Featured Post Today
print this page
Latest Post

Pengo akemea masilahi binafsi Bunge la Katiba

Pengo akemea masilahi binafsi Bunge la Katiba


PENGOPX_1c0c7.jpg

"Ni vyema tukatambua kuwa Watanzania ni wapenda amani, hivyo wasingependa kuona kukijitokeza tofauti kati ya wajumbe wa Bunge hilo.

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinal Pengo amesema shughuli za mchakato wa Katiba zifanyike kwa amani na kwamba ziwalinde Watanzania katika umoja na mshikamano waliyokuwa nao.

Pia, amewataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuweka masilahi yao kando na kutanguliza masilahi ya taifa kwa faida ya Watanzania.


Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa Katisa Katoliki Magomeni, Kardnali Pendo alisema ni vyema viongozi wakafahamu kwamba Watanzania ni watu wanaopenda amani, na kwamba yeye angepAenda kuona amani iliyopo inadumu.

Alisema: "Niseme kwamba, shughuli za mchakato wa kuandika Katiba Mpya zifanyike kwa amani."
Aliongeza: "Ni vyema tukatambua kuwa Watanzania ni wapenda amani, hivyo wasingependa kuona kukijitokeza tofauti kati ya wajumbe wa Bunge hilo,"
Alisema kama tunataka nia ni kupata katiba bora, ni lazima wajumbe wabunge la Maalum la Katiba kuweka masilahi ya yao kando na kuangalia yale ya taifa kwa faida ya Watanzania wote.

Alitoa mfano kwa baadhi ya vingozi wa nje ya nchi wanavyotambua mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwa ni mtu aliyependa amani, umoja na mshikamamno.

Alisema leo (jana) alifuatilia vyombo vya habari na kusikia kuwa Rais wa Zimbabwe (Robert Mugabe) akimuelezea Mwalimu Nyerere kama kiongozi shupavu aliyeweka misingi ya amani Tanzania kwa kuwa alikuwa mpenda amani.

Naye, Paroko wa Kanisa hilo Joseph Matumaini alisema Kanisa hilo limejengwa kwa ghalama ya Sh1.25 bilioni fedha ambazo zimetokana na michango ya waumini wao.
Alisema: "Kanisa hili limejengwa kwa jitihada za waumi kwa kujitolea, na kwamba tunawashukuru wote kwa kuijenga nyumba ya mungu,"

Alisema Kanisa hilo lina uwezo wa kuchukua waumini 1500.
Chanzo, mwananchi. (R.M)
0 comments

Kawambwa akerwa daraja la tano kuitwa sifuri

Kawambwa akerwa daraja la tano kuitwa sifuri

kawambwapx_3ff8e.jpg

Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Dodoma. Waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa sifuri.

Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alivishutumu vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.

Alisema kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.

"Ndugu zangu waandishi wa habari, kitu ambacho hamkufanya haki kwa Watanzaniasafari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja sifuri," alisema na kuongeza:

"Unakuaje na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne lakini unapofika la tano unaita sifuri katika namna ambavyo waandishi wa habari walipenda."
Dk Kawambwa alisema vyombo vya habari vimekuwa vikipenda taswira ya nchi ionekane kuwa ni kufeli. "Lakini ninachosema ni kwamba, pointi ni zile zile tulichoondoa ni daraja la tano."

Chanzo, mwananchi (R.M)
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger