Featured Post Today
print this page
Latest Post

STARS YAWASILI SALAMA BANJUL KUIVAA GAMBIA KESHO!!


STARS YAWASILI SALAMA BANJUL KUIVAA GAMBIA KESHO!!

211447612Pichani juu ni wachezaji wa Taifa stars walipovaana na Gambia jijini Dar es salaam mechi ya kwanza ambapo Stars ilishinda mabao 2-1
Na Boniface Wambura, Banjul
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama hapa Banjul, Gambia tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji itakayochezwa kesho (Septemba 7 mwaka huu).
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili hapa jana (Septemba 5 mwaka huu) saa 11 jioni ikitokea Dakar, Senegal ambapo ilichelewa kuunganisha ndege, hivyo kuamua kutumia usafiri wa barabara kwa vile ni karibu na baadaye kupanda kivuko kuingia Banjul badala ya kulala na kuchukua ndege nyingine siku inayofuata. 
Wachezaji wako katika hali nzuri na leo jioni wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Independence ulioko Bakau ambao utatumika kwa mechi ya kesho. Timu imefikia hoteli ya Seaview iliyoko kandokando ya Bahari ya Atlantic.
Mechi hiyo itaanza saa 10.30 jioni kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 1.30 usiku, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda Munyemana Hudu. Waamuzi wasaidizi ni Theogene Ndagijimana, Honore Simba na Issa Kagabo. Kamishna ni Andy Quamie kutoka Liberia.
Washabiki na vyombo vya habari vya hapa wanaizungumzia mechi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa pande zote, huku Gambia ikiwa imeita wachezaji tisa wanaocheza barani Ulaya na Marekani. Gambia ambayo imepata uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Gambia (GFA) imepania kuhakikisha haimalizi mechi za mchujo ikiwa na pointi moja tu.
Kwa upande wa Tanzania, Kocha Kim Poulsen amesema nia ni kuona Stars yenye pointi sita inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ambayo tayari imechukua tiketi pekee ya kucheza raundi ya mwisho kutoka kundi hili la C.
“Mechi hii ni muhimu kwetu kwa vile tunataka matokeo mazuri ugenini. Lakini kikubwa ni kuwa matokeo mazuri si tu yatatuweka katika nafasi ya kuwa wa pili, lakini vilevile yatatusaidia kuongeza pointi kwenye viwango vya ubora vya FIFA, na kikubwa zaidi hii ni sehemu ya maandalizi ya sisi kucheza Fainali za Afrika za 2015,” amesema Kim.
Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha.
0 comments

BAVARIA WAFADHILI MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGEREZA KWA SHULE ZA SEKONDARI MKOA WA TANGA .

BAVARIA WAFADHILI MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGEREZA KWA SHULE ZA SEKONDARI MKOA WA TANGA .

WANANFUNZI WAKIFUATILIA MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGEREZA AMBAYO YALIANZA JANA KATIKA HOTEL YA REGAL NAIVERA YAKIFADHILIWA NA KINYWAJI KISICHO NA KILEVI CHA  BAVARIA HOLLAND


BAADHI YA WALIMU KUTOKA SHULE MBALIMBALI MKOA WA TANGA WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI POPATLALY NA ST.CHRISTINA WAKIWA TAYARI KWA AJILI YA MASHINDANO HAYO.

MEZA YA MAJAJI WA MASHINDANO HAYO WAKIWA KWENYE MICHAKATI YAO KUHAKIKISHA KILA KITU KINAKWENDA SAWA NA BINGWA ANAPATIKANA BILA MALALAMIKIO.


OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI  AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO KULIA NA KUSHOTO KWAKE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,MUSTAPHA SELLEBOSS WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO.

HAPA WAKITETE JAMBO.





OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI  AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AMBAO HAWAPO PICHANI KUHUSU MASHINDANO HAYO.

PICHA ZOTE NA PASKAL MBUNGA,TANGA.
0 comments

CHEKA ATINGA BUNGENI NA UBINGWA WA WBF

MOHAMED BAWAZIRI AKUTANA NA WAZIRI MKUU PINDA KUHAMASISHA NGUMI NCHINI

Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na  promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt,Fenela Mukangala wa pili kushoto akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdala pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na 
Catherini Matili  Picha www.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na  promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


PROFESA MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI PAMOJA NA PROMOTA MOHAMEDI BAWAZIRI


Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI
Mbunge Wa Same Mashariki, Anne Kilango  katikati akiwa  na bingwa wa unia wa wbf fransic Cheka kulia kwake na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia na wadau wengine wa mchezo wa masumbwi nchini walipotembelea Bunge la Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakiongozwa na Mohamed Bawazir Katikati wakiwa katika picha ya pamoja kabla awajaingia ndani ya bunge kusikiliza bunge la Tanzani Super d Wa nne kulia nae akiungana nao pamoja
Bondia fransic Cheka akiwa na wabunge mbalimbali pamoja na mwanaseria mkuu wa Selikari le alipotembelea bungeni

Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt,Fenela Mukangala wa pili kushoto akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdala pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na 
Catherini Matili  Picha www.superdboxingcoach.blogspot.com

Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa na mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Fransic Cheka wakati walipo tembelea bungeni Dodoma kwa ajili ya kutambua mchango wao na kuwapongeza picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
0 comments

BAADHI YA MAWAZIRI NA MAPOLISI WATAJWA KUWA NDIO WATEJA WA MACHANGUDOA

BAADHI YA MAWAZIRI NA MAPOLISI WATAJWA KUWA NDIO WATEJA WA MACHANGUDOA

BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa.

Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam.

Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani.

‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.
  
Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao.

Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili yao, wataacha kujiuza.
0 comments

JINSI NILIVYOTESWA NA UJIKO WA KUWAFIKISHA WANAWAKE KILELENI

JINSI NILIVYOTESWA NA UJIKO WA KUWAFIKISHA WANAWAKE KILELENI

Jamani, leo nimeona nielezee jinsi nilivyo geuzwa mtumwa na tamaa zangu mwenyewe.
Baada ya kupitia jeshi la kujenga BALEHE na kufuzu, nikaanza kujihusisha na wanawake.
Mwanzoni nilikuwa najua kuwa wanawake huwa hawasikii raha kabisa wakati wa majamboz na ndio maana huwa wanazingua sana hadi uweze kuwachapa nao.
Baassss, mimi nilikuwa nikikamata mizigo, najipigia zangu kamoja ka kichovu mno kisha nalala kama mdogo wa maiti.
Basi bhana kwenye kuhanja hanja kwangu nikaibua ka hausi geli ka jirani, kalikuwa kajanja sana, kwanza kabla sijaenda kukagonga nao, kakaanza kunipiga mikwara kibao, mi mwanaume wa bao moja simtaki, tena asiponifikisha kileleni anisahau kabisa.
Binti alikuwa ni mzuri, mwemba, mrefu, toto la Kiburushi, kwa jinsi nilivyokuwa na miusongo naye, akili yangu ikabadilika kabisa, namna ya kumfanya mwanamke afurahie majamboz.
Hapo nikapata jawabu kwa nini watu huwa wananyonya na kuzilamba Tukuyu bila kuona kinyaa wala kichefuchefu.

Baba Mwanaasha anasema akili za kuambiwa changanya na za kwako, kudadadeki mwana wane, na mimi nikajiongezea maarifa. Nikasema huyu binti lazima leo nimkomeshe, akienda kuwasimulia wenzake, awaambie kabisa kuwa Mbozi ya Bujibuji ina matawi, maana alichonitendea leo ni zaidi ya muujiza.

Mzee nikajisogeza zangu glosare ya jirani, hapo ilikuwa mida ya saa mbili asubuhi, nikaagiza supu na bapa la konyagi.
Nikagonga supu na konyagi huku niki buy time matajiri wa kimwana waende dukani kwani (walikuwa na duka mjini, wakienda asubuhi hawarudi hadi jioni)
Mida ya saa tatu, binti akaja home, akanikuta jicho limewakaaa, halafu mjomba Bujibuji kasimama kama mwavuli uliofungwa kwenye kijimfuko wake.
Alipoingia tu, nilimnyanyua juu, nimkamkandamiza kwa madenda moto moto, ulimi nikaugeuza dekio.
Unaambiwa ulimi ulichezeshwa midfielder ya kufa mtu, kuanzia unyayoni hadi utosini, huku ukizichambua nywele za kiarabu, moja baada ya nyingine.
Kudadadeki, nilimshughulisha yule mwanamke mpaka, akaanza kutoa mlio kama wa beberu huku akitetemeka.
Baada ya hapo sisimulii kilichotokea.
Kesho yake asubuhi, nikiwa naangalia BBC news binti akajileta mwenyewe, mzimamzima, huku akinisifia kuwa hajawahi kuona mautundu na maujuzi kama ya kwangu, mzee nikakandamiza tenda, tena kwa fujo za kufa mtu. 
Nikaomba kupelekwa topeni, nikakataliwa, baada ya kusaundisha sana, nikakubaliwa kwa masharti kwamba nipige 0713 kwa na niongee kwa sekunde chache, kwa kuwa alikuwa hajawahi.
Mzee nikatafuta mafuta ya mgando, nikasindilia, mzee, unaambiwa Bujibuji haina mabega, kikiingia kichwa ujue ndio mwili mzima hivyo, basi hiyo ikawa ni second chapter.

Basi, kwa maraha yote hayo mzee unaweza shangaa mbona heading na body hamna uhusiano, madhara niliyoyapata ni kwamba nikawa siwezi ku ku do bila kupiga konyagi za kufa mtu, nikawa mlevi kupindukia, nikawa mtumwa wa tigo na kwa kweli nikawa mdogo wa shetani. Sasa nimebadilika, namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa Mamndenyi ambaye amekuwa ni mvumilivu sana kwangu, na amekuwa akiniombea ni kiumbe bora zaidi.
0 comments

Picha tatu za Rais Kikwete alipokutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda huko Uganda.


Picha tatu za Rais Kikwete alipokutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda huko Uganda.
Rais Jakaya Kikwete leo amefanya mazungumzo na Rais Paul 
Kagame wa Rwanda katika mkutano wa saba wa kimataifa wa 

nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda.
 Haijafahamika mara moja walichozungumza, hizi ni picha za mkutano wao. 

 9676681299_b3707d20a5_c
  9679917620_3f83a214d0_b
 Marais hao wamekutana wakati ambapo uhusiano kati 
ya nchi hizo mbili unaendelea kuzorota.
0 comments

COASTAL UNION KUUMANA NA BANDARI JUMAPILI MKWAKWANI

COASTAL UNION KUUMANA NA BANDARI JUMAPILI MKWAKWANI

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga ambaye imesheheni nyota wake Juma Said Nyosso na Haruna Moshi ‘Boban’, itashuka kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili kumenyana na Bandari ya Mombasa, Kenya katika mchezo wa kirafiki kudumisha ujirani mwema baina ya miji hiyo ya Pwani.

Akizngumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Mratibu wa Mechi hiyo George Wakuganda alisema maandaliiz yanaendelea vizuri ambapo timu zote hizo zitatumia mechi hiyo kwa ajili ya maandalizi yao mechi zao zinazowakabili.

Kama ilivyo Coastal, ni moja ya timu tishio katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, kadhalika na Bandari inasumbua katika Ligi Kuu ya Kenya msimu huu ikijivunia baadhi ya wachezaji wa Tanzania kama David Naftali, Meshack Abel, Thomas Maurice na Mohamed Banka.

Ligi mbalimbali Afrika zimesimama wikiendi hii kupisha mechi za kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil na baadhi ya klabu zinatumia fursa hiyo kwa mechi za kirafiki.

Kwa Coastal ni mchezo unaokuja baada ya kucheza mechi za Ligi Kuu ugenini, ikishinda 2-0 dhidi ya JKT Oljoro mjini Arusha na kutoa sare ya 1-1 na Yanga Dar es Salaam, tena ikisawazisha kwa penalti dakika ya 90.

Utakuwa mchezo mwafaka katika wakati mwafaka kwa kocha Hemed Morocco ili kuangalia mapungufu katika kikosi chake kabla ya Ligi Kuu kurejea wiki ijayo. Coastal msimu huu imesajili kikosi tishio haswa kikiundwa na mseto wa wachezaji kutoka Kenya na Uganda.

Kikosi cha Coastal 2013 kimesheheni wachezaji mahiri akiwemo Seleman Kassim Seleman, Philip Mugenzi Metusela, Jerry Salim Santo, Razak Juma Khalfan, Othman Omar Tamimu, Abdulla Othman Ali (mpya, Huru), Mohamed Sudi Athumani, Crispine Odula Wadenya (mpya, kutoka Bandari FC ya Kenya), Marcus Rafael Ndeheli (mpya kutoka JKT Oljoro FC), HusseinIssa, Haruna Mosh(mpya kutoka Simba SC), Uhuru Seleman (mpya kutoka Azam FC), Juma Said Nyoso (mpya kutoka Simba SC) na Pius Kisambale.

Wengine ni Shaaban Hassan Kado, Mbwana Hamis Bakari, Kenneth Abeid Masumbuko (mpya kutoka Polisi Morogoro), Daniel Reuben Lyanga, Said Seleman Lubawa (mpya, kutoka JKT Oljoro FC), Abdi Hassan Banda, Mohamed Miraji Mtindi, Mansoor Alawi Mansoor, Hamadi Juma Hamisi, Behewa Sembwana Behewa, Yusuph Ibrahim Chuma, Yayo Wasajja Fred
0 comments

SAFARI YA MWISHO YA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA KIOMONI GEORGE MAYALLA.

SAFARI YA MWISHO YA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA KIOMONI GEORGE MAYALLA.


WAKAZI WA TANGA WAKIUAGA MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA KIOMONI JIJINI TANGA,GEORGE MAYALLA NYUMBANI KWAKE JANA.

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI (ALIYEVAA SHUTI NYEUSI NA KUKUNJA MIKONI)AKIWA NA WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA MSIBANI HAPO JANA.

MKUU WA MKOA WA TANGA ,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA WA KWANZA KULIA KUSHOTO KWAKE ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO ,MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA WILAYA YA TANGA,KASIMU KISAUJI,ALIYESHIKA TAMA NI MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA TANGA,COMRADE KASSIM MBUGHUNI.

JENEZA LA MAREHEMU MAYALLA LIKICHUKULIWA NA VIJANA WA GREEN GADI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAYARI KWA AJILI YA KUPELEKWA MAKABURINI,

MWILI WA MAREHEMU MAYALLA UKIWA TAYARI KWA AJILI YA KUHIFADHIWA KWENYE MAKAZI YAKE YA MILELE.

UMATI WA WAOMBOLEZAJI WALIOJITOKEZA KWENYE MAZISHI HAYO. HABARI PICHA NA PASCAL MBUNGA ,KIOMONI TANGA.
0 comments

RC GALLAWA AONGOZA MAZISHI YA DIWANI MAYALLA

RC GALLAWA AONGOZA MAZISHI YA DIWANI MAYALLA

Na Paskal Mbunga, Kiomoni-Tanga
 
MAMIA ya wakazi waTanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, leo wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiomoni, jijijini Tanga, George Mayalla aliyefariki juzi katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na maradhi ya kansa ya ubongo.


Akizungumza katika mazishi hayo, Gallawa aliwataka  viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali Mkpani hapa kujenga  mashirikiano ya dhati kati yao na wananchji ili kuleta maendeleo  ya haraka katika maeneo yao.
 

Gallawa alisema kata ya Kiomoni umesifika na kupata  maendeleo kunatokana na jitahada za marehemu Mayala  ambaye hakuchoka kuwashirikisha wananchi katika masuala ya maendeleo shirikishi.
 

Alisema enzi za uhai wake, marehemu Mayalla alitumia muda wake mwingi kutekeleza dhana ya maendeleo shirikishi ambapo alizishirikisha idara za serikali , taasisi na mashirika ya umma  na binafsi kusukuma  gurudumu la maendeleo.
 

Diwani Mayalla alichaguliwa kushika nafasi ya udiwani kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo tangu kipindi hicho amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maendeleo na hilo alilitimiza kwa vitendo.
 

Marehemu Mayalla alizaliwa   mwaka 1948 mkoani Shinyanga ambapo baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari,alichaguliwa kuingia chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1970 hadi 1973 alipomaliza na kutunukiwa shahada ya kwanza.
 

Mwaka 1974 diwani Mayalla alichaguliwa kwa masomo ya juu  katika chuo kikuu cha Nairobi ambako alihitimu digrii ya maendeleo na mipango miji.
 

Baada ya kufuzu masomo yake huko Nairobi, Kenya  Mayalla aliajiriwa mkoani Dar es Salaam mwaka 1975 kama Ofisa Mipango Miji.
 

Mwaka 1978, Mayalla alihajishiwa Mkoani Tanga ambapo aliajiariwa kuwa Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Tanga mpaka 1988 alipostaafishwa na kuwa mkulima huko Kiomoni, nje kidogo ya jiji la Tanga.
 

Katika mwaka 1994 hadi 2001, aliteuliwa kuwa mshauri wa kujitegemea wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira katika Manispaa ya Tanga.
 

Kulingana wa wasifu wa marehemu, Mayalla alipata kushika nyadhfa mbalimbali katika Halmashauri na baadaye Jiji la Tanga hadi anakutwa na mauti.
 

Marehemu George Mayalla ameacha mjane mmoja na watoto saba na wajukuu 11.  

Mashishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Tanga wakiwemo viongozi wa Chama na Serikali ambapo Meya wa Jiji la Tanga, Mstahiki Meya Omar Ghuledi alimsifia marehemu wa weledi katika utendaji kazi akisema kwamba amewahi kufanya naye kazi kwa awamu mbili.

Alisema alipata kufanya naye kazi mwaka 1984, yeye (Ghuledi) akiwa Naibu Meya wa Manispaa na marehemu akiwa Ofisa Mipango Miji.


Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga, Kassimu Mbughuni, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kassim Kisauji, Katibu wa CCM wilaya ya Tanga, Lucy Mwiru  na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa, Shekimweri na viongozi wengine mbalimbali.


Mwenyezi Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu Mayalla. Amin
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger