Featured Post Today
print this page
Latest Post

KATIBU MKUU MPYA SIXTUS MAPUNDA AKABIDHIWA OFISI YA UVCCM NA SHUHUDIA SHIGELA JIJINI DAR ES SALAAM.

KATIBU Mkuu mstaafu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa UVCCM, Sixtus Mapunda, faili wakati wa makabidh
iano ya Ofisi, waliyofanya, Makao Makuu ya UVCCM, mjini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni, Naibu Katibu Mkuu UVCCM (Bara), Mfaume Ally Kizigo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Seki Kasuga. (Picha na Bashir Nkoromo).
0 comments

HIZI NI FAIDA KATIKA MWILI WA BINADAMU ENDAPO TU UTAKULA FENESI.

File:Jackfruit wkm 2.jpgFENESI ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki    endapo litaliwa na mwanadamu.
Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutub
isho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.
Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa  mengine kadha wa kadha.
Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha  madini ya potassium  yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.
Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:
Kinga:  
Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.
Nishati:  
Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake  huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.
Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula  tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.
Asthma:  
Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini. MWANANCHI
0 comments

Yule msanii aliyekua akisubiriwa kwa hamu toka Ghana Fuse ODG amekuja tayari na yupo Bongo kama unavyoona tumepozi nae hapa kwa picha, cha msingi jiandae na show pale Ustawi Wa Jamii kesho...

Yule msanii aliyekua akisubiriwa kwa hamu toka Ghana Fuse ODG amekuja tayari na yupo Bongo kama unavyoona tumepozi nae hapa kwa picha, cha msingi jiandae na show pale Ustawi Wa Jamii kesho...
 
 Kutoka kushoto no Fuse ODG, wa katikati ni manager wake na Ezden The Rocker
 
 Swag za Mrs. Ezden
 
Azontoooo LIVE in Dar
0 comments

Kichaa cha Mpanda na kuanza Kupiga Puny**to Hadharani Baada ya Kuachwa na Mpenzi Wake

Kichaa cha Mpanda na kuanza Kupiga Puny**to Hadharani Baada ya Kuachwa na Mpenzi Wake

 Huyu  ni  mdada  ambaye  presha  ilimpanda  ghafla  na kujikuta  akivua nguo  zote  na kuanza  kupiga puny*to  hadharani  baada  ya kutemwa na mpenzi  wake......
Mashuhuda  wa  tukio  hili wanada  kwamba, binti huyu  alikuwa  ndani ya  gari  la  kibosile  ambaye  inadaiwa kuwa  he was her boyfriend
 Baada  ya  muda  wa  dakika kadhaa, mashuhuda  hao  walishuhudia malumbano  ya  wapendanao ndani ya  gari hilo na  ndipo  binti  huyu  alipoamriwa  ashuke  na jamaa kutokomea  kwa  speed kali.......
Binti  kuona hivyo, alianza kulia  huku  akirukaruka , mikono  ikiwa  kichwani  huku  akitamka  "baby  kwa  nini unaniacha?"....
Hasira zilipompnda zaidi, mrembo huyu  aliamua kuvua  nguo mbele  ya  umati uliomzunguka na kuanza  kujipiga  puny*eto.....
 Cha  kushangaza  ni kwamba, badala  ya  watu kumsaidia, ndo kwanza     walimwacha  na  wakaendelea  kushuhudia  SINEMA YA  BURE...
0 comments

SHOGA LAFUMANIWA NA MKEWE LIKILIWA "TIGO" .., LINA WATOTO WAWILI LAKINI SIO LIZIKI


SHOGA LAFUMANIWA NA MKEWE LIKILIWA "TIGO" .., LINA WATOTO WAWILI LAKINI SIO LIZIKI

Kuna kitu ningependa niwashirikisha marafiki wa ukurasa huu ingawa ni aibu lakini ni vyema pia na akina dada wenzangu na hata vijana wa kiume wajifunze kutoka kwangu.

Mimi ni binti wa miaka 30 na nimebahatika kupata watoto wawili wakiume na wakike na namshukuru muumba kwani wana afya tele.

Niliolewa miaka 5 iliyopita na kijana mmoja ambaye tulikuwa wapenzi kwa takribani miaka sita na baadae tukaona ni vyema tuoane.

Katika maisha yetu ni kweli baba watoto amekuwa mtu asiye na makuu na mwenye kujali na mara nyingi tumekuwa hatuna matatizo madogo madogo kwani yeye ni mzee wa mesheni town.

Nianza kusikia mtaani kuwa mme wangu sio riziki lakini nilipuuzia kwani siku hizi kijana akiwa na maendeleo kidogo na ni handsome basi watu hawataacha kumpa kashfa kibao na hasa ukizingatia kazi za mishemishe nazo huwa na majanga yake.

Hata nilipoambiwa kuwa kwa nini anakuwa karibu sana na waarabu nilipuuza kwani mimi nilimwamini sana mme wangu. Na pia nilijiuliza mbona deal zake nyingi ni dubai na oman kwa hiyo ni kawaida tu ukizingatia huko ndio kuna watu wa rangi hiyo.

Kuna wakati nakumbuka niliwahi kumuomba ruhusa niende kijijini kwetu nikawasalimie wazazi na bila hiyana akaniwekea gari tayari pamoja na vijisenti vya kuwapa wazazi na kuwa ningekaa kule kwa muda wa wiki mbili.

Kwa bahati mbaya sikuweza kukaa siku zote kwani kuna tatizo lilijitokeza ikanibidi nirudi mapema bila kumwambia nikijua tungejadiliana kunako nyumbani nikifika

Sikuamini kwani kufika nyumbani tena kwenye chumba.chetu cha kulala nikaona boxer ngeni nikamuuliza hii ni ya nani? Nakumbuka akanijibu kuwa ni ya shamba boy, nikajaribu kuuliza ilifikaje ndani kwetu akadai usiku alikuwa anaogopa hivyo akawa akilala na shamba boy.

Ulikuwa ni mtihani kwangu ingawa ilinibidi niamini huku nikijiuliza kama baba anakuwa muoga sie wana famialia tunaohitaji ulinzi wake itakuwa vipi? Basi yakaisha na maisha yakaendelea.

Ilipita miezi na sasa ni miaka ambapo wiki iliyopita nimemfumania live akiwa na jibaba la kiarabu tena bila aibu juu ya kitanda chetu cha ndoa.

Nilishtuka na kidogo nizirai lakini nilijikaza hasa ukizingatia sikutaka majirani wapate hili, kwa aibu akanifuata na kuniambia nimsamehe kwani ni mara ya kwanza na amefanya hivyo ili apate deal la kwenda Dubai kufanya shoping ya nyumba na ofisi yetu mpya.

Kweli niliamua kumuachia nyumba na nimeondoka na wanangu mpaka sasa nipo nimepanga sehemu ambapo nimeanza maisha mapya na kamwe hata niona maana ni laana.

Nawaasa vijana hakuna haraka ya kukimbilia maisha mazuri, one step at a time.....

Dunia imeisha
0 comments

HALI YA MSANII BANZA STONE NI MBAYA...

HALI YA MSANII BANZA STONE NI MBAYA...

NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani.

Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba. 



“Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa,” alisema Banza na kuongeza:

“Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.”
0 comments

Ili kuchochea kasi ya maendeleo, watendaji wilayani Handeni waapa kufunga mkanda

Ili kuchochea kasi ya maendeleo, watendaji wilayani Handeni waapa kufunga mkanda

Na Kambi Mbwana, Handeni
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, amesema kwamba wameamua kufunga mkanda kuhakikisha kuwa kasi yao inazidi kushika kasi kwa kufanya kazi bila kuchoka na kuonyesha mfano kwa watendaji wengine wote.
Katibu Tawala wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog ofisini kwake, Ticky alisema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakifunga mkanda kuhamasisha pia ufanyaji wa kazi za kijamii badala ya kusubiria kutoa maagizo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani
Alisema hilo limechangia kuharakisha maendeleo katika wilaya yao, sambamba na kutoa mwanya wa kusubiri ‘madudu’ kutoka kwa watendaji wavivu.

“Sisi kwa pamoja na Mkuu wetu wa wilaya, Muhingo Rweyemamu, tumeamua kufanya kazi kwa nguvu zote, zikiwamo zile za kufyatua matofali, usafi na mengineyo yote.
“Mara kwa mara haya yamekuwa yakifanywa kwa kutoa maagizo tu, jambo linalochelewesha maendeleo, hivyo tunahakikisha kuwa kasi hii inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa maendeleo ya wote,” alisema.
Tangu kuteuliwa kushika nafasi ya DC wa Handeni, Muhingo amekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watendaji wote wa wilaya hiyo sanjari na wananchi kwa ujumla, jambo linaloweza kuchangia maendeleo ya haraka kwa wilaya hiyo ya Handeni.
0 comments

Jeshi la Polisi wilayani Handeni kutangaza vita ya bange na gongo

Jeshi la Polisi wilayani Handeni kutangaza vita ya bange na gongo



Na Kambi Mbwana, Handeni
JESHI la Polisi wilayani Handeni, mkoani Tanga, limesema wilaya hiyo kwa sasa inakabiriwa na changamoto ya matumizi ya bange na gongo, hivyo wanajipanga vilivyo kulidhibiti suala hilo.
OCD wilayani Handeni, mkoani Tanga, Zuberi Chembera, akizungumza jambo na Handeni Kwetu Blog wilayani hapa.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani humo, OCD Zuberi Chembera, alipotakiwa na Handeni Kwetu Blog aelezee hali ya uhalifu katika maeneo yote ya Handeni.
OCD Chembera alisema hali ya uhalifu kwa sasa wilayani humo imepungua kwa kasi na kubakia suala la gongo na bange.

Alisema kutokana na suala hilo, ofisi yake inajipanga imara kuhakikisha kuwa linaondoa kabisa hali hiyo kwa ajili ya kuifanya wilaya hiyo ya aina yake katika mkoa wa Tanga.
“Hakuna matukio makubwa ya uhalifu kwa wilaya hii kutokana na utendaji wa jeshi la Polisi wilayani na Taifa kwa ujumla, hivyo hili tunajivunia na kuwashukuru wananchi.
“Hata hivyo, jukumu letu tuliokuwa nalo ni kudhibiti pia matumizi ya bange na gongo kwasababu hayo ndiyo kero kubwa na lazima tujipange kwa ajili ya kulitokomeza suala hilo,” alisema.
Kwa mujibu wa OCD Chembera, vijana wake wamejipanga imara na kugawana vyema majukumu ya kiutendaji hali inayopunguza matukio ya uhalifu wilayani hapa.
0 comments

KIZIMBANI YAIADHIBU JAMHURI LIGI KUU ZANZIBAR.

KIZIMBANI YAIADHIBU JAMHURI LIGI KUU ZANZIBAR.

Na MASANJA MABULA,ZANZIBAR.
TIMU ya soka Kizimbani Leo imeanza vema michuano ya Ligi Kuu Zanzibar baada ya kuibamiza Jamhuri mabao 2-0,katika mchezo uliochezwa dimba la soka Gombani kisiwani Pemba.

Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kubwa ambapo Kizimbani waliweza kuandika bao lao la kwanza kupitia Othumani Mussa katika dakika ya 30 baada ya kupiga shuti kali lililomshindi lililotinga moja kwa moja wavuni.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi,ambapo Jamhuri iliweza kuingia uwanjani hapo kwa lengo la kusawadhisha bao hilo huku Kizimbani wakiwa na lengo la kuongeza bao hilo.

Wakionekana kujipanga na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mithili ya mbogo aliyejeruhiwa alimanusura Jamhuri wapata bao lakini mchezaji wao alishindwa kuunganisha vizuri pasi aliyeipokea na kucheza fungo na kutoa mpira huo nje ya uwanja huo.

Kutokana na shambulio hilo,Kizimbani waliweza kuzinduka na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Jamhuri na kufanikiwa kuongeza bao lao la pili ambalo lilifungwa na Mfanyeje Mussa na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Kizimbani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri.

AFRICAN SPORTS KUWAVAA MGAMBO SHOOTING KESHO MKWAKWANI.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Mgambo Shooting kesho itashuka kwenye dimba la CCM Mkwakwani kuwavaa African Sports "Wanakimanumanu"ikiwa ni mchezo wa kirafiki utakaochukua nafasi majira ya saa kumi jioni.

Akizungumza na Tanga Raha,Ofisa Habari wa timu ya African Sports "Said Karsandas amesema maandaliiz ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekamilika kwa asilimia kubwa.

Karsandas alisema mchezo huo ni maalumu kwa Mgambo shooting kujiandaa na michezo yao ya ligi kuu Tanzania bara ili kuweza kufanya vema wakati African sports watatumia mchezo huo kwa ajili ya maandaliiz ya ligi ya mkoa wa Tanga.

Aidha aliwataka mashabiki na wadau wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.


Akizungumza mechi yao inayofuata ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati yao na Ruvu Shooting,Kocha Mkuu wa Mgambo Shooting ya Tanga,Mohamed Kampira alisema maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa .

Kampira alisema matumaini yao makubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao iliyosali kwenye michuano hiyo ili kuweza kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa katika nafasi tatu za juu.
0 comments

AIBU..!. MUME AMRUHUSU MKEWE AJIUZE ILI WAPATE PESA YA CHAKULA...!

AIBU..!. MUME AMRUHUSU MKEWE AJIUZE ILI WAPATE PESA YA CHAKULA...!

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, hivi karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina.
Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.

Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu baada ya wanahabari  kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.

Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa , ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:

“Pigeni hizo picha mnadhani nani ana wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula.


“Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu akiona picha zangu ataniacha mmenoa. Mume wangu yeye anajua niko wapi saa hizi, hata nikichelewa kuja huku usiku yeye ndiye hunihimiza ili nije kupata pesa.”


Mwanamke huyo aliyatoa maelezo hayo kwa ujasiri mkubwa na bila kujali kwamba anapigwa picha huku akiwa ameshikilia upande wa khanga.

Baadhi ya majirani waliposikia mkwara wa mwanamke huyo walitoka kushuhudia lakini walipokutana na mwanga mkali wa kamera   walirudi majumbani mwao na kujifungia milango huku wakidai hayawahusu .
0 comments

DAZ BABA ACHANGANYIKIWA NA KUWA KICHAA..!!! MADAWA NA UNGA ZAWA CHANZO..

DAZ BABA ACHANGANYIKIWA NA KUWA KICHAA..!!! MADAWA NA UNGA ZAWA CHANZO..

 
Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu.
 
Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake.
Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia  mwandishi wetu  jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye  ni  Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu.

 
“Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa Afande usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz hayuko sawa,” alisema.
Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu  alimtafuta Afande Sele, ndipo alipothibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema ameshampatia taarifa dada yake Daz wa Dar es salaam.

 
“Kweli hali ya Daz ni mbaya sana nimejaribu kumuweka sawa lakini nimeshindwa labda wakamfanyie matambiko ya kwao kwasababu baba na mama yake walifariki na walikuwa hawaelewani labda kuna matatizo ya kifamilia.” alisema Afande.

0 comments

Agnes 'Masogange na Melisa wawataja waliowatuma baada ya mateso makali.

Agnes 'Masogange na Melisa wawataja waliowatuma baada ya mateso makali.


Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga’ Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.


Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.

Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.


MATESO SAA 24
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.
USHUHUDA
“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.

“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.

“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.

“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.

“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.

“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.

“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.

“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.
WALIOWATUMA
“Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.
MTOTO WA KIGOGO ATAJWA
Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).

Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.

Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.

Gazeti hili lilipozungumza na Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.
ULINZI KAMA SHEHE PONDA
Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.
WAPANDISHWA TENA KORTINI
Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.

Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.
0 comments

Kambi Ya Upinzani Bungeni Imesema Haitaunga Mkono Muswada Wa Sheria Ya Marekebisho Ya Katiba Ya Mwaka 2013.


Kambi Ya Upinzani Bungeni Imesema Haitaunga Mkono Muswada Wa Sheria Ya Marekebisho Ya Katiba Ya Mwaka 2013.

Kambi ya upinzani bungeni imesema kutokana na mtafuruku uliotokea bungeni kwa kutolewa nje kiongozi wa kambi hiyo Mh. Freeman Mbowe amesema hawaungi mkono muswada  wa sheria ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2013 kwa kuwa  haiwatendei haki watanzania.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni mjini Dodoma kuhusiana na mtafuruku uliotokea bungeni kiongozi huyo wa kambi ya upinzai bungeni Mh Freeman Mbowe amesema hawatashiriki katika mjadala huo kwa kile walichodai kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kina ajenda ya siri na kushiriki kwao hawatakuwa wanawatendea haki watanzania 
Akizungumzia juu ya kile kinachoonekana kwa sasa kuwa ni uhusiano mwema baina ya chama cha wananchi (CUF) na Chadema,mbunge wa Mkanyageni kupitia CUF  Mh Habib Mnyaa amesema siasa haina adui wala rafiki wa kudumu na hivo wameungana na Chadema katika kutetea haki,usawa na maslahi ya wananchi wa Zanzibara na wale wa Tanzania Bara
Katika tukio jingine  wanasheria wa masuala ya haki za binadamu wamesema kilichotokea bungeni ni kutokana na kitendo cha naibu spika kuchelewa kutoa majibu ya miongozo kama ilivyoombwa na baadhi ya wabunge na kuwafanya wabunge wa upinzani kuona wanaburuzwa na kuamua kutoka nje na kuongeza kuwa hawakufurahishwa na jambo hilo kwa kile alichodai kuwa mawazo yawachache yanapigwa kumbo
0 comments

Kiini cha vurugu bungeni chabainika

Kiini cha vurugu bungeni chabainika

mbowe ad941

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe akizungumza kwenye kikao cha maamuzi ya pamoja na Vyama vingine juu ya kususia mjadala wa Marerkebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Bungeni juzi jioni.Kushoto ni Mbunge wa Mkanyageni,Habib Mnyaa(CUF)na Mbunge wa Kuteuliwa NCCR Mageuzi,James Mbatia.Picha na Fidelis Feli

Maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 yanadaiwa kuwa yalibadilishwa dakika za mwisho na kwamba suala hilo ndicho kiini cha vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma juzi.
Gazet  la mwananchi limefanikiwa kuona nakala inayodaiwa kuwa ni maoni ya awali ya kamati hiyo ambayo yalikuwa na mapendekezo yanayotaka kuwapo kwa marekebisho kadhaa kwenye muswada huo, tofauti na yale yaliyowasilishwa bungeni juzi na Mwenyekiti wa Kamati, Pindi Chana.

Jumatano na Alhamisi wiki hii kulikuwa na mvutano mkubwa bungeni kiasi cha wabunge wa upinzani kutoka vyama vitatu vya NCCR -Mageuzi, Chadema na CUF kuungana na kususia mjadala kuhusu muswada huo.

Imedokezwa kuwa mvutano mkali kuhusu muswada huo ulianza ndani ya kamati hiyo wakati wajumbe wake ambao ni wabunge wa CCM walipotumia wingi wao kubadili maoni ya awali na kuweka maoni mapya, hatua ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa na msukumo wa Serikali nyuma yake.

Ndani ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, wabunge wa upinzani ambao kwa idadi yao ni wachache walishindwa kuzuia mabadiliko hayo ya "lala salama" yanayodaiwa kuwa yaliwekwa Septemba 2, mwaka huu, hivyo waliazimia kuhamasisha wabunge wote wa upinzani kupinga marekebisho hayo kutokana na sababu kuu mbili.
Sababu hizo ni kutofanyika kwa mikutano ya wazi kwa umma (public hearing) upande wa Zanzibar na hatua ya kuwapo kwa mapendekezo ya Rais kurundikiwa madaraka makubwa ya uteuzi wa wabunge kutoka asasi za kijamii watakaoingia katika Bunge la Katiba.

Habari zinasema wakati fulani Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alitembelea kamati hiyo wakati ikiedelea na vikao vyake na kukuta mvutano mkali kuhusu suala la marekebisho ya sheria ya sheria hiyo na alishauri kwamba pale ambapo hawataweza kuelewana basi wasubiri uamuzi ndani ya Bunge.

Jana gazeti hili lilimtafuta Chana kupitia simu yake ya mkononi na baada ya kumweleza kuhusu madai hayo alisema: "Tafadhali sana kwa sasa niko kwenye kikao, kwanza simu yako nimeipokea kwa heshima tu, tutafutane wakati mwingine".
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alikiri kwamba kulikuwa na mapendekezo ya kuongeza idadi ya wabunge na namna ya kuwapata, lakini Serikali iliyakataa katika hatua ya majadiliano kabla ya suala hilo kufikishwa bungeni.

Tofauti ya maoni
Nakala ya taarifa ya awali ilipendekezwa kuwa katika kuteua wajumbe 166 wa Bunge la Katiba, Rais azingatie kikamilifu mtiririko wa mapendekezo ya kila kundi lililoainishwa katika kifungu cha (1) (c).

"Na endapo Rais hatazingatia mapendekezo ya kundi mojawapo, Rais afanye mrejesho kwa taarifa kwa kundi husika juu ya sababu za kutozingatia mtiririko wa mapendekezo yaliyowasilishwa kwake," inasema taarifa hiyo.Taarifa hiyo inaongeza kuwa kamati hiyo ilikuwa na maoni kwamba makundi mengine ya kijamii yaongezwe katika kifungu cha 22(1) (c) cha sheria mama, ili kupanua wigo wa uwakilishi mpana katika Bunge la Katiba, hivyo kuongeza idadi ya wabunge hao kutoka idadi ya awali 166 hadi kufikia 201.

"Kamati inashauri kuwa idadi ya wajumbe iwe 201 badala ya idadi ya wajumbe 166 iliyotajwa katika sheria mama, ili kupata idadi ya wajumbe watakaounda Bunge Maalumu la Katiba," inasomeka taarifa hiyo.
Hata hivyo, maoni hayo yanatofautiana na yale yaliyowasilishwa bungeni juzi na jana, kwani yanaonyesha kwamba kulikuwa na majadiliano na mashauriano baina ya kamati na Serikali, hivyo ilikubaliana kuwa "Rais apewe mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe Bunge la Katiba" huku idadi ya wabunge wa kuteuliwa wakibaki 166.
Kifungu hicho kiliondoa haki ya kila taasisi kuteua jina la mjumbe wake katika Bunge hilo na badala yake, ikapendekezwa kuwa Rais atapelekewa matatu ili ateue moja kati ya hayo.
Hata hivyo, jana wakati Bunge lilipoketi kama kamati kwa ajili ya kupitia vifungu vya marekebisho ya muswada huo, Serikali iliwasilisha marekebisho ya nyongeza ambayo yanazitaka asasi za kiraia ziteue majina tisa na kati ya hayo Rais anaweza kuteua jina moja na kama asiporidhika anaweza kuteua mtu kutoka nje ya orodha hiyo.
Kuhusu suala hilo Chikawe alisema: "Tangu awali ilikuwa inaonyesha wajumbe ni 166. Ni kweli Kamati ilipendekeza wajumbe hao waongezeke hadi 201 lakini pendekezo hilo halikukubaliwa, ikabakia wajumbe watakuwa 166."
Ushiriki wa Zanzibar
Itakumbukwa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilipewa wiki nne za kuendesha vikao vyake kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 12 wa Bunge uliomalizika jana, tofauti na kamati nyingine ambazo zilipewa wiki mbili.
Baadhi ya wabunge (hasa wa upinzani) wanasema madhumuni ya kupewa muda huo ni kama hayakutimia kwani hawakuweza kupokea maoni kutoka kwa makundi muhimu hasa ya upande wa Zanzibar kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo, jana Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idd, alilihakikishia Bunge kuwa upande wa Zanzibar ulishirikishwa katika kutoa maoni ya muswada huo.
Hatua ya Balozi Idd kutoa ufafanuzi ilitokana na mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba(CCM) aliyeomba kwa vile Balozi Seif yuko ndani ya Bunge basi apewe fursa kufafanua utata huo.
Kauli ya Balozi Idd inapingana na ile iliyotolewa juzi jioni na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye alisema ni kosa kubwa kamati kutochukua maoni ya Wazanzibar.Lissu alisema kulikuwa na njama tangu mwanzo za kuhakikisha kuwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala haichukui maoni ya Wazanzibari na hilo linathibitishwa na ratiba zilizokuwa zimeandaliwa na kamati.
"Katika orodha ya wadau wote 22 waliokuwa wameorodheshwa katika kutoa maoni yao juu ya muswada huu hakukuwa na Mzanzibari hata mmoja...tulipoipitia tukasema hapana Wazanzibari wako wapi," alisema.
Lissu alisema yeye, Mwenyekiti wa Kamati, Chana na Makamu Mwenyekiti, William Ngeleja walikwenda kumwona Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na kumweleza azma yao ya kwenda kuzungumza na wadau wa Zanzibar.
"Katibu akatwambia kwamba yeye ana fedha za kutuwezesha kukaa Zanzibar hata wiki moja, kwa hiyo tukarudi kwenye kamati tukatengeneza ratiba mpya na tukaongeza wadau sita wa Tanganyika na Wazanzibari wanane," alisema Lissu.
Aliwataja wadau hao kuwa ni Chuo cha Taifa Zanzibar, Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chama cha Mawakili Zanzibar, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar, Chama cha Walemavu Zanzibar na Profesa Abdul Shariff.
Wadau wengine walikuwa ni Shirikisho la Vyama visivyo vya Kiserikali Zanzibar (Angoza) na Jumuiya ya Misikiti Zanzibar na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, lakini hatukuwahi kukutana nao na kupokea maoni yao.
"Tukakubaliana kuwa tutakaa Zanzibar kwa siku tatu kuanzia Julai 14 hadi Julai 16 mpaka leo hatujawahi kuambiwa kwa nini tulizuiwa kwenda Zanzibar, lakini maneno yaliyokuwa yakisikika eti kwa sababu za kiusalama," alisema.
Lissu alisema wakati kamati yao ikiambiwa haiwezi kwenda Zanzibar kwa sababu za kiusalama, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge hilo ilikuwa Pemba ikiendelea na ziara zake.CHANZO MWANANCHI.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger