MILIONI 20 KUTUMIKA UKARABATI UWANJA WA CCM MKWAKWANI
Na Oscar Assenga,Tanga.
UONGOZI wa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga umetenga kiasi
cha sh.milioni 20 kwa ajili ya ukarabati
wa uwanja huo ambapo fedha hizo zitatumika kwa awamu mbili tofauti.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM),Gustav Mubba akiwa eneo la uwanja huo leo wakati harakati za kuukarabati zikiendelea |
sehemu ya uwanja wa Mkwakwani ikiwa imetifuliwa kwa ajili ya ukarabati leo |
Akizungumza na TANGA RAHA BLOG leo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(CCM) Gustav Mubba(pichani Juu)alisema awamu ya kwanza ya ukarabati huo ilianza tokea Novemba Mosi kwa kukarabati vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji pamoja na kuuweka imara mfumo wa maji taka na safi.
Mubba alisema matengenezo mengine ni ufumuaji wa mfumo wa
kumwagilia maji uwanjani badala ya kuweka mpira uwanjani wanaweka mfumo wa
kumwagilia kupitia mashine ya paipu.
Aidha alisema awamu ya kwanza inatarajiwa kutumia sh.milioni
7 mpaka kumalika kwakea na kiasi kilichobakia kitatumika kwa awamu inayofuatia
lengo ni kuhakikisha uwanja huo unakuwa wa kisasa zaidi.
Alisema matengenezo mengine yatakayofanyika ni kuweka mageti
ndani ya uwanja ili kuweza kuzuia mashabiki wa soka kuingia uwanjani mara baada
ya mechi kumaliza ambapo suala hilo
linasababisha vurugu kutokea au timu pinzani kuletewa fujo.
Katibu huyo alisema pia ukarabati huo utaendana sambamba na
uwekaji upya wa mabenchi ya ufundi uwanjani ambayo hutumiwa na timu shiriki
wakati wa michezo mbalimbali ikiwa inaendelea.
Post a Comment