Featured Post Today
print this page
Latest Post

Wanajeshi wa UN mali wanahitaji vifaa

Wanajeshi wa UN mali wanahitaji vifaa

kk_8edb7.jpg

Umoja wamataifa umeomba usaidizi wa vifaa kuwawezesha wanajeshi wake wa amani nchini Mali kushika doria.
Kikosi hicho cha UN kilianza kulinda amani nchini Mali mwezi Julai , na kina chini ya nusu ya wanajeshi 12,000 wanaohitajika kushika doria

Mjumbe maalum wa UN nchini Mali, Bert Koenders, amesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni yamekuwa dalili ya changamoto zinazowakumba wanajeshi hao.
Aliongeza kuwa kikosi hicho kinachojulikana kama Minusma, kinahitaji rasilimali zaidi ili kuweze kudhibiti hali Kasakazini mwa nchi.

Wanajeshi wa Ufaransaka , waliongoza operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu na kuwaondosha kutoka katika eneo hilo.

Uchaguzi wa Urais ulifanyika mwezi Julai lakini wapiganaji hao wakaanza tena kufanya mashambulizi Kaskazini mwa nchi ambako kundi linalotaka kujitawala la Tuareg pamoja na wapiganaji wengine wamekitaka kambi.
 
Lakini Bert Koenders, anasema kuwa tisho la usalama linasalia kuwa changamoto kubwa.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alishambulia mji wa Timbuktu tarehe 28 Septemba huku wapiganaji wa kiisilamu nao wakilipiza mashambulizi hayo kwa kurusha makombora.

Kikosi cha kulinda amani cha UN kilipata pigo jengine mwezi Agosti baada ya idadi nyengine kubwa ya wanajeshi wa Nigeria kurejea nyumbani kupambana na wanamgambo wa Boko Haram.
Hatua hii iliwaacha wanajeshi wa UN na chini ya wanajeshi elfu sita. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi wanajeshi 12,640 ifikapo mwezi Disemba.

UN inatarajiwa kuwapeleka wanajeshi wengine huko kuchukua nafasi ya wanajeshi wa Ufaransa waliorejea nyumbani baada ya kuingilia kati mgogoro huo wapiganaji walipotishia kuvamia mji mkuu wa Mali Bamako mwezi Januari.

Wapiganaji hao wenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeeda walidhibiti Kaskazini mwa Mali, ikiwemo miji mingine mikubwa ya Gao, Kidal na Timbuktu, baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka 2012.
0 comments

HEBU ONA UNYAMA HUU MUME AMKATA MKE WAKE MGUU

HEBU ONA UNYAMA HUU MUME AMKATA MKE WAKE MGUU

aa_11477.jpg
bb_f747f.jpg

Na Waitara Meng'anyi, Tarime.

Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.

Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.

"Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema Ghati.

Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata alifiki kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.

" Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia ukakatika kama unavyoona" alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.

Wakati anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo hayo.
"Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa" alieleza .

Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
" Nimeishi naye kwa miaka mine sasa na tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka linguine ni baada ya kuoa mke wa pili ambapo alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu" alisema Ghati.

Ghati hataweza kurudiana na mume wake huyo kwa kitendo alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo jera ili ajifunze kutokana ukatili aliomfanyia.

" Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula" alisema.
Wananchi walioshuhudia kitendo hicho walionesha kusikitishwa na kukilaa kuwa kinaendelea kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .

" Sikifurahii kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu mwenzako na hii inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku kutuona sisi ni wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu huyu mtu adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho kwa wengine" alisema Mwita Machera aliyekuwa hostalini hapo.

Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.

Hata hivyo siku mojs baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu nza wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.

" Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote" alisema Kamugisha kwa nija ya simu
0 comments

Urithi wa Nyerere utaendelea kuisaidia Afrika kuimarisha umoja

Urithi wa Nyerere utaendelea kuisaidia Afrika kuimarisha umoja

Urithi ulioachwa na rais wa zamani wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere utaendelea kuzisaidia nchi za Afrika kuimarisha umoja na maendeleo yenye ufanisi.
Hayo yamesemwa na balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Liu Jieyi, katika mkutano wa kuadhimisha siku ya Mwl. Nyerere iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Amesema, miaka 14 imepita toka kifo cha Mwl. Nyerere, lakini kujitolea kwake kutetea uhuru wa nchi za Afrika, mtazamo wake kuhusu Afrika, uadilifu, na maadili yake vinakumbukwa kama urithi wa thamani.
Amesema kwa juhudi zake na kujitolea, Umoja wa Nchi Huru za Afrika,OAU, ambao sasa unajulikana kama Umoja wa Afrika, ulianzishwa na kubadilisha sura ya kisiasa ya kimataifa.

 

0 comments

UNHCR yaokoa maisha ya mtoto Albino aliyekimbia DR Congo

UNHCR yaokoa maisha ya mtoto Albino aliyekimbia DR Congo


Wakimbizi kutoka DRC walikokimbilia ikiwemo familia ya Jeff ambao walilazimika kukimbia
Kijana mmoja mwenye ulemavu wa ngozi au albino amelazimika kukimbia kutoka DR Congo si kutokana na machafuko bali kutokana na watu wanaodaiwa kumsaka ili wachukue viungo vyake kwa ajili ya ushirikina.

Anaclet ambaye ni baba mzazi wa kijana huyo aitwaye Jeff ameliambia shirika la kuhudumai wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR nchiniBurundikuwa wamekimbilia kituo  cha  muda cha wakimbizi cha Kajaga, hukoBujumburaili kuokoa maisha ya mwanae mwenye umri wa miaka Sita.
Tayari UNHCR inawapatia hifadhi na ulinzi ili kuondokana na kitendo cha kuhamahama ambapo Mwakilishi wa shirika hilo nchini Burundi, Catherine Huck amesema wakati umefika kwa serikali kuchukua hatua muafaka dhidi ya fikra potofu dhidi ya Albino na kuhakikisha wanalindwa ili haki zao za msingi kama vile elimu ziweze kuzingatiwa.
0 comments

Idadi ya watu duniani wanaokosa mlo kwa siku yapungua: FAO

Idadi ya watu duniani wanaokosa mlo kwa siku yapungua: FAO


Idadi ya wanolala njaa yapungua:FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema idadi ya watu wanaoshinda njaa kutwa duniani imepungua lakini bado juhudi zahitajika ili kutokomeza njaa. FAO imesema hata hivyo harakati za kuimarisha lishe bora hazitafanikiwa iwapo hakuna mifumo bora ya uhakika wa chakula na hata ya kupata mlo bora. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
(Ripoti ya Assumpta)
Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kila siku imepungua kutoka Milioni 870 mwaka 2012 hadi Milioni 840 mwaka huu, amesema Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jose Graziano Da Silva kwenye kilele cha siku ya chakula duniani huko Roma. Amesema kupungua idadi hiyo kunaonyesha matumaini kuwa mifumo sahihi ya uzalishaji, uhifadhi na usambazaji chakula inafanya kazi. Amesema nchi 62 zinazoendelea kati ya 128 zinazofuatiliwa na FAO zimefikia lengo la Milenia la kupunguza njaa, lakini bado kuna kazi kubwa ili kila mtu awe na uhakika wa mlo bora na wa uhakika…
(Sauti ya Graziano)
Naye Mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Etharin Cousin ametaka uwekezaji zaidi kwenye lishe kama njia ya kubadilisha kiuchumi maisha ya jamii zote duniani.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni ajabu zaidi ya Watu Milioni 840 duniani wanashinda na njaa ilhali kuna rasilimali za kutosha duniani. Amesema jibu pekee ni kuhakikisha kila mtu anapata mlo sahihi kwa kuhakikisha kuna mifumo, sera na uwekezaji bora unaoweka fursa ya mazingira bora na watu kuzalisha mazao bora na salama na kufikia watu kwa uhakika.
0 comments

Dunia yaadhimisha siku ya chakula

Dunia yaadhimisha siku ya chakula

  Jana16.10.2013 ni siku ya chakula duniani. Na kwa ajili hiyo shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limetoa mwito wa kuweka mkazo katika kuhakisha upatikanaji wa mahitaji ya chakula duniani kote.
Wafanyakazi wakipakua chakula kutoka kwenya gari nchini Sudan Kusini.
Wafanyakazi wakipakua chakula kutoka kwenya gari nchini Sudan Kusini.
Kila mwaka katika siku ya leo tarehe 16 mwezi wa oktoba Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Umoja wa Mataifa FAO linaidhmisha kuwa siku ya chakula duniani. Ni siku ambapo shirika hilo liliundwa mnamo mwaka wa 1945 baada ya kumalizika vita kuu vya pili. Lengo la maadhimisho ya leo ni kuweka mkazo juu ya kuimarisha juhudi za kupambana na adui njaa duniani.


Watoto wa Kisomali wakipatiwa chakula mjini Mogadishu. Somalia ni moja ya mataifa yanayokabiliwa na uhaba wa chakula duniani.
 
 
Watoto wa Kisomali wakipatiwa chakula mjini Mogadishu. Somalia ni moja ya mataifa yanayokabiliwa na uhaba wa chakula duniani.
 
Ni siku ya kuhamasisha ufahamu wa masuala ya njaa na uhaba wa chakula duniani, yanayomgusa kila mwanadamu . Kauli mbiu ya mwaka huu inasema "kudumisha mfumo endelevu wa upatikanaji wa chakula na lishe." Akitoa ujumbe katika kuiadhimisha siku hii ya leo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO Jose Graziano da Silva amesema binadamu wenye afya wanategemea uhakika wa kupatikana kwa chakula.

Baadhi walia njaa, wengine huvimbiwa

Naye afisa mwandamizi wa shirika la FAO Alexander Meyback amesisitiza juu ya umuhimu wa siku hii. "Leo ni siku ya kuhamisha ufahamu juu ya baa la njaa, uhaba wa chakula na ni hatua gani tunaweza kuzichukua .Wapo watu milioni mia nane na 42 wanaosibika na njaa duniani. Pia wapo watu bilioni mbili wasiopata chakula cha kutosha duniani achilia mbali wale wasiopata lishe bora."

Afisa huyo wa sera, Mayback amekumbusha kwamba wakati watu wengi hawana chakula cha kutosha duniani, wapo watu wengine wenye maradhi ya kuvimbiwa kutokana na shibe ya kupita kiasi. Bwana Meybeck ameeleza kuwa hali hiyo inaweza kusababisha kuongezeka kwa matumizi ya raslimali. Ongezeko hilo litayaathiri mazingira na kusababisha matumizi makubwa ya maji, ardhi na raslimali nyingine.

Chakula kikiwa kimetupwa mjini New York. Utafiti moja nchini Uingereza ulionyesha kuwa nusu ya chakula kinachozalishwa duniani huishia katika mapipa ya taka.  
 
Chakula kikiwa kimetupwa mjini New York. Utafiti moja nchini Uingereza ulionyesha kuwa nusu ya chakula kinachozalishwa duniani huishia katika mapipa ya taka.
 
Malengo yanahitajika

Katika madhimisho ya siku ya leo duniani kote, Shirika la FAO linatoa mwito wa kwa kila mtu wa kufikiria juu ya kutafuta njia na kuweka malengo ya kipaumbele katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula duniani. Shirika la FAO pia limetahadharisha juu ya ugeu geu wa bei za vyakula duniani.

Shirika la FAO limesema hali hiyo huenda ikaendelea kuisakama dunia kwa muda mrefu. Murugenzi mkuu wa shirika la FAO Jose Graziano da Silva amesema bei zitaendelea kugeuka geuka. Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema ughali umepungua kulinganisha na hali ya mwaka uliopita kutokana na ongezeko la uzalishaji wa nafaka.

Mkurugenzi huyo amezitaka nchi wanachama waitumie fursa ili kujitayarisha na hivyo kuweza kuikabili hali ya ugeu ugeu wa bei za vyakula kwenye soko la dunia.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger