Featured Post Today
print this page
Latest Post

Tanga Cement yaahidi kuendelea kudhamini Kili Marathon

Tanga Cement yaahidi kuendelea kudhamini Kili Marathon

01
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Saruji Tanga (TCCL) wakishiriki mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro jana. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio hizo ikitoa maji ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji.
02
Mmoja wa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Kilomita tano za Vodacom Fun Run, Tsadia Jessie Bercuvitz (5) raia wa Uingereza akipewa sponji lenye maji kwa ajili ya kupunguza joto na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Saruji Tanga, Mtanga Noor wakati wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.
03
Waziri wa Habari  Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo ,Dkt Fenella Mukangara akimpa cheti Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Leslie Massawe (wa pili kulia)  kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yaliyomalizika juzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Kushoto kwa Waziri Mukangara ni Waziri wa Mifugo, Dk Titus Kamani.
 
04
Wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga, Changwa Mjella (kulia) na Mtanga Noor (katikati) wakimpa maji mmoja wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.
05
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart (kulia) akimpa maji mmoija wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro juzi. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio hizo ikitoa maji ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji . Wengine ni maofisa wa kampuni hiyo.
0 comments

JK AKAGUA MADARAJA YA KIJESHI

JK AKAGUA MADARAJA YA KIJESHI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua madaraja ya kijeshi yakiwemo yale ya kuelea juu ya maji wakati alipokagua zana za kijeshi jana, Jumatatu, Machi 2, mwaka huu, 2014.
CHANZO:MROKI MROKI
0 comments

WAHUSIKA... MNAIONA HALI HII?

WAHUSIKA... MNAIONA HALI HII?

taka_1_f30be.jpg
Pichani ni pipa la taka taka lililojaa uchafu karibu na mtaa wa chuo kikuu huria kilichopo katika manispaa ya Iringa, pipa hilo lipo karibu na makazi ya watu hali ambayo inaweza kupelekea mlipuko mkubwa wa magonjwa na hatimaye kuathiri afya za watu.
taka_2_3b2b9.jpg
Taka taka zilizomwagwika chini baada ya kukosekanika kwa nafasi ya kuzihifadhi katika pipa hilo zikiwa karibu na barabara itumiwayo na wakazi wa eneo hilo.
taka_3_ce954.jpg
Pichani ni pipa hilo lililojaa uchafu ambao unatapakaa mpaka kwenye misingi ya nyumba za wakazi wa eneo hilo, hali hii ni ya hatari kiafya hasa kwa wakazi wa eneo hilo pia wapitaji.
taka_4_1a2de.jpg
jitihada za kumpata bwana afya wa manispaa hiyo hazikuzaa matunda hivyo msemaji mkuu wa kuelezea tatizo hilo hakuweza kupatikana kwa muda muafaka lakini jitihada za kuwapata wahusika wakuu wa eneo hilo bado zinaendelea.

Na Riziki Mashaka.
0 comments

Imebainika kuwa wananchi 7 kati ya 10 wanaamini mtu tajiri hawezi kuadhibiwa kwa uhalifu au kosa alilotenda.





Na Keneth Johni Maganga, Tanga leo


Imebainika  kuwa  wananchi  7  kati  ya  10  wanaamini   mtu  tajiri   hawezi  kuadhibiwa  kwa  uhalifu  au  kosa  alilotenda.

Takwimu  hizo  zimetolewa  jijini  Dar es  salaam  na  mkuu  wa  Twaweza  Bw; Rakesh  Rajani   alipokuwa  akitoa  muhtasari  wa  utafiti  wenye  jina  la  “JE,  TUKO  SALAMA?” ambapo  wananchi   6  kati ya  10  ilibainika  kuwa  wanaamini  viongozi  wa  dini, maafisa  wa  polisi, viongozi  waandamizi  wa  serikali  na  viongozi  wa  umma  hawawezi  kuadhibiwa  kwa  makosa  au  uhalifu  wao.
Aidha  Rajani  amesema  kuwa  katika  tafiti  hiyo  wananchi  walipoulizwa  ni  kwanini  watu  hawaripoti  uhalifu  kwa  polisi, Watanzania  walionekana kulaumu  suala  la  rushwa  na  polisi  kutowahudumia  ipasavyo, ambapo  takwimu  zilionyesha  kuwa  Mwananchi  mmoja  kati  ya  watano  amesema  kuwa  atalazimika  kumlipa  polisi  kiasi  cha  pesa  ili  apatiwe  msaada,na  huku  idadi  hiyo  hiyo  ikisema  polisi  wasingewasikiliza  au kuwajali  pindi  wanapofikisha  taarifa   kituoni.
Rajani  ameendelea  kusema  kuwa  tafiti  hiyo  pia  ilichunguza  mtazamo  wa  watu  kuhusu  mfumo  wa   sheria, ambapo  kwa  hali  ya kawaida  watu  wanaporipoti  uhalifu  kwa  polisi,  ni  haki  yao  kutarajia  kuwa   polisi  watajaribu  kumkamata  mhalifu  na  kisha  kumfikisha  mahakamani  na hukumu kutolewa  kwa  mujibu  wa  sheria. Lakini  hali  ilionekana  tofauti  kwani  takwimu  zilionyesha  kuwa  Watanzania  wana  imani   ndogo   kama   hayo  yanatendeka. Huku  nusu  yao  (52%)  wakiamini   kama  mwananchi  wa  wakawaida  atafanya  kosa  au  uhalifu  ataadhibiwa  kwa  mujibu  wa  sheria,  jambo  lililoashiria  kutia  shaka, Halikadharika  wananchi  pia  walionekana  kuwa  na mtazamo  wa  kutokuwepo   kwa  usawa  mbele  ya  sheria  kulingana  na  hadhi  ya  mtu.
Hata  hivyo  takwimu  za  tafiti  hiyo  zimeonyesha  kuwa  wananchi  wanapokumbana na uhalifu, wangependa  kuripoti  polisi, ingawa  ni  nusu  tu  ya  wananchi  wote  (47%)  wanaofanya  hivyo  na  huku  idadi  ikionekana  kuwa   kubwa  zaidi  mijini  ambako  watu  6  kati  ya  10  (59%) waliripoti  kuwa  wangeweza  kuripoti  uhalifu  polisi, ikilinganishwa  na  maeneo  ya  vijijini  ambako  watu  4  kati  ya  10 (39%)  pekee  ndiyo  wangefanya  hivyo. Ingawaje   takwimu  hizo   zinaweza  kusababishwa  na  uwepo  wa  polisi  kwenye  maeneo  ya  mijini  kuliko  vijijini.


 Pamoja  na  hayo  Rajan  amesema  kuwa  takwimu  za  tafiti  hiyo  zimeonyesha  kuwa  vurugu  katika  jamii  hutokea  kwa  wingi  zaidi  kuliko  wizi, ambapo  Februari  19,2014  Dar  es salaam  karibu  nusu  (46%)  ya  watanzania  wote  wamearifu  kuwa  wameshawahi  kushuhudia  vurugu  katika  jamii  ndani  ya  kipindi  cha  miezi  sita  iliyopita, ikilinganishwa  na  idadi  ya  mtu  mmoja  kati  ya  watano  anayeripoti   kuwa  amewahi  kuibiwa  kitu  na  wezi,Na  huku  nusu  ya  watanzania  wote  wanaripoti  kuwa  hawajawahi  kuibiwa  kitu, halikadharika  watu  wanne  kati  ya  kumi  ndio  hawajawahi  kushuhudia  vurugu  au ghasia  katika  jamii.

0 comments

wanahabari nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo serikali na taasisi zisizo za serikali, wameobwa kutangaza na kuelimisha jamii mifano bora inayoonyesha jinsi mwanamke na msichana akipewa fursa na kuwezeshwa

Kuelekea  maadhimisho   ya  siku  ya  wanawake  duniani  tarehe  8 Machi,2014, wanahabari  nchini  kwa  kushirikiana  na  wadau  mbalimbali  ikiwemo  serikali  na  taasisi  zisizo  za  serikali, wameobwa  kutangaza  na  kuelimisha  jamii  mifano   bora  inayoonyesha jinsi  mwanamke na  msichana  akipewa fursa  na  kuwezeshwa



tanga-wananwake-5.gif




Na  Keneth Maganga, Tanga leo



Kuelekea  maadhimisho   ya  siku  ya  wanawake  duniani  tarehe  8 Machi,2014, wanahabari  nchini  kwa  kushirikiana  na  wadau  mbalimbali  ikiwemo  serikali  na  taasisi  zisizo  za  serikali, wameobwa  kutangaza  na  kuelimisha  jamii  mifano   bora  inayoonyesha jinsi  mwanamke na  msichana  akipewa fursa  na  kuwezeshwa  hutoa  mchango  mkubwa  sana  kwa  familia  yake  na  taifa  kwa  ujumla.

Ombi  hilo  limetolewa  na   Wizara  ya  Maendeleo ya  Jamii, Jinsia  na  Watoto  kupitia   katibu  mkuu  Anna  T.  Maembe  ambapo  amesema  kuwa  hilo  ndilo  lengo  kuu  la  kuadhimisha  siku  hiyo  na  kuongeza  kuwa  wanawake  ni  zaidi  ya  asilimia  50  ya  Watanzania  wote  kwa  hiyo  wakishirikishwa  ipasavyo  katika  shughuli  za  maendeleo  ni  dhahiri  mchango  wao  ni  mkubwa  sana.

Aidha  wizara  hiyo  imetoa  wito   kwa  mikoa  yote  kushirikisha  wananchi  na  wadau  wote  katika  kuadhimisha  siku  hiyo  kwa  namna  watakavyoona  inafaa  kwa  kuzingatia  kauli  mbiu ya  mwaka  huu  2014   isemayo   “Chochea  Mabadiliko  Kuleta  Usawa  wa  Kijinsia” Na  kuongeza  kuwa  kwa  pamoja  tunaweza  kushiriki  kujiletea  maendeleo  ya  familia  na  Taifa  kwa  ujumla.

Pamoja  na  hayo  wizara  imebainisha  kuwa  kila  mwaka  ifikapo  Machi  8  Tanzania  huungana  na  nchi  nyingine  wanachama  wa  Umoja  wa  Mataifa  kuadhimisha  siku  ya  wanawake  ambapo  madhumuni  ya  maadhimisho  hayo  ni  kutoa  fursa  ya  kupima  utekelezaji  wa  maazimio, matamko  na  mikataba  ya  kimataifa, Kikanda  na Kitaifa  inayohusu  masuala  ya  maendeleo  ya  wanawake  na  usawa  wa  jinsia .Na  huku  madhumuni  mahususi  ya  siku  hiyo  yakiwa  ni  kuhamasisha  jamii  juu  ya  umuhimu  wa  kutambua uwezo  wa  wanawake  katika   kuchangia  kuleta  maendeleo  endelevu, kuelimisha  jamii  kuhusu  jitihada  mbalimbali  zilizofanywa  na  serikali  na  wadau  katika  kuwajengea  uwezo  wa  kiuchumi  na  kijamii   ili  waweze  kushiriki  kikamilifu  kujiletea  maendeleo  yao , familia  zao  na  Taifa  kwa  ujumla.

Akifafanua  kuhusiana  na  kauli  mbiu  ya  mwaka  huu  Maembe  amesema  kuwa  ujumbe  huo  unasisitiza  kuhamasisha  na kuelimisha  jamii  kuhusu  umuhimu  wa  kuzingatia  masuala  ya  jinsia  katika  kupanga  na  kutekeleza  mipango  ya  maendeleo, sambamba  na  muelekeo  wa  maendeleo  kijamii, kitaifa  na  kimataifa,  Na  kuongeza  kuwa  unasisitiza  na  kuhimiza  kuandaa  na  kutekeleza  mipango  inayozingatia  ushirikishwaji  na  ushiriki  stahiki  wa  wanawake  na  wanaume  katika  kujiletea  maendeleo  yao.Huku  akisema  kuwa  maadhimisho  hayo  kwa  mwaka  huu  2014  yatafanyika  ngazi  ya  miko.

Sambamba  na  hayo  Maembe  amebainisha  kuwa   maadhimisho  hayo  pia  hutoa  fursa  maalum  kwa  Taifa, Mikoa, Wilaya  na  wadau  wengine  kupima  mafanikio  yaliyofikiwa  katika  kumwendeleza  mwanamke,Lakini  pia   na  kubainisha  changamoto  zinazowakwamisha  kufikia  azma  ya  ukombozi  na  maendeleo  ya  wanawake  na  kuweka  mikakati  ya  kukabiliana  na  changamoto  hizo.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger