliieleza mahakama hiyo kwamba Thomas hawezi kupata majibu ya vipimo vyake vya virusi vya ukimwi hadi Ijumaa na amekuwa na hofu kubwa ya matokeo hayo.
"Ni kosa lake mwenyewe, kama asingefanya kosa hili asingejiweka mwenyewe mahali hapa."
0 comments

WANAUME WAPENI DOSE YA NGUVU WANAWAKE ZETU WAFIKE KILELENI

WANAUME WAPENI DOSE YA NGUVU WANAWAKE ZETU WAFIKE KILELENI 

Nasikitisha na kushangaza,unakutana na Msichana wa miaka 28-30 anakwambia tangu aanze Mapenzi akiwa na Miaka 19 hakuna Mwanaume yoyote amewahi kumfikisha kileleni...Imagine,anafanya Mapenzi miaka karibu 10 lakini anatumika yeye tu...
Amekuwa Sugu sasa na kilele pekee anachokijua ni cha Mlima Kilimanjaro,amekata tamaa kama kuna kitu kama hicho duniani.. Ukikutana na mwanamke wa namna hii ili umridhishe inapaswa kwanza uende Gym,ule Siagi na jibini,dozi ya karanga na supu ya pweza wiki 2 umkeshee kisawasawa..

Lakini unapaswa pia kumfanyia Counselling ili aamini tena kwamba kilele sio Kibo na Mawenzi tu...inataka Moyo...WANAUME:Msiwafanyie hivyo Wasichana,wapeni dozi inayostahili,ukipewa chezo kamua haswa,sio unakurupuka tu hueleweki unachofanya ni nini Robo saa unakoroma..

Huo sio uanaume..Uanaume kazi..Mnatupa shida tunakuja kuoa Wanawake wamekomaa,hata utumie Mwiko kilele hakionekani hata kwa darubini... 

Ukipewa Kazi itendee haki kazi...Kama hujui kukuna nazi waachie wakwezi...Girls wanapata shida sana,halafu we mtaani unajitamba kumbe huna lolote.


 

0 comments

SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO.


SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO.
 
Siri  ya  Aunt Ezekiel  kupigwa  chupa  club  na  kujeruhiwa  mkono wake imefichuka.Habari  za  uhakika  zinadai  kwamba  Aunt  alipigwa  chumba  na  mrembo  wa  kike  katika  harakati  za  kugombea  penzi  la  mwanaume...


 Mwanaume  aliyekuwa  akigombaniwa  ni  Jeff  ambaye  anadaiwa  kuwa  ni boyfriend  wa  Yvonne ( aliyempiga  aunt  chupa )..

Kutokana  na  aibu  hiyo, mastaa  kadhaa  wameongea  na  mpekuzi  kwa  nyakati  tofauti  na  kueleza  masikitiko  yao  dhidi  ya  aunt  Ezekiel  ambaye  ni  mke  wa  mtu... 

Katika  maongezi  hayo, mastaa  hao  walidai  kwamba  mambo  anayofanya  aunt  hayaendani  na  matendo  ya  mke  wa  mtu. Aunt amekuwa  ni mtu wa baa, club  na  madanguro  mengine  ya  usiku, hali  inayotia  shaka  uhai  wa  ndoa  yake. 

" Aunt  kapata mume mwelewa sana  ambaye  kakiheshimu sana  kipaji  chake  kwa  kuto-mbana.

"Cha  ajabu yeye ameanza  kufanya  mambo ya aibu  kwa kuendekeza ngono  nje  ya  ndoa  yake" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake ..

Muigizaji mwingine wa kike ambaye hakuwa  tayari  kuchorwa  mtandaoni  alisema:
  
 "Aunt ajiangalie sana.Yeye  ni mke wa mtu kwa  sasa. Kitendo  alichokifanya kimemchafua mpaka ukweni na asipokuwa makini  atampoteza mume wake... 

"Yvonne alikuwa anamlinda bwanake, mi  siwezi kumlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"


0 comments

Majonzi simanzi vyatawala jijini Mwanza,maelfu wauaga mwili wa Askofu Dr.Moses Kulola.

Majonzi simanzi vyatawala jijini Mwanza,maelfu wauaga mwili wa Askofu Dr.Moses Kulola.

Mwili wa Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT na baba wa kiroho wa watumishi wengi Askofu Moses Kulol




0 comments

UJUMBE MZITO KUTOKA KWA AFANDE SELE.

UJUMBE MZITO KUTOKA KWA AFANDE SELE.


#Nimekumbuka wakati naanza hiphop music, kuna kipindi #Taji Liundi alikua na matamasha yake ya ukimwi/beach bam, halafu msanii mkubwa alikuwa ticha wangu #joseSugu ndio pekee alikua akilipwa elfu 50 kwa show siku moja akagoma, Taji kapagawa akamuongezea elfu 20, Sugu akazikataa, akampitishia chini ya mlango huku anambembeleza sana kaka Taji, Hili game noma safari ndefu sana,
acha #niggaJ aitwe #profesa , #sele aitwe #afande , #gk aitwe #king#msafiri aitwe#solo na #JOSE AWE #MBUNGEsugu
follow me twitter @afandesele_king or Selemani Msindi
waweza share post hii.






0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger