MAKAMBA AZIPIGA TAFU SHULE ZA SEKONDARI BAGA NA TAMOTA
Na Raisa Saidi,Bumbuli,
Mbunge wa jimbo la
Bumbuli January Makamba amekabidhi msaada wa
shilingi milioni mbili katika shule ya
sekondari ya Baga na Tamota kwa ajili
ya ujenzi wa Maabara kwa lengo la
kuinua masomo ya sayansi.
Pamoja na msaada huo wa milioni moja moja kwa kila shule pia
ametoa msaada wa mabati mia moja kwa kila shule kwa
ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa na
nyumba za walimu katika shule hizo.
Alitoa msaada huo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye
mahafali ya kidato cha nne kwenye shule hizo.
Makamba ambae pia ni Naibu
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Tenknolojia
alisema kuwa lengo la kutoa misaada
hiyo ni kutaka kuongeza na kuinua
kiwango cha elimu katika shule
zilizopo katika jimbo hilo.
Mbunge huyo alisema kuwa msaasa huo ni sehemu ya utekelezaji
wa mpango wa serikali katika kuhakikisha kila shule ya kata inakuwa na
maabara katika kuhakikisha kiwango cha ufaulu na hususani katika masomo
ya sayansi hapa nchini kinaongezeka.
Wazazi na walimu wa Shule hizo wameeleza kufurahishwa
kwao na juhudi za Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba katika kukukuza kiwango
cha elimu na kuondokana na usemi usemao Wasambaa hawajasoma na ni watu wa
sokoni tu.
Diwani wa kata ya Milingano Hozza Mandia akiwa katika
mahafali hayo alisema kuwa juhudi za Mbunge huyo ni mfano
mzuri wa kuigwa na wanasiasa wengine
ili kuwaletea maendeleo wananchi huku akiongeza kuwa
jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono.