Featured Post Today
print this page
Latest Post

PANGANI YAHITAJI MIL 200 ILI KUTEKELEZA MIRADI YA AFYA.

PANGANI YAHITAJI MIL 200 ILI KUTEKELEZA MIRADI YA AFYA.

Na Oscar Assenga,Pangani
JUMLA ya shilingi milioni 200 zinahitajika kila mwaka ili kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo katika Idara ya Afya wilayani Pangani mkoani Tanga  iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi mzuri.

Kaimu Mganga wa wilaya ya Pangani,Dr.Frank Makunde aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari za vijijini mkoa wa Tanga (Taruja)walioitembelea halmashauri ya wilaya hiyo kwa lengo la kuzungumza na waataalamu kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.

Waandishi hao walikuwa wilayani Pangani kwenye semina ya wandishi wa habari za mazingira ambayo iliratibiwa na chama hicho na kufadhiliwa na shirika la hifadhi ya Taifa ya Tanzania (Tanapa) yenye lengo la kuwapa uelewa wanahabari juu ya umuhimu na uhifadhi wa mazingira.

Makunde amesema idara hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti hali ambayo inapelekea kukwamisha baadhi ya miradi yao muhimu kwa jamii zinazowazunguka na kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Aliongeza kuwa mfumo manunuzi uliowekwa na serikali unakwamisha sana watendaji mbalimbali kwenye halmashauri hasa katika idara ya afya na kupelekea kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.

   "Mfumo wa kuwalazimisha kununua vitu MSD wanapeleka maombi ya vitu wanaambiwa havipo hali ambayo inawapa usumbufu mkubwa wa kusubiri wakati uhitaji wetu ni kwa wakati huo hivyo kupelekea kukwambisha shughuli zetu za kila siku ....tunaiomba serikali iangalie mfumo wa MSD usiwe mmoja uwe zaidia ya mmoja ili kuleta ushindani "Alisema Makunde.

Aidha alisema idara hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa watumishi hali ambayo inapalekea watumishi wengine kufanya kazi za ziada na kueleza suala lengine linalowapa wakati mgumu sana ni kutokuwepo wa nyumba za kutosha za watumishi kitendo ambacho kinachangia watumishi wengine kutopenda kufanya kazi wilayani
humo.

Alieleza changamoto nyengine wanayokabiliana nayo ni uhaba wa vitendea kazi hasa kwenye wodi ya wakina mama wajawazito ikiwemo uchangia mdogo wa wananchi katika mfuko wa afya ya Jamii (CHF).
0 comments

TANAPA KUANZISHA MIRADI YA VIVUTIO VYA ASILI KWENYE VIJIJI VYA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI HIZO.

TANAPA KUANZISHA MIRADI YA VIVUTIO VYA ASILI KWENYE VIJIJI VYA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI HIZO.

NA AMINA OMARI,PANGANI

Hifadhi ya Taifa TANAPA inatarajia kuanzisha miradi ya vivitio vya asili vilivyoko kwenye vijijini vya maeneo yanayozunguka hifadhi hizo ili kuimarisha uchumi wa maeneo hayo na jamii inayozunguka hifadhi hizo nchini.

Hayo yameelezwa na Meneja Ujirani mwema Taifa Ahmed Mbagi wakati akiongea na  waandishi wa habari za mazingira Mkoani Tanga TARUJA walipotembelea hifadhi ya saadani ikiwa ni sehemu ya mafunzo yaliyoandaliwa na TANAPA .

Amesema miradi huyo ni sehemu ya mipango waliyokuwapo nayo ya kuhakikisha vijiji vinavyopakana na hifadhi za taifa kunufaika na wageni waoingia kwa njia ya vivutio vilivyoko kwenye maeneo yao kwa lengo la kujiongeza kipato.

“Nia yetu ni kuona wanachi wananufaika na raslimali walizokuwapo nazo kwa kuweka utaratibu wa kila maeneo kutangaza vivutio walivyonavyo zaidi ya wanyama walioko kwenye hifadhi basi wajionee mila na tamaduni zilizoko sehemu husika “.AlisemaMbagi.

Nae Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Hussein Mselo amesema kuwa bado wananchi wa maeneo hayo hawana muako wa kutangaza vivituo vilivyoko kutoka na kukosa uwelewa wa taratibu za uendeshaji wa vivutio hivyo.

“Hapa kijijini tuna vivutio kama soko la watumwa,mbuyo nyonga ambao ulitumika kuwanyonga watumwa pamoja na makaburi ya wajerumani wakwanza kurika saadani lakini kutoka na kukosa uwelewa wa kuvitangaza vivutio hivyo tunakosa fedha kutoka kwa watalii”alisema Mselo.

Alisema kwa sasa waandaa utaratibu wa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi  wa maeneo ya jirani yenye vivutio hivyo ili kujua umuhimu wake pamoja na fursa zilizopo ili waweze kuiongezea kipato kitakacho saidia kijiji na wananchi wake.

Hifadhi ya Saadani licha ya kuwa na mbuga za wanyama ni moja ya eneo la kwanza kuanzishwa kwa biashara ya soko la watumwa na waarabu waliowahi kuishi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki karne ya 14 iliyopita.
0 comments

HIVI WEMA ALIMKOSEA NINI DIAMOND, KAMPIGA TENA KIJEMBE KWENYE WIMBO WAKE MPYA

HIVI WEMA ALIMKOSEA NINI DIAMOND, KAMPIGA TENA KIJEMBE KWENYE WIMBO WAKE MPYA 

Leo video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.

Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.

Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno amabyo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.

Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???
0 comments

KASHFA YALIKUMBA JESHI LA POLISI TENA-CCTV ZAZIMWA KURUHUSU UJAMBAZI

KASHFA YALIKUMBA JESHI LA POLISI TENA-CCTV ZAZIMWA KURUHUSU UJAMBAZI 

SIKU chache baada ya tukio la wizi mkubwa wa fedha katika Benki ya Habibu mjini Dar es Salaam, siri nzito zimeanza kuvuja kuwa polisi wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo kwa kuhujumu kamera za usalama za CCTV zinazomilikiwa na jeshi hilo. Katika tukio hilo, watu wanaodaiwa kuwa majambazi walipora dola za Marekani 20,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 32 za Tanzania.

Katika tukio hilo, Polisi Mkoa wa Ilala inamshikilia askari mmoja kwa kosa la kuhusika katika tukio hilo kutokana na kushindwa kuchukua hatua za haraka wakati tukio linatokea.
Habari za uhakika kutokana ndani ya jeshi hilo, zinasema siku ya tukio polisi waliokuwa zamu kuongoza mitambo hiyo, kwa namna moja au nyingine wanadaiwa kufanya hujuma hiyo, kwa lengo la kupoteza mawasiliano na maeneo mengi ya polisi.

Chanzo chetu hicho, kiliongeza kuwa siku ya tukio eneo lote la mzunguko wa barabara ya Uhuru na maeneo ya jirani na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), sehemu zote hazikuwa na huduma ya kamera za usalama, jambo ambalo si la kawaida kutokea.

“Hatua iliyofikia sasa ni mbaya, huwezi amini siku ya tukio kamera za CCTV zinazotumiwa na polisi zilizimwa kabisa, kitendo hiki kilisababisha polisi makao makuu wasijue nini kinachoendelea pale.

“Ndiyo maana utaona kuna askari mmoja anashikiliwa katika tukio lile, haiwezekani kituo kikuu kishindwe kubaini uwapo wa tukio hili, wakati kuna mawasiliano ya kutosha, umefika muda wa kulisafisha jeshi letu kwa kasi,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho, kilisema mitambo ya kamera hizo, ilizinduliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa mwaka 2004 na imekuwa ikifanya kazi bila matatizo yoyote.

“Nimekuwapo hapa tangu mwaka 2004, kamera hizi zilipozinduliwa rasmi na hazijawahi kuharibika hata siku moja, iwe siku ya tukio zisifanye kazi,” kilihoji chanzo chetu.

Askari aliyekamatwa katika tukio hilo, anadaiwa anafanya kazi katika kituo cha Oysterbay Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alithibitisha kukamatwa kwa askari huyo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa na MTANZANIA jana, alisema ameipokea taarifa hiyo na wanaifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

“Taarifa hii tumeipokea, tunaifanyia kazi haraka sana ili kupata ukweli, naomba tuwe na subira,” alisema kwa kifupi Kamishna Kova.

Alisema bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba watu waliokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya dola.

 

0 comments

MWANAMKE ANASWA NA RUNDO LA SARE ZA JESHI JWTZ

MWANAMKE ANASWA NA RUNDO LA SARE ZA JESHI JWTZ 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Saida Mohamed (30), mkazi wa Mwasonga Kigamboni, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 31, mwaka huu, katika eneo la Mwasonga, Kigamboni.

Alisema Saida alikamatwa na suruali saba, mashati saba ya kombati, kofia 10, shati mbili nyepesi, fulana mbili na kofia moja aina ya bareti, vyote vikiwa mali ya JWTZ.

Alisema mtuhumiwa huyo, alikuwa na begi moja la kuwekea nguo za jeshi, cheo kimoja cha Koplo na mikanda miwili ya kijeshi. 

Alisema uchunguzi unaendelea juu ya mwanamke huyo ili kubaini sababu za kumiliki sare za jeshi, kabla ya kufikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, polisi wamemkamata Husein Mkondoa (25), mkazi wa Gongolamboto Mzambarauni, akiwa anaendesha pikipiki huku akiwa amevaa nguo za kiraia na kofia ngumu ya kijani yenye nembo ya Polisi.

Alisema polisi walimtilia mashaka na kumkamata mtuhumiwa na anaendelea kuhojiwa.

“Naomba kutoa onyo kwa watu wote wenye silaha na sare za jeshi wazisalimishe kwa polisi au ofisi yoyote ya Serikali, msako wa kuwakamata wahalifu utakuwa endelevu na tutaingia nyumba hadi nyumba kuwatafuta wahalifu.

“Sambamba na operesheni hii, licha ya kubadilisha uongozi katika kituo cha Polisi Ubungo, tumeamua kutupia macho vitendo vya utapeli katika eneo la Ubungo Bus Terminal, ambalo watu wengi wanajifanya askari.

“Licha ya hilo, tumeunda kikosi cha kutumia video kamera na kamera za picha mnato ili kubaini na kuchukua hatua na nyendo mbalimbali ili kujenga ushahidi wa wahalifu hao wasiepuke mkono wa sheria,” alisema Kova.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kuchonga hati mbalimbali zinazotaka kufanana na za Serikali.

Kamishina Kova, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shadrack Samwel (27) mkazi wa Mbagala Sabasaba na Mwangi Samwel (38) mkazi wa Kimara Baruti.

Alisema watu hao, hawana ofisi maalumu hivyo hufanya shughuli hiyo sehemu yoyote na ofisi zao kuu ni mkoba pamoja na gari ambalo wanatembelea, lenye namba za usajili T 397 ADX aina ya Crester.

“Watuhumiwa hawa, tuliwakuta na mihuri 27 ambayo ni ya Serikali na taasisi binafsi, mihuri ya mawakili wa kujitegemea na wa serikalini, mhuri wa Jeshi pamoja na mhuri wa Serikali za mitaa.

“Pia tumewakamata na nakala mbalimbali za SUMATRA, ikiwemo karatasi za kukagulia magari, pleti namba za magari pamoja na nakala mbalimbali za ofisi hiyo,” alisema.

Katika hatua nyingine, polisi wanawashikilia watu watano, akiwamo Enea Dawsoni, ambaye ni mfanyakazi katika Kapuni ya Ndege ya Fast Jet, kwa jaribio la kutaka kupora fedha kiasi cha Sh 60,000,000 katika Kampuni hiyo.

Alisema watuhumiwa hao walinaswa katika Mtaa wa Samora na iligundulika walikuwa wana mawasiliano ya simu.

“Baada ya kuwakamata watu hawa, Polisi walielekea katika ofisi hizo na baada ya kufika walichukua simu ya watuhumiwa hao na kuona ujumbe mfupi wa maneno, ulioeleza kuwa fedha zipo karibu na chooni.

“Polisi walichukua simu ya wahalifu na walipopiga simu hiyo iliyokuwa na mawasiliano na majambazi hao, simu iliita kwa sauti kubwa ndani ya maungo ya mmoja kati ya watumishi wa Fast Jet.

“Mtumishi Enea Dawson alikuwa ameficha simu hiyo sehemu za siri katika nguo zake ambapo aliumbuka na kugundulika kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na majambazi hao,” alisema Kova

Source:Mtanzania

 

0 comments

HUU NDO UKWELI JUU YA MASANJA KUHUSU UVUMI ULOVUMA KUWA ANAHUSIKA NA MADAWA ZA KULEVYA.

HUU NDO UKWELI JUU YA MASANJA KUHUSU UVUMI ULOVUMA KUWA ANAHUSIKA NA MADAWA ZA KULEVYA.

 Jana zilisambaa  habari  kwamba  masanja  mkandamizaji  na  msanii Diamond  wamedakwa  na  polisi  na  possport  zao  za  kusafiria  zimezuiwa....
Taarifa  hizo  zimemfanya  Masanja  afunguke  na  kudai  kwamba  habari  hizo  si  za  kweli, ni  habari  zenye  lengo  la  kumchafulia  jina.

Masanja  ameenda  mbali  zaidi  na  kudai  kwamba yeye  ni  mtumishi  wa  Mungu, yeye  ni  mjasiliamali  na  ni  mkulima  pia.

Mali  alizonazo  zinatokana  na  juhudi  zake  za  kazi. TBC wanamlipa  milioni  5  kwa  mwezi.Stoo  ana  magunia  ya  mpunga  zaidi  ya  1000  na  kila  gunia  linauzwa  zaidi  ya  200,000.
0 comments

RWANDA YAPANDISHA USHURU WA MAGARI YA MIZIGO YANAYOTOKA TANZANIA.

RWANDA YAPANDISHA USHURU WA MAGARI YA MIZIGO YANAYOTOKA TANZANIA.

Serikali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara (ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo (Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.
Kwa taarifa ambazo sio rasmi, kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka Rusumo  ambapo  ni  mpakani mwa Tanzania na Rwanda na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo yana plate number  za Tanzania.
Wamiliki wa Malori wameiomba serikali kuingilia kati ili kunusuru hali  hiyo.
0 comments

MAPOKEZI YA BINGWA WA DUNIA MKANDA WBF FRANCIS CHEKA NI VURUGU TUPO MOROGORO.

 Mwendesha pikipiki akiendesha pikipiki huku akiwa amesimama wakati wa mapokezi ya bingwa wa dunia mkanda wa WBF Francis Cheka (SMG) wakati akitokea jijini Dar es Salaam baada ya kumdunda Mmarekani Phil Williams kwa pointi
 
 
 
CHEKA akiwaonyesha mashabiki mkanda wa duniani wa WBF eneo la stendi kuu ya daladala ziend
azo nje ya Manispaa ya Morogoro wakati akitokea Dar es Salaam. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Msafara ukiwa eneo la Masika ukitokea Msamvu baada ya kupokewa Nane Nane mjini Morogoro.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akifafanua jambo katika hafla fupi ukumbi wa Olduvai Lodge Mafiga, kushoto ni Frnacis Cheka.
Hapa Cheka akiwakabidhi mkanda viongozi wa serikali katika hafla hiyo kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzina katikati ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jovis Sembeye.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jovis Sembeye naye kifafanua jambo katika hafla hiyo.
Huyu ni miongoni mwa waendesha pikipiki ambaye kwa namna moja ama nyingine alikuwa akifanya vurugu kwa kuendesha pikipiki bila kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Huyu naye alikuwa akiendesha pikipiki akiwa amekaa hivyo.
Hawa nao hivyo hivyo sijui kwanini wana usalama nao wasiwachukulie hatua za kisheria.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
BINGWA wa dunia mkanda wa WBF uzani wa Super Middle, Francis Cheka ‘SMG’ amewaeleza maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika mapokezi yake kuwa ubingwa alioutwaa baada ya kumtwanga bondia Phil Williams wa Marekani kuwa ni ubingwa huo ni wa wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa mapokezi yake katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Olduvai Mafiga Morogoro Cheka alisema kuwa endapo angepigwa katika pambano lake na bondia, Williams aibu ingewaangukia wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla hivyo ubingwa huo ni wa watanzania wote.
Cheka alisema kuwa yeye ndiye alikuwa mwakilishi kwa Tanzania katika ulingo kupambana na Mmarekani katika kuwania ubingwa wa dunia wa WBF kupitia mchezo wa ngumu na ameshukuru kumkung’uta kama angepoteza pambano hilo ana imani kila mtanzania angejisikia vibaya kutokana na matokeo hayo.
“Nimefurahi kuona watanzania kunipa sapoti katika mchezo huu na nawaomba waendelee hivi hivi kutuunga mkono mabondia wote katika michezo yetu ya kimataifa ili kuweza kufanya vizuri lakini kwa sababu nimemchapa Phil Williams na kutwaa ubingwa huo wa dunia na kubakia Tanzania kuna kila cha kujivunia katika hili”. Alisema Cheka.
Aliongeza kuwa namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya njema iliyoniwezesha kunipa nguvu katika pambano lile na kumtwanga mpinzani wangu, sifa hii sio ya Cheka pekee bali ni kwa wana Morogoro na Tanzania kwa ujumla hivyo kila mmoja wetu anayo haki ya kutembee kifua wazi kwa ubingwa huu”. Alisema Cheka.
Cheka alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwake kutokana na aina ya bondia na nchi anayotoka ina mabondia wenye viwango bora duniani hivyo alikuwa makini muda wote wa mchezo kuhakikisha anamtandika makonde mpinzani ili kuweza kumshinda.
Naye mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi alisema kuwa hatua aliyofikia Francis Cheka ni hatua ya kupongezwa kwa kila mkazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla hivyo baada ya mapokezi yaliyofanyika serikali itapnga hafla maalum ya kumpongeza.
Amanzi alisema kuwa Cheka ameiletea sifa Tanzania lakini na Morogoro ambako ndiko makazi yake hivyo vijana kujituma katika shughuli zao na serikali ikishaona juhudi binafsi serikali huingiza mkono wake katika kusapoti juhudi hizo.
Katika mapokezi hayo yaliyoanza majira ya 9 alasiri kwa wakazi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kando ya barabara eneo la Nane Nane huku Cheki akiwa amekaa katika gari la wazi anyanyua mkanda juu kuanzia Msamvu, Masika, Posta, Stendi kuu ya daladala na kuelekea katika ukumbi wa Olduvai Mafiga ambako hafla hiyo ilimalizika majira ya saa 12 jioni.
Cheka alipokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na chama cha mapinduzi (CCM) wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Afisa Michezo mkoa wa Morogoro Neema Msitta na maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake.
0 comments

Pacha aliyeungana sasa atolewa ICU

Pacha aliyeungana sasa atolewa ICU 

pacha1 2e1b7

Mtoto Kudra aliyekuwa ameunganika na kiwiliwili cha pacha mwenza, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mtoto huyo alifanyiwa upasuaji Alhamisi iliyopita katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na kulazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), lakini mwishoni mwa wiki iliyopita alitolewa katika wodi hiyo.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Pili Hija, alisema hivi sasa Kudra ananyonya vizuri na kwamba amekuwa akitaka kufanya hivyo kila wakati .

"Kwa kweli kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zimemweka hai mpaka leo hii, nilikuwa nimeshakata tamaa kuwa nampoteza mwanangu, nazidi kumuomba Mungu amwekee mkono wake apone kabisa," alisema Hija.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Dk Zaitun Bokhary, alisema mtoto huyo anaendelea vizuri na mwishoni mwa mwezi huu atafanyiwa upasuaji mwingine.
"Tunamwacha achangamke kwanza, mwishoni mwa mwezi huu tutamfanyia upasuaji mwingine wa kumwekea njia ya muda ya kutolewa haja kubwa, kwa kumpasua ubavuni baada ya hapo ataruhusiwa kwenda nyumbani," alisema Dk Bokhary.

Kudra alipewa jina hilo Alhamisi usiku, saa kadhaa baada ya upasuaji kufanyika chini ya jopo la madaktari saba, walioongozwa na Dk Hamis Shaaban, mtaalamu wa Ubongo na Uti wa Mgongo kutoka Moi.

Alizaliwa Agosti 18, baada ya mwanamke huyo kujifungulia nyumbani watoto pacha, huku mmoja akiwa hajakamilika viungo vyote. Pia, kiwiliwili kilichoungana hakikuwa na kichwa, macho, maini, figo ila alikuwa na mshipa mmoja wa fahamu ambao ulikuwa umeshikana na mwenzake na kulazimisha madaktari hao kumfanyia upasuaji.
CHANZO:MWANANCHI

 

0 comments

USAJILI WA MESUT OZIL NI TIBA YA UGONJWA UNAOKABILI ARSENAL?

USAJILI WA MESUT OZIL NI TIBA YA UGONJWA UNAOKABILI ARSENAL?

Mesut-Ozil-Arsenal-2245395_dab07.jpg
Klabu ya Arsenal jana imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil kwa ada ya uhamisho ambayo imevunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.

Arsene Wenger amewatimizia ahadi mashabiki wa klabu hiyo kwamba atasajili mchezaji bora mwenye jina kubwa katika dirisha la usajili ambao lilifunguliwa Julai na kufungwa September 2.


Lakini pamoja na usajili huo wa Ozil, wachambuzi wa mpira duniani wanasema kwamba Ozil ataisadia Arsenal, lakini klabu hiyo bado haijapata ufumbuzi wa matatizo yao makubwa ambapo ni kwenye ulinzi na ushambuliaji kidogo.

Arsenal pamoja na kushika nafasi ya nne kwenye ligi ni timu ambayo ilikuwa miongoni mwa vilabu vilivyokuwa vikiongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kupitia viungo wake Aaron Ramsey, Rosicky, Santi Cazorla, Jacky Wilshare na mawinga kama Theo Walcott na Lukas Podolski. Tatizo kubwa la Arsenal katika misimu kadhaa iliyopita limekuwa kwenye nafasi ya kiungo cha kukaba na upande wa ukuta wao nyuma.

Lakini mpaka dirisha la usajili linafungwa timu hiyo haijasajili beki hata mmoja huku wakiwa na mabeki wao wale wale ambao kiukweli wamekuwa wakiiangusha sana timu hii.

Ni sawa wamemsajili Ozil - lakini walikuwa na mahitaji makubwa kwenye nafasi ya kiungo cha ushambuliaji kama ilivyokuwa kwenye nafasi ya ulinzi kwa maana ya mabeki?
Ni namna gani Arsenal wataweza kumtumia vizuri Ozil ambaye ana sifa ya upishi wa mabao - ndani ya timu yao?
Je usajili wa Ozil uliogharimu fedha nyingi kuliko wowote katika Premier League msimu huu ni sahihi kwa mahitaji ya Arsenal?
Chanzo: shaffih Dauda

 

0 comments

AMNYWESHA MWENZAKE VIROBA KISHA AMLAWITI


AMNYWESHA MWENZAKE VIROBAKISHA AMLAWI

ESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.

Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.

“Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha na kupoteza fahamu,” alisema.

Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.

Alisema kuwa wasamaria wema walimshuhudia mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama huo dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu kumkamata, aliwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.

“Raia wema hao walimbeba muathirika na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye aliweza kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu makali sehemu yake ya haja kubwa,” alisema.

Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.
0 comments

WASANII MAARUFU HAPA BONGO WAONA DILI KUKIMBILIA UBUNGE 2015.


WASANII MAARUFU HAPA BONGO WAONA DILI KUKIMBILIA UBUNGE 2015.
 


Wamo,Judith Wambura (Lady Jay Dee) anaandaliwa jimbo moja Musoma,
Selemani Msindi (Afande Sele) anaandaliwa jimbo la Morogoro Mjini


Fredy Maliki (Mkoloni) anaandaliwa jimbo moja mkoani Tanga.
Jacob Steven (JB) anaandaliwa jimbo moja la jijini Dar es salaam.

Inasemekani ni kutokana na ushawishi wa wabunge vijana Halima Mdee, Zitto Kabwe, Joseph Mbilinyi na John Mnyika.
0 comments

AZAM TV RASMI, YANGA YATOSWA RASMI.

AZAM TV RASMI, YANGA YATOSWA RASMI.

Wakati Kampuni ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikisaini rasmi mkataba wa kuonyesha Ligi Tanzania Bara, Klabu ya Yanga imeshangazwa na hatua hiyo ikisema imefanyika kinyume na mapendekezo yake.

Jana, TFF na Azam Media zilisaini mkataba huo wa miaka mitatu utakaogharimu Sh5.6 bilioni, ambapo zitalipwa kwa vipindi vitatu.

Awali, pande hizo mbili ziliingia mkataba wa makubaliano kabla ya jana kusaini mkataba rasmi.

Katika mkataba huo, kila klabu itaweka kibindoni kitita cha Sh100 milioni kutoka Azam Media, ambayo itakuwa inaonyesha ‘Live’ mechi za Ligi Kuu kupitia Azam TV.

Hata hivyo, mkataba wa makubaliano kati ya Azam Media na TFF ulipingwa na klabu ya Yanga, ambayo ilidai ulikuwa na upungufu na kuomba upitiwe upya kabla ya kusainiwa mkataba rasmi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo, Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alisema, fedha zitakazotolewa na Azam Media zitazisaidia klabu kutekeleza mipango ya maendeleo.

“Soka haliwezi kuendeshwa kwa viingilio, mkataba huu utazisaidia klabu kutekeleza mipango ya maendeleo sambamba na kuifanya ligi yetu iwe bora,” alisema Nyamlani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema ameshangazwa na uamuzi wa Azam Media na TFF kusaini mkataba wakati mapendekezo yao hayajafanyiwa kazi.

“Taarifa za kusaini mkataba nimezisikia leo asubuhi, kweli zimenishangaza. Makubaliano yalikuwa, bodi ya Ligi na Azam ziupitie upya kisha mwanasheria wetu auone ndiyo mambo mengine yafuate,” alisema Mwalusako.

Aliongeza: “Siwezi kulizungumzia sana hili, lakini ndiyo yalikuwa makubaliano yetu sasa kama wamesaini bila mapendekezo yetu kufanyiwa kazi ni jambo linaloshtua.”
0 comments

HII NI MAALUM KWA AKINA DADA AMBAO HAWAJAOLEWA!!

HII NI MAALUM KWA AKINA DADA AMBAO HAWAJAOLEWA!!

Inasemekana Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia.
Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.
Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu.
Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote. Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi. Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa.
Girls mfunguke ni kweli haya.
0 comments

HALI YA MANDELA BADO MAHUTUTI INGAWA AMETOLEWA HOSPITALINI NA KURUDISHWA NYUMBANI.

HALI YA MANDELA BADO MAHUTUTI INGAWA AMETOLEWA HOSPITALINI NA KURUDISHWA NYUMBANI.

 

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani, Nelson Mandela, ametolewa hospitali ambako amekuwa akitibiwa mapafu tangu mwezi wa Juni.


Taarifa katika tovuti ya rais wa Afrika Kusini imeeleza kuwa Bwana Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwengine inabadilika.

Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.

Nyumba ya Bwana Mandela imebadilishwa ili kumruhusu kupata matibabu ya mgonjwa mahtuti akiwa nyumbani.

Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.

 

 

0 comments

MADAKTARI, MANESI WADAIWA KUFANYA VITENDO VYA KINYAMA IKIWEMO KUMNYWESHA KICHANGA MAJI YA DRIPU HOSPITALI YA ZAKHEM JIJINI DAR ES SALAAM,

MADAKTARI, MANESI WADAIWA KUFANYA VITENDO VYA KINYAMA IKIWEMO KUMNYWESHA KICHANGA MAJI YA DRIPU HOSPITALI YA ZAKHEM JIJINI DAR ES SALAAM


HOSPITALI ya Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam, inakabiliwa na kashfa nzito, baada ya madaktari na wauguzi wake kudaiwa kuwafanyia vitendo vya kinyama wagonjwa, ikiwamo kumfukuza mama mjamzito mwenye uchun
gu usiku wa manane na mtoto mchanga kunyweshwa maji ya dripu.
Tuhuma hizo zimetolewa hivi karibuni na watu waliokumbwa na matukio hayo wakati walipofuata tiba hospitalini hapo.

Madai ya watu hao yalitolewa mbele ya Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, wakati alipokutana na wananchi wa Mbagala Kichemchem kujua kero zinazowakabili.

Hata hivyo, madai hayo yalionyesha kumpa wakati mgumu mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Julius Nyakazilibe, ambapo ilibidi aokolewe na mbunge huyo kufuatia wananchi hao kupinga utetezi wake.

Mwananchi wa kwanza kuituhumu Hospitali hiyo yenye hadhi ya Wilaya, alikuwa Omar Lipweremwike (50), ambaye alidai mke wake alifukuzwa usiku akiwa katika hali ya mwisho ya kujifungua na muuguzi mmoja kwa kile alichoelezwa muda huo hawezi kuzalisha mtu.

"Mama mjamzito akiwa katika hatua ya mwisho ya kujifungua hawezi kusubiri, lakini yule muuguzi alituambia tuondoke na turudi pale asubuhi ndipo atakuwa tayari kumuhudimia," alisema Lipweremwike.

Hata hivyo, alidai baada ya kuona hali hiyo, ilimbidi kumuwahisha kituo cha Afya cha Roundtable na alifanikiwa kujifungua salama muda mchache.

"Jambo hili ni baya sana tena linawanyanyasa wanawake kwa ujumla, haiwezekani Hospitali kubwa ikawa na wafanyakazi wazembe huku vituo vya afya vikisifika kwa huduma bora," aliongeza kusema.

Naye Ester Makunda. (25) alisema mtoto wake mchanga, Mariam Mohamed alinusurika kupoteza maisha baada ya wauguzi kukataa kumuwekea dripu ya maji kwa njia ya kawaida, badala yake walimlazimisha mama yake kumnywesha maji hayo kwa kutumia chupa ya maji safi.

Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 15, mwaka huu, baada ya mtoto wake kuugua ugonjwa wa kuharisha.

Makunda alisema alipofika hapo alifuata taratibu zote ikiwamo kumuona daktari na mtoto kufanyiwa vipimo, baada ya majibu kutoka ilionekana ameishiwa maji, hivyo ilihitajika kuongezewa.

"Kitu cha kushangaza nilipofika wodini ili mtoto awekewe maji, wale wauguzi wakaanza kushindana wenyewe na baadaye walikataa wakanilazimisha nikanunue chupa ya maji ili niweke yale maji ya dripu ili nimnyweshe mwanangu, kwa kweli nilikataa," alisema Makunda.

Kama hiyo haitoshi, Makunda, alisema hata yeye mwenyewe wakati aliporudi kwa mara ya pili kupata matibabu kutokana na afya yake kutokuwa nzuri, aliambiwa maini yake yameharibika jambo ambalo si la kweli.

Alisema alibaini kitu hicho baada ya daktari aliyemuona siku hiyo kumshauri kumtafuta daktari bingwa wa maini wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini baada ya kumtafuta daktari mwingine kwa ajili ya kuomba msaada zaidi alimueleza mtu aliyemuona awali hakuwa na utaalamu kwa sababu majibu ya vipimo vyake vinaonyesha yupo safi.

Tuhuma hizo zilimfanya Dk. Ndugulile kumuinua Mganga Mkuu wa hospitali hiyo kujibu, huku akimuambia afanye uchunguzi wa kina kubaini wafanyakazi wanaofanya vitendo visivyofaa kwa wagonjwa.

Wakati akijibu, Nyakazilibe aliwataka wananchi kumpigia simu haraka endapo watapata manyanyaso wakati wanapokwenda kupata huduma.
Alisisitiza ofisi yake ipo wazi muda wote kupokea malalamiko ya wananchi na kuyafanyia kazi.

Hata hivyo, aliwakasirisha wananchi hao na kuanza kupiga kelele za kumtaka akae chini, baada ya kuwaambia wananchi hao waache kutoa tuhuma kwenye mikutano ya viongozi kwani wanaweza kumuona yeye na kutatua kwa wakati.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 

0 comments

HAYA NI MAAJABU MENGINE YA DUNIA, KIONGOZI WA DHEHEBU LA WANAODAIWA KULA NYAMA ZA BINADAMU AUAWA KIKATILI NEW GINEA

HAYA NI MAAJABU MENGINE YA DUNIA, KIONGOZI WA DHEHEBU LA WANAODAIWA KULA NYAMA ZA BINADAMU AUAWA KIKATILI NEW GINEA

 
KIONGOZI mmoja wa madhehebu ya wanaokula nyama za watu akijiita Yesu Mweusi, ambaye aliwachinja wafuasi wake wa kike wanaojulikana kama 'Flower Girl' na kunywa damu yao, amejiua mwenyewe kwenye misitu minene ya Papua New Guinea. 
 
Akiwa kavalia majoho, Stephen Tari, mwenye umri wa miaka 40, mwanafunzi aliyeshindwa masomo ya Biblia, aliwahi wakati fulani kuongoza 'wafuasi' 6,000 kwenye mikoa ya milimani nchini humo, lakini alituhumiwa kwa kuua wasichana wasiopungua watatu na, huku mama zao wakilazimishwa kutazama, akinywa damu zao.

Akijiita mwenyewe 'Yesu wa ukweli', alitiwa hatiani kwa ubakaji miaka mitatu iliyopita - kabla ya nchi hiyo kutunga sheria mpya zinazosema wauaji wanaotiwa hatiani na wabakaji wanaweza kuhukumiwa adhabu ya kifo - na alikuwa miongoni mwa wafungwa 48 ambao walitoroka gerezani miezi sita iliyopita.

Tangu wakati huo amekuwa mafichoni akiwa na wafuasi wake wa kutosha waaminifu, lakini maisha yake ya vioja yalifikia mwisho pale aliposemekana kumuua mwanakijiji wa kike wiki hii na kujaribu kukatisha maisha ya mwingine.

Akiwa amezingirwa na wanakijiji wenye hasira kali Alhamisi, anaaminika kupigwa na kukatwakatwa hadi kufa, sambamba na kibaraka wake kwenye kijiji kinachofikika kwa tabu cha Gal kilichoko katika jimbo la kaskazini la Madang.

Uchunguzi rasmi uliofanywa na Daily Mail miaka sita iliyopita uliwahoji wanawake watatu ambao walisema walishuhudia Tari akinywa damu ya binti zao waliouawa kwenye sherehe za kafara ya ajabu katika vibanda vya kijiji huku akiongoza wafuasi wake kukatisha kwenye msitu huo mnene.

Sababu ya eneo hilo ambako aliuawa kutofikika kwa urahisi, polisi hawakuwa na uwezo wa kusema kama alituhumiwa kumuua mwanamke sababu alianzisha upya dhehebu lake la zamani na alihitaji kafara zaidi za binadamu.

Mkuu wa polisi wa jimbo la Madang, Sylvester Kalaut alieleza kwamba kijiji hicho ambacho Tari alikumbwa na mauti yake kiko maili kadhaa kwa miguu kando ya njia za msitu mnene kutoka mji huo mdogo wa karibu.

"Tunapeleka polisi na daktari kwenye kijiji hicho kuchunguza chanzo cha kifo hicho.

"Kijiji hicho ambacho alikuwa akiishi ni masaa manne kutembea kwa miguu na kutokana na ushauri na ripoti zilizopatikana za hali ya mwili wake, atalazimika kuzikwa haraka iwezekanavyo baada ya uchunguzi kufanyika," alisema Kalaut.

Ofisa huyo wa polisi alionya kwamba wafungwa wengine ambao bado wamejificha na ambao wamekuwa wakijihusisha na Tari wajisalimishe wenyewe.

"Kwa sasa amekufa na hii inaweza kuwa maajaliwa ya wengine ambao pia wamezitoroka mamlaka husika. Ninaonya na kuwatahadharisha wote waliotoroka kujisalimisha wenyewe kwa mamlaka husika."

Katika kilele cha uovu wake, Yesu Mweusi alikuwa akivaa majoho meupe huku akisimama juu ya mwamba kwenye msitu mnene akitakasa na kuhubiri aina yake ya injili kwa wafuasi wake. Aliueleza umati huo kwamba watapokea zawadi kutoka mbinguni kama wakimfuata yeye.

Lakini nyuma ya mahubiri yake alikuwa na dhamira ya kishetani. Akiwashawishi wasichana wadogo aliowaita 'Flower Girls' kuingia ndani ya vibanda, aliwachinja shingoni na kunywa damu zao, kinamama walithibitisha baadaye.

Mwanamke mmoja alisema aliamriwa kunywa damu ya binti yake mwenyewe katika moja ya matukio hayo.

Polisi hawakuwa na uwezo wa kumkamata, licha ya kufahamu alikokuwa sababu ya uwepo wa 'kundi' lake kubwa - alikuwa akilindwa na kibaraka aliyekuwa akibeba bunduki kubwa, mikuki na pinde na mishale.
 
Lakini wanakijiji hatimaye walifanya 'nguvu ya umma' mwaka 2007 na hatimaye Tari akahukumiwa kifungo jela.

Sasa, ni nguvu ya kijiji kwa mara nyingine tena ambayo imehitimisha mafundisho yake haramu. Inatarajiwa atazikwa karibu na ja
mii ndogo ya msituni ambako aliuawa.

 

0 comments

WAZANZIBAR WATAKA WAJITEGEE KILA KITU.

WAZANZIBAR WATAKA WAJITEGEE KILA KITU.

 
                                                              ZANZIBA.
   
KAMATI ya Maridhiano imetoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutaka Zanzibar ijitegemee karibu kwa kila kitu.
Maeneo inayotaka yaondolewe kwenye Muungano ni uraia na uhamiaji, sarafu na Benki Kuu, mambo ya nje na usajili wa vyama vya siasa.
Kamati hiyo inayounga mkono muundo wa muungano wa Serikali tatu inayoongozwa na mwanasiasa mkong
we, Hassan Nassor Moyo, iliwasilisha mapendekezo hayo juzi katika Ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema kuwa maoni hayo ndiyo mawazo ya Wazanzibari wengi.
Mapendekezo hayo yalisomwa na Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Ismail Jussa katika Kongamano la Katiba lililoandaliwa na kamati hiyo.
Msimamo wa kamati hiyo unaelezwa kuwa chanzo cha mmoja wa wajumbe wake, Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uanachama wa CCM, Agosti 26 mwaka huu.
Akisoma mapendekezo hayo, Jussa alisema kwa kuwa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar uliziunganisha nchi zilizokuwa huru, unatakiwa kuitwa Muungano wa Jamhuri za Tanzania, kusisitiza kuwa rasimu hiyo inatakiwa kueleza wazi kwamba nchi nyingine zinaweza kuingia kwenye muungano huo.
Alisema kamati hiyo imependekeza kuwa mambo ya nje yasiwe suala la muungano na badala yake nchi washirika zisimamie zenyewe eneo hilo.
Alisema kwa kuwa muungano umetokana na nchi mbili  zilizokubali kuungana na kuunda shirikisho,  msingi wa uraia wa shirikisho utokane na msingi wa mtu kuwa raia wa nchi mshirika na si kinyume chake.
“Kila nchi mshirika (Zanzibar na Tanganyika), ibakie na uraia wake na mtu kuwa na uraia wa nchi mshirika ndiko kumpe uhalali wa kuwa raia wa shirikisho,” alisema.
 Pia kamati imependekeza Rais wa muungano ambaye atakuwa na madaraka ya juu katika shirikisho lote kwa mambo yote ya Muungano, hivyo nchi washirika zinapaswa kuwa na haki sawa katika kutoa watu wa kushikilia Baraza la Mawaziri la Muungano, Bunge na Mahakama.
Alisema rasimu inatakiwa itamke wazi kwamba urais wa Muungano utashikwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya nchi washirika yaani Tanganyika na Zanzibar na kwamba Rais atangazwe mshindi baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 50 kutoka Tanganyika na Zanzibar.
Alisema badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa Makamu wa Rais kupatikana kutokana na mgombea mwenza, marais wa nchi washirika (Zanzibar na Tanganyika) moja kwa moja wawe makamu wa kwanza  na makamu wa pili wa Rais wa Muungano. MWANANCHI

 

0 comments

MEYA WA CCM BUKOBA AKESHA OFISINI IKIDAIWA KUBADILISHA NYARAKA KISA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.

MEYA WA CCM BUKOBA AKESHA OFISINI IKIDAIWA KUBADILISHA NYARAKA KISA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.

MEYA wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani, anadaiwa kukesha ofisini na baadhi ya watendaji wake, hatua inayoibua taharuki kwa wananchi kuwa huenda anabadili nyaraka kabla ya kukaguliwa.

Hali hiyo imekuja zikiwa ni siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua miradi inayotek
elezwa na meya huyo baada ya madiwani kudai ina harufu ya kifisadi.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu kutoka mjini Bukoba, Amani alionekana kwa siku mbili na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo ofisini usiku wa manane, hatua iliyowalazimu baadhi ya wananchi kuhoji ni kazi gani zinafanyika usiku kucha hasa wakati huu wa mgogoro.

Hatua ya Amani kujihami kila anapotakiwa kukaguliwa ilijitokeza hata miezi michache iliyopita wakati timu ya wakuu wa mikoa iliyoundwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kushughulikia mgogoro huo.
Kabla viongozi hao hawajafika mkoani humo, Amani alimrejesha kazini katibu muhtasi wake aliyekuwa amestaafu ili aweke mambo sawa.

Tayari baadhi ya madiwani wanaompinga meya huo, wamemtaka akae kando ili kupisha wataalamu wa CAG kufanya kazi yao bila kuingiliwa.

Wakizungumzia kitendo hicho cha meya kujifungia ofisini usiku na baadhi ya watendaji kabla ya CAG kuanza ukaguzi, walisema kinatia mashaka na kuitaka serikali imchukulie hatua haraka kabla ya kupoteza ushahidi mhimu.

“Tunatoa tahadhari mapema kwa serikali na CCM wajue kuwa mtuhumiwa ameanza kujihami kwa kukesha ofisini na watendaji wake, hili si jambo la kawaida CAG atapaswa kuwa makini zaidi,” walisema madiwani hao.

Amani hakupatikana kujibu tuhuma hizo kwani simu yake ya kiganjani haikupatikana hewani alipotafutwa.

Katika kumaliza mgogoro wa umeya mjini Bukoba, Kamati Kuu ya CCM (CC) ilitengua uamuzi wa kuwafukuza madiwani wanane wa manispaa hiyo, ambapo chama kilidai kuwa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera iliyokuwa imewafukuza ilikiuka katiba.

Kamati Kuu chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ilimwagiza CAG kwenda mjini Bukoba wiki hii ili kukagua tuhuma hizo dhidi ya meya na kisha ripoti hiyo kuwasilishwa kwenye baraza ka madiwani ili hatua zaidi zichukuliwe ikithibitika alifanya ufisadi.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha CC kilichoketi hivi karibuni mjini Dodoma zilisema kuwa Kikwete alikiri timu iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza mgogoro huo kuwa ilibaini mianya ya ufisadi katika manispaa hiyo.

“Rais alisema hawezi kumfukuza meya kwa vile mamlaka hayo yako kwa madiwani waliomchagua, hivyo aliagiza CAG aende Bukoba kuchunguza tuhuma hizo halafu ripoti iwasilishwe kwenye baraza la madiwani hatua zichukuliwe,” alisema mtoa taarifa.
Hatima ya meya itategemea kitakachokuwa kimegunduliwa na CAG na kuwekwa katika ripoti hiyo.

“Baada ya hapo madiwani wanaweza kufanya lolote wanalotaka.
“Kama ni kumfukuza meya au la wataamua wao, kwa maana sasa watakuwa na vielelezo halisi mbele yao,” kilisema chanzo hicho.

Madiwani hao wanane waliorejeshwa na kata zao kwenye mabano ni Richard Gaspar (Miembeni), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza.

Wengine ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya (Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Karumuna (Ijuganyondo).

Vile vile, Rais aliwataka meya na mbunge wafanye jitihada za kupatana na kufanya kazi pamoja kama ilivyokuwa zamani; hata wakitaka kutumia viongozi wa dini au wa kisiasa.

Katika hali inayoonyesha kuwa hoja ya ufisadi ndiyo ilikuwa kiini cha uamuzi wa CC kutofukuza madiwani, iliamuliwa pia viwanja 800 vilivyokuwa na mgogoro, warudishiwe wananchi waliokuwa wanavimiliki na wasitozwe hata senti tano.

Madiwani hao wamekuwa wanamlalamikia meya kuwa ameiingiza manispaa katika ufisadi kwenye miradi kadhaa. Miradi hiyo ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) ambao haukufuata taratibu na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Tuhuma nyingine ni mradi wa ujenzi wa soko.

Meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.
Anatuhumiwa pia kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani.

Vilevile alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90 lakini hakueleza misingi yake.
Upo pia mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka.

Ameshindwa pia kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya mradi ya kiasi cha sh milioni 134 za ujenzi wa kituo cha mabasi.
Kwa mujibu wa kanuni za manispaa hiyo yenye madiwani 24, watatu wa CUF, wanne wa CHADEMA na 17 wa CCM, ili kupitisha uamuzi huo wa kumuondoa meya, ni lazima robo tatu ya madiwani yaani 16, wapige kura ya kuunga mkono hoja hiyo. TANZANIA DAIMA.

 

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger