Na Mwandishi Wetu, Handeni
BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa
kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa
kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani
Tanga.
Mkuu
wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani. DC ni miongoni mwa
viongozi wa juu serikalini wanaoliunga mkono Tamasha hili linalofanyika
kwa mara ya kwanza wilayani Handeni, huku likisubiriwa kwa hamu na wadau
wa utamaduni na maendeleo hapa nchini.
Kambi
Mbwana, Mratibu wa Tamasha la Utamaduni Handeni, maarufu kama Handeni
Kwetu 2013, pichani. Maandalizi yamezidi kupamba moto na watu wote
wanakaribishwa kujionea burudani za aina yake kwenye tukio hili la aina
yake.
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa
Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi
hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso
wa aina yake.
Alisema taratibu zote zimeshafanyika ikiwamo
kutembelea vikundi vitakavyotoa burudani, ambapo Mkuu wa wilaya ya Handeni,
Muhingo Rweyemamu, alitumia muda mwingi kuwahamasisha wadau kuhudhuria kwa
wingi katika tamasha hilo, kupitia sherehe za Uhuru zilizofanyika wilayani humo
Desemba 9 mwaka huu.
“Kila kitu kimekamilika, tukiamini kuwa wadau
wote watakaohudhuria kwenye tamasha hilo watapata fursa ya kula vyaku7la vya
asili, maana pia ni sehemu ya utamaduni wa Handeni.
“Sisi tunaamini hili ni tamasha la aina yake
ambalo litashangaza watu wengi kutokana na kuandaliwa kwa kiwango cha juu, huku
likianzia kwa maandamano katika Ofisi za Halmashauri ya mji Handeni kuanzia saa
2 asubuhi na kuelekea Uwanja wa Azimio,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana, watu hawataruhusiwa kuingia
uwanjani na vyakula wala vinywaji ili kudhibiti suala la afya za watu kwa
kupitia tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, hususan
wapenzi wa utamaduni hapa nchini.
Wadhamini
katika tamasha hilo ni gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, Phed
Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters, Saluti5.com,
Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B
SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD), Michuzi Media
Group, duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind &
Partnership, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie
Blog na Taifa Letu.com.
Posted by
Unknown
10:46 PM