Featured Post Today
print this page
Latest Post

WARSHA KUHUSU KUENEA KWA HALI YA JANGWA NA UKAME NA MAENDELEO ENDELEVU YA ARDHI YAANZA MJINI BAGAMOYO

WARSHA KUHUSU KUENEA KWA HALI YA JANGWA NA UKAME NA MAENDELEO ENDELEVU YA ARDHI YAANZA MJINI BAGAMOYO

Sehemu ya wajumbe wa warsha ya  mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo wakiskliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete
 Kaimu Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya Makamu wa Rais bibi
Magdalena Mtenga akimkaribisha mgeni Rasmi Injinia Angelina
Madete aweze kufungua warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa
hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo
 Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina
Madete akifungua warsha ya siku mbili kwa wafanyakazi kutoka
sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu
kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya
ardhi mjini Bagamoyo leo
Wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya
jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi
katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete amesema ukame umekuwa tatizo kubwa linaloleta athari katika swala zima la mazingira katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
Inakadiriwa kuwa aslimia 73 ya nchi za Afrika zimepunguza uwezo wa kuzalisha chakula kunakotokana na ukame jambo linalosababisha kuwepo upungufu mkubwa wa chakula. 
Madete ameyasema hayo leo mjini Bagamoyo  wakati wa  ufunguzi wa warsha ya  siku mbili kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo endelevu ya ardhi.
Alitaja baadhi ya mikoa iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga, Mara, Iringa, Manyara na Arusha.
Warsha hiyo imewashirikisha wafanyakazi kutoka wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa lengo  kuepuka  janga la ukame.
Akiongea katika warsha hiyo Injinia Madete alisema  kuwa ukame unaleta umaskini na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda sehemu zingine zisizo na ukame.
Aliendelea kusema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala hilo la ukame amabapo mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupamabana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame (United Nations Convetion to Combat Dessertification UNCCD)
Serikali inatekeleza mkataba huo kupitia Programu ya Taifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya Jangwa na ukame (National Action Programme to Combat Dessertification-NAP) ambapo kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za Ukame.

Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa Mataifa (UNDP)

Picha na Habari na Monica Sapanjo
Afisa Habari
Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments

Mtu Mrefu Kuliko Wote Duniani Sultan KosenAfunga Ndoa Uturuki.

Mtu Mrefu Kuliko Wote Duniani Sultan KosenAfunga Ndoa Uturuki.

Hakika hili ni jambo la heri na kuvutia kwa namna moja ama nyingine, ama sivyo Sultan Kosen angeweza kuwa na wakati mgumu kuweza kumpata mwanamke ambaye wangeweza endana ili waweze kuishi naye maishani.

Mtu huyu mrefu kuliko wote duniani ana urefu wa mita 2.51 zaidi ambazo ni sawa na futi mbili na inchi saba ambazo amemzidi mwanamke aliyemuoa aitwaye Merve Dibo.

Jamaa huyu ambaye ni mkulima wa nchini Uturuki alifunga ndoa iliyofuatiwa na sherehe kubwa mwishoni mwa juma, hakika ni furaha sana kwake mara baada ya kupoteza tumaini kwa muda mrefu kama angeweza kuja kumpata atakayempenda.


0 comments

Avunja Rekodi ya Kuwa Mwanamke Mwenye Matiti Makubwa Asilia Duniani.Tazama Picha zake 4 Hapa!!

Avunja Rekodi ya Kuwa Mwanamke Mwenye Matiti Makubwa Asilia Duniani.Tazama Picha zake 4 Hapa!!

Annie Hawkins-Turner ndio jina lake halisi, kwa sasa ana umri wa miaka 53 toka Atlanta, Georgia ambaye anavaa bra ya saizi 102ZZZ, hakika naye ni mashuhuri kwa maana dunia inamfahamu kutokana na rekodi yake ya kuingia kwenye Kitabu cha Guinness World Record kwa kuwa ni mwanamke mwenye matiti makubwa zaidi kuwahi tokea duniani.

Matiti yake yameweza kumsaidia kumpa nafasi ya kuingia kwenye tasnia ya uigizaji na filamu kutokana na umbile la kipekee alilonalo, kituambacho kinamfanya kuwa ni modo wa kipekee. Mpaka sasa ameshashiriki kwenye video anazojiongoza yeye binafsi katika kuzitengeneza zinazoweza kufika ya zaidi ya 250.

Cheki picha zaidi hapo chini....


0 comments

MWANAMKE ALIYEPIGWA RISASI ARUSHA AMPA WAKATI MGUMU RPC WA ARUSHA

MWANAMKE ALIYEPIGWA RISASI ARUSHA AMPA WAKATI MGUMU RPC WA ARUSHA

Toka jana jioni wakazi wa jiji la Arusha wameendelea kuwa katika taharuki na minong'ono hapa na pale kutokana na tukio la kupigwa risasi binti mmoja aitwaye Violeth Mathias katika ofisi za TRA Arusha.


Mwanadada huyu aliyeonesha jeuri ambayo haikutegemea si tu Arusha bali katika Taifa hili hasa lile la kwenda na kuchukua Bastola na kutaka kummaliza askari aliyekuwa akitimiza wajibu wake katika Bank ya CRDB. Kitendo hiki kimelfanya wakazi wa jiji hili kuwa na Maswali mengi kuliko majibu. Hasa juu ya anakota jeuri ama kiburi mwanadada huyu.


Viola alikwenda CRDB kuchukua pesa na kilichotokea yeye alipaki gari eneo lisiloruhusiwa kwa mazingira yale ya Bank. Hivyo askari Polisi alimfuata na kumwelekeza kwamba haruhusiwi kupaki gari eneo hilo ila yeye (Mwanadada) huyu hakutaka kusikiliza alichokuwa akiambiwa. Akashuka na kwenda bank ndani.


Hata hivyo Polisi alimfuata ndani ila cha kushanga mwanamke huyu akagoma tena. Ndipo Polisi kwa ajili ya usalama alirudi nje na kutoa upepo matairi yote ya gari kwa tahadhari. Cha kustaajabisha ni pale binti huyo aliporudi na kukuta hali hiyo alipoulizwa alijibiwa polisi ndiye aliyefanya hivyo. Alichofanya alienda kwenye gari lake na kutoka na bastola ati akitaka kumlenga yule askari polisi ndipo yule askari alipoaamu kujihami na kumshug begani.


Baada ya watu kuchunguza wakajua kuwa kiburi hicho anakitia kwa RC wa Arusha Bwa. Magesa Mulongo kwa kuwa anajipumzisha kwake. Wakazi wengi wa hapa wameshangazwa sana namna RC anavyozidi kuchafua nafasi yake hiyo na hata yule aliyempatia.


Cha kusikitisha zaidi ni RPC kuamua kukimbia waandishi wa habari baada ya waandishi kumfuata na kumtaka atoe maelezo juu ya hilo tukio. RPC kuona waandishi wa habari alimwamuru dereva kugeuza gari na kuondoka jambo lililopelekea waandishi wa habari kuamini kuwa RPC atakuwa amepokea maeleekezo toka kwa RC. 


RPC alipopigiwa simu aliishia kusema anaelekea Hospitali kwa kuwa Sukari yake haiko sawa hili limepelekea kuaminika kuwa Mulongo anawaweka viongozi wenzie katika wakati mgumu kutokana na tabia zake hizi.

-Jamii Forums
0 comments

PICHA ZINATISHA: ANAYEDAIWA KINARA WIZI WA ‘POWER WINDOW’ AKAMATWA,APEWA KICHAPO NUSURA AFE

PICHA ZINATISHA: ANAYEDAIWA KINARA WIZI WA ‘POWER WINDOW’ AKAMATWA,APEWA KICHAPO NUSURA AFE


MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne iliyopita alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota Harrier, Ijumaa limeinyaka. 
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema Mbaga na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda mtandao wa kuiba power window kwenye magari walifika eneo la tukio wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Noah.
Mbaga akisulubiwa na wananchi.
“Lengo lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya Marie Stop lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema shuhuda huyo.
Gari aina ya Toyota Harrier walilotaka kuiba power window Mbaga na wenzake.
Shuhuda huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari hilo na kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
Wananchi wakiwa wameandaa tairi tayari kumtia kiberiti Mbaga kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kumnusuru.
Inadaiwa watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari walilofika nalo lakini mlinzi aliwahi kumng’ang’ania Mbaga na kuanguka naye chini.
Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.
Kipondo kikiwa kimepamba moto kwa Mbaga.
Wakati akipewa kichapo hicho, Mbaga alijitetea kwamba hakuwa mwizi bali ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.


Mbaga akiwa hoi baada ya kichapo.
Mbali na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa Fausani na kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe Mlimani City.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila nawafahamu,” alisema Mbaga.

Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio. 

Polisi wakimbeba Mbaga kumpeleka kwenye difenda.
Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.

Mbaga akiingizwa kwenye difenda. 

Safari ya kuelekea Mwananyamala ikaanza.
0 comments

BABU SEYA, PAPII KOCHA VICHEKO VYAANZA

BABU SEYA, PAPII KOCHA VICHEKO VYAANZA

Stori: Richard Bukos na Denis Mtima
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ pamoja na ndugu zao, Jumatano iliyopita walitoka kwa vicheko katika Mahakama ya Rufaa Tanzania baada ya kuridhishwa na utetezi uliotolewa na wakili wao, Mabere Marando, anayepinga hukumu ya kifungo cha maisha jela, waliyopewa wanamuziki hao.

Mbele ya majaji watatu wa Mahakama hiyo, Marando alikabiliana na timu ya mawakili watano waandamizi wa serikali ambao ni Jackson Brashi, Angaza Mwaipopo, Imaculate Banzi, Joseph Pande na Apimark Mabruk.

Miongoni mwa hoja ambazo Marando alionekana kuwabana mawakili wa serikali ni jinsi Jamhuri ilivyowatia hatiani wateja wake kwa kutumia ushahidi uliotolewa na watoto katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar, akisema zipo taratibu za kuchukua katika ushahidi kwa mtoto ikiwemo kurekodiwa, jambo ambalo halikufanyika.

Marando alizidi kuweka wazi kuwa katika ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ulionesha nyumba iliyodaiwa kufanyiwa uhalifu huo ilikuwa na mlango wa siri uliotumiwa na watoto hao kupenya hadi ndani pasipo kuonekana jambo ambalo baadaye lilidhihirika si kweli kwani nyumba hiyo haikuwa na mlango mwingine zaidi ya wa uani na barazani.

Hata hivyo, jopo la mawakili wa Jamhuri licha ya kukumbana na wakati mgumu kutoka kwa wakili Marando, liliendelea kusisitiza kuwa hukumu iliyotolewa dhidi ya washitakiwa hao ilikuwa sahihi.

Baada ya mawakili hao kusisitiza hivyo Marando alipewa nafasi nyingine ya kutoa utetezi wake, ambapo aliendelea kufafanua makosa mbalimbali yaliyofanyika kuwahukumu wateja wake kwa kutaja vifungu vya sheria ambavyo vilionekana kama kuwasafishia njia wateja wake hao hali iliyozua tabasamu na vicheko mahakamani hapo.

Baada ya kupitia marejeo ya kesi hiyo kwa pande hizo mbili, jopo la majaji akiwemo, Salum Masatti liliahirisha kesi hiyo na kusema litapanga siku ya hukumu huku wafungwa hao wakirejeshwa gerezani wakiwa na vicheko vya furaha huku ndugu na jamaa nao wakikumbatiana kwa shangwe.

0 comments

Serikali yatangaza viwango vipya vya ufaulu elimu ya sekondari

Serikali yatangaza viwango vipya vya ufaulu elimu ya sekondari

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu  ya mwanafunzi  na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.
 Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani).
Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani). Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO).
0 comments

WANANCHI WENYE HASIRA WAUCHOMA MOTO MSIKITI WA ANSAR SUNNI KILINDI.

WANANCHI WENYE HASIRA WAUCHOMA MOTO MSIKITI WA ANSAR SUNNI KILINDI.

PASKAL MBUNGA,KILINDI
WANANCHI wenye hasira na ambao bado hawajafamika wameuchoma moto na kuubomoa kabisa msikiti unaotumiwa na  waumini wa dhehebu la dini ya kiislamu la Ansar Sunni wanaoaminika kuwa chanzo cha  chokochoko  na machafuko yaliyosababisha  mauaji ya watu hivi karibuni katika kijiji cha Lulago, Kata ya Lwande wilayani Kilindi.
 
Sambamba na ubomoaji huo wa msikiti, lakini pia wamezichoma moto nyumba 16 zinazokaliwa na wafuasi hao wa Ansar baada ya wao kukimbilia misituni wakikwepa kukamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na kuhusika kwao na mauaji ya mwanamgambo kijijini hapo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari i waliotembelea kijiji hicho mwanzoni mwa juma hili, Mwenyekiti wa kijiji cha Lulago, Mohamed Waziri Mwariko (48), alisema kwamba baada ya kuzusha furugu na machafuko kijijini hapo  juma lililopita ambapo walimwua askari mgambo kwa kumkata mapanga, , walikimbia na kwenda kujificha misituni ambapo mpaka sasa hawajonekana.
 
Mwariko alisema wafuasi hao ambao wanajinadi kuwa ni waislamu safi na kuwaita waislamu wengine ni makafir, walianza kukinzana na uongozi wa serikali ya kijiji kwa kuwashawishi watu wasiiti serikali iliyoko madarakani wakidai kuwa ni ya kikafir na hivyo kukataza wasilipie ushuru kwa kijiji.
 
Akisimulia chanzo cha vurugu kilichopelekea mauaji hayo, Mwariko alisema kuwa tarehe 23 Oktoba mwaka huu, mfanya biashara Haji Mtana alinunua iliki gunia mbili na kulipia ushuru wa  kijiji wa shilingi 20,000 ambapo walitokea wafuasi hao na kumtaka mnunuzi huo asilipie kwa madai kuwa serikali ya kijiji na serikali kuu zote ni za kikafiri.
 
Uongozi wa kijiji ulipowaita kuja kutoa maelezo ya matamshi yao, walikataa wito na ndipo uongozi wa kijiji uliwatumia mgambo ambaye walimwua  kwa kumkata mapanga na kisha kuanza kutamba kijijini hapo kwa kufyatua ovyo risasi.
 
Mwenyekiti huyo alieleza kwamba pamoja na uongozi wa kijiji kutoa taarifa polisi, lakini wananchi waliingiwa na hofu baada ya kuchinjwa mgambo huyo kwani wananchi walizihama nyumba zao na kukimbilia porini kujificha
 
”:Kwa kusaidiana na majeshi ya ulinzi na usalama, wananchi hao waliweza kuwakamata wafuasi 16 pamoja na silaha walizotumia zikiwemo bunduki 4 bastola 2, mapanga 18 na visu 12”, alisema Mwariko na kuongeza kwamba viongozi wakuu wa kikundi hicho walikimbilia misituni  na hawapatikana hadi sasa..    
 
Mwenyekiti huyo wa kijiji alisema kutokana na hasira walizokuwa nazo wanakijiji juu ya watu hao ambao walihamia kijijini hapo mwaka 2009 wakitokea Dar es Salaam hawataki warudi tena katika maeneo yao waliyoyahama.
 
Idadi kubwa ya wakazi wa Kijiji cha Lulago chenye watu 4063 ni Waislamu ambao ni karibu 99.5% ya wakazi wote. ,
0 comments

CCM WILAYA YA TANGA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA KIJIJI CHA PANDE B JUMAMOSI.


CCM WILAYA YA TANGA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA KIJIJI CHA PANDE B JUMAMOSI.
 
Na Oscar Assenga, Tanga.
CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tanga kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Pande B kata ya Kiomoni jijiniTanga lengo likiwa kuwashukuru wananchi kwa kukiwezesha chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi serikali ya kijiji hicho uliofanyika hivi karibuni.
 
Katibu wa Siasa, Uenezi wa Chama hicho wilaya ya Tanga, Lupakisyo Kapange alisema mikutano hiyo itafanyika Jumamosi wiki hii eneo la Lwande na baadae jioni watafanyia kwenye kitongoji cha Kivuleni katika kata hiyo ambapo viongozi mbalimbali watapata nafasi ya kuzungumza na wananchi hao.
 
Kapange alisema ushindi wa chama hicho unaonyesha jinsi gani wananchi walivyokuwa na imani kwao kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati na barabara.
 
Katika uchaguzi huo wa serikali ya Kijiji cha Pande B wapiga kura waliokuwa wamejiandikisha walikuwa ni 686 waliopiga kura ni 674,zilizoharibika ni 97 hivyo kura halali kuwa ni 577 ambapo kati ya hizo,Chama cha Mapinduzi (CCM)kilipata kura 418,Chama cha Wananchi (CUF) kilipata kura 128 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )walipata kuwa 31.
 
Kwa upande wa wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Pande B Chama cha Mapinduzi kilifanikiwa kupata wajumbe 11 ambao ni Ally Jabiri,Ally Mohamed, Kauli Makame,Yakwesa Samweli,Salim Kibwana,Salim Bakari, Ally Mchaga,Said Abdallah,Mtoa Bakari,Hussein Salim na Said Kilo.
 
Aidha alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani hapa ili kuhakikisha wanaharakisha kasi ya maendeleo yao pamoja na kueleza sera za chama hicho.
 
Hata hivyo Kapange aliwashukuru wananchi wote wa wilaya ya Tanga kwa kuungana na mkoa katika shughuli mbalimbali za kiserikali na kichama ikiwemo mapokezi makubwa ya viongozi wa kitaifa .
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger