Featured Post Today
print this page
Latest Post

DENGUE HAIPO TANGA.



DENGUE HAIPO TANGA.

Na Peter Mtulia.

WIZARA ya afya na ustawi wa jamii, kupitia serikali Mkoani Tanga imekanusha madai ya yanayo enezwa wa wananchi juu ya kuwepo wagonjwa wanaougua homa ya  dengue mkoani hapa.

Akizungumzia uvumi wa kuenea kwa ugonjwa huo Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Asha Mahita, amewaambia waandishi wa habari kuwa may 12 walipokea mgonjwa aliyeonesha dalili za ugonjwa huo hatahivyo baada ya kufanyika vipimo ikaonekana hana ugonjwa huo.

Mahita amesema kuwa hata baada ya kufanyika mawasiliano katika wilaya zote za mkoa wa Tanga tarifa za kitabibu zimethibitisha hakuna mgonjwa aliyedhaniwa kuugua Dengue

Hata hivyo Mganga mkuu amewataka wananchi kutosita kuchunguza afya zao katika vituo vya afya pale inapoonekana dalili za ugonjwa huo na kutilia mkazo umuhimu wa kuendelea kufanyIKa usafi wa mazingira ili kuzuia uwezekano wa mbu wa Aedes anaeambukiza ugonjwa huo kuzaliana.
0 comments

WILAYA YA HANDENI YAJIZATITI KTK UZALISHAJI WA CHAKULA



WILAYA YA HANDENI YAJIZATITI KTK UZALISHAJI WA CHAKULA.

Na Peter Mtulia.

WILAYA ya Handeni mkoani Tanga imetangaza kuwa haitaomba tena chakula cha mtaada kutoka serikali kuu kwa msimu ujao kutokana na matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao yakiwemo mahindi na ufuta ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.

Mkuu wa wilaya ya Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ya kumtaka kila mwananchi kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

Akiwa katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi, Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni, Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni, Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema katika msimu ijao, wilaya hiyo haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana uhakika wa kuvuna chakula cha kutosha.

Amesema pamoja na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote zimekuwa zikileta madhara kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya Handeni mvua hizo zimeleta neema na faraja kwa wakulima kutokana na kuimarika kwa mazao yao mashambani.

Bw. Rweyemamu  amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha hasa mahindi na ufuta.

Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu.
 
Na kwa upande wao baadhi ya wakul;ima wilayani humo wamesema chakula kitakachopatikana msimu huu wilayani humo hakijawahi kupatikana zaidi ya miaka 30 iliyopita.


0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger