Featured Post Today
print this page
Latest Post

NANI MTANI JEMBE 2 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR




TAARIFA KUTOKA KILIMANJARO PREMIER LAGER.


Awamu ya pili ya kampeni ya Nani Mtani Jembe imezinduliwa leo kwa waandishi wa habari na itazinduliwa kwa wadau wa Simba na Yanga kesho tarehe 4 Oktoba 2014 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam na itajulikana kama Nani Mtani Jembe 2.

Akiongea katika mkutano na waandishi leo, George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, alisema, “Dhumuni la kampeni yetu ya pili ya Nani Mtani Jembe ni kuisogeza Kilimanjaro Premium Lager karibu na wateja wake na wananchi na kuhamasisha ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kushindanisha mamilioni ya mashabiki wa  klabu hizi nchi nzima kwa kipindi cha wiki kumi kuanzia Oktoba hadi Disemba.


Alisema, “kampeni hii itazinduliwa  na mlolongo wa matukio ambapo tukio la pili litakuwa ni uzinduzi rasmi kwa wadau jijini Dar es salaam ambapo Nani Mtani Jembe 2 itatambulishwa kwa wadau na mashabiki wa Simba na Yanga. Uzinduzi huu utafuatiwa na hafla fupi za kuzindua kampeni hii katika viwanda vyote vya  bia ya TBL nchini katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Moshi na Arusha lengo likiwa ni kuongeza uelewa wa wafanyakazi wa TBL kuhusu Nani Mtani Jembe 2 ili waweze kuwa mabalozi wazuri. Pamoja na kampeni hiyo, tutakuwa na uzinduzi wa kipindi cha  televisheni  kiitwacho “Kili Chat ”ambacho kitarushwa hewani kwa muda wa wiki kumi kikijumuisha watu maarufu nchini ili kuitangaza Nani Mtani Jembe 2 zaidi na kuhakikisha  uwanja wa Taifa unajaa  siku ya mechi. ”

Akieleza utaratibu wa kampeni hiyo, Kavishe alisema kampeni hiyo itahusisha mashabiki wa Simba na Yanga ambapo jumla ya shilingi milioni 100 zitatolewa na kugawanywa kama ifuatavyo;
a) Shilingi milioni 20 itakuwa zawadi ya fedha kwa ajili ya mechi ya Nani Mtani Jembe 2, ambapo timu itakayoshinda itaondoka na kitita cha shillingi milioni 15 na shillingi milioni 5 zitatolewa kwa timu itakayofungwa mechi.
b) Kampeni hiyo itaendeshwa kwa njia ya sms ambapo mashabiki watapiga kura kwa njia ya sms na shilingi milioni 80 zitagawanywa kati ya timu hizo mbili. Kwa hiyo kila timu itaanza na shillingi milioni 40 kwenye benki maalum  mtandaoni kwa ajili ya shindano.

Kavishe alisema kwa kila bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa  500ml mnunuzi atakuta namba maalum chini ya kizibo cha bia hiyo, namba hizo atazitumia kutuma  sms kwenda kwenye namba maalum 15415.

Alendelea kusema kuwa ni lazima mnunuzi aandike kwenye sms kuwa yeye ni shabiki wa timu ipi kwa kuandika neno SIMBA au YANGA ikifuatiwa na namba zilizopo chini ya kizibo, na anapotuma sms ataweza kupunguza shilling 10,000 kwenye benki ya timu pinzani na kuweka kiasi hicho kwenye timu yake.

Mwisho wa kampeni hiyo kila klabu itakuwa imeongeza au kupoteza kiasi cha fedha kwa timu pinzani, kulingana na jinsi mashabiki walivyopiga kura.

 Alisema, “kwa mfano, kama mashabiki wa Simba watapiga kura zaidi ya mashabiki wa Yanga itamaanisha kwamba Simba itashinda na kupata fedha zaidi kutoka kwenye kiasi cha milioni 80, hivyo hivyo kwa mashabiki wa Yanga kama watapiga kura zaidi kuliko mashabiki wa Simba itamaanisha Yanga itapata fedha zaidi ”

Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa mashabiki kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Kampeni hii itafungua mlango kwa  Kili kuendelea kuwa karibu zaidi na mashabiki na vilevile itazisaidia klabu hizi kuongeza idadi ya mashabiki na kuimarisha ushabiki na mapenzi kwa timu zao.

Mbali na kampeni ya sms, Nani Mtani Jembe 2 itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga katika  promosheni mbalimbali na kuwawezesha kushinda zawadi mbalimbali kila wiki pamoja na fedha taslimu. Kampeni hii itafika kileleni mwezi Disemba ambapo itahitimishwa na mechi ya Nani Mtani Jembe 2 kati ya Simba na Yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam mbele ya mashabiki wa timu hizo. IIi timu ziweze kujiandaa vizuri, kila timu itapata kiasi cha shilingi milioni 30 kwa ajili ya maadalizi ya mechi hiyo zikiwa ni ongezeko kutoka shilingi milioni 20 za mwaja jana.
0 comments

PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI

PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI

NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MFUKO wa pensheni wa PPF umesema utawafikisha mahakamani waajiri ambao hawapeleki michango kwa wakati kwani hali hiyo inasababisha usumbufu kwa wateja wao.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa Kanda ya Kinondoni, Tanga na Pwani, Zahara Kayugwa wakati wa semina ya waajiri wa sekta mbalimbali jijini hapa.
Alisema hatua hiyo inaweza kusaidia waajiri kufikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
“Kwa kweli inatubidi tuchukue hatua, kwa sababu unakuta mfanyakazi anakuja kudai mafao halafu mwajiri amechangia asilimia tano tu, sasa wateja wanatuona kama sisi ni wababaishaji… hatutawavumilia tena," alisema Kayugwa.
Aidha, akifungua semina hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Salim Chima, alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini, hasa katika suala zima la kukuza na kuimarisha uchumi.
0 comments

KINANA AWASILI TANGA MJINI NA KUPOKEWA KWA SHANGWE.

KINANA AWASILI TANGA MJINI NA KUPOKEWA KWA SHANGWE.

 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka na kivuko cha MV.Pangani kuelekea Wilaya ya Tanga mjini ambapo anatazamiwa kukagua miradi mbali mbali na kushiriki ujenzi wa maendeleo,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Pangani Ndugu Hamis Mnegero.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Pangani baada ya kuvuka na MV.Pangani

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumuaga wakati akielekea Tanga mjni.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kigombe ,Pangani ambapo  aliwaeleza lazima kuwa makini katika kuchagua viongozi wa kijiji kwani wengi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi kiholela na kusababisha matatizo makubwa ya ardhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga mjini Mh.Omari Nundu wakati wa mapokezi katika kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini.
 Wananchi wa kata ya Marungu wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata yao
 Wasanii wa Tanga All Star wakionyesha ujuzi wa kuimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Marungu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60 wa kata ya Marungu kutoka upinzani wamejiunga CCM .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60
 Bibi Saumu Ngoma mama mzazi wa Diwani wa kata ya Marungu Ndugu Bakari Mambeya akirudisha kadi ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na kujiunga na  CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuezeka ofisi ya CCM kata ya Marungu.
 Wazee wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wakiwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alishiriki kutoa kadi za mfuko wa afya ya jamii na kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wilaya ya Tangamjini.
  
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Machui katika kata ya Tangasisi

 
 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na Wazee waasisi wa CCM Tanga mjini kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.

 
Mzee Athumani Makalo (wa kwanza kulia) akiwa na wazee waasisi ndani ya ukumbi wa mkutano Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.
 
0 comments

KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO

KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO

Meneja wa Kampeni haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akifungua Mdahalo huo na mafunzo juu ya Kujenga hoja ya upatikanaji wa Chakula na haki ya chakula, Kufuatilia upatikanaji wa haki kwenye Rasilimali za Ardhi na matumizi yake,na kuhamasisha uwekezaji kwa wakilima wadogo wadogo Hususani wanawake kwenye Muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, katika kampeni ya GROW   
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo akielezea matarajio yake akiwa kama Mama shujaa wa Chakula na Mkulima mwanamke Jinsi ambavyo wameweza kusaidiwa na Oxfam kufikia malengo yao katika kilimo na kuwa wakulima Bora wenye mfano wa Kuigwa

Mshindi wa Maisha Plus 2012 Bernick Kimiro akitoa mchango wake Jinsi kilimo kinavyo weza kumsaidia mwanamke na kufikia Malengo yake.(P.T)

Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2014 , akiendelea kuchukua Maoni mbalimbali , Mchango na mawazo ya watu mbalimbali katika Mdahalo huo.

Oscar Munga kutoka Forum CC akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mahusiano ya kilimo na mabadiliko ya Tabianchi, Pia alizungumzia ni namna gani watu wanaweza kujikomboka katika kilimo na kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Balozi wa Oxfam kupitia kampeni ya GROW Khadija Mwanamboka akielezea umuhimu wa kilimo bora na uwezeshaji wa wanawake katika kupata haki za Ardhi lakini pia jinsi gani Mwanamke anaweza kujikomboa katika kilimo na kuwa wanawake wanahaki sawa katika swala zima la kumiliki Ardhi.

Wa kwanza kulia ni mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 kutoka Zanzibar akitoa Mchango wake kuhusu Umiliki wa Ardhi na kuelezea jinsi gani wanawake wasivyo na haki ya Ardhi hiyo, na kuomba kwamba nao ni binadamu na wanahaki sawa ya kumiliki ardhi hiyo


Wakili Joseph Chiobola ambaye ni Afisa Programu kutoka Haki Ardhi akitoa ufafanuzi wa kina juu ya haki za watu kumiliki Ardhi, pia alieleza kwa kina sababu za watu mbalimbali kugombania Ardhi na kueleza namna gani Migogoro ya Ardhi inatokea na Njia za kuimaliza Migogoro hiyo.


Mkamiti Mgawe kutoka Oxfam Akichangia Jambo katika Mdahalo huo 



Afisa Ushawishi wa Ardhi kutoka Oxfam Naomi Shadrack akiendelea kutoa muongozo katika mdahalo huo.



Mchoraji Maarufu wa Katuni Muhidini Msamba akitoa mchango wake juu ya mada ambayo ilikuwa inahusu mazao kuto kuwa na thamani kuwa ndio moja ya chanzo cha wakulima waliowengi kutoka Tanzania kukosa  Masoko katika mazao yao, aliongeza ushauri kuwa kunahitajika nguvu ya ziada ili kujikwamua katika swala hilo kwa ujumla 



Mama Shujaa wa Chakula 2012 akitoa ushuhuda wake jinsi Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Jinsi walivyo weza kumpa Shamba ambalo mpaka sasa Linamsaidia yeye pia watu wengine kupitia elimu anayoitoa ya Shamba Darasa kwa wakazi wa eneo analoishi huko Morogoro. na kusisitiza kuwa na matumizi Bora ya Ardhi.


 
Mmoja wa Washiriki Akichangia Mada juu ya rushwa kuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa wakulima na kuwa kuna Baadhi yao wanamazao mazuri lakini kutokana na kuwa mkulima mdogo anashindwa kuuza mazao yake na badala yake anayeuza mazao hayo ni Mkulima mkubwa ambaye huweza kutoa hongo na Mazao yake kununuliwa kirahisi 



Mshindi wa Shindano la Maisha Plus 2014 Boniface akitoa maelezo na kuchangia katika Mdahalo huo 



Tajiel Urioh kutoka Forum CC akihitimisha Mdahalo huo





Washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini Mdahalo huo 



 Kila mmoja akiwa makini kuhakikisha anapata Somo na kulielewa ili apate kwenda wafundisha na wengine.


 Washiriki wakiwa katika Mdahalo huo
0 comments

SOSOPI AHUTUBIA WAKAZI WA MANISPAA YA IRINGA

SOSOPI AHUTUBIA WAKAZI WA MANISPAA YA IRINGA


MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Taifa, Patrick Ole Sosopi.


MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Taifa, Patrick Ole Sosopi,akihutubia umati wa wakazi wa manispaa ya iringa na katika mkutano wa hadhara wa chama hicho jana katika viwanja vya kihesa sokoni.(Picha na Friday Simbaya)(P.T)

 Wakazi wa kihesa akifuatilia mkutano juu ya lori.
Na Friday Simbaya

MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Taifa, Patrick Ole Sosopi, amemtaka vijana, wanawake na wazee wajitokeze kwenye daftar la ukazi ili kuwa wapigakura halali wakati uchaguzi za serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Desemba 14 mwaka huu pamoja hule uchaguzi mkuu wa 2015.

Alisema kuwa bila kufanya hivyo watakosa haki ya kuchagulia na kuchagua wakati chaguzi hizo.

Ole Sosopi ambaye kabla ya kuchaguliwa ngazi ya Taifa, alikuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Ismani mkoani Iringa na anat kuwasili jimboni kwake Jumatano.

Ole Sosopi katika msafara huo aliaambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Iringa mjini Leonce Marto.

Hata hivyo Ole Sosopi aliwataka vijana kwa wazee wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali kupita chama hicho wakati uchaguzi wa serikali za mitaa utakafika hapo baadaye.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger